Header Ads

Header ADS

Simulizi: Tabasamu langu sehemu ya tisa (09)

 

 



"Mi naogopa" niliongea kwa hofu.


 


"Nifuate"


 


"Siwezi, kwanza haujaniambia umenileta huku kwasababu gani"


 


"Utajua"


 


Baada ya muda nilipelekwa sehemu nakuwakuta vijana wawili wamelala huku wakiugulia kwa maumivu. Chief wao alikuwepo pamoja na mabaunsa kadhaa.


 


"Ombi letu kwako, nikuwafanya warudi kwenye hali zao. Endapo ukishindwa tutakuua" aliongea Chief kwa msisitizo mkali. Hofu ilinitawala nikageuka kumtazama oppa, wagonjwa hao walionekana walipigwa risasi hivyo nilitakiwa niwaondoe risasi hizo jambo ambalo nilikuwa sina uzowefu nalo.


 


Vifaa na baadhi ya dawa niliwekewa mbele, kisha Chief akasema.


 


"Endapo wakafariki na wewe unakufa"


 


Hapo Ndipo nilijuta kujifanya kutafuta kazi kwenye mahospitali mbalimbali, Hyun Joong alipoona namtazama Sana aligeuza mgongo ili kuondoka.


 


"Oppah...." Kwa mara ya kwanza nilimuita kaka tena kwa hofu kali, Hyun Joong alisimama kwa sekunde kadhaa na kuondoka zake bila kugeuka nyuma.


 


 


 


"Anza" ilikuwa ni sauti nzito yenye msisitizo mkali kutoka kwa mmoja ya baunsa aliyokuwepo hapo, alinishtua na kunifanya niwawahi majeruhi, niliwatazama nikagundua siyo levo yangu. Nilipotaka kujitetea nilikoromewa haraka nikavuta vifaa, nilivaa gloves nikitetemeka, kwa bahati mbaya mkono ulikufa gazi hata nilipojitahidi kuuinua nilishindwa, macho yao yalikuwa kwangu hivyo niliamua kuangua kilio na kuanza kumuita Hyun Joong. Nilimuita huku nikilia kwa uchungu Ndipo akatumwa mtu akamuite, Hyun Joong aliponifikia alisimama na kunitazama.


 


"Oppah siwezi, mkono wangu u..." Niliishia hapo na kujiinamia ishara wafanye watakalo.


 


Baada ya muda waliniacha kwanza, tulikuwa tumekaa na Hyun Joong aliniambia nimuonyeshe hapo panapouma. Niligoma kidogo mwisho nikasogeza brauzi na kumfanya aone kidonda, Hyun Joong alinitazama usoni na kuangalia pembeni, alichokifanya alileta baadhi ya dawa na kuniuliza.


 


"Hizi ni sahihi?"


 


"Hapana"


 


Ndipo alifuata boxi ya madawa na kuileta.


 


Upande wa Chief walikuwa wakitazama kinachoendelea.


 


"Tusiburi akiwa sawa atawatibu wenzetu" aliongea Chief.


 


"Ila huyu mwanamke ni mmarekani. Kama marekani ikigundua tumemteka si itakuwa tatizo kwetu?" Aliongea mmoja wapo.


 


Upande wetu Hyun Joong alianza kuosha kidonda changu kupitia dawa yenye ukali kama haujapigwa gazi kwanza, kuvumilia ningumu. Nilikaza meno kikomando mwisho nilishindwa na kupiga kelele kwa maumivu.


 


Baada ya muda aliniwekea dawa na kuniambia.


 


"Nenda sasa"


 


Nilikuwa na hofu mno kuwatibu vijana wale hivyo nilimgeukia Hyun Joong na kumshika mkono.


 


"Oppa naogopa"


 


"Hii ni lazma"


 


"Basi niue tu"


 


"Watakuua wale endapo utashindwa, jitahidi kwasababu mmoja ya wagonjwa ni mdogo wa Chief" baada ya kuniambia aliondoka.


