Header Ads

Header ADS

Chombezo: house girl wa dada sehemu ya pili (02)



Lakin baada ya muda kidogo alikuja bibi mmoja mzee sana ambaye alivalia mavazi meusi na mekundu na kusema mchukue huyu na mlete huku alice alinipeleka hadi chumba kile wakati naingia chumbani kwa bibi ulivumaa upepo wa ajabu sana sikuwez kujua tena tumepitia wapi na nitatokea wapi maana chumba kile kilikuwa yai na mimi nilijiona Niko ndani ya yai ambalo halina mlango wala dirisha kwa muda huo niliachwa peke yangu alice alikuwa ameshaondoka zake




Bibi aliingia tena na sikujua anetokea wapi mle ndami kwa muda ule sikuona kiti cha kukalia wala meza lakin Mara baada ya bibi kuingia alibonyeza tu sehemu moja ukutani na viti vikaja na niliambiwa nikae kwenye kiti kile.




Bibi kizee alianza kuniambia umezini na mwanangu inamanisha anakupenda na unampenda hivyo yakupasa ukubaliane na masharti ya huku kwetu na huyo ndio atakae kuwa mkeo maana anakupenda na huku kwetu kazi yetu kubwa ni kutafuta watoto wachanga kuchukua damu zao kuanzia sasa utakuwa katika jukumu la kuzunguka mahospitalini na kuchukua watoto wachanga sawaaaaaaaa aliongea huku amenikazia macho na alikuwa anabadilikabadilika kiufupi alikuwa hana umbo maalumu kwa upande wangu sikuweza kujitambua na mashart yale niliona magumu kwangu nilimuwekea ngumu kukubali kuweza kua!




Tulibishana pale na yule bibi kwa dakika kadhaa na alivyoona nimezidi aliniziba mdomo na sikuweza kuongea tena kwa muda ule nilikaa kimya na alianza kunipaka vitu vyake na kuniambia binti yangu anakupenda na alowe wako useme kuwa ni mchawi nitakuua.


CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


Alimaliza kuongea aliweza kunyoosha mkono na mlango ulionekana nilichukuliwa kama upepo kutoka mle ndani aiseee usiku huo sikuweza kulala nyumbani kabisa yan baada ya kutolewa mle ndani nilipelekwa sehemu ya kutolea adhabu na sehem ya kutunzia dam duuuuuuu damu zilikuwa nyingi sana na sehemu ya adhab alikuwepo nyoka mkubwa mno.




Nilizungushwa maeneo mengi huku bado nikiwa bubu siongei chochote muda wa kurudi duniani uliwadia maana asubuhi ilikuwa imekaribia kwenye saa kumi moja asubuhi.




Alice alirudi na kunichukua hadi nyumbani tulitokezea chumbani kwake palepale aliponipigia mkia wake alinipiga tena mkia wake ule kichwani maraa tatu na kunizunguka.




Hapo akili ilirudi na niliweza kujitambua nilikurupuka na kumuangalia alice alininyoshea kidole na kusema usiropoke chochote kwa Dada yako au kwa mtu yeyote nitakuua Mara moja aliongea hivo macho yake yalikuwa yamebadilika na kuwa kama ya paka yaani yalibadirikabadirika na kuwa rangi tofauti tofauti!




Aliweza kufungua mlango wake kwa nguvu zake za giza ulifunguka na nilitoka nakimbia kuelekea chumbani kwangu nilimuogopa sana alice kuanzia siku hio maana alikuwa sio binadam wa kawaida nilanza kukaa nae mbali.




Lakini yeye aliona kawaida sana hapo nyumbani nilwaza hivi dada yangu anajua hii hali ya alice kuwa sio mtu mzuri niliwaza kumwambi lakini nilihofia usalama wangu maana bibi yule kule tulikoenda alisema nikisema tu nitakufa .




Na Alice nae hivyohivyo nilibakia tu kuwa mpole na kuacha afanye anavyojua yeye vituko vilianza pale nyumbani alice alianza vituko kuna Siku alikuwa anatenga chakula akiwa uchi wa mnyama na mimi tu ndiye nilikuwa namuona wengine walikuwa hawaoni hali ile




Siku moja ilikuwa asubuhi sana Dada yangu alikuja kuniamsha na kunitaka niende ubungo kwa ajili ya kukata tiketi ya bus ambapo shemeji alikuwa akitaka kusafiri kuelekea Mwanza


CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


Niliamka na kujianda kwa ajili ya kwenda ubungo nilienda kupanda gari na kuelekea ubungo huku nyumbani alice alibakia peke yake na kazi zilikuwa nyingi kidogo maana maji yalikata hivyo ikabidi achote kwa jirani yetu wakati anachota yale maji huku nyumbani kulikuwa kazi ya kuosha vyombo na kudeki ndani mimi nilienda nikakata tiketi nivyorudi niliona maajabu sana kusema ukweli.




Nilingia ndani nikamkuta alice anadeki nikamsalimia ,nilivyotoka nje nikamkuta anaosha vyombo wakati bado nazubaa na kushangaa nikamuona amebeba ndoo ya maji hapo mimi nilichanganyikiwa maana alikuwa amejigawa Mara tatu na wote walikuwa wanafanya kazi!.....


BONYEZA HAPA KUPATA VICHEKESHO KUPITIA SIMU YAKO


ITAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.