Header Ads

Header ADS

Simulizi: Tabasamu langu sehemu ya pili (02)



Upande wa baba, boss wa kampuni alitoka nje kama Kawaida yake kuwa na walinzi wakumlinda, baba alipomuona aliomba kuonana nae na Mimi muda Huo nilikuwa nasikia kila kitu kinachoendelea maana hakukata simu, ila ajabu boss Yule kwa jauli akamjibu: kwa sasa Sina muda Labda uje mwaka kesho.

 

Baba hasira ilimpanda akamuambia kwa sauti ya Juu sana: niambie mwanangu umempeleka wapi?

 

Upande wangu presha ilinipanda nikatamani kupaa ili nitue eneo lile.

 

Boss Yule akamuuliza huku akijifanya kushangaa shangaa: mwanao yupi? Kwani hayupo nyumbani?

 

Baba alirusha simu pembeni ili kumrukia ikiwezekana ampige hata kibao kimoja, Ila walinzi wa boss Yule walimshika na kumtuliza kisha boss akaingia ndani ya gari huku akicheka kicheko cha kiunafiki.

 

Simu Ikiwa Ipo Chini Mlinzi mmoja aliikandamizia Chini baada ya kunisikia nikisema: Hallo! Hallo! Halloooo!

 

Baada ya simu ya baba kupasuliwa simu ilikata nikapatwa na wasi wasi mwingi, bila kupoteza muda nikaelekea kule kwenye ile kampuni, nilipofika sikukuta mtu maana muda wa kazi ulikuwa umeisha.

 

Siku mbili zilipita tukiwa tunaendelea kumfuta mtoto ila hatukuweza kumuona, baba kwa Mara nyingine alirudi kule kwenye ile kampuni alipokuwa akifanyia kazi siku zilizopita, alipofika aliomba kuonana na boss akaruhusiwa, alipofika ofisini kwa boss wake wa awali alisimama na kumuuliza: hivi wewe Robert unataka nini kwangu?

 

Robert: Alaa! Leo umepata wapi ubavu wa kuniita kwa Jina langu?

 

Baba akiwa amekunja uso akasema: kwasababu wewe ni nusu shetani.

 

Robert: anha! Umekuja kunitisha si eti?

 

Baba kwa hasira alimfuata akamkwida shingoni na kumuuliza: mwanangu yuko wapi?

 

Robert: tsa tsa tsa! Nasikitika mwanao hayupo tena duniani.

 

Robert Baada ya kuongea maneno Yale aliachia kicheko cha kiunafiki bila kujali ni maumivu ya kiasi gani mwenzie anayapata.

 

Baba uvumilivu ulimshinda akampiga ngumi ya shavuni huku machozi yakiwa yameanza kumlenga lenga machoni.

 

Robert aliinua kichwa na kumuuliza: hasira zako zimekutoka sasa eee?

 

Baba akaendelea kumuangalia kwa hasira ndipo Robert akanyanyuka na kusema: mwenyewe Ndo umeyataka haya, nilikuambia toka mwanzo namuhitaji mkeo ukagoma ona sasa wenzio wanavyoneemeka.

 

Baba: kwa nini unafanya yote haya?

 

Robert: kwasababu Haiwezekani kampuni niliitafuta kwa Jasho yangu watu wengine waje wawe wanapata mshahara bila kujuwa wapi ilianzia.

 

Baba: ili uwalipe si kwasababu wanafanya kazi?

 

Robert: kwangu hayo siyahesabu! Kwasababu masikini yeyote namchukulia kama mtumwa, hii nchi inabahati Sana ningekuwa Raisi mimi, Yatima, wajane, walemavu wote ningeua, watu masikini nao ningewageuza kuwa watumwa wangu na wake zao ningewachukuwa mimi.

 

Baba hakuweza kuvumilia akampiga ngumi tena ya shavuni, ndipo Robert akasema: wewe Fanya yote unayojisikia ila muda mwingine utayajutia haya.

 

Muda mdogo walikuja walinzi wake wakamshika baba na kumzimisha hapo hapo.

 

Baada ya masaa kadhaa kupita Upande wetu nyumbani, Munira alikuwa ni wa kulia tu akimhitaji pacha wake, nilimfuata alipokuwa amekaa sebuleni nikamuambia: baba ameenda kumleta Abdallah muda si mrefu wanakuja nae.

 

Munira akiwa Analia akaniambia: namtaka kaka.