 


Kazi ilianza hata nilipoomba gazi iletwe kwasababu wagonjwa walikuwa wanapata shida, niliambiwa nifanye hivyohivyo kikubwa wapone. Nilihangaika mwili mzima nikajaa damu ya wagonjwa, jitihada zangu zilimsaidia mmoja nikafanikisha kumtoa risasi. Wakati huo Hyun Joong alikuwa anakuja na kuondoka, wagonjwa walikuwa wawili hivyo nikamuanza aliyebaki ambaye ni mdogo mtu, haikuwa kazi rahisi damu zilimvuja mpaka akazimia, kitendo cha yeye kuzimia kiliwafanya wote wachanganyikiwe. Chief alichomoa bastola na kuninyooshea ishara akifa tu, roho yangu mali yao. Alivuja damu nyingi ikanibidi niombe msaada wajitolee kumtolea damu, pango hilo tulichanganyikiwa nikachukua jukumu lingine la kuchota damu kwa watu wengine. Zoezi likaendelea, kila nikijaribu damu zinaruka na kunirukia ukija kuangalia risasi ilikuwa sehemu mbaya karibu na moyo. Yaani nikikosea kidogo mtu hayupo, nilipambana kishujaa mwisho nikafanikisha kutoa risasi. Wote walifurahi na kunipigia makofi, mdomo wa bastola uliokuwa juu yangu ulishushwa nikapata kupumua.


 


"Tokeni sasa wagonjwa wapate hewa" niliongea kwa jazba na kuwafanya wakunje nyuso zao, Ndipo Chief aliwafukuza wote.


 


Nilitoka taratibu huku nikiwa nimejaa damu kama vile natoka machinjioni, wote walikuwa wananitazama Ndipo mbele nilimuona Hyun Joong akiwa amekaa, nilisimama na kuendelea kumtazama hata hivyo yeye ndiye namfahamu. Hyun Joong aliponiona namtazama Sana alinifuata na kunishika mkono tayari kunitoa nje ya pango. Moja kwa moja kwenye mto flani. Nilianza kunawa taratibu


Ndipo Hyun Joong alivua koti yake na kuweka chini kisha akavua tisheti na kubaki kifua wazi. Nilishtuka mno na kuangalia mbele huku nikijisemea.


 


"Anataka kunibaka mbona anavua?"


 


Hyun Joong alinirushia tisheti yake na kuniambia.


 


"Vaa na ufue yako"


 


Niliishika kama sekunde kadhaa nikamwambia.


 


"Toka sasa nivae"


 


Hyun Joong alinigeuzia mgongo ila imani kwangu ilikuwa sifuri.


 


"Toka bhana, kwa bahati mbaya ukigeuka na ukanichungulia..."


 


"Sahau"


 


Aligoma kutoka kwakuhofia huwenda nikatoroka.


 


Majira ya usiku nikiwa bado nimevaa tisheti ya Hyun Joong, nilikuwa nimejikunja pekeeyangu kwa kuhofia mazoea na wahuni hao. Ghafla walikuja wanaume watatu, kabla sijakaa sawa mmoja alishuka na kunikunja kisawasawa kisha akaniziba mdomo nisiweze kupiga kelele, wenzie walianza kulazimisha kunibaka ila nikajitahidi kurusha miguu licha kwa shida. Ghafla Hyun Joong alitokea akiwa na sahani ya chakula, walipomuona waliniachia na kunyanyuka, Hyun Joong aliwapiga wenzie kisha wakatoka wakikimbia, hofu ilinitawala nikaanza kutetemeka. Hyun Joong alishuka na kuchuchumaa karibu yangu.


 


"Oppah Walitaka kunibaka" niliongea huku akinitazama.


 


"Uliondoka na kuniacha pekeeyangu na unajua hakuna ninayemfahamu zaidi yako"


 


"Shika chakula"


 


"Kwanini unanifanyia haya, hata kama damu zetu hazijaendana hauwezi kuninyanyasa kama hivi... Hujui nimepitia mangapi kwenye huu ulimwengu, naishi kwa kujificha kama swala kweli? Hivi Ulitoa mchango gani kwa mwenyezimungu siku anaiumba dunia hii ili useme Madina sihitaji kumuona akitembea kwa amani? Adui yangu ananiwinda hadi wewe nisiyekufahamu unayawanda maisha yangu? Mdogo wangu abdallah aliffariki akafuata Baba yangu, haikuchukua muda mama aliuwawa na huyo mpuuzi anayeniwinda. Mdogo wangu kipenzi Munira asiyekuwa na hatia aliingizwa kwenye friji mpaka akakata roho, why! Kwanini unanipeleka puta hivi? Hebu peaneni zamu na Jacob kama yeye ananiwinda wewe upumzike kwanza. Acheni jamani majonzi niliyonayo ndiyo yataniua, sina muda mrefu ntawatokea kwenye ulimwengu wenu mniache" niliongea kwa huzuni mpaka nguvu zikaniishia taratibu nikamuangukia kifuani, Hyun Joong alitafakari kwa muda na kuinua mkono taratibu kunishika begani.


