Header Ads

Header ADS

Simulizi: Tabasamu langu ni majonzi sehemu ya kwanza (01)

 




IMEANDIKWA NA : AISHA KHAN

*********************************************************************************


 

UTANGULIZI: naishi katika jiji kubwa la Kenya liitwalo Nairobi Pamoja na wazazi wangu wote wawili na wadogo zangu wawili mapacha mmoja wakiume Jina lake Abdallah na mwingine Munira umri wao miaka mi 6, jina langu naitwa Madina Nina umri wa miaka 24 nimefanikiwa kuhitimu chuo kikuu kwa maswala ya udaktari.

 

Familia yangu Haina uwezo wa kifedha kivile, Ila maisha ya nyumbani vile vile sio mabaya kivile.

 

 

SONGA NAYO!

 

Kila siku nyumbani Mimi nilikuwa nikisikia baba na mama wakigombezana Mara kwa mara Jambo ambalo sikuwahi kulisikia kabla.

 

Siku moja tulikuwa tumekaa mezani huku tukiwa tunatumia msosi wa jioni, kila mmoja alikuwa kimya Sana tofauti na siku zote ndipo Munira akasema: baba Mbona hatuongei?

 

Baba alitabasamu na kusema: Ooh Leo Umesoma vizuri?

 

Munira: ndio Ila dada hakuja kutuchukuwa shule.

 

Mama alinitazama na kuniuliza: kwa nini Madina?

 

Nilitabasamu na kumjibu: nilikuwa nimeenda kutafuta kazi ila usijali Munira kesho ntakuja kukuchukuwa sawa!

 

Muda Huo baba alinyanyuka akidai ameshiba kisha akaelekea chumbani kwake.

 

Nilimtazama mama na kumuuliza: lipo Jambo muhimu nafichwa humu ndani.

 

Mama: sio hivo binti yangu endeleeni kula mi Nimeshiba.

 

Nikamuuliza: hata wewe umeshiba?

 

Mama: utawapeleka wadogo zako chumbani kwao.

 

Mama aliondoka na kutuacha pale, Abdallah alinitazama na kuniuliza: mama Anaumwa?

 

Nikamuuliza: kwa nini?

 

Abdallah: Jana alikuwa Analia.

 

Nilitabasamu na kusema: usijali atakuwa sawa.

 

Siku iliofuata niliamka mapema nikawaandaa wadogo zangu Ili kuwapeleka shule, tulipotoka nje nilishangaa kumuona mama akiwa amekaa pembeni huku akilia, Nilipotaka kujaribu kumuuliza alinijibu: wapeleke shule Utarudi tuongee Baadae.

 

Nilimsikiliza tukaendelea na safari Pamoja na wadogo zangu.

 

Nilipowafikisha shule wadogo zangu sikutaka kupoteza muda niliairisha safari yangu ya kwenda kuomba kazi nikarudi nyumbani ili kujuwa nikipi kinamsibu mama yangu.

 

Nilipofika nyumbani niliingia moja kwa moja chumbani kwa mama nikamkuta akiwa amelala ndipo nikamuita: mamy!

 

Mama aliamka na kuniuliza: umerudi?

 

Nilitabasamu huku nikiwa nakaa kitandani ndipo mama akaniuliza: unaona kazi utapata kweli?

 

Nikamjibu: natakiwa kujiajili mwenyewe.

 

Mama: Ni kweli! Unajua nini Madina.

 

Nikamjibu: Mmhh!

 

Mama: hapa mimi na baba yako tuna Ugomvi mkubwa ambao hata kukuelezea Nashindwa nianze wapi.

 

Nikamuuliza: anzia popote tu.

 

Mama: kuna siku baba yako aliniambia nijiandae tutoke out, Nikamuuliza vipi kuhusu Watoto Akanijibu ni out ya mke na Mume sasa tulipofika sehemu yenyewe Ilikuwa ni hotel ya kifahari toka nizaliwe sikuwahi kutembelea tulimkuta tajiri mmoja mzee kakaa, na Sisi tukaungana nae, baba yako akanitambulisha kuwa ni boss wake nilifurahi nikamsalimia kwa shobo, cha ajabu baba yako akatoka akidai anaenda kupokea simu, tukabaki wawili pale Yule boss mpumbavu akaanza kunitongoza tulipotoka pale Mimi na baba yako nikamueleza kila kitu, cha kushangaza Akaniambia nimkubali tu, Ndio maana binti yangu unaona hapa hautuelewi.

 

Niliendelea kumtazama huku nikijaribu kumfikiria baba yangu alivyo mwema kwetu hata kwa mama pia aisee Sikuamini Nikamuuliza: hivi kweli baba anaweza kufanya hivo?

 

Mama alianza kulia huku akisema: Mimi mwenyewe nashindwa kumuelewa Mume wangu amebadirika mno maana kila akirudi nyumbani ananiambia nimpe nafasi boss wake hata kuongea nae, mwanangu sina usemi tena nataka nirudi kwetu.

 

Nilishusha pumzi kwa kishindo, hasira ilinipanda nikanyanyuka na kutoka nje, nilichukuwa beskeli yangu nikaelekea kule baba anakofanyiaga kazi, nilipofika kwenye kampuni kubwa inayohusika na usafirishaji wa (abila) watu (basi zao zilikuwa zikisafirisha abilia kwenda nje ya nchi na zingine mikowani) niliiangalia kwa nje aisee mmiliki wa kampuni ile kwa haraka haraka ni vigumu kuamini kuwa angemtaka mama yangu, hasira ilinipanda nikaingia ndani, nilipofika Mazingira ya ndani yalikuwa mazuri mno tofauti na kampuni zingine.

 

Mdada mmoja alieonekana kuwa mfanyakazi ndani ya kampuni ile nilimsimamisha na kumuuliza: naweza kupata nafasi ya kuonana na boss wa hii kampuni?

 

Alinitazama kuanzia juu mpaka Chini kisha akaniuliza: unamjua boss vizuri?

 

Nilikubali kwa kutikisa kichwa ndipo Akanijibu: Mimi sio secretary wake ila huwezi kumuona kirahisi.

 

Nikamuuliza: vipi kuhusu Mussa?

 

Akanijibu: Mussa Yule enjinia?

 

Nikamjibu: Ndio baba yangu Yule.

 

Mdada Yule alinipeleka moja kwa moja mpaka baba alipokuwa anafanyia kazi na wenzie, Jasho Ilikuwa inamfumuka huku akiwa amevaa nguo chafu kutokana na kazi anayoifanya, kazi yao walikuwa wameajiliwa kwenye kampuni hio walikuwa watengeneza gari pindi zikipita panchi, baba aliponiona alitabasamu na kusema: Madina umekuja kumuona baba!

 

Nilitabasamu na kumjibu: Ndio dad.

 

Baba: nenda unisubiri nje nakuja.

 

Nilitoka pale sikutaka kwenda nje nilianza kuzunguka ndani ya kumpuni ile, wafanyakazi wa pale ambao wao Kidogo wanakazi nzuri wengi wao walikuwa matajiri mno ndipo nikaanza kujiuliza iweje baba ni mchapa kazi mzuri tena yeye ndie Anafanya kazi ngumu kuliko baadhi ya wengine pale ila maisha ya nyumbani ni ya Kawaida? sikupata majibu nikaendelea kutazama watu wanavyopita pita.

 

Nilikaa pale masaa ma 5 yakapita nikiwa bado nimemsubiri, Mpaka saa 8 muda wa kazi kuisha ndipo baba alikuja akiwa amevaa nguo nzuri Pamoja na wenzie, waliponifikia baba mmoja aliniambia: njaa itakuwa inakusumbua?

 

Nilitabasamu na kumjibu: nikimuona dad njaa inaisha.

 

Tulicheka kwa Pamoja kisha baba akanishika mkono tukawa tunatoka nje Pamoja na wafanyakazi wenzie.

 

Kabla hatujatoka nje watu walisimama huku wakimsalimia mtu flani, hata Kina baba walisimama nao pia wakamsalimia mzee flani tajiri muonekano wake Tosha ndie boss wa kampuni ile, nilimtazama anavyowachekea wafanyakazi wake ndipo akamuuliza baba yangu: Huyu ni binti yake?

 

Nikiwa namuangalia jicho mbaya nikamjibu: Ndio Kwani kuna tatizo?

 

Watu wote akiwemo baba walishtuka mno mpaka boss mwenyewe akawa anajiuliza huyu binti ni Nani? Hakutaka marefu Alitabasamu na kutoka zake nje huku walinzi wenye miili mikubwa wakiwa wamemzunguka.

 

Tulipotoka nje Niliendelea kumtazama Yule boss anavyozama ndani ya gari lake ambalo kwa haraka haraka ukiliangalia utahisi ni gari la muheshimiwa Raisi kutokana na ubora iliokuwa nayo.

 

Wale wafanyakazi wenzie na baba walituaga kila mmoja akaenda kupanda gari lake na kuondoka, aisee nilizidi kujiuliza maswali mengi Kwa nini wenzie wamiliki gari ila baba hata beskeli Hana?

 

Baba alinishika mkono na kuniuliza: una njaa twende tukale?

 

Nilitabasamu na kukubali, Jambo lile la kumjibu vibaya boss wake mbele ya watu alilipotezea kwa Muda Huo.

 

Tulipanda beskeli niliokuja nayo akanibeba kisha tukaelekea mgahawani, njiani tulikuwa na furaha sana mimi na baba yangu.

 

Baada ya muda tulifika tukaagiza chakula tukaanza kula, tukiwa tunakula baba akaniambia: haukutakiwa kufanya vile muda ule.

 

Nikamjibu: kwa nini wewe Hauongei vizuri na mama?

 

Baba: kwasababu....

 

Nikamjibu: kwasababu boss wako anamtaka mama.

 

Baba alishtuka na kuniuliza: ulijuwaje?

 

Nikamjibu: dad! mama unampa wakati mgumu Sana, kwa muonekano wa Yule boss wenu sio mstaarabu kabisa, hivi kwa nini usiache ile kazi?

 

Baba: Madina binti yangu! Ile kazi imekusomesha wewe Mpaka ukahitimu je! nikiiacha wadogo zako maisha yao ya Baadae yatakuwaje?

 

Nikamjibu: kwa nini sasa boss wako amtake mama! Dad wewe unauwezo mkubwa kazi utapata hata sehemu nyingine please achana na hio kazi familia yetu kwasasa imemiss Utani.

 

Baba alishusha kijiko Chini na kuniambia kwa sauti ya uchungu mno: Ipo sababu kubwa inanifanya Nifanye haya, ukweli nampenda Sana mke wangu ila boss alisema kama sijampatia mke wangu ata............

 

Nilibaki nikiwa nimeduwaa huku nikimtazama usoni.

 

 

Baba alimalizia akisema: ......boss alisema kama sijampatia mke wangu ataua Kati ya Abdallah na Munira.

 

Nilibaki nikiwa nimeduwaa huku nikimtazama usoni.

 

Baba alishusha kichwa Chini huku akiyafuta machozi yake ndipo Nikamuuliza: eti kasemaje baba?

 

Baba Akanijibu: sikutakiwa kukuambia haya I'm sorry.

 

Kuamini kirahisi rahisi ilikuwa ni vigumu mno ndipo Nikamuuliza: kwa nini akuambie vile?

 

Baba aliinua kichwa akanitazama na kuniambia: binti yangu! Baba yako hapa nipo Kama kichaa.

 

Nikamjibu: Aache kukutisha acha kazi Sisi tutaendelea kuishi.

 

Baba: Yule mtu huwezi kumkimbia ana pesa ndefu Sana mwanangu.

 

Nikamjibu: Kwani pesa kitu gani, usikubali, sisi tuondoke zetu twende Mombasa.

 

Baba: unajua kwa nini wenzangu wote wanamiliki gari?

 

Nikamjibu: sijui.

 

Baba: wake zao ni wake wa boss wetu.

 

Nilishangaa na kumuuliza: unasemaje?

 

Baba: hivi hivi ninavyofanyiwa mimi ndivyo wanavyofanyiwa na wenzangu ndio maana mshahara wanapewa wakutosha.

 

Nikamuuliza: kwahio hata wewe unahitaji mshahara uwe mwingi?

 

Baba: Mimi sipo huko nalilia maisha ya wanangu tu, asingenipa masharti haya ningeacha kazi.

 

Niliangua kilio kwa uchungu ndipo baba Akaniambia: usilie.

 

Nikamjibu: nalia kwasababu yako baba! Unapitia wakati mgumu Sana kwa ajili yetu.

 

Baada ya muda tulirudi nyumbani tukamkuta mama akiwa anacheza na wadogo zangu kibarazani ndipo nikawasalimia: Asalaam aleykum.

 

Munira alinijibu kwa sauti ya Juu kuliko wote: Walaykum salam.

 

Nilitabasamu na kumuuliza: Leo una hasira na Mimi Ee!

 

Munira alikunja uso na kuniuliza: kwa nini haukuja kutuchukuwa shule?

 

Nikamtania: aaahhh wewe si ni askali ndo maana unaniuliza, ngoja sasa tuone Kati ya askali na jambazi Nani mkali, Abdallah Piga kipenga mechi ianze.

 

Muda Huo baba na mama walikuwa wanatabasamu huku wakituangalia tunachokifanya ndipo Abdallah akapiga kipenga ishara tuanze.

 

Tulianza kupigana Kung Fu Mimi na Munira huku kila mmoja akicheka kwa furaha ndipo nikaigizia kama vile nimechomoa bastola mfukoni nikamshuti kwenye paji lake la uso.

 

Munira aliendelea kupambana kisha nikamuambia: nimekuua kufa sasa!

 

Munira hakutaka kushindwa akaendelea kupambana huku baba na mama vicheko vikawa vinataka kuwaua ndipo Abdallah akasema: we Munira tayari umekufa Mbona unaendelea kupambana sasa.

 

Munira akiwa yupo bize akamjibu: Nina roho Saba siwezi kufa kirahisi rahisi.

 

Mama aliongeza kicheko na kumuambia Munira huku akiwa anacheka: kwahio wameua roho moja zimebaki Sita!

 

Munira akamjibu: mimi nikambale kufa sio kirahisi.

 

Abdallah akamtania: wewe ni bata.

 

Nilimnyanyua mdogo wangu Munira baada ya kumuona amechukia kisha nikaingia nae ndani.

 

Baada ya muda tulipo maliza kula chakula cha usiku nilitengua meza na kusema: Abdallah! Munira! Nendeni kulala nakuja kuwasomea kitabu.

 

Abdallah akasema: utanisomea kitabu cha sungura na simba.

 

Munira akadakia: Mwaya cha Romeo na Juliet.

 

Mama na baba walishtuka na kuniangalia, kwa aibu nikaanza kujichekesha chekesha huku nikisema: Munira jamani! Kitabu gani hicho?

 

Munira: kile ulichonisomea siku ile.

 

Niliziba maskio yangu na kusema: sorry baba! Sorry mama.

 

Mama akasema: Munira nenda ulale sawa.

 

Munira alimkiss mama na baba kisha akaenda huku akisema: dada nakungoja.

 

Nikamjibu kwa hasira: toka!

 

Baada ya hapo tukiwa tumetulia mimi na baba Pamoja na mama nikasema: dad please usimfiche chochote mama naomba umuambie ukweli ili swala hili tulitafutie suruhu.

 

Baba na mama waliangaliana ndipo mama akamuuliza: huwezi kuongea chochote?

 

Baba aliamua kumueleza mama kila kitu bila kumficha chochote ndipo mama akasema: Nilijua tu maana Mume wangu unavyonipenda huwezi kunifanyia hivo.

 

Nikasema: idea yangu baba Acha kazi eneo lile.

 

Baba: Nikweli sijakataa Ila tatizo Yule mtu hakimbiliki.

 

Mama: nisikilize baba Madina! huo ni mkwala tu, Hawezi kufanya chochote we acha kazi.

 

Tulikubaliana hivo kila mmoja akaenda kulala, nilipofika chumbani ninakolalaga na mdogo wangu Munira nilimkuta akiwa anatafuta tafuta kitu kwenye vitabu vyangu, nikajishika kiunoni na kumuuliza: una tafuta nini?

 

Munira alishtuka na kusema: kitabu cha Romeo na Juliet.

 

Nilimfuata nikamshika maskio huku nikimuambia: unataka kufa Eee!!

 

Muda Huo Abdallah alifika na kuniambia: dada Usingizi hauji please Njoo unisomee sungura na simba.

 

Nikamjibu: wewe ndo mtoto bora twende.

 

Niliongozana nae Mpaka kwenye chumba chake, nikamlaza kisha nikaanza kumsomea, nikiwa namsomea Munira alikuja mbele ya mlango na kuniuliza kwa sauti ya Chini sana: bado tu?

 

Abdallah alifumbua macho na kusema: we Munira toka nilale zangu.

 

Nilimtazama Munira nikampidishia mdomo kisha nikaendelea kumsomea.

 

Baada ya muda Abdallah Usingizi ulimvuta nikamuacha na kuelekea chumbani kwangu, nilipofika nilimkuta Munira akiwa anasoma kile kitabu cha Romeo na Juliet, nilimtazama na kumuuliza: wewe unaweza kusoma kweli? Na kaangalie kanajifanya bize eti Kanasoma Kumbe hata A hakaelewi.

 

Munira: unanichanganya dada!

 

Nilimnyanganya kitabu na kusema: wewe bado mdogo.

 

Munira: I'm sorry nisomee.

 

Nikamjibu: Ole wako umuambie mtu yeyote.

 

Munira: sitasema.

 

Nilianza kumsomea huku tukiwa tunacheka kwa furaha.

 

siku iliofuata niliwasindikiza shule Munira na Abdallah, upande wa baba hakutaka tena kufanya kazi eneo lile alienda kuomba barua ya Kuacha kazi, akapewa.

 

Nikiwa nipo nje ya shule ya wadogo zangu Munira alitoka na kunifuata aliponifikia akaniambia: mama alisema usiende sehemu yoyote ubaki hapa.

 

Nikamuambia: toka mbele yangu we mtoto ni wa familia ipi Mbona Huna adabu?

 

Mdada ambae alikuwa amekaa karibu yangu alicheka na kusema: Munira hapendi kusoma nenda ukae karibu na darasa lao muda mwingi anakuwa yupo nje.

 

Nilimshika mkono Munira nikampeleka darasani, nikiwa nipo nje karibu na dirisha lao Munira akiwa yupo darasani alitabasamu na kuniambia: ubaki hapo.

 

Nilimkunjia ngumi kwa hasira ndipo akanionesha kitu mbele, nilichungulia nikamuona mwalimu wao kijana handsome wa maana akiwa anawafundisha ndipo Nikamuuliza: kwahio?

 

Munira: yeye ni Romeo.

 

Nilipindisha mdomo na kushuka Chini, Munira akiwa yupo darasani Alimuita mwalimu wao akaja na kumuuliza: una Matatizo gani?

 

Munira akamuambia: angalia huku Chini.

 

Mwalimu alisogea karibu na dirisha akaangalia Chini, na Mimi kwa Muda Huo niligeuka kumtazama tukagonganisha macho, kwa aibu akamuangalia Munira na kumuuliza: kuna nini?

 

Munira: ni dada yangu Huyo.

 

Mwalimu: aah mmefanana sana.

 

Upande wangu simu iliita nikapokea na kusema: Ndio mamy!

 

Mama: Watoto wapo Salama?

 

Nikamjibu: Eee bado nimewawekea ulinzi.

 

Mama: sawa.

 

Nikamuambia: nakupenda maa!

 

Mama: hata mimi pia mwanangu.

 

Baada ya muda ulikuwa ni muda wa mapumziko wanafunzi wote wakatoka nje, nikiwa namuangaza angaza Abdallah nilishangaa kumuona Munira akiwa amemshika mkono mwalimu wao huku akiwa anamleta nilipo, presha ilinipanda nikanyanyuka na kusema: Ndo mmetoka?

 

Waliponifikia Munira akaniambia: dada! Huyu Ndo Yule niliekuambiaga.

 

Macho yalinitoka maana toka tuanze kuongea na Munira hatukuwahi kuzungumzia kuhusu mwalimu wao, ila nikapotezea na kusema: Oohh habari.

 

Nilimpa mkono mwalimu wa Munira tukasalimiana kisha akaniambia: naitwa Jack.

 

Nikamjibu: Mimi ni Madina.

 

Jack: nimefurahi kukujuwa.

 

Muda Huo mwalimu wa Abdallah alifika na kuniuliza: Abdallah Mbona Leo hajaonekana darasani kabisa?

