Header Ads

Header ADS

Simulizi: safari sehemu ya nane (08)



Basi binti BERALITA alipoona hivyo, alimsukuma kijana YOROBI pembeni na kumtazama sana NGUVA, kama ame dhurika kiasi gani, alimwona akipiga kelele kuashiria risasi ile imempata barabara. Binti BERARITA alimlaumu sana kijana YOROBI, kwa kitendo hicho huku kijana YOROBI, akijiona kafanya jambo la kishujaha, ndipo alipokaa chini akimsikiliza binti BERALITA akifoka sana juu ya tukio, yeye hakumjari zaidi aliwaimiza vijana wake wazidi ku piga makasia nakuinuwa tanga ili jahazi liongeze mwendo, haya sasa ni atuwa gani atachukuwa Binti Nguva? isome kisha nijulishe ili nikujuze kuamuzi alio chukuwa Binti Nguva




Vijana nao walifanya kile alicho sema kiongozi wao YOROBI, kwa kuchochea chombo kile na kuanza safari, huku binti BERALITA akimsihi YOROBI japo amwonyeshe yule binti NGUVA aliye wasaidia, ishala ya kumuomba samahani kwa kile kilichotokea, lakini YOROBI hakuwa tayri kufanya hivyo kwani alijihisi yupo sahii kumtandika risasi, binti NGUVA, ndipo binti BERALITA yeye pekee ndie aliye inuwa mkono wake nakuupunga kwa binti NGUVA, kumuaga na kumpa ishara nzuri ambayo hata NGUVA yule nae alijibu kwakunyoosha mkono juu ana kuupunga.


binti NGUVA alishindwa kuwatahadhalisha juu ya huko waendako, alibaki akitazama mabaki yalio salia kwani alihisi kazi bado ya kupambana na PAPA wale, lakini alipoona hali iko shwali wala hakutaka kuangaika, na ndipo alipo jitizama kidonda chake, ambaacho kilianza kuhuma kwanguvu akashikilia jelaha, na kuangalia JAHAZI kwa machungu, kwani alipata tabu ya kupambana nao lakini hawakuona kazi aliyokuwa kafanya, na kumzawadia kidonda ambacho hakusitahiri kukipata, basi nae hakutaka kuonesha kinyongo kwao, alibaki akijisemea moyoni, "hawa ndiyo binaadamu, nilikuwa nawasikia tu," alimkumbuka sana binti BERALITA kwani ndie aliye onesha kuwa anafahamu mchango wake alioutoa wakati huo.


kwenye jahadhi nako, BERALITA alibaki akimlaumu sana YOROBI, kwa kitendo alichofanya kwa binti NGUVA, alimkumbusha kuwa ndiye aliye wasaidia yeye pamoja na MWAIPAMBA, na kumuelezea vizuri juu ya alichofanya, mpaka sasa wao ni wazima, YOROBI alichoshwa na kelele za binti huyu, akamtazama kwa mcho makali sana, hakutaka kuongea mengi, zaidi ya kumuomba asirudie tena kuobgea upuuzi wake, akidai yeye anaamini vipi kuwa yule bint alikuwa nimwema kwao, "mtu akikusaidia japo na wewe muoneshe shukrani" maneno hayo aliyatamka binti BERALITA, kwasauti ya upole yenye hisia kali, huku akimtaka sana YOROBI kuacha visa na pindi aonapo msahada, asitie jeuri zake maana alionekana kuwa kama BEPARI, kumzidi mpaka kiongozi wao chifu.


waliendelea na safari yao huku ikionekana kuwa yenye mikosi, sana licha ya kila mmoja wao kujipa matumaini juu ya kufika, lakini kukweli hali ilikuwa mbaya kwao, safari ya kurudi kwenye makazi yao ilipo kuwa ikiendelea,lakini akuna ata mmoja aliekuwa anajuwa, wanapo pelekwa na mfalme huyo, maana siunajuwa kwenye maji ataukigeuka ulipo toa wewe uelewi labda uwe na compas,ndipo kijana MWAIPAMBA nae alipo changia juu ya swala alilokuwa akipewa somo YOROBI na binti BERALITA, huku akimwambia kile kilichotokea ndani ya maji, na msaada mkubwa alikuwa ni huyo NGUVA, nae MWAIPAMBA alimlaumu, pia huku akimsihii asije fanya tena hayo, kamaita watokea tena mbele ya safari, basi nae alipoona hayo nae YOROBI alikubaliana nao, na kuwaomba radhi juu ya kile kilicho tokea, basi nao hawakutaka kujibizana basi yaliisha na kila mmoja wao kuelekea kwneye sehemu yake ya kukaa, safari ilikuwa imepambamoto, hivi huko wanakokwenda kuna nini? 