 


 


Baada ya muda Hyun Joong alikuwa na Chief wakiongea.


 


"Binti anauzoefu mkubwa Sana" aliongea Chief.


 


"Ndiyo"


 


"Nahitaji tuendelee kumtumia"


 


"Halitowezekana boss"


 


"Kwanini?"


 


"Naomba kama amemaliza nimrudishe kwao"


 


"ningumu kwasababu tayari siri zetu anazo, kama hatoweza kuwa miongoni mwetu Basi tutamuua"


 


"Haiwezekani" aliongea Hyun Joong na kuondoka kwa hasira, Chief alimshangaa mno maana moyo wa huruma huwaga hanaga kabisa, hivyo aliagiza vijana wake waje kumzuia.


 


Hyun Joong aliniamsha na kuniambia.


 


"Tuondoke nyumbani"


 


Sikuamini niliachia bonge la tabadamu. Kabla hatujaondoka vijana kadhaa walifika na kutuweka Kati ili tusiondoke, niliogopa mno na kumshika mkono.


 


"Usiogope"Hyun Joong aliniambia na tayari kuanza kupigana na wenzie, uwezo wake ulikuwa mkubwa mno mpaka Chief aliyekuwa pembeni na wenzie akatikisa kichwa kuashiria hawawezi kumzuia.


 


Hyun Joong alijitahidi kadri ya uwezo wake na kufanikisha kuwazuia na hapo Ndipo tulipata nafasi ya kuondoka.


 


Majira ya asubuhi nilizinduka na kujikuta chini ya mti ila katikati ya mji, niliangaza kona zote sikuweza kuona mtu Ndipo nikaamua kufanya mawasiliano na proscuter Han.


 


Nilifika nyumbani kwake nikaoga na kubadili nguo.


 


"Ooh my God tisheti yenye harufu nzuri tena ya kiume umeitoa wapi?" Aliongea salome huku akiikagua kagua.


 


"Achia hapo" nilimjibu na kutoka chumbani, Ndipo nilimkuta Han pekeeyake sebuleni.


 


"Ulinipa wakati mgumu Sana" aliongea Han.


 


"I'm sorry" nilimjibu na kukaa.


 


"Nana aliniambia mara ya mwisho ulipanda pikipiki ya mtu aliyeziba uso wake, nini kiliendelea?"


 


"Han naogopa sana, maisha yangu yako hatarini Sana"


 


"Haupaswi kuogopa kwasababu uko na Mimi"


 


Baada ya kuniambia neno hilo la kunifariji niligeuka kumtazama usoni tukaangaliana kama sekunde kadhaa.


 


"Mamaaa" Nana aliniita na kunifanya nishtuke.


 


"Ooh Nana" nilimkumbatia kwa furaha huku nikimuangalia Han kwa aibu, Ndipo Han alitabasamu na kuangalia juu.


 


"We Nana, naitwa Aisha" nilimnong'oneza huku nikiendelea kutabasamu.


 


Majira ya usiku tukiwa tumelala, ukweli uliniwasha nikakosa amani na kuamua kuamka. Nilielekea kunako chumba cha proscuter Han ili kumueleza ukweli kuhusu kile kilichotokea, kabla sijafika nilisikia Sauti akilia hivyo nilisogea haraka na kufungua mlango taratibu, nilimshuhudia akiwa ameshikilia nguo ya kike pamoja na picha kifuani, kiukweli hali yake ilinidhihirishia anamajonzi makali juu ya marehemu mke wake. Nilimtazama kwa muda mrefu mwisho nilivuta mlango na kuondoka huku nikiwa nimenyong'onyea.


 


"Habari za siku Han"


 


Ilikuwa asubuhi tulivu huku nikiandaa chai kwa ajili ya Han mfanyakazi, vilevile na mwanae mwanafunzi.


