Header Ads

Header ADS

Chombezo: safari sehemu ya nne (04)



wakati BERAITA akijinyoosha viungo vyake, ndipo alipomwona kijana MWAIPAMBA, akimsogelea kwa tahadhari, hapo binti huyu alishituka sana, na kujiuliza kafata nini hapa, pindi alipokuwa kwenye hali hiyo ya mshangao binti BERALITA, kijana MWAIPAMBA alishituka kuwa binti huyu kesha mstukia, akahisi kuwa binti huyu, yuko na machale ya hatari sana, yaani yupo makini sana. Ndipo akutaka kupoteza muda, huky akijipa moyo kuwa, yulebinti nizaifu, kijana MWAIPAMBA aliluka na kuuwai mkate ule, uliokuwa mikononi mwa binti BERALITA, wakati huo BERALITA alikuwa kazubaa kidogo, akimshangaa MWAIPAMBA, kijana MWAIPAMBA alifanikiwa kuunyakuwa mkate huo, na kuuweka mikononi mwake, na hapo binti BERALITA alitahamaki sana, kwa kile kitendo alichokuwa kafanya kijana MWAIPAMBA, "haijawai kuwa lahisi hivyo" alisema kwa sauti kubwa huku akipandwa na hasira kali, tena zilizidi mno, BERALITA alisimama kuonesha ya kuwa hasira zilikuwa zimemfika mahali pake,! "na haitawai kuwa lahisi kamwe" alisema Belarita na sasa alikuwa anamfwata MAIPAMBA, ambae alikuwa anaelekea kule alikokuwa amekaa mwanzo, alipo mfikia kijana MWAIPAMBA, kwa sauti kali mwambia "naomba mkate wangu kabla sija uchukuwa kwanguvu"


ITAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.