 Basi kila mmoja wao alurudi mahali pake na kuangalia chombo kikichana maji huku kikisonga mbele, ili kufika hitimisho


la safari yao, Basi kijana.YOROBI aliendelea kuongoza vijana wenzake, kukipa nguvu chombo ili wawai safari, yao ndipo nae


alipo tulia, na kufikilia kile alicho ambiwa na binti BERALITA juu ya kufanya makosa kwa binti NGUVA, ane alifikiria sana


nakukili kimoyo moyo, huku akiapa mwenyewe, hatofanya tendo kama hilo endapo akiona NGUVA yoyote akiwapa msaada.


binti BERALITA alikuwa akitizama sana maji huku yeye akifikiria juu ya safari yao, ambayo misuko suko na vijimambo,


vilivyokuwa vikiwaandama kwenye safari yao, basi alifikilia sana, juu ya hayo yanayotokea, kwani lengo lake ni kufika kwenye


kijiji chake salama, hakufahamu ya kuwa walikuwa wameuzwa na licha ya kudanganywa sana, nae alikuwa na imani ya kufika kwao


basi jioni iliingia kwa kasi, kwani matazamio yao hayakuwa ya kulala kwenye maji, ila vile vikwazo vilivyokuwa vikitokea


njiani vilifanya mpaka giza kuingia wakiwa ndani ya maji,


Waliamuwa kuwasha taa, kwenye jahazi lao, huku nae alikuwa nataa yake ndani ya begi lake, nae alipoona wakiwasha taa, nae


aliwasha ili apate mwanga maeneo yalio mzunguka, huku akilinda usalama wake kwani toka kijana MWAIPAMBA kufanya tukio, lile


hakupenda tena itokee juu yake, binti BERALITA.


Basi nae alikuwa makini sana, kwani hakutaka tena kuamini mtu, bali kujiamini yeye mwenyewe tu, kwani wote walikuwa ni


watumwa, nahakilizao uwa wanazijuwa wenyewe, ndipo kwa mbali aliona kitu kama mwangaza flani, lakini hakutaka kujifanya


kimbelembele, kuwa kaona kijiji chao, basi alikaa kimya, akiamini kuwa nawenzake watakuwa wameona, maana sasa likuwa


zikionekana taanyingi sana walizidi kukisogelea, huku akitafakali ule ni mji gani, kwani kulionekana kuwa ni mji mkubwa na


siyo kijiji kama alivyo zowea, kwani taa ziling'aa sana, na kuwaka kila kona, nae akaamua kutulia, mpaka atakaposikia tamko


kutoka kwa kijana YOROBI,


kijana MWAIPAMBA nae alikuwa amekaa pembeni, nyuma ya mrembo wetu, alibaki akimtizama sana binti BERALITA, akimtafakari


binti huyu maana siyo wa kumchezea, asa kwa kile kichapo alichopatia ,hato kaa na kumsahau binti huyo, alipokuwa akimtizama


alimpa heshima zake, kimoyo moyo huku akitupa huusika aliokuwa kauvaa juu ya binti, japo kuwa ni mdogo kuliko kwakw, lakini


kwake ilionekana tofauti sana, na kuwa kinyume chake,...




alibaki akimtizama sana binti BERALITA, akimtafakari binti huyu maana siyo wa kumchezea, asa kwa kile kichapo alichopatia ,hato kaa na kumsahau binti huyo, alipokuwa akimtizama alimpa heshima zake, kimoyo moyo huku akitupa huusika aliokuwa kauvaa juu ya binti, japo kuwa ni mdogo kuliko kwakw, lakini kwake ilionekana tofauti sana, na kuwa kinyume chake, safari ilizidi kusonga mbele, binti BERALITA alianza kujiliwaza kwa kuimba wimbo ambao hata kijana MWAIPAMBA alipousikia tu alivutiwa nao, lakini cha kushangaza hakuweza kumsogelea zaidi, sababu alitokea kumuogopa sana binti huyo, kwa kipigo ambacho hato sahau miaka nenda rudi, basi alicho amua ni kusaidia kuimba wimboule sambamba na mrembo BERALITA, MWAIPAMBA alizidi kuimba kwa sauti ya chini huku akimfatisha binti BERALITA. YOROBI alizidi kuwa amuru vijakazi wake wafanye haraka kwani safari ilionekana ya kutumia muda mrefu sana, huku giza nalo lilitanda, nakusaidia zile taa wanazoziona mbele yao wazione vizuri, huku kila mmoja wao akiwa na hofu juu ya kulala ndani ya maji, huku wakijionea visa na mikasa inayotokea, walianza kupata matumaini ya kufika mapema sana kwenye kijiji chao, na ndipo YOROBI alichukua kifa chake cha kutazamiambali, ambacho kina uwezo wa kuona kilomita ata 20, kwenye maji, na kujua wamefikia wapi, wahenga wanakiita jicho la jini, basi nae alifanya hivyo hivyo, alipoweka tu jicho lake kwenye kionw mbali, akaona kitu ambacho kilimshangaza sana, hakuamini alicho kiona kwa wakati huo, akapachika tena ilikujilidhisha, ndipo alipoona vizuri tena kwa mara ya pili, taa zikimulika kwakung'aa sana. Ndipo alipo wageukia wenzake nakuanza kuangua kicheko, huku akiwachanganya vijakazi wake, na vijana hao walimuuliza "vipi kiongozi kulikoni? mbona unacheka mwenyewe?, tujuze nasi tucheke pamoja na wewe" nae alijibu kwa kujiamini na kusema "haaaaah nimeona kitu ambacho hata nikiwaambia, mtafurahi sana, kwakifupi lisaa limoja mbele tuna weza tukawa tumefika" kauli hiyo ilifwatiwa na shangwe na Vicheko, vilitawara mahari pote, huku sasa ule wimbo wa BERALITA, ulikuwa ukiimbwa na karbia nusu ya jahazi, safari ilizidi kuendelea nawakazidi kusogea, dakika chache baadae, walianza kuona vizuri kabisa bila kutumia kifaa cha jicho la jini, walifanya sherehe, huku wakisahau yaliopita kuwa bahari hiyo ilikuwa ya mahajabu sana, basi walizidi kuongeza kasi ya kukifata kijiji au mji huo maana ulionekana ni kama mji wakisasa, matazamio yao ni kufika haraka, kwani safari iliwachosha huku chakula nacho ni chashida, walishindia mkate mdogo kutwa nzima, binti BERALITA waki wote, akiyashuhudia, hayo nae alitoa tabasamu, ambalo lilimchanganya akili kijana YOROBI, huku kijana huyo alijionesha yuko bize na shangwe za vijana hao. muda ulizidi kuhesabiwa na kijana YOROBI, huku mkadilio wake ni kufika yalikuwa ni kutumia saa limoja au moja na nusu, huku akijitamba kuwa ataonekana shujaaa pindi washukapo ndani ya JAHAZI hiyo. wakati bado watu wana shangilia huku wakiona kile kijiji au mji wanasogelea kwakasi, lakini YOROBI gunguwa jambo lakushangaza juu ya mji ule, kwanza kabisa..