 

Nikamjibu: subiri Kidogo anakuja.

 

Nilimshika kichwani Munira nikamlaza kwenye mapaja yangu huku nikiwa namgusa gusa kwenye Nywele, mawazo kichwani mwangu Zidi ya mdogo wangu wakiume yalikuwa makali mno nikajikuta machozi yananitiririka mashavuni, nilitabasamu na kujisemea moyoni: natokwa na machozi bila kujielewa aisee it's too much?

 

Ghafla taarifa ya habari ilianza kutoa taarifa kuhusu mtoto aliepoteza maisha muda uliopita, moyo ulishtuka nikaangalia TV huku nikiwa namsikiliza kwa umakini mdada mtangazi aliekuwa anatoa taarifa ile.

 

Mtangazaji: mtoto mwenye umri wa miaka 6 ambae Jina lake bado halijaweza kufahamika vizuri ameweza kuuwawa kwa kuchomwa kisu na mtu anaesadikika kuwa............ Bado tunafanya upelelezi.

 

Presha ilinipanda baada ya kuona picha ya mdogo wangu Abdallah akiwa ametapakaa damu mwili mzima, uzalendo ulinishinda nikapaza sauti nikimuita mama: mamyyyyyyyy!!!!

 

 

 

Mtangazaji: mtoto mwenye umri wa miaka 6 ambae Jina lake bado halijaweza kufahamika vizuri ameweza kuuwawa kwa kuchomwa kisu na mtu anaesadikika kuwa ni baba yake mzazi, chanzo bado hakijafahamika na mshtumiwa kwasasa yupo kwenye mikono ya police na Bado tunafanya upelelezi.

 

Presha ilinipanda nikapaza sauti nikimuita mama: mamyyyyyyyy!!!!

 

Munira aliamka huku akinishangaa, mama haraka akawa amefika sebuleni na kuniuliza: kuna nini?

 

Machozi yangu yalivyokuwa yanatiririka Ilikuwa ni ishara Tosha kuwa kuna Jambo baya limejitokeza, mama alipogeuka kuangalia TV alishtuka mno Baada ya kuona picha ya mwanae kipenzi wa kiume akiwa amefariki kwa kuchomwa kisu tumboni, kuamini Ilikuwa ngumu Sana maana maelezo alikuwa hajayasikia, taratibu akageuka kunitazama na kuniuliza: eti ni kweli?

 

Niliendelea kuduwaa huku nikiwa kama vile sio Mimi, muda Huo taarifa ile ikarudiliwa tena, mama maelezo Yale akayasikia vizuri kuwa ni Mume wake ndie kamuua mwanae kwa mikono yake, hakuchukuwa Muda alidondoka Chini na kupoteza fahamu hapo hapo.

 

Nilimpeleka mama moja kwa moja hospito.

 

Baada ya muda nilipotoka nje ya hospital ili kuelekea kituoni ikiwezekana nionane na baba yangu, waandishi Wa habari walikuwa wapo nje wamenisubiri, bila kupoteza muda wakanifuata huku kila mmoja akiwa anauliza yake: * eti ni kweli baba yako ndie kamuua mdogo wako wakiume* *ni nini kilipelekea akafanya yote Yale? Au alikuwa hampendi mwanae maana yule marehemu bado alikuwa mdogo sizani kama kuna kosa atakuwa alimkosea baba yako Mpaka akafikia hatua ya kumuua kupitia kisu? embu tuweke sawa kwa hilo*

 

Niliposikia mdogo wangu Anaitwa Jina la marehemu niliangua kilio na kuwauliza: ni kweli Abdallah wetu amefariki?

 

Watangazaji na waandishi wa habari walinishangaa wakaendelea kunitazama kwa unyonge, ndipo nikawaambia huku nikiwa nalia: tafadhali nahitaji kuonana na baba yangu najua yeye ni innocent.

 

Maswali yalizidi Ila nikapata penyo nikaondoka zangu, nikiwa nipo njiani simu yangu iliita nikapokea na kusema: Hallo!

 

Akanijibu: Mimi Jack! Pole kwa Yale yaliotokea kwenye familia yenu.

 

Nikamjibu: Nimeshapoa, tafadhali Naomba umuwekee ulinzi mdogo wangu Munira maana Sina mtu mwingine ambae anaweza kumuangalia kwa sasa.

