Simulizi: Tabasamu langu sehemu ya kumi (MWISHOO)
"Jamani we kaka usinifanyie Hivi"
Haraka nilipanda pikipiki bila kuambiwa kisha nikamkumbatia na kulala mgongoni kwake Jambo ambalo lilimuacha mdomo wazi.
Alinipeleka moja kwa moja kwenye lile gorofa, tulipofika kunako chumba chetu alishangaa kuona sijali.
"Hapa ndo chumbani kwako?" Nilimhoji baada ya kufika chumbani kwake.
"Yeah"
"Unaishi na nani?"
"Pekeeyangu"
"Maskini na wewe ni mpweke kama mimi, yule mpuuzi amenichania nguo yangu"
Nilimuonyesha akabaki kunitazama usoni kama nadanganya au laa.
"Aliivuta kwa roho mbaya. Kwanini sasa weusi wenzangu wananiandama Hivi?"
"Pole"
Baada ya muda Hyun Joong alikuwa jikoni akipika, Ndipo nilimfuata nikiwa na kioo.
"Ona ulivyoniharibu sura"
"Pole"
"We kaka... Eti we kaka, oppah...."
Hyun Joong aligeuka kunitazama baada ya kukumbuka kuna siku niliwahi kumuita oppah wakati nimelazimishwa kuwatibu majeruhi.
"Yeah"
"Angalia uso wangu ulivyo"
"Pole"
Nilimuwahi na kumshika mkono.
"Utanitibu?"
"Ndiyo"
"Yeeeee" nilitoka hapo nikikimbia kwa furaha.
Baada ya muda nilioga nikavaa shati yake nyingine kisha tukakaa ili kula.
"Oppah, mi sielewi familia yangu iko wapi na sijui inawaza nini juu yangu... mbona wewe hauli?" Nilimhoji.
"Nimekuandalia wewe"
"Wow wewe uko tofauti na yule mjinga, niliona kinaingia na bangi mkononi iiiiii niliogopa Sana" nilijifanya kulia huku chakula kikiwa mdomoni, Hyun Joong kwa mara ya kwanza alitabasamu kwa ajili yangu.
"Kweli nakwambia, kilianza kupiga ngumi ukutani kikaanza kuniambia eti nilimuua kaka yake. Jamani wapi na wapi mimi kuua mtu, alipoongea hivyo ndo nikaamini watu weusi hatupendani"
Baada ya muda nilimaliza nikaanza kushona tisheti, ghafla sindano ilinichoma.
"Uwiii mama...."
Hyun Joong aliniwahi na kuniangalia mkono.
"Puliza naumia"
Alianza kupuliza mwisho akaanza kuishona.
"Oppah we ni mtu mzuri sana, unaroho nzuri halafu wewe ni bonge la handsome"
Baada ya kumuambia alinitazama kwa muda, kumbukumbu ikamrudisha mbali enzi za utotoni mama yake alipenda kumsifia kuwa yeye ni handsome na ni mwema kwa watoto wenzie. Ndipo alinyanyuka na kuondoka.
Majira ya usiku alinipeleka kwenye chumba chetu cha zamani ili nikalale lakini miligoma.
"Kama umenichoka si unasema tu, kuliko kunitelekeza namna hii"
Nilirudi chumbani kwake bila kujali.
Majira ya usiku tulilala, yeye kitandani mimi chini.
"Oppah, oppah" nilimtikisa akaamka.
"Eti mwanamke akiwa na kovu usoni ni vibaya?"
"Ndiyo"
"Anakosa mume"
"Ona uso wangu jamani, ntakosa mwanaume wa kunioa eti"
Hyun Joong aliamka na kuchukua jukumu la kunipaka dawa.
"Ooohh eti rudisha kumbukumbu zako, Hivi kale kabinti kafupi kanahakili kweli? Sikapendi kabisa"
Alimaliza tukalala, wakati nimelala nilianza kuhangaika huku nikiita majina ya ndugu zangu.
"Mama, mama, Munira wetu...."
Hyun Joong aliamka na kusogea nilipo, alivuta shuka yake kisha akanifunika taratibu. Alimaliza na kutaka kutoa mkono, kabla hajautoa nilimshika kwanguvu nikisema.
"Usiondoke, naoga, usiniue"
Nilimshika kwa nguvu Ndipo alisogeza mkono wa kushoto karibu ya uso wangu akanishika kwenye komwe. Alinituliza baadaye nikatulia.
Asubuhi na mapema nilikuwa wa kwanza kuamka ila ajabu Hyun Joong alikuwa hayupo kitandani, nilianza kumtafuta kona zote Ndipo nilimuona akifanya mazoezi, ndani ya chumba hicho kilikuwa na picha nyingi mno hivyo nilianza kushangaa shangaa, Hyun Joong aliponiona alinifuata na kunitoa nje.
"Oppah..."
"Mtu yeyote akija hapa jifiche" aliniachia agizo hilo na kuondoka.
Majira ya mchana nilikuwa nje huku nikifanya usafi, ghafla nilimuona Hyun Joong na marafiki zake wakija. Haraka nilirudi ndani nikajifungia kwenye kabati, waliingia na kutoa risasi kisha wakaanza kuzipanga vizuri. Hakika Niliogopa Sana.
Baada ya muda waliondoka Hyun Joong akabaki.
"Oppah mbona wanatisha Sana" nilimhoji baada ya kutoka Ndipo alinikata kijicho.
"Inabidi nikurudishe kwenu"
Haraka nilimsogelea na kumkumbatia.
"Nataka kubaki na wewe"
"Nihatari Sana wewe kuwa hapa"
"Kwanini? Umeanza kunichoka we ongea tu ukweli. Mbona sili Sana"
Baada ya muda tulikuwa mtaani Hyun Joong nia yake anipeleke kwa proscuter Han ila alinidanganya tunaenda matembezini. Tulipofika karibu na nyumba ya proscuter aliniambia nimsubirie anakuja.
Wakati anaondoka, proscuter Han alimuona, alijiuliza amfuate au anifuate mimi kwanza hata hivyo alikuwa na presha juu yangu. Haraka alinifuata na kunishika mkono.
"Madina ulikuwa wapi siku zote hizi"
"Mi staki unishike"
Muda huo salome alitoka, nilipomuona nilianza kumpigia kelele Hyun Joong, Han alinikumbatia kwa nguvu ili nisiondoke.
Baada ya muda walinifungia kwenye chumba changu kwasababu nilitaka kutoroka.
"Hyun Joong alikuwa naye siku zote hizi?" Proscuter Han alijiuliza mwenyewe.
"Kaka tutafanyaje, mi naona tumpeleke tu hospitalini" salome alitoa wazo.
"Hapana kikubwa nikutafuta namna ya kumrejeshea kumbukumbu zake"
"Mtu mwenyewe jeuri Sana, umesikia maneno aliyoniambia"
"We kabinti kafupi nasema fungua mlango, oppah wangu akija atawauwa nyote" niliongea kwa kupaza Sauti.
"Unasikia sasa"
"Picha za familia yake zipo?" Alimhoji.
"Ndiyo ila kwenye simu"
"Naomba hiyo simu kwanza"
"Simu iko chumbani"
"Nenda kailete"
"Kama umenichoka ntaenda ila kama bado unahitaji niendelee kuishi utaenda wewe"
Han alicheka na kufuata chumba, alipofika alifungua na kuzama ndani.
"Ntakuua ukinishika" nilimuambia.
Han alivuta droo na kutoa simu Ndipo alikaa kitandani huku akiikagua.
"We kaka" nilimuita kwa upole.
"Niambie"
"Yule binti mweusi ni mtu mbaya ukimfukuza ntaishi na wewe ila akiendelea kukaa hapa ntakufanyia fujo"
"Kwanini?"
"Alinitelekeza pekeeyangu akaondoka zake, unajua nilikaa masaa mangapi kumsubiri? Akaniuza kwa kijana mweusi"
"Kijana mweusi?" Han aligeuka kunitazama.
"Ndiyo, hicho kijamaa kina sura ngumu yaani kinatisha, kilinipeleka kwake kikataka kunibaka oppah akatokea"
Han alinitazama kwa muda Ndipo alisogea nilipo na kunionyesha sehemu ya kukaa. Ilikuwa ni chini pembeni ya kitanda karibu na ukuta.
"Kwanini?"
"Kaa kwanza ntakuambia"
Nilikaa kisha akachuchumaa mbele yangu akisema.
"Ulipoteza kumbukumbu, naomba tumia muda wako vilevile na nguvu kukumbuka mambo ya zamani"
Aliniondoa wasiwasi na kunihakikishia atakuwa bega kwa bega na mimi. Ndipo alitoka baada ya muda alirudi na picha mkononi, alinirushia picha hizo huku akisema.
"Ukatili uliofanyika, unyama walioufanya kwa wazazi wako unasahau vipi? Kumbuka Madina"
Baada ya kuniambia alizima taa kisha akatoka na kufunga mlango. Muda kidogo IC ilizimwa nikaanza kupokea joto nzito, Nilivuta picha hizo na kuanza kuangalia moja kwa nyingine, kila nikijaribu kuzumu picha kumbukumbu haziji, nilihangaika ndani ya chumba hicho madhara yake kichwa kikaanza kuuma. Mpaka usiku Hali ilikuwa vilevile, Ndipo niliufuata mlango na kuanza kuwagongea.
"Jamani mnaniua kifo kibaya"
Ndipo Han alikuja kufungua.
"Salome washa IC" Han aliongea kwa Sauti huku akinipepea.
Baada ya siku mbili kupita, Proscuter Han aliitwa kazini, nyumbani tukabaki watatu. Salome aliamua kujifungia chumbani kwa kuniogopa tukabaki wawili.
"Twenzetu kutembea, tutabakije ndani kama watumwa" nilimnong'oneza Nana Ndipo tuliondoka.
Wakati tupo njiani tulikutana na Chief, ila sikumkumbuka. Kabla sijampita alinishika mkono na kunirudisha mbele yake kibabe.
"Bado uko hai?" Alinihoji nikabaki kumshangaa.
"Samahani baba, unanifahamu?"
Hapo Ndipo nilimvuruga, alinikamata kisha akanipeleka kunako gari yake akaniingiza na kufunga mlango, kama bahati wakati Nana anapiga kelele, baba yake alifika. Aligeuka na kuona gari inaondoka, haraka alichukua bodaboda ya mtu kisha akasema.
"Nana nisubirie hapo"
Moja kwa moja alianza kufukuzia gari, Nana aliamua kukaa pembeni huku akifuta machozi.