 

Nilishtuka na kumuuliza: hajaonekana?

 

Mwalimu: Ndio sasa sijui atakuwa na tatizo gani nyumbani au Anaumwa?

 

Simu nilidondosha Chini bila kujielewa nikamuambia: mdogo wangu Nimekuja nae Mbona!

 

Mwalimu: Mmhh!

 

Sikutaka kupoteza muda nilielekea anakosomea nilipowafikia marafiki zake nikawauliza ndipo mtoto mmoja Akanijibu: kuna mtu ali..........

 

Jicho lilinichomoka huku nikiwa najiuliza ntafanya nini kwa muda ule.

 

 

TULIPOISHIA: Sikutaka kupoteza muda nilielekea anakosomea nilipowafikia marafiki zake nikawauliza ndipo mtoto mmoja Akanijibu: kuna mtu ali..........

 

Jicho lilinichomoka huku nikiwa najiuliza ntafanya nini kwa muda ule.

 

SONGA NAYO!

 

Mtoto mmoja Rafiki yake na mdogo wangu Abdallah Akanijibu baada ya kumuuliza Abdallah yupo wapi: kuna mtu alikuja akamchukuwa akasema eti baba yako anamuita.

 

Jicho lilinichomoka huku nikiwa najiuliza ntafanya nini kwa muda ule ndipo Nikamuuliza: huyo mtu alipokuja mwalimu Nani alikuwa anafundisha?

 

Akanijibu: Hakuna.

 

Nikamuuliza: mwalimu alikuwa bado hajafika?

 

Akanijibu: ndio.

 

Nikamuuliza: Yeye Abdallah hakukuambia wapi anaenda?

 

Mtoto yule aliendelea kunitazama bila kunijibu chochote ndipo nikasema: nimegeuka kichaa! Maswali gani namuuliza mtoto mdogo Kama huyu.

 

Nilitoka hapo mbio nilipowafikia kina Jack walipokuwa wamesimama na Munira Nilimchukuwa Munira nikamuweka mgongoni safari ikaanza ya kuelekea nyumbani, nilipofika nyumbani niliwakuta wazazi wangu wote wawili wakiwa wanaangalia movie kwa furaha kisha nikawaeleza kuhusu kile kimetokea, mama kwa presha alinyanyuka na kuniuliza: wewe muda wote ulikuwa wapi?

 

Nikamjibu: I'm sorry maa!

 

Mama alianza kulia huku akisema: ntamtafuta mwanangu.

 

Mama alitoka nje tukabaki na baba ndipo baba akasema: ngoja niende kumtafuta.

 

Nilikubali akatoka nje, nilipoona Abdallah ni kama alipotea kwa uzembe wangu nilimuambia Munira anisubiri ndani asitoke naenda kumtafuta pacha wake.

 

Baada ya muda nilikuwa Nipo njiani huku nikiwa namtafuta.

 

Upande wa baba moja kwa moja alielekea kule kazini kwake akaomba kukutana na boss wake Ila hakuweza kupewa nafasi, moyo wake ulimsukuma akihisi Labda boss wake ndie kafanya yote alichoamua kufanya alitulia nje akiwa amemsubiri.

 

Upande wangu nikiwa nipo njiani nilikumbana na teacher Jack akiwa anatembea zake, aliponiona alinisimamisha na kuniambia: sorry muda ule simu uliiacha.

 

Alinipa simu kisha nikamjibu: Nashukuru.

 

Jack: vipi bado tu hamjampata?

 

Nikamjibu: bado kabisa.

 

Nilimuacha pale bila kumuaga nikaanza kumpigia simu baba.

 

Baba alipopokea Nikamuuliza: umempata?

 

Baba kwa sauti ya Chini Akanijibu: bado subiri Kidogo tutampata.

 

Baba alikata simu nikabaki nimesimama huku nikiwa najiuliza kiaje mtu huyo akaja akamchukuwa mtoto na Mimi hali ya kuwa nilikuwa pale.

 

Nilimpigia baba kwa Mara nyingine, akapokea na kuniuliza: kuna tatizo lingine limejitokeza?

 

Nikamjibu: Hapana nataka kujua tunafanyaje?


INAENDELEA

 

No comments

Powered by Blogger.