Header Ads

Header ADS

Simulizi fupi; kama uliona ni siri si ungekaa nayo.



Naona hatuwezi kuishi pamoja, nimevumilia kwa muda mrefu lakini nahisi kama najiumiza, kila siku nazidi kukuchukia, nakupenda sana mke wangu lakini kila nikifikiria kuwa sikuridhishi na unanitangaza basi nahisi kuchanganyikiwa, naona tupeane muda, nahitaji kuwa peke yangu.” Mume wangu aliniambia, kwanza nilishtuka, ilikua ni usiku nimelala nimepitiwa na usingizi wangu mtamu mume wangu akaniamsha.


Ghafla usingizi ulikata nilinyanyuka kutoka kitandani na kumuuliza mume wangu.
“Unasemaje? Una kitu gani kimetokea, haya mambo ya kuniridhisha yamekujakujaje?” Nilimuuliza kwa msahngaao, kusema kweli mume wangu alikua ni kila kitu katika maisha yangu, alikua ananipenda, ananijali na kunihudumia kwa kila jkitu. Katika tendo la ndoa alikua ananimudau vizuri naweza kufika kileleni hata mara tatu.

Kulikua na giza hivyo niliwasha taa, mume wangu alionekana kuwa alikua aalia muda mrefu.
“Unamaanisha nini kusema huniriodhishi?” Nilimuuliza mume wangu, aliniangalia kwa uchungu kisha akatoa simu yake, aliifungua na kunionyesha picha flani. Zilikua ni Screenshot za meseji ambazo nilikua nachart na Rafiki yangu, shoga yangu kipenzi ambaye ndiyo alikua ni msiri wangu, yeye ndiyo nilikua namuamini kupita maelezo namuambia kila kitu cha maisha yangu.

“Nakuambia leo nimemkumbuka Juma, huwezi amini sijawahi kukutana na mwanauem kama yule….” Mimi nilimtumia shoga yangu.
“Acha hizo, mume wako anavyokudekeza unamkumbuka yule mshenzi alivyokua anakupiga, nilishachoka kukubembeleza kila siku.” Alinijibu.
‘Aisee, alikua naanipiga ila yule mwanaume ana mb** tamu, yaani kuna wakati naingia Instagramna kafekero kangu kumuangalia tu. Natamani siku moja nimtafute anipe mambo mpaka kizazi kitingishike, mume wangu anajitahidi lakini kikubwa uhai, hakuna kitu, namvumilia tu kwakua ni baba mzuri, anajua kunidekeza ila Juma….”

Zilikua ni screenshot nyingi ambazo nilikua nachart na shoga yangu. kwanza nilikua nishazisahau kwani kila nikituma meseji za namna hiyo nilikua nikifuta.
“Umetoa wapi hizo?” Nilimuuliza, mume wangu hakunifisha, aliniambia kuwa hizo meseji alionyeshwa na shoga yangu, mwaka mmoja nyuma na alijaribu kuzipuuzia ila zimemnyima amani.

“Sasa hivi hata kukugusa nashindwa, sijisikii raha kufanya mapenzi na wewe, yaani nikikugusa tu naona kama unaniigizia, nahisi tupeane muda, nahitaji kuwa peke yangu.” Aliniambia, nilijitahidi kumuelewesha mume wangu, kumuambia kuwa mimi nampenda na hizo meseji ulikua ni utani tu wawanawake, ila hakuniamini.
“Najua unanipenda lakini siwezi kuishi na wewe najikuta nina hasira sana, nahisi naweza kufanya kitu kibaya. Kama umeamua kunitangaza kwa shoga yako unafikiri nimedhalilika kwa namna gani?

Niwatu wangapi umewaambia kuwa mimi sikuridhishi, kuwa unataka kurudiana na X wako?” Nilijitetea sana lakini mume wangu aliniambia anaondoka. Aliondoka kweli na kwenda kupanga chumba sehemu nyingine, nilijua kama utani lakini mwezi uliisha, miezi sita na hatimaye mwaka. Alikua anakuja kuwangalia watoto basi nikajua atarudi lakini ghafla akaja na kuniambia kuwa anataka talaka ya mahakamani kwani yeye anataka kuoa mwanamke mwingine.

Nilishangaa, nilijaribu kumuomba msamaha lakinia linipa jibu ambalo lilizidi kuniumiza.
“Huna haja ya kuniomba msamaha, si kosa lako kuwa mimi sikuridhishi, ni kosa langu, kama mwanaume nilipaswa kukuridhsiha ila nilishindwa, nashukuru kwa sasa nipo na mtu ambaye tunaridhishana. Uamuzi ni wako, kukubali talaka au tubaki hivi hivi lakini mimi sitarudi kwako.” Niliumia sana, nililia sana, niliomba msamaha nikashirikisha ndugu lakini mume wangu aligoma.

Alianzisha mchakato wa talaka lakini haukufika mbali kwani nilikataa kwenye baraza la usuluhishi, tukarudishwa kanisani ila mume wangu aligoma hata kwenda. Sasa hivi anaishi na mwanamke mwingine, kaniachia nyumba na watoto, anakuja kuwasalimia mara mojamoja. Naumia kwa meseji ambazo nilimtumia mtu ambaye nilimuamini kama rafiki. Nilimuuliza kwanini alifanya hivyo akanijibu.

“Unaringa sana mwanaume anakupenda kila siku kujishaua, Kaka wawatu anahitaji amani!” Sikujua kuwa maisha yangu ya mahusiano yalikua yanamchoma sana shoga yangu, alikua anaumia jinsi ambavyo kila siku namuambia mambo yangu, namna mume wangu anavyonijali wakati yeye kila siku analalamika vipigo na matusi. “Kama ulikua unaona ni siri si ungekaa nayo, kama wewe yamekushinda kukaa nayo mimi nani nikubebee dhambi zako, aliniambia”.

MWISHO

No comments

Powered by Blogger.