Safari iliendea mwisho Han aliipita gari akatangulia mbele kabisa, Ndipo aligeuza pikipiki ikawa uso kwa uso na gari hiyo, aliongeza gia akarudi kwa spidi kali. Han alionyesha kudhamilia tukio hilo linaloenda kutokea, wakati dereva anageuza gari ili kukwepa kwa bahati mbaya taili ilipinda gari ikaenda mzima mzima. Wakati nagonga gonga kichwa kwa maumivu ndivyo kumbukumbu zilizidi kunirejea. Gari ikatulia huku moshi ukitoka, kila aliyekuwa humo Hali ilikuwa nitete. Wa kwanza kutoka alikuwa ni Chief ila kwa bahati mbaya dereva alifariki papo hapo, nilijitahidi kujitoa nikafanikisha. Damu zilikuwa zinanibubujika mno, Chief licha Hali yake haikuwa sawa alianza kupigana na proscuter Han.
Proscuter Han alitaka Chief ajisalimishe lakini hakuwa tayari, wakati huo Hyun Joong alikuja kwenye pikipiki na kupaki pembeni, nilimkumbuka vizuri ishara kumbukumbu zimerejea.
Hyun Joong alimuomba Chief achukue pikipiki aondoke ili yeye aendelee kupambana na Han.
"Tafadhali msipigane" niliongea kwa jazba baada ya Chief kuondoka.
Mapigano yalianza walipigana style za kila aina mpaka hofu ikanitawala, uwezo wa Hyun Joong ulikuwa mkubwa nikaogopa atamuua hata hivyo Hyun Joong hana huruma.
"Han tafadhali muache aondoke"
Niliendelea kulalamika lakini haikusaidia kitu, nilichokifanya nilipiga hatua na kusimama katikati ya barabara na mbele kabisa kulikuwa na gari ilikuwa na spidi kali.
"Kama mnataka kuuwana bora muuwane nimeshakufa" niliongea
Han alimuacha na kuniwahi Ndipo Hyun Joong aliondoka zake, kumbe gari hiyo ilikuwa ya proscuter mwenzie.
"Yule si Hyun Joong?" Proscuter huyo aliongea baada ya kutoka kwenye gari.
"Mfukuzie" Han aliongea.
"Dah! Pekeeyangu kweli?"
"Au mpeleke nyumbani mi nimfuate"
Wakati anataka kuniachia nilimkumbatia kwa nguvu ili asiondoke.
Baada ya muda tulikuwa hospitalini maana Hali yangu haikuwa sawa.
"Unauhakika umerudisha kumbukumbu zako" Han alinihoji.
"Ndiyo, wewe ni Han siku ya kwanza kuonana ni kwenye jumba la maproscuter"
"Thx God" Han alinishika mkono kwa nguvu, wakati huo Salome alifika.
"Salome jamani..." Nilimuita akabaki kushangaa.
"Kumbukumbu zimerudi"
"Kweli dada?"
"Ndiyo"
Salome alifurahi mno na kulala pembeni yangu.
Siku iliyofuata nilikuwa vizuri huku nikipanga nguo kwa ajili ya kuondoka, wakati salome anarudi alishikwa na kizunguzungu akadondoka na kupoteza fahamu.
Baada ya muda dokta aliomba akafanyiwe vipimo mbalimbali, niliomba kuingia naye ila dokta akakataa ikanibidi kusubiri nje. Wakati nimetulia salome alipitishwe kwenye machela na kupelekwa chumba kingine, nilishangaa na kumhoji dokta.
"Nini kinaendelea?"
"Nifuate ofisini"
Tuliongozana, tulipofika alianza kunielezea.
"Mdogo wako ni mjamzito"
"What!" Nilimhoji kwa mshangao maana salome alikuwa hana tabia za wanaume, moja kwa moja nikajua mimba itakuwa ya pack jin.
"Na ujauzito una miezi mitano na nusu"
Hapo Ndipo nikichanganyikiwa zaidi.
"Alipopewa taarifa hizi ilimletea mshtuko" dokta aliongea.
Nilitoka hapo nikiwa nimechoka, Mdogo Mdogo mpaka aliko salome. Baada ya masaa kadhaa alirejesha fahamu.
"Salome....."
"Abeee!"
"Tulia kwanza"
Alitulia Ndipo alikumbuka na kuangua kilio.
"Usilie jamani"
Baadaye tulikuwa nyumbani.
"Ntafanya nini jamani" muda wote salome alikuwa akilia.
"Usijilaumu kila kinachotokea ni mipango ya mungu"
"Madina mimba ni ya Jacob"
"Naelewa Wala isikupe presha"
Kwakweli ilikuwa ni pigo kubwa, licha nilijitahidi kumbembeleza haikusaidia kitu.
Baada ya muda nilikuwa na proscuter Han nje.
"Atakuwa sawa kikubwa ni kuwa naye karibu" nilimuambia Han.
"Ntamkamata Jacob"
"Imeshakuwa tatizo kubwa, ninachokifikiria nikuondoka"
"Mnaelekea wapi?"
"Kenya"
"Bakini tu, tumeshawazoea"
"Hata hivyo tumekuwa mzigo kwako, kila siku nakuletea matatizo"
"Usiongee hivyo"
"Ukiwa na mkosi hata ukijikwaa kwenye kijiko lazma udondoke, unabakwa na mimba inaingia? Dah!"
"Nafikiri kwasasa siyo muda wa majuto"
"Kwanini wale majambazi mnashindwa kuwakamata?"
"Hii iko nje ya uwezo wangu, ambacho ntafanya nikuua kwasababu inaonekana kuna mtu Yuko nyuma yao, kesi ikienda mahakamani tu, ujue imetoka"
"Dah! Lakini Han mbona wewe tu ndo unajali kuhusu hili, wenzio wako bize"
"Yeah walisababisha kifo cha mke wangu"
"Kivipi?, I'm sorry sikupaswa kukuuliza" Ndipo nilinyanyuka ili kuelekea ndani, kabla sijampita alinishika mkono na kuniambia.
"Bakini na mimi"
Nilimtazama kwa sekunde Ndipo nikatabasamu na kuelekea ndani, nilipofika niliingia chumbani na kumkuta salome kashikilia dawa nyingi kwa madhumuni ya kujiua, sikujali Zaidi ya kufuata kilichonileta.
"Mi najiua" aliongea huku akilia.
"Ni sawa tu, ila dawa hizo hazitakuua madhara yake utamuua mtoto. Unafikiri nini kitafuata kama siyo majonzi ? Wala sikuzuii hata mimi Hivi karibuni ntajiua"
Niliondoka na kumuacha akilia, nilipofika nje niliangua kilio kwa uchungu maana uchungu aliokuwa nao mwenzangu ulikuwa siyo wa kawaida. Ndipo nilimpigia pack jin.
"We pack jin" nilimuita kwa jazba.
"Uko sawa?"
"Funga mdomo, unataka kujifanya ujumbe wangu haujauona?"
"Nimeuona lakini sister, ningumu upande wangu muache tu aishi na ampendaye"
"Naomba sasa Hivi njoo"
Siku zilisonga, miezi ikakatika na muda mwingi pack jin alikuwa upande wetu, sikupata kumuona tena Hyun Joong na uharifu ulipungua kutokana asilimia kubwa ya majambazi waliuwawa.
"Uliambiwa na dokta acha uvivu usipende kulala lala amka fanya mazoezi" nilimuambia Salome na ilikuwa ni asubuhi. Ndipo nilitoka kwa ajili ya kuendelea na majukumu.
"Unafikiri kwenye kampuni ile, utapewa mshahara unaouhitaji" Han aliniambia huku akichezea simu.
"Hata uongee vipi siwezi kuacha kazi, Hivi karibuni naenda kuitwa mamkubwa"
"Nasema kwasababu boss wako anakutamani"
"Hata anitamani vipi siachi kazi"
"Madina haujijali?"
"Yes mimi si chochote"
Ndipo Han alinyanyuka na kuanza kunifuata huku akiwa serious, nilimtazama na kujiuliza anafuata nini ila ajabu akaanza kunisogelea, taratibu nilianza kurudi nyuma mpaka ukutani. Han alinisogelea na kuweka mkono ukutani.
"Ha ha ha ......." Niliishia kumuita Ndipo nikaamua kufumba macho nikizani anataka kunibusu. Han alitabasamu na kuniambia.
"Usiku jiandae nahitaji tutoke out nina maongezi na wewe"
Han aliniacha na kuondoka zake, kiukweli toka niishi naye sikuwahi kufikiri kama angeweza kuniambia neno hilo tamu, moyo ulipata furaha nikaanza kufanya kazi kwa Kasi.
Ilipofika usiku niliwahi kuoga kwasababu muda wote tulikuwa tunachati, nilijipodoa na ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kujipodoa kiasi hiko, Ndipo nilivaa gauni nzuri na kiatu kirefu vilevile na mkoba wa thamani. Wakati najipulizia pafiumu, Nana alikuja kwa Kasi akisema.
"Dada salome....."
Haraka nilitoka nikashangaa kumkuta chini akiugulia maumivu ya uchungu. Inshu ikafeli nikabadili nguo na kumpeleka moja kwa moja hospitalini.
Wakati niko hospitalini, Han alifika pamoja na pack jin. Mwenyezimungu alisaidia Salome akajifungua mtoto wa kike. Tuliruhusiwa baada ya siku mbili.
"Salome, nikisema nimpange jina ntajikuta nampanga majina ya ajabu kama mahangaiko, mateso...." Nilimtania huku nikiwa nimemlea mtoto, na kweli salome alicheka. Wakati huo Han alifika na kusema.
"Ataitwa jina la kikorea"
"Heeeeee!"
"Yeah si ndo vizuri"
"Ataitwa Munira" Salome aliongea na kunifanya nistuke.
"Yes huyu ni Munira wetu" Salome aliongea na wakati huo machozi yalianza kunibubujika.
Siku iliyofuata nilimuomba Han anisindikize sokoni nikanunue nguo kwa ajili ya mtoto. Nilimuaga salome kisha tukaondoka, tukiwa tupo kwenye duka kubwa kwa ajili ya vitu vya watoto wa changa nilimuona Hyun Joong akitembea, kiukweli sikujua kwanini nilitamani kumuona . Na muda huo Han alikuwa mbali na mimi kidogo.
Haraka nilianza kumfuata Hyun Joong, wakati nakimbia Han aliniona hivyo alianza kunifuata huku akijiuliza kuna nini kinanikimbiza.
"Oppah.." nilimuita akasimama lakini hakugeuka. Alipotaka kuondoka nilimshika mkono.
Upande wa nyumbani salome alipokuwa jikoni alisikia Sauti ya mtoto akilia hivyo alielekea chumbani, alipofika alishangaa kumkuta Jacob kasimama huku mkononi kashikilia bastola vilevile akivuta bangi kwa hasira.
"Umenitia mkosi Sana we mwanamke, sizani kama ni haki kuzaliwa mtoto na mwanamke kama wewe"
Upande wetu Hyun Joong aliniachia lakini nikamng'ang'ania Jambo ambalo lilimshangaza Han. Wakati Hyun Joong anageuka alimuona Han Ndipo akapelekea nimemzuia kwasababu ya Han. Aisee alinishika kichwa na kunipiga bonge la busu mbele ya watu.
Han alibaki mdomo wazi, nilijitahidi kujitoa akaning'ang'ania kweli. Ndipo aliniacha nikamtwanga bonge la kofi. Hyun Joong alichomoa bastola na kuninyooshea.
"Niue..... Niueeee! Umeona roho yangu imekataa kutoka umeamua kunidhalilisha mbele ya watu?"
Proscuter Han alichomoa bastola na kumnyooshea Hyun Joong kisha akaanza kusogea kwa makini. Alitufikia mapigano yakaanza.
Upande wa salome hakuwa na chakumueleza Jacob zaidi ya kumtazama kwa chuki. Ndipo jocob aligeuza bastola alipo mtoto.
"Tafadhali....." Salome aliongea kwa Sauti ya chini mno, hakika mwili wake ulikuwa baridi kutokana na hofu. Jacob bila huruma alimpiga risasi mtoto mchanga mwenye siku kadhaa tena bila huruma, Sauti ndogo ilitoka kwa mtoto damu mbichi ikaruka na kumrukia Jacob usoni. Salome alibaki ameganda kama sanamu.
Upande wetu walidhamilia kuuwana, Hyun Joong kwa uwezo wake mkubwa alikuwa serious kabisa kuyaondoa maisha ya Han. Nilichokifanya nilivuta bastola iliyoko chini nikawanyooshea wote kama kichaa.
"Nasema acheni"
Hawakunisikia wakaendelea na wakati huo watu wote walikuwa tayari wamekimbia. Nilichokifanya nilipiga risasi juu na kumnyooshea Hyun Joong.
Hyun Joong alibaki kunitazama Ndipo niliachia risasi ikapita karibu na mkono wake, hakukwepa bali alishangaa ujasiri huo nimeutoa wapi.
"Hata mimi Naweza kuua vilevile" nilimuambia na kutupa bastola chini, wakati huo ving'ola vilisikika Hyun Joong akakimbia akielekea upande mwingine, sijui kwanini nilikuwa mzito kichwani nilijikuta tu namchukia kila mwanaume kwa wakati huo, nikatoka na kuondoka zangu.
Nilipofika nyumbani nilimkuta Nana mlangoni akilia, sikujali kuhusu yeye niliingia moja kwa moja. Wakati nafika chumbani nilishangaa chini ya kitanda kuna toni za damu, pembeni nikamuona salome kakaa, nilipoangalia kitandani sikuamini wallah. Nilimuwahi mtoto nikashangaa Sana Hali hiyo. Nikama nilipigwa msumari utosini, nguvu ziliisha tukio la kifo cha Munira likanirudi. Ubongo ukavurugwa nikavaa vazi la chuwi. Sikuwa na haja ya kuambiwa ni Jacob katenda nilijua ni yeye. Taratibu nilimuacha mtoto kitandani na kuelekea kunako chumba cha Han, cha kwanza nilianza kusachi sehemu zote kama ntaona bastola, kwa bahati nzuri niliipata nikatoka na pikipiki ya Han.
Moja kwa moja mpaka ndani kwa Jacob, nilimkuta katulia huku usoni akiwa bado na damu ya mwanae.
"Ooohh Mungu wangu, nilijua tu ungekuja" aliongea huku akicheka Sana vilevile akipiga makofi.
"Mimi na wewe anakufa mmoja" niliongea kwa msisitizo na mkazo.
"Umekuja kunitisha? Maskini kifo kinakuita"
Jocob alipandisha mzuka akaanza kunikumbuka kifo cha kaka yake, aliongea Sana kisha akaanza kunifuata ili animalizie, kabla hajanifikia nilichomoa bastola na kumnyooshea.
"Hahahaha! Wenye moyo wa kuua ni wachache mno, unahisi unaweza?"
Sikutaka kumchelewesha nilimpiga risasi ya mguuni baada ya kumuona anazidi kusogea, Jacob alishangaa kwa maumivu, hakika tukio za vifo vya familia yangu zilijirudia nakunivuruga mazima, nikawa kama kichaa nilimtwanga risasi za miguuni nikaona haitoshi nikampiga mabegani.
Kilichofuata nilimfunga kamba kwenye mikono kisha nikaunganisha kwenye pikipiki, Jacob alipiga kelele kuniomba msamaha lakini nilikuwa nimevurugwa. Nilipanda pikipiki safari ikaanza, njiani watu walishangaa ukatili huo lakini ndicho kilichokuwa kinamsahili.
"Baba, mama, abdullah, Munira, Munira mtoto, Jack na mr Choi...... Mnaendeleaje? Niko sawa, salome tu hayuko sawa, lakini furaha upande wangu inaanza kurejea" niliongea maneno hayo niko kwenye spidi mia moja themanini na tisa. Barabarani damu ikatapakaa, gari za maposi zikanizuia kwa mbele.
"Hata hapa inatosha tu" nilijisemea na kusimamisha pikipiki, wakati huo jocob alikuwa tayari kapoteza maisha maana tumbo ilisagika utombotumbo ukatoka. Nilishuka na kupandisha mikono juu.
Hakika kwa tukio hilo ilisimamisha nchi nzima yaani niseme ulimwengu kwasababu haijawahi kutokea. Salome na pack Jin waliona taarifa hiyo kwenye vyombo vya habari.
Moja kwa moja nilipelekwa sero, kesi hiyo ilikuwa nzito mno licha Han alijitahidi kadri ya uwezo wake lakini aliambiwa akijiendekeza atakufa.
Nilitoa maelezo kuhusu vifo vya ndugu zangu lakini hawakunielewa eti mpaka ushahidi, ila kifo cha Munira mtoto walikubali na kwenda kufanya upepelezi zaidi. Mtoto alizikwa kesi yangu ikapelekwa mahakamani, kilichofanyika taarifa ilitolewa kenya na wakaagiza ikiwezekana aje mtu na vidhibitisho kuwa kweli Jacob alikuwa muarifu na anatafutwa na nchi. Tulisubiri mpaka nikakata tamaa ukija kuangalia nyumbani sikuwa na ndugu yoyote angeweza kufuatilia kesi yangu. Siku hiyo kabla ya kwenda mahakamani ili kukatiwa kifungo cha maisha, proscuter Han alikuja kunitembelea.
"Vipi kuhusu salome?" Nilimhoji.
"Amekumiss na alisema hajutii tena kwa kilichotokea, kikubwa Jacob alishafariki ila anahofu na wewe"
"Ni sawa tu, hata hivyo ningehukumiwa kunyongwa"
"Kukoje huko?"
"Kila mtu anatabia yake"
"Hawakukutesa?"
"Nilipofika niliwaambia huko raiani nimeua mtu kwa kumsaga barabarani kwahiyo atakaenisogelea maisha hana"
Han alicheka mno huku akiumia kwa kunionea huruma. Mwisho machozi yalianza kumbubujika.
"Kesho ntakuwepo mahakamani, tumejaribu kuwasiliana na baadhi ya watu wa kenya but mambo yameenda wrong, kwahiyo I'm sorry ntashindwa kukutetea" Han aliniambia.
"Ni sawa tu, hata hivyo...." Nilianza kukohoa mpaka kukohoa damu, Jambo ambalo lilimshangaza Sana Han.
Siku hiyo ilikuwa siku mbaya kwangu, sikuwa na wakili hivyo nilisimama mimi kama mimi. Hakuna wakili angeweza kukubali kujiinga kwenye kesi hiyo hata umpe shiingapi, Hali yangu kiafya haikuwa sawa muda wote nilikuwa nakohoa. Proscuter Han pamoja na salome walikuwepo. Hukumu iliyotolewa juu yangu nikifungo cha maisha bila mdhamana.
mwili ulisisimka nikaanza kuwaomba wanivumilie ntaleta vidhibitisho lakini haikuwezekana.
"Jamani marehemu aliniulia familia yangu kiukatili, Basi angalieni kifo cha mtoto mchanga nani mwenye moyo na nyama angeweza kuvumilia ukatili ule? Mara ngapi nimekuja kumshtaki lakini anaachiwa?" Niliendelea kulalamika huku nikikohoa damu, askari wawili walianza kunivuta kisha wakanitoa hapo.
Mimi pamoja na baadhi ya wafungwa tulikuwa njiani kuelekea magereza, tumaini yangu iliishia hapo hata hivyo niliamini baada ya siku kadhaa ntapoteza maisha kutokana na afya niliyokuwa nayo.
Wakati tuko njiani tulivamiwa na kikosi cha majambazi, askari wakaanza kupigana na majambazi hao. Risasi zikarindima kweli, wakati wote nilikuwa nimetulia huku wenzangu wakijaribu kujificha. Ghafla kuna mtu alinitikisa begani, nilipomuangalia nilishangaa kumuona Hyun Joong kavaa mask. Ndipo alinivua pingu na kunitoa.
Haraka tulipanda pikipiki na kutoroka, kusema ukweli bado nilikuwa sijaamini kwa kile kinachoendelea.
"Oppah......" Nilimuita kwa upole lakini hakunijibu.
Mpaka kwenye jengo flani kubwa lililowazi, ambalo hawajamalizia ujenzi.
"Kwanini umenisaidia?" Nilimhoji baada ya kushuka kwenye pikipiki.
"Nijibu tafadhali" niliendelea kumuomba.
"Sikujua unapelekwa gerezani, sikuja kwa ajili yako kuna kazi ilinileta, nikakuona"
"Asante kwa kuyasaidia maisha yangu, lakini mwisho wangu nimgumu Sana" nilimuambia, wakati huo proscuter Han alifika na kuomba tunyooshe mikono juu, wakati Hyun Joong anamtazama kwa makini, proscuter Han alimtwanga Hyun Joong risasi ya begani, sikuamini nikaanza kukohoa damu.
Hyun Joong wakati anagusa mfukoni ili achomoe bastola, Han alitaka kuachia lakini akatokea yule binti anayeishi poleni pekeeyake Eun chae na kuzuia. Hauwezi kuamini Han nguvu zilimuisha baada ya kumuona Eun chae.
"Mke wangu....." Han aliongea kwa uchungu bastola ikashuka chini, upande wa Eun chae alimtazama tu na kumgeukia Hyun Joong.
"Oppah.... Oppah" alimshikashika huku akilia, proscuter Han naye machozi yalianza kumtiririka wakati huo mimi niko chini.
Ghafla askari polisi walifika na ving'ola juu.
Polisi walinikamata vilevile wakamkamata Hyun Joong, wakati Eun chae analalamika proscuter Han alimshika na kumuuliza.
"Ni wewe?"
"We kaka vipi, hebu niache"
Upande wangu nilipelekwa moja kwa moja sero, sikujua wapi Hyun Joong alikopelekwa lakini nilijua atauwawa tu. Wakati niko sero proscuter Han alifika na kuniambia.
"Usijali na Wala usiwe na mawazo Sana, kuna moja ya mawakili kutoka kenya amefika kwa ajili ya kesi yako"
Nilishangaa mno na kunyanyuka. Sikujua nguvu hizo zimetoka wapi. Ghafla alifika mzee pamoja na askari wawili, nilipomuona nilimkumbuka. Mara ya mwisho kuoanana naye wakati niko kenya nilienda kuandamana mahakamani ili kesi ya marehemu baba yangu ifuatiliwe na yeye ndiye alikuja kunipa moyo na kuniambia nimfuate nyumbani kwake anamzungumzo na mimi.