 


"Why umeamka asubuhi yote hii na hali ya kuwa ningefanya mwenyewe" Han aliniambia.


 


"It's okay, nilikuona ulikuwa unalia jana, nikaona itakuwa vyema nikikuandalia supu"


 


"Ooh! Uliniona?"


 


"Ndiyo tena ulikuwa na nguo ya mwanamke pamoja na picha umeiweka kifuani"


 


"Aaaa! Nilimmiss mkewangu"


 


"Nilijua hilo, kama ukitoka kazini naomba njoo moja kwa moja nyumbani nikwambie wapi majambazi waliko"baada ya kumwambia niliondoka na kumuacha akitafakari.


 


"Hii siyo haki kabisa"niliongea baada ya kumkuta Salome bado kalala.


 


"Siko vizuri ndo maana"


 


"Nenda hospitalini sasa"


 


"Staki"


 


"Sijui proscuter Han atarudi saa ngapi nimwambie ukweli"


 


"Ukweli gani?" Salome aliamka na kukaa kitako.


 


"Hujui kama nilitekwa na Hyun Joong"


 


"Ndo nani huyo?"


 


"Yule jambazi nguli"


 


"Ooh my God, Madina ndo unawashwa kusema ukweli hivyo?"


 


"Lazma niseme"


 


"Jamani achananayo yatakuponza"


 


"Naenda sokoni, ntawahi kurudi"


 


Nilivuta koti nyeusi na kuondoka, baada ya masaa kadhaa kupita, nilikuwa sokoni huku nikichagua baadhi ya vitu. Ndipo alitokea pack jin nyuma yangu na kunistua.


 


"We Jin jamani"


 


Tulienda mgahawani tukaagiza vinywaji story zikaendelea.


 


"Nimekumiss Sana, toka muondoke nyumbani hamna habari na sisi" aliongea Jin na kunifanya nitabasamu. Nilichokifanya nilimueleza ukweli kuhusu kifo cha baba yake mr Choi, vilevile nikamuonyesha video niliyotumiwa na Jacob. Kiukweli Jin alishindwa kujizuia akaanza kulia kwa huzuni, nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kumbembeleza mpaka akapoa.


 


"Ni sawa tu, sijui mama ntamueleza vipi kuhusu hili"


 


"Usijali, ntamueleza mimi, haijalishi hataki kuniona ila ntamuambia tu"


 


"Vipi kuhusu salome?"


 


"Yuko sawa ila Jin... Salome anakupenda Sana anashindwa tu kukwambia"


 


"What!" Jin alibaki kushangaa, wakati huo nilimuona mwanamke flani nikamfananisha na Eun chae, haraka nilinyanyuka na kutoka mgahawani, nilimkimbilia mwisho nikamfikia.


 


"Ooohh, miss vipi mkono wako?" Alinihoji baada ya kusalimiana.


 


"Niko sawa, mbona unakasi Sana na umevaa kofia kubwa hivyo?" Nilimhoji wakati huo proscuter Han alikuwa maeneo hayo, hivyo alituona, baada ya kuniona nikizungumza na mwanamke aliyemgeuzia mgongo, alitafakari na kuanza kutufuata ili ajue naongea na nani, kabla hajatufikia Hyun Joong alifika akiwa ameziba mdomo na mask kama kawaida huku akiwa kwenye pikipiki yake, alifika na kumpakia Eun chae tayari kuondoka naye.


 


 


 


Wakati nashangaa shangaa Han alifika na kunishika mkono.


 


"Ulikuwa unaongea na nani?" Alinihoji huku akipumua kwa Kasi.


 


"Na Eun chae kwani kuna tatizo?"


 


"Eun chae ni nani?"


 


"Ni mpenzi wa Hyun Joong"


 


"Madina nini kinaendelea mbona unanichanganya"


 


"Ntakwambia ukweli nilikuahidi"


 


Baada ya muda tulikuwa mgahawani tukitumia chakula. Nilimuahadithia kile kilichotokea na Wala sikumficha kitu, alichukuwa ushahidi na kupiga simu kazini kwake, haraka alinitaka niondoke nyumbani kisha yeye akaelekea kwenye jumba lao la ma proscuter, wakati natoka mgahawani nilimuona Hyun Joong amesