George; natamani nife shemu ya pili (02)
Kitu kilipiga “Paaap!” Kwenye moyo wangu nilikua na hasira kidogo lakini kuna namna falani ni kama nilikua najisikia raha tena sana. Muda mrefu ulikua umepita bila kuwasilianan na Salma, nilkikua nishaanza kumsahau ingawa mara moja moja nilikua nikimkumbuka huku nikiwaza “Hivi kwanini aliniacha?”
“Kumbe bado ananipenda, yaani mpaka kuchunguza kuwa nina mwanamke mwingine itakua ananifuatilia na amenikumbuka, aisee! Nataka anayeye aumie kama nilivyoumia mimi!” Niliwaza huku nikitabasamu. Jackline (Sio jina lake halisi) aliniangalia kwa mshangao kidogho kwani sisi hatukua wapenzi na hakuna hata simu moja nilishawahi kumuambia kuhusu mimi kuwa wkenye mahusiano.
“Sikujua hata ananipenda kiasi hiki mpaka kufikia kukufuatilia, usijali nitaongea naye na nitemuelezea kuhusu wewe, sitaki aje kukusumbua.” Nilimuambia kwa mkato, hata alipotaka kumjua huyo mwanamke sikua na chakumuambia, kusema ukweli nilimtamani kujisifia mbele yake, kumuambia kuwa ni mwanamke wengi, niko naye na tunampenda, ana wivu sana lakini bado nilikua sijawa na uhakika ni kwanini Salma aliamua kumtafuta rafiki yangu na kumpa vitisho kana kwamba ni mwanamke wangu.
Nilijiaminisha kuwa nishaachana naye na sina mpango naye kabisa, lakini katika kipindi chote cha mahusiano hakuna siku niliyojisikia vuzuri na kijisikia kama mwanaume zaidi ya siku ile. Ilikua ni mara yangu ya kwanza kugombaniwa na mwanamke, aisee nilisikia raha. Mara nyingi wakati mimi nasumbuliwa, namfumania mwanamke wangu na kunifanyia vituko vingi nilikua nikisikia rafiki zangu wakiwaongelea wanawake zao
Niliongea huku nimkimshika na kumkumbatia Jack kwa nyuma, yaye alikua ni mfupi kwangu hivyo nilimshika kwa nyuma nikamkumbatia kama nainama huko makalio yake makubwa yakihangaika na mwili wangu, alikua ni mzuri, kila siku nilimuona kama ni mzuri lakini hakuna hata siku moja nilishawahi kumtamani. Mara zote nikiwa naye hata akikaa vibaya nilikua nikimuona kama mwanaume mwenzangu, hata kusisimkwa nilikua sisisimkwi.
*****
Furaha yangu haikudumu kwa muda mrefu, nikiwa naamini kabisa kuwa Salma ananifuatilia ndiyo maana amemtafuta Jack, nikiwa naamini kuwa labda atarudi kwangu atannitafuta yeye mwenyewe wiki ilipita bila kiusikia simu yake. Ni kitu ambcho nilikua ninakingojea kama mfanyakazi anavyosubiria msharaa mwisho wa mwezi, kila dakika kuangalia kwenye simu yake kama meseji ya muamala imeingia.
Sikutaka kuanza kumpigia ingawa namba yake nilikua nayo kichwani, nilitaka anitafute yeye ili nimjibu vibaya na kumuambia kuwa sitakia anisumbue mimi nina mtu wangu nampenda sana. Kichwani nilikua nikiamini kuwa huko aliko mambo si sawa, wiki nzima nilikua nikiiangalia simu kila dakika, wiki nzima nilikau situlii, sina amani lakini huwezi amini hakunitafuta. Raha yote niliyokua nayo iliyeyuka, kila kitu kilibadilika, nikajikuta nakua na hasira basi mimi ndiyo nikaanza kumfuatilia.