wakati bado watu wana shangilia huku wakiona kile kijiji au mji wanasogelea kwakasi, lakini YOROBI gunguwa jambo


lakushangaza juu ya mji ule, kwanza kabisa, jinsi awalivyokuwa wanausogelea ulemji, japo mwendowao ulikuwa wakawaida, lakini


walionekana wakiusogelea kwaharaka sana, kingine mwonekano waule mji, nitofauti ya alivyozowea kuuona, Basi walizidi


kukata maji, huku kelele za shangwe, zikichangia kuwapa nguvu ya kuendelea na safari yao, wakiamini inaenda kufika tamati,


kufika mahari walipokuwa wakienda. ndipo binti BERALITA,alipojipa moyo kuwa mambo yako sawa, ile kutazama vizuri, mbele


zaidi, aliona wamezidi kukaribia, alizidi kuimba kwa hisia, akisidiwa na wenzake, huku moyoni mwake akiwa mwingi na shauku


ya kukanyaga aridhi yao, kwani kilikuwa ni kipindi kirefu sana, tangu atoke kwenye aridhi yao,


YOROBI aliendelea kuwaahimiza vijakazi wake, kufanya haraka kufikisha chombo inchi kavu, kulikuwa na wengine wakisita


kufanya upesi kufikisha chombo hicho, lakini akilini mwake alikuwa ikiwaza sana, na huku kichwa chake kikiwa kimejaa sifa,


mpaka kikataka kuonekana kupasuka, kwa sifa alizokuwa akizitaka pindi atakapo shuka na kuwafikisha watumwa kwenye ngome yao.


pindi watakapo fika tu atapandishwa cheo, na kumpa ngazi kubwa sana lakini huku akiendelea kuwaza hayo, alishangaaa kuona


kitu kidogo kikitoka kwenye maji na kufika mahari alipo na kuzama tena, ndani ya maji hilo tukio lilimshangaza kijana huyo,


huku ajui nini afanye kwani tukio hilo aliliona mwenyewe tu!, na kuwaza sana kiashirio cha hilo tukio, lakini alitupa kule


mawazo hayo chini, na aliposikia shangwe zikiendelea, alijawa na furaha tele, huku na kule alisahau hata tukio lilitokea


mda mfupi tu na kubaki akitazama mbele nakuona viashilio vyote vya kuwa wamefika.


Upande wa binti BERALITA, yeye alikuwa akiendelea na nyimbo zake, huku akiwa akimkosha sana kijana MWAIPAMBA mpaka kijana


huyo aliona kuvunja ukimya na kumfata binti huyo, uku akiendelea kuimba, ili apate kufurahia pamoja, kuwa wemefika safari


yao, basi nae alifanya hivyo kwa tahadhari sana, maana alijuwa kitachotokea, endapo atakosea kidogo, lakini hatimaye


alimfata, kumbe binti BERALITA hakuwa na mawazo hayo, aliyokuwa akiwaza kijana MWAIPAMBA, yeye alikuwa kawaida tu, yale ya


nyuma alikuwa ameyasahau, basi nae alipomuona tu kijana MWAIPAMBA ..





ITAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.