SITASAHAU NILIVYOFANYA KAZI YA KUNUNUA KONDOMU ZILIZOTUMIKA.
Sehemu ya Kwanza ( 1 )
***********
Umeshawahi kufanya mapenzi lodge kwakutumia kondomu kisha ukaitupa kwenye dustbin ? Umewahi kufanya mapenzi na kahaba halafu salama uliyotumia ukaiacha au kuitupa eneo mlilofanyia mapenzi?
Kwa majina naitwa Richard Onesmo, mkazi wa Mbinga mkoa wa Ruvuma. Mwaka 2018 kaka yangu aishie marekani alinipa kazi ya kununua kondomu zilizotumika. Wakati ananiambia nilijua utani lakini baadae nikajua ni kweli haukuwa utani.
Kunithibitishia yuko serious alinitumia million kumi kwa ajili ya hio kazi. Pia aliniahidi kunilipa vizuri kama nitafanya kazi vizuri.
“ Kwahiyo bro kondomu moja iliyotumika tutainunua sh ngapi?” Nilimuuliza.
“ Kila kondomu moja tutanunua elfu 25.” Aliniambia.
Niliduwaa.
Elfu 25 kwangu ilikuwa nyingi sana kulipia salama iliyotumika. Niliona ni ufujaji wa fedha, maana paket ya kondomu yenye salama tatu ndan inauzwa elfu moja,Sasa kununua kondomu moja iliyotumika kwa elfu 25 sikuona kama ni sahihi.
“ Naomba nisikilize Richard! Nunua kwa bei hio hio niliyokuambia.” Alinisisitza kaka. Nilikubali. Muda ule ule alinitaka nianze kazi! Nami sikuvunga. Nijiweka sawa, niliita pikipiki nikaanza kuzunguka kwenye nyumba za kulala wageni yaani lodge na guest house.
Lodge ya kwanza kwenda ilikuwa inatwa Double M lodge.
“ Karibu kaka unataka chumba?” ALiniuliza muhudumu .
“ Hapana! Shida yangu sio chumba.” Nilimwambia. Nilisogea kwenye sofa lililokuwa pale mapokezii na kukaaa. Nilimtazama yule dada usoni kisha bila hofu nilimueleza shida yangu. Yule muhudumu hakunielewa, alihisi namfanyia utani usiokuwa na maana.
Kumuonesha nipo serious, nilingiza mkono mfukoni nikatoa laki moja, nilimkabidhi na kumtaka anipigie simu akipata kondomu nne zilizotumika.
“ Eeeh! Yaan kondomu nne zilizotumika ni laki moja?” ALiuliza kwa mshangao. Macho yalimtoka asiamini anachokiona.
“ Ndio, kwasababu kondomu moja ni elfu 25.” Nilimwambia. Macho yalizidi kumtoka yule dada. Alinitaka nisubiri. Alitoka mapokezi na kuelekea mlango wa nyuma, nusu saa mbele alikuja akiwa na mfuko, alinikabizi, kuutazama ndani ulikuwa umejaa kondomu zilizotumika.
“ Hizo ni kondomu walizotumia jana wateja wetu, nilikuwa nimezimwaga shimoni nizichome moto.” Aliniambia.
Nilimtazama kisha nikazitazama zile salama tena. Aliniletea ndoo nikazimwaga ndani ya ndooo zilikuwa kumi na 6.
“ Utanipa sh ngap kwa hizi zote?” ALiniulza.
“ Fanya 16 mara 25.” Nilimwambia. Wakati yeye akibonya bonya simu kupiga hesabu, mimi niliingia watsup na kumpigia watsup call kaka.
“ Nipo lodge hapa, kuna kondomu kama 16 hizi zimepatikana, ila nina mashaka nazo maana zilitupwa shimon.” Nilimwambia.
“ Usijali, la msingi hizo salama zilitumka, yaani mwanamke na mwanaume walizifanyia mapenzi.” Aliniambia.
Sawa .
Nilimjibu na kurudi ndani.
“ Umepata sh ngap baada ya kuzidisha 16 mara elfu 25?’ Nilimuulza muhudumu. Aliniambia kapata laki nne. Sikujali. Niliingiza mfukoni nikatoa laki tatu, na ile moja niliyompa ikawa laki nne. Nilimwachia namba yangu kisha nkaziweka zile salama vizur na kutoka nazo.
Nikiwa getini yule dada aliniwahi.
“ Hadi sasa sielew aiiseee! We salama zilizotumka unaenda kuzifanyia nni had unanipa hela nyingi hivi?” Aliniuliza.
“ Hilo halikuhusu dada, wateja wako wakitoka vyumbani ingia uchukue salama zote zilzotumka kisha nipigie simu.” Nilimwambia. Nilipanda kwenye pikipiki na kuondoka.
…………………
Masaaa matano mbele nilikuwa na furushi la kondomu zilizotumka! Lodge na guest house zote ninazozifahamu nilipita. Majira ya saa mbili usiku nikiwa chumban kwangu, nililifungua furushi lililojaa kondomu nikawa nazitazama.
“ Cheeeeeeeeeeeee……chiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii…” Harufu mbaya ya manii ilinifanya nipige chafyaaaa.
“triiiiiii..triiiiiiiiiiiiiii..” Simu yangu upande wa watsup iliita. Nilishika na kuitazama alikuwa kaka.
“ Afadhali kapiga… nataka anipe utaratibu wa hizi kondomu.. kukaa nazo ndani sio sawa.” Niliwaza huku nikipokea simu yake, lakini kaba sijasema lolote, kaka alinambia jambo lililonishtua sana.
“ Unasemaje?” Nilimuuliza kwa hamaki kana kwamba sijamsikia alichoongea.
Mkiwa wavivu kucoment namimi nakuwa mvivu kupost hivyo comment kwa wingi jamani ili mnie mizuka
# PIA USISAHAU KUNI FOLLOW ILI USIWE UNAPITWA NA STORY ZANGU FAIDA YA KUNI FOLLOW NI KUWA WA KWANZA KUPATA STORY KILA NINAPO POST
No comments