Simulizi: safari sehemu ya sita (06)
Lakini japo alikatishwa tamaa ya kuingia ndani ya bahari, ili kuwaokoa kijana pamoja na binti, lakini moyoni mwake YOROBI hakuridhika na kile walicho amua wenzake, yeye alitaka kuwasaidia watumwa hao.alibaki akiwa mtu mwenye unyonge flani, ambao uliwatia shaka wenzake, kumbuka pia alitokea kuvutiwa na binti BERALITA, japo kuwa alitaka kumwambia tokea mwanzo, lakini alikuwa ajapata nafasi nzuri, na huku akihisi hii ndio nafasi ya kumsaidia na kupatana vizuri, maana lengo lake lilikuwa ni kumchomoa kwenye utumwa na kumfanya mke kabisa, basi mbinu zake ziliishia hapo, akapoteza ata uwezo wakufanya kazi vizuri, huku akifikiria tukio lililo tokea kwa binti mrembo kudumbukia majini na kijana, na pili alihofia sana mda waliotumia ulikuwa ni mwingi kwa kwaida ya binadamu kuwa na pumzi nyingi kiasi hicho.
Sakata lilikuwa likiendelea majini huku binti akiendelea kuongoza kwa kumsurubisha kijana MWAIPAMBA, kwani maji yalianza kumzidia kijana huyo kwa kuchoka sana, kwamaumivu ya vipigo na pumzi, kiukweli hakutegemea kufanywa mfuko wa mazowezi na binti, kwa kichapo kile maana binti aliendeleza kumtwanga mpaka alipoona huyu atazidiwa, na ndipo kwa mbali binti aliona PAPA mmoja akikatiza katiza maeneo walipo, kwa mbali kidogo na maeneo hayo walipokuwa wakizipiga na kijana mwaipamba, basi aliogopa na ndipo kumshitua mwenzie, naye alipoona, hapo MWAIPAMBA jicho lilimtoka na kupata nguvu nyingi, kwani alijua ndio mwisho wake, kwani PAPA hakuwa mmoja , sasa walionekana wakija kwao kwawingi, na walionekana kuwa na njaa kali, ambayo itawafanya wapate hamu ya kuwala vijana hao.Basi kila mmoja alionekana kuwa mtulivu, iliwasi wajulishe papa kuwa wao ni msosi wao, na ndipo kijana MWAIPAMBA alipoonekana kuanza kunyata mdogo mdogo, lakini ghafla alishituka na kugeuka, na kukuta PAPA wamewazingira kila kona, huku wakikosa namna ya kutoka kwa wakati huo, mwaipamba akiamini kuwa, ndio mwisho wao, akaanza kujilahumu kwaujinga wa kujitumbukiza baharini, lakini kwa binti BERALITA alionekana kuwa shujaa, alionekna kupata wazo flani ambalo lingewasaidia, alianza kunyata na kumsogelea MWAIPAMBA, ili watakapo toka watoke wote, japo kuwa walikuwa maadui, lakini binti huyu hakuwaza hilo, nae roho ilikuwa safi, ili wajipange wapambane na hao PAPA, lazima bifu likae pembeni,
MWAIPAMBA kuona hivyo binti akisogelea akatulia, na ndipo waliposhikana na kuoneshana ishara nini wafanye, ili kutoka kwenye msitu huo wa mdudu PAPA. ndipo walipo anza kupiga maji kwa kasi na kwenda chini zidi, kwani PAPA hao walionekana kuwa juu yao,.
ITAENDELEA

No comments