Kwakweli nilimkumbuka vizuri.
"Baba...." Nilimuita kwakiswahili.
"Usijali hapa nilipo ujue ni taifa ya kenya ipo"
Neno hilo lilinipa faraja nikaona kweli mwenyezimungu hamtupi mja wake, unaweza kupitia kwenye misukosuka mingi lakini mwisho wa siku akakufariji.
Baadaye alienda mahakamani akatoa vidhibitisho kuwa Jacob alikuwa ni muharifu na alikuwa anatafutwa kwa kushirikiana kuyaondoa maisha ya familia yangu na wengine, hakimu mkuu aliuliza kwanini nimemuua kifo chakikatili namna hiyo, Ndipo mzee alitoa vidhibitisho vya hospitalini toka kenya kuwa nilipata ukichaa baada ya kuondokewa na familia yangu na hapo Ndipo nilishinda kesi hiyo, haikuwa rahisi bali ni Mungu tu.
Nilifurahi mno nikamkumbatia baba huyo pamoja na salome huku nikiamini hata nikirejea nyumbani amani itakuwa pale pale.
Siku iliyofuata proscuter Han alimfuata Hyun Joong jela kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mkewe.
"Kama umeletwa na hilo naomba ondoka" Hyun Joong alimuambia.
"Kuondoka ntaondoka, ila nataka uniambie kuhusu yule mwanamke anaefanana na marehemu mke wangu"
"Sijui chochote"
"Tafadhali Hyun Joong, kesi yako kuiepuka ningumu Sana Chief wenu tayari kashauwawa na wenziyo wote. hata wewe unaweza kufa muda wowote"
"Kwahiyo unamaana gani?"
"Endapo ukiniambia kuhusu yule mwanamke ntahakikisha umetoka salama"
"Nakuamini vipi?"
"Tumewahi kuongea mimi na wewe?"
Hyun Joong alibaki kumtazama kwa umakini.
"Ndiyo ni mkewako"
Proscuter Han alishangaa mno.
"Wakati ule jengo linateketea wenzangu waliniacha ndani, mkewako aliniomba Sana nimsaidie kwahiyo hivyo ndivyo ilivyokuwa" Hyun Joong alimuambia ukweli.
"Sasa.... Kwanini anajifanya hanijui Wala kumjua mtoto?"
"Alipoteza kumbukumbu, Na wewe utanisaidiaje?"
Baada ya muda proscuter Han alikuwa njiani kuelekea nyumbani, furaha iliyojaa majonzi ilimtawala akajikuta anapiga kelele kwa furaha, alipofika nyumbani alimtazama mkewe ambaye alikuwa bize kumbembeleza Nana.
Ukweli Nana alikuwa anamkumbuka vyema mama yake lakini alishangazwa mama hataki kutoa ushirikiano kama mama aliyemmiss binti yake.
"Babaa....!" Nana alimkimbilia baba yake huku akilia, Ndipo Eun chae alinyanyuka na kuwatizame.
"Mama hanitaki tena...." Nana aliongea.
"Hapana, mama anakupenda Sana.... Hae Soo!......" Proscuter Han alimuita mkewe kwa jina lake halisi tena kwa hisia kali. Eun chae alimshangaa na kusema.
"Mimi siyo Hae Soo, mimi ni Eun chae"
"Tafadhali rudisha fahamu zako, kumbuka mimi ni mume wako, Basi jaribu kumkumbuka hata mwanao" Han aliongea kwa uchungu mno, wakati huo nilifika pamoja na askari kadhaa kwa ajili ya kunilinda nisitoroke Wala kufanya ujinga ule.
Baada ya muda nilikuwa na Han tumekaa sehemu.
"Kwahiyo mtaondoka?" Han alinihoji.
"Ndiyo, pia nashukuru kwa jitihada zako, nilikusikia siku ile Eun chae unamuita mkeo"
"Ndiyo ni mkewangu"
"Ningeitambua sura yake kwenye picha Basi ningekuambia kwasababu nilikuwa namfahamu"
"Hata hivyo hana kumbukumbu yoyote, anashindwa kumkumbuka mtoto wake"
"Kwani ilikuwaje kifo chake"
"Siku hiyo ilikuwa ni birthday ya Nana, tulienda kijijini kwa ajili ya kusherekea, wakati tuko ndani kikosi cha Chief akiwemo Hyun Joong walitokea na kuvamia, nilipigwa Sana mpaka kunyanyuka nikashindwa, watu waliuwawa na walichokifanya walimfunga kamba mkewangu na kuchoma nyumba nzima. Nilijua aliteketea lakini Hyun Joong aliniambia wakati mkewangu Yuko ndani na yeye pia alikuwa ndani"
"Aaaa ndo akamsaidia!"
"Yeah ila Ntamfanya arudishe kumbukumbu haraka"
"Vipi kuhusu Nana?"
"Kwa bahati nzuri alipigwa kitu kizito akazimia hivyo walimrusha nilipo ili kunitia majonzi zaidi"
"ooh my God, pole sana, ok vipi Hali yako?"
"Niko sawa, nahisi ugonjwa ule ulitokana na hofu"
"Pole Sana"
Ntakusaidia kurejesha kumbukumbu za mkeo, kwanza vipi kuhusu Hyun Joong?" Nilimhoji.
"Tumeingia mkataba, nimeahidi kumsaidia"
"Unauhakika atatoka salama?"
"Yeah kikubwa amekubali kusema ukweli, kumbe kuna kiongozi alikuwa nyuma yao, na yeye ndiye alitoa oda wakavamie Basi la wafungwa kwasababu mmoja wenu alikuwa ni binamu yake"
"Kesi ya Hyun Joong ni nzito Sana mpaka naogopa, naomba kabla ya kuondoka nikaonane naye"
Proscuter Han alinifanyia mpango nikaonana na Hyun Joong.
"Kwanini umekuja?" Hyun Joong alinihoji.
"Kwasababu ulinisaidia"
"Ok"
"Oppah..."nilimuita Ndipo alinitazama.
"Nashukuru kesi yangu imefutwa na Hivi karibuni naondoka"
"Wapi?"
"Nyumbani kwetu, kenya"
"Kwahiyo unataka nini?"
"Usiongee hivyo mbele yangu, kama ningekufa ungemuambia nani? Mi nahofu juu yako na sijui kwanini uliamua kuwa gaidi Hali ya kuwa unajua gaidi maisha yake ni mafupi"
"Unataka kujua?"
Nilishangaa na kukubali kwa kutikisa kichwa maana sikutarajia kama angeweza kuufungua moyo wake na kunieleza hata kwa ufupi.
"Mama yangu aliolewa kwa mtu flani, kwani lazma nimtaje?" Alinihoji.
"Hapana ni sawa tu"
"Ni katili Sana alimuua mama yangu kwa kumtumbukiza kwenye pipa ya maji, baadaye akaanza kunifundisha ugaidi, nimekaa na mbwa wa kali kwenye chumba kimoja na yote alitaka niwe na moyo wakikatili, ndiyo alifanikiwa na mpaka sasa naishi kwa kauli yake"
"Kumbe mpaka huku wapo binadamu wakatili kama marehemu mr Robert?"
Alibaki kunitazama.
"Proscuter Han ameahidi kukusaidia, na naimani utatoka. Lakini hautonikuta"
"Kwani nilazima wewe kuondoka?"
"Ndiyo ni amri kutoka kwa raisi wetu. Oppah......"
Alinitazama.
"Mimi hapa nakupenda Sana wewe"
Hyun Joong alishangaa huku akinitazama, nakweli mapigo yangu yamoyo yalikuwa juu kabisa. Siyo rahisi kujitoa ufahamu na kusema kauli hiyo kwa mwanaume.
"Nashukuru kwa tisheti yako, endapo nikikumiss Sana ntaivaa" niliongea ndipo Nikanyanyuka ili kuondoka lakini akasema.
"Basi ukae huko kwa kunisubiri"
Baadaye nilifika nyumbani kwa proscuter Han, nikamuomba aondoke na Nana ikiwezekana ntapigia simu na kumuambia kilichojili.
Han alitoka na Nana, tukabaki watatu.
"Hivi unauhakika nahichi?" Salome alinihoji?
"We usijali"
Chumba tulikipamba maua mazuri huku kila kona tukaandika Happy birthday Nana, na baadhi ya maboxi ya mazawadi tukaweka pembeni, nilitoka nikamuomba Eun chae aingie ndani ya chumba hicho kuna surprise yake.
Eun chae aliingia na kushangaa mazingira hayo, alibaki kuangalia ila haikusaidia kitu Ndipo niliingia na kamba nikamchota mtama kisha salome akanisaidia tukamfunga vizuri na kutoka, kilichofuata nilirusha kiberiti kwenye maua yakapamba moto kisha nikabana mlango.
"Jamani kesi nyingine tena" salome aliniambia wakati huo Eun chae alianza kupiga kelele akiomba msaada. Moshi ulitawala mpaka salome akaanza kulia kwakohifia jela.
Ghafla Eun chae alikaa kimya akaanza kuhangaika, taratibu kumbukumbu za miezi iliyopita zikaanza kujirudia mpaka akajikumbuka yeye ni nani. Ghafla proscuter Han alifika na kushangaa tukio hilo.
"Honey ........" Eun chae Alipoita Honey hapo Ndipo sote tulishtuka tukajua hapa kumbukumbu zimerejea maana korea honey mara nyingi ni kwa wanandoa, proscuter Han alifungua mlango haraka tukavuta mipira na kuanza kuzima moto kwa maji.
Han alifanikisha kumtoa nje, wakati anamlaza Eun chae alimshika shavuni huku machozi yakimbubujika.
"Mume wangu jamani"
Hapo Ndipo proscuter Han aliamini na kumkumbatia kwa nguvu, wakati huo tulitoka ndani tukiwa tumechakaa. Tulitabasamu kwa furaha baada ya kuwaona.
Safari iliwadia tulikuwa airport pamoja na mzee wetu huku tukisindikizwa na proscuter Han vilevile na pack jin. Tuliagana kwa furaha nikaahidi tutarudi tena lakini kikubwa kesi ya Hyun Joong ifuatiliwe kwa makini, proscuter Han aliniahidi kufanya hivyo na akasema endapo tukichelewa Basi atakuja yeye.
Safari ikaanza tukaondoka zetu kuelekea jijini nairobi.
NA HUU NDIYO MWISHO WA SIMULIZI HII, SHUKRAN ZA DHATI ZIENDE KWAKO WEWE ULIYEPOTEZA MUDA WAKO KWA KUIFUATILIA MWANZO MPAKA SASA.
BONYEZA HAPA KUPATA VICHEKESHO
MWISHO

No comments