 

Jack: ondoa Shaka kuhusu hilo, vipi mama hali yake?

 

Nikamjibu: yupo hospital Naomba tuongee Baadae maana naelekea kituoni.

 

Nilikata simu kisha nikazidi kusonga mbele.

 

Baada ya muda nilifika police station Nikaomba kuonana na baba ila sikuruhusiwa niliambiwa nirudi ntaonana nae ma saa 48 yakiisha, nilikaa nje ya kituo kile huku nikiwa naendelea kulia maana nilijuwa baba yangu Hana hatia.

 

Baada ya ma saa ma 8 kuisha huku kila police akiwa ananishangaa kwa nini sirudi nyumbani, mvua ilianza kunyesha ila sikuweza kujali nanyeshewa au laa.

 

Mvua yote iliniishia hapo kila mtu Aliekuwa anakuja hapo kituoni alikuwa ananibembeleza niangalie sehemu ya kujikinga Mvua ila hakuna nilieweza kumsikia maana hakili nikama zilikuwa zimeruka.

 

Baada ya ma saa ma 4 kupita ilikuwa tayari ni usiku saa 2 sikuweza kutoka eneo lile Niliendelea kukaa huku nikiwa nimejikunja kama mtoto Yatima.

 

Muda Huo askali polisi mkuu wa kituo hicho alifika aliponiona alipewa taarifa kuhusu Mimi baada ya kunionea huruma aliruhusu nionane na baba.

 

Nilipewa nafasi ya kuonana na baba yangu, alikuwa amefungwa pingu kwenye mikono, muonekano wake alikuwa mwenye majonzi makali ndani na nje, sura ya baba yangu kwa wakati ule sikuweza kuichoka Niliendelea kumtazama bila kuongea chochote, ndipo baba kwa Mara ya kwanza kulia mbele yangu aliangua kilio kikali ikanipelekea na Mimi pia kulia.

 

Baba alijikaza na kuniambia: sijafanya chochote my daughter.

 

Nikamjibu: najua sana, Ila nataka kujuwa je ni kweli Abdallah wetu hatupo nae tena au Yale niliokuwa naona ni maneno ya watu tu?

 

Baba: Nikweli hatupo nae tena.

 

Niliendelea kulia kisha nikamuuliza: Ila sio wewe uliemuua?

 

Baba: I'm innocent my daughter ( mimi Sina hatia binti yangu)

 

Nikasema: watu wote mtaani wanaamini umemuua mwanao kwa mikono yako, mama alipopata taarifa alizimia sasa hivi yupo hospital.

 

Baba: vipi kuhusu Munira?

 

Nikamjibu: yupo mikononi mwa Jack.

 

Baba: nakujuwa vizuri binti yangu wewe hupendi kufedheheshwa Ila tafadhali Jambo hili liache lipite taratibu usitake kuliingilia Kati maana na wewe unaweza kujumlishwa ndani.

 

Nikamuuliza: Robert ndie kafanya haya?

 

Baba: ndio Ila please msikilize baba yako kwa umakini usifanye chochote.

 

Nikamjibu: lazma nikutoe eneo hili.

 

Baada ya siku kadhaa mama alipona, mwili wa marehemu mdogo wangu ukazikwa na kesi ya baba ilikuwa bado haijapelekwa mahakamani.

 

Siku moja mama alimfuata baba kituoni akaomba kuonana nae, akaruhusiwa, wakiwa wamekaa baba alisema: Nisamee mke wangu.

 

Mama alianza kulia huku akisema: najua sio wewe.

 

Baba: mwanangu amezikwa Salama?

 

Mama: ndio, vipi kuhusu wewe?

 

Baba: sio mbaya Sana but I'm sorry.

 

Mama: ni sawa tu! Ila nahitaji kujuwa ilikuwaje haya yote yakatokea? Na Kwa nini wakatae usiwe na wakili?

 

Baba alimuadithia ilivyokuwa siku ile anaenda kwenye Ofisi ya Robert ndipo mama akamuuliza: kwahio ulivyozimishwa haukuelewa nini kiliendelea tena?

 

Baba: Nikweli mke wangu Nilikuja kuzinduka Najikuta kwenye nyumba flani ghafla nikamuona Abdallah Halafu unajua kauli ya mwisho ya mwanao alioisema?

 

Mama alimtazama kwa umakini akitaka kujuwa nikipi Abdallah alichokisema kabla hajafa.

 

Baba: alisema *dad nimemmiss mamy* hio ndio Ilikuwa kauli ya mwisho kuisikia kwa mwanangu maana nilipita nazimishwa tena.

 

Mama alilia mno huku akisema: I'm sorry mwanangu Na Mimi pia nimekumiss please Njoo nimechoka kukutana na wewe ndotoni.

 

Baba akamuambia: baada ya kuzimishwa nilikurupuka nashangaa nikiwa nimeshika kisu kilichotapakaa damu huku mkono wangu nao pia ukiwa umejaa damu, kuangalia pembeni nikamuona mwanangu akiwa yupo pembeni, Kibaya zaidi uso wake ulionesha aliumia sana akiwa anakata roho, I'm sorry kukuambia haya.

 

Mama akamjibu: ni sawa tu kuniambia, mtoto wangu alikuwa mpole ntammiss sana.

 

Baba: Robert sio mtu mzuri tofadhali kaa mbali nae.

 

Mama: nakupenda sana Mume wangu.

 

Baba: hata mimi pia, mleteni Munira nimuone.

 

Mama: anatusumbua sana nyumbani anamtaka kaka yake na baba yake.

 

Baba: muambieni ukweli.

 

Mama: haamini, Madina ndo anamdanganyaga kuwa Mpo safarini.

 

Baba: ni kweli.

 

Baada ya siku kadhaa kesi ya baba iliweza kuwa kubwa Mara dufu tofauti na tulivyokuwa tunatarajia mwanzo, wale wafanyakazi wenzie ambao alikuwa akifanya nao kazi ya uenjinia huwezi kuamini walitoa mashtaka kuwa baba Muda mwingi alikuwa akitumia madawa ya kulevya na alisema ataua mtoto mmoja baada ya mwingine.

 

Tulifuatilia kadri ya uwezi wetu Ila unaambiwa siku zote mwenye pesa ndie mwenye neno, kumbe siku ile baba alipokuwa yupo ndani ya Ofisi ya Robert akampiga ngumi tukio lile lilirekodiwa Ila sauti haikusikika, hata siku ile anataka kumpiga nje walinzi wakamzuia ilichukuliwa ikawa kama ushahidi, Robert kwa kinywa chake alisema mbele ya mapolisi kituoni: Huyu kijana alikuwa ni kama kijana wangu, nilikuwa Nikimpa mshahara wakutosha Ila siwezi kukuambia wapi alikuwa akizipeleka maana familia yake ni ya njaa siku zote, nilipokuwa nikijaribu kumshauli madhara yake alikuwa akihitaji kuniua na Mimi Mpaka nikaamua kumfukuza kazi na ushahidi huu hapa.

 

Alitoa documents wakaangalia mkataba waliokubaliana na pesa aliokuwa akipewa mwisho wa mwezi na karatasi ya kumfukuza kazini, ila yote Yale yalikuwa ni ya kufoji tu, ila askali wale waliamini.

 

Tulipambana kadri ya uwezo wetu Ila huwezi kuamini ................., tulipata wakati mgumu Sana ukija kuangalia haijapita hata mwezi tumempoteza mdogo wangu wa kiume na Matatizo mengine yakajirudia.

 

 

 

 

TULIPOISHIA: Alitoa documents wakaangalia mkataba waliokubaliana na pesa aliokuwa akipewa mwisho wa mwezi na karatasi ya kumfukuza kazini, ila yote Yale yalikuwa ni ya kufoji tu, ila askali wale waliamini.

 

Tulipambana kadri ya uwezo wetu Ila huwezi kuamini ................., tulipata wakati mgumu Sana ukija kuangalia haijapita hata mwezi tumempoteza mdogo wangu wa kiume na Matatizo mengine yakajirudia.

 

SONGA NAYO!

 

Tulipambana kadri ya uwezo wetu Ila huwezi kuamini baba alikatiwa kifungo cha maisha bila hata kesi yake kupelekwa mahakamani, tulipata wakati mgumu Sana ukija kuangalia haijapita hata mwezi tumempoteza mdogo wangu wa kiume na Matatizo mengine yakajirudia.

 

Mama Mara nyingi alikuwa ni wa kunifariji sana, siku moja nilikuwa nimeenda Kuhangaika ili kuweza kupata cha kutumia usiku, niliporudi nyumbani Majira ya saa moja usiku nilimkuta mama akiwa Analia mno mpaka mwenyewe nikashindwa kuelewa, bila kupoteza muda Nilimuwahi na kumuuliza: eti mama kuna nini?

 

Mama akamuambia Munira akalale kwanza, nilipoona Munira nae hayupo sawa nilimshika mkono na kumuambia: nenda ukalale nakuja kukusomea Romeo and Juliet.

 

Munira alitabasamu kwa furaha kisha akatangulia chumbani, nilikaa kwenye kochi na kumuuliza mama: kuna nini kimetokea mbona upo kwenye hali hio?

 

Mama akiwa Analia akaniambia: naona ntamfuata mwanangu mapema.

 

Nikamjibu: usiseme hivo mama Nipo hapa Pamoja na Munira, na kuhusu baba bado nafuatilia lazma akate rufa.

 

Mama: sio hilo tatizo ni huyu shetani anaejiita Robert.

 

Nilishtuka na kumuuliza: Kafanyaje?

 

Mama: ametoka hapa sasa hivi.

 

Moyo ulilaruka kwa Mara nyingine Nikamuuliza: kufanya nini?

 

Mama: amekuja eti kunipa pole, alivyompumbavu Akaniambia nijiandalie ndoa yangu na Yeye siku za usoni, I'm sorry sikutakiwa kukuambia haya ila Najikuta tu Sina wa kumuambia.

 

Nilimsogelea mama nikamkumbatia huku nikiwa nambembeleza asijali, mama akiwa yupo kifuani kwangu alitabasamu na kuniambia: nakukumbuka ulipokuwa bado mdogo nilikuwa nikikubembeleze kama hivi.

 

Nikamjibu huku machozi yakiwa yananibubujika: kweli eeee!

 

Baada ya siku nilifunga safari ili kuelekea ofisini kwa Robert ikiwezekana nimchafulie Jina kwenye vyombo vya habari, nikiwa nipo njiani Jack alikuja na kusimama mbele yangu, ndipo Nikamuuliza: unafanya nini?

 

Jack: hautakiwi kufanya hivo.

 

Nikamuuliza: hivi unajua Huyu mtu ni mbaya wa familia yangu kiasi gani?

 

Jack: Naelewa ila please don't be like that.

 

Nikamjibu: lazma.

 

Jack: basi Nipe muda tuongee.

 

Tulitoka Kidogo tukakaa sehemu huku tukiongea.

 

Jack: mama yako ndie kaniambia kuwa wewe unaenda kwa Robert nije kukuzuwia.

 

Nikasema: aaahhh nimuoga sana.

 

Jack: Madina! Please acha yapite kama nilivyokuahidi mwanzo lazma nishilikiane na wewe baba yako akate rufa.

 

Nikamjibu: nashukuru kwa kujitolea kiasi hiko ila Natamani kufanya kitu kwa Huyu mshenzi.

 

Jack: please stop!

 

Jack aliniomba tuzunguke zunguke mtaani ili kuniondoa mawazo.

 

Tukiwa tupo mtaani niliona picha ya marehemu mdogo wangu Abdallah Ikiwa Ipo kwenye TV ya barabarani, ikanipelekea kusimama huku nikiwa naangalia, Kumbe ni taarifa mpya Ilikuwa inapeperushwa, mkaka flani Mtangazaji akaanza kusema: mshtumiwa namba 182 ameweza kujinyonga usiku wa kuamkia Leo baada ya kujionea aibu kumuua mwanae wa kiume mwenye umri mdogo Sana miaka 6 ambae Hana hatia na kumuacha mkewe mwenye mtoto mkubwa mwenye umri wa miaka 24 na mwingine Wakike mdogo kabisa ambae ni pacha wake marehemu, hayo Ndio maneno alioacha ameandika kwenye karatasi...........

 

Sikuweza kumsikiliza tena Nilishuka Chini katikati ya barabara nikakaa huku nikiwa najiuliza Inawezekana vipi.

 

Kila mtu alikuwa ananishangaa, baadhi wanaonifahamu wakawa wananinyooshea vidole, uzalendo ulinishinda nikanyanyuka na kupiga kelele huku nikisema: Hapana dad!

 

Jack aliwahi kunishika, nikawa najaribu kujitoa kwake ili niweze kwenda huko kituoni.

 

Baada ya mama kupewa taarifa zile alijikatia tamaa kabisa.

 

Nilichokifanya nilimuomba Jack anisaidie twende hospital kwanza basi ikiwezekana nikauone mwili wa marehemu baba yangu.

 

Baada ya muda tulifika, bila kinyongo wakaturuhusu kuuona mwili wa mzee.

 

Tukiwa tupo ndani ya chumba maalumu wanapohifadhigi maiti, mkono wangu niliupeleka karibu na kichwa cha marehemu baba yangu huku nikiwa natetemeka kwa uchungu ili kufunua shuka waliokuwa wamemfunika mwili mzima, Jack alipoona natetemeka aliushika mkono wangu na kuniuliza: utaweza?

 

Nilimtazama nikakubali kwa kutikisa kichwa, taratibu nilimfunua, ukweli mzee wangu alikuwa hayupo tena duniani, uchungu ulinizidi Ila nikajikaza kisabuni ndipo doctor Aliekuwa yupo pembeni yetu Akaniambia: pole Sana.

 

Nikamuuliza: naweza kupata barua alioiacha?

 

Doctor: Ipo mikononi mwa police.

 

Nikamuuliza: naweza kuukagua mwili wa baba?

 

Doctor: una ruhusiwa.

 

Nilimtazama shingoni vizuri baba inakosadikika kuwa amejinyoka Nikaona mstari mwekundu shingongo ishara alitumia kamba kwa kujinyoja, nilimfunua kwenye mkono wake nikashangaa kukuta mkono wake kama vile umechanwa na kitu chenye ncha Kali, bila kupoteza muda nikamuomba doctor aje kuona, doctor alipoangalia alinishika begani na kuniinua taratibu, ndipo Nikamuuliza: umeona?

 

Doctor: mwili wa baba yako nimeufanyia uchunguzi una majeraha mengi mno, mgongoni alipigwa Fimbo nyingi kabla ya Kifo chake, baba yako hakujinyonga, ameuwawa, nahisi kuna mparangano mkubwa ulitokea walipotaka kumuua, embu angalia hapa.

 

Tulipoangalia kwenye bega lake la kushoto tuliona alama za kucha Kama vile kuna mtu kamkwaruza, ndipo doctor akasema: hii mikwaruzo nahisi mtu huyo alikuwa anajaribu Kutaka kumzimisha ila Wakaanza kuparangana, sio hilo tu Upo ushahidi mkubwa mwingine tofauti na huo.

 

Mimi na Jack tulitamani kujuwa zaidi, ndipo akasema: muda ule wanaparangana na mtu asiefahamika inaonekana alizidiwa akafunikwa na kitambaa Chenye madawa ya kulevya kwenye mdomo, na nimepima nimegundua alikuwa sio mtumiaji wa madawa ya kulevya kabla na alikuwa hajawahi hio Ilikuwa ni Mara yake ya kwanza, na madawa hayo yamemletea madhara kwenye mapafu, mirija ya kusafirisha damu kupeleka kwenye mafafa iliziba baada ya kupokea madawa Yale, na akapoteza maisha, hapo sasa inaonekana Baada ya kufariki walimfunga kamba wakamning'iniza akaonekana kama amejinyona.

 

Nilikuwa namsikiliza kwa huzuni bila kujuwa Baada ya pale ntafanya nini, ndipo doctor akaniuliza: unanikumbuka?

 

Nikamjibu kwa uchungu mkali huku nikilia mno: Hapana! Kwani we Nani?

 

Doctor yule ajabu aliangua kicheko cha kiunafiki mpaka Sisi wenyewe tukashindwa kumuelewa, ndipo Jack akamuuliza: una maana gani kufanya hivo?

 

Doctor alivua mawani yake kisha akajigusa kwenye mifuko iliopo kwenye suruwali aliokuwa amevaa na kusema: Mimi ni mdogo wake Robert naitwa Jacob vipi hapo!

 

Nilishtuka mno na kumuuliza: unasemaje?

 

Jacob Akanijibu huku akiwa amejiamini mno: yes! Mimi sio doctor na kwa taarifa yako hayo maelezo niliokuambia yote ni ukweli hivyo ndivyo baba yako alivyouwawa, umefurahi Eee au Inauma! Maskini pole.

 

 

Jack kwa hasira Alimuwahi na kumpiga ngumi ya shavuni, muda wote nilikuwa nashangaa shangaa tu.


BONYEZA HAPA KUSOMA MAKALA ZA MAFANIKIO


ITAENDELEA

 

No comments

Powered by Blogger.