Nilifuatilia nikaja kujua kuwa alikua bado alikua akiishi na yule mwanaume wake, Biashara ilishakua kubwa na huyo mwanaume ndiyoa likua akiisimamia, niliuliza kuwa mbali na huyo mwanaume aliyekua naye alikua na mwanaume mwingine ambaye kipindi hicho alikua ni mbunge tena maarufu sana, ni mara kibao alikua akienda Dodoma na huyo mwanaume, mbali na huyo alikua na wanaume wengine wawwili, mmoja alikua ni Dereva Bajaji na mwingine alikua ni mume wa rafiki yake.
Nikisema rafiki yake namaanisha ni rafiki yake damudamu, yaani walee wapika na pakua. Rafiki yake ambaye hata kipindi ananiacha nilijaribu kumtafuta ili kujua shida ni nini kaanz akunitukana namna nilivyokua nikimnyanyasa rafiki yake na kuniambia nimuache na maisha yake. Alikua akitembea na mume wake tena mara nyingi akisafiri anaenda kulala mpaka kwa huyo rafiki yake.
“Sasa kama ana wanaume wote hawa kwanini anahangaika na mimi? Anashida gani huyu mshenzi?” Nilijiulzia lakini sikupata majibu. Baada ya kuona kuwa hanitafuti na hahangaiki na mimi basi niliamua kumuonyesha kwua na mimi nilikua na furaha, sina mpango na yeye na mimi nina maisha yangu.
Tangu kutokea kwa lile tukio nilikua bado sijaongea na Jack, tulikua tunakutana ofisini lakini nikimsalimia alikua anajifanya kutokusikia na kama tunakua mbele za watu basia taitiokia kidogo tui kwa shingo upanda. Baada ya kuona kwua kule mambo hayendi vizuri niliamua kumtafuta, nikaomba kuongea naye, ni kama naye alikua anasubiri nimtafute, ni kama alinimisi kwania linipa nafasi ya kuongea naye.
Nilimuomba msamaha na kuamua kumuambia kuhusu mahusiano yetu ya nyuma. Sikumuambia kama niliachwa na mwanamke akanidhalilisha, hapana, nilimuambiambia kuwa nilikua naishi na huyo wmanamke, namlelea mtoto wake lakini nilikuja kuachana naye kwasababu ya dini.
“Wakati nakutana naye alikua na ujauzito wa mwanaume mwingine, mimi nilimsaidia kama rafiki kwakua tangu mwanzo nilijua kuwa yeye ni muislamu na mimi nilishaapa kuwa siwezi kuoa muisalamu.lakini kwa jinsi tulivyokua karibu bila kujijua tukaingia kwenye mahusiano, ile kujakuja kwangu tukazama, aliniambia kuwa atakubadili kubadilisha dini na kwelia likua tayari kwa hilo.
Lakini yalipokuja masuala ya nyumbani, kwao waligoma kabisa asibadilishe dini, kuona hivyo namimi nikaona hakuna namna kwani mbali ya kwamba mimi mwenyewe sikua tayari kuao muislamu lakini nyumbani nako waligoma. Hapo nikampa mtaji na kumuambia tuachane, naona bado hajanisaidau kwani ni karibu miaka miwili sasa ila bado ananisumbua. Siko kwenye mahusiano nayeye na niko karibu nawewe kwakua unanivuria ila sikutaka kukurupuka nilitaka tujuaje vizuri kwanza.”
Nilimuambia, ulikua ni uongo lakinia mbao uliendana kidogo na ukweli, nilijua kama ningemdanganya sana ipo sikua ngegundua kuwa nilishawahi kuishi na mwanamke na ingekua shida. Alinisikia na kunielewa ila bado alikua na hasira, nilimuombakumtoa out siku hiyo ili tukaongee vizuri na kweli alikubali.
Kusema kweli sikua na mpango kabisa wa kutoka naye lakini nilishachunguza ratiba ya Salma, sehemua bazo anapenda kwenda hivyo nilitaka kutoka naye nikiamini kuwa hata kama asipo9niona yeye, watu hao hao aliowatumia mpaka kujua kuwa nipo na Jack, akapata wivu angewatumia kuchunguz anajujua kuwa siku ile nilitoka naye. Nilitaka sana ajue kuwa nina maisha yangu na sihangaiki tena nayeye. Ukweli nikuwa nilikua naumia na nilitaka kwenda kila sehemu ambayo niliambiwa kuwa huwa anaendaga.
Nilihangaika sana kutoka na Jack karibu kila siku lakini hakuna hata siku moja ambayo nilikutana na Salama, hali hiyo ilizidi kiniumiza. Ni kama alikua na maisha yake mengine na hana shida na mimi. “Lakini kwanini alimtafuta, kwanini anakumbushia maumivu?” Nilijiuliza bila majibu. Baada ya kuona hanitafuti na wala sikutani naye niliamua kuanzisha mahusiano rasmi na Jack, tulishakua marafiki kwa muda mrefu na niliona kumbe nayeye alikua akinipenda, nilianzisha mahusiano rasmi huku nikilazimishia kuwa nataka kuzaa naye.
Sijui kanini lakini bado maneno ya kuwa siwezi kumpa mwanamke ujauzito yaliniingia kichwani nilitaka kuwa na mtoto ili kuuonyesha ulimwengu mzima kuwa mimi ni kidume. Jack alikua akinijua, nilikua rafiki yake na alikua anapenda kuwa na mimi, nilipomuambia suala la mtoto aliniambia hawezi kubeba mimba yangu mpaka nijitambulishe kwao.
“Hakuna shida, kama ni kukuchunguza nilishakuchunguza sana hivyo naamini wewe ndiyo utakua mke wangu. Nilienda kujitambulisha kwao mimi kama mimi huku tukipanga namna ambavyo nitatuma watu. Nilikua na wasiwasi sana nikamuambia kuwa nahitaji mtoto kwanza kabla ya chochote, hata yeye ni kitu alichokua akikitaka sana. Alibeba ujauzito wangu, kusema kweli sikuamini kwani kila siku nilishajua kuwa sina uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito laklini tulipojaribu siku moja tu mimba ailiingia.
Alipima kwanza kwa kipimo cha haraka kisha kwenda hospitalini kabisa, baada tu ya kuhakikisha kweli ana mimba nilijikuta naanza kutangaza. Mara napost picha Mama kijacho, mara nampenda na kila kitu nikitaka ulimwengu kuona kuwa nimeweza kumpam mwanamke ujauzito.
“Hongwara naona unaenda kuwa Baba….” Siku moja usiku wa manane simu yangu iliita, ilikua ni namba mpya lakini nilipopokea sauti ilikua ni ya Salma. Ni simu ambayonilikua naisubiria kwa muda mrefu, karibu ya kila kitu nilichokua nikikifanya nilifanya kwaajili yake, nilitaka kumuonyesha kuwa mimi ni kidume!
“Ningetaka kuzaa na wewe ningezaa, hivi unajua ni mimba zako ngapi nilizitoa? Asikutaka kuharibu maisha yangu kwa kuwa na mwanaume kama wewe! Huyo dada naye atakua fala tu!” Alijibu kwa hasira na kukata simu, ingawa niliumia kuwa alikua anatoa mimba zangu lakini sikujali sana, nilimpotezea kama siku mbili hivi bila kumtafuta huku nikiendelea kupost picha zangu nikiwa na Jack.
Siku ya nne hivi jioni Salma alinipigia simu, aliniambia kuwa anataka kuonana na mimi hivyo anaomba kuja kwangu. Nilimkatalia sana na kumuambia kuwasimhitaji lakinia likazania, nikiwa sina hili wala lile huyu hapa mlangoni, alianza kugonga kwa fujo huku akilazimishia kuingia, ili kukwepa kudhalilika nilimfungulia mlango.
Je, salama ndiyo Baibai au itakuaje, vipi Jack akisikia atafanya nini, usijali.
ITAENDELEA…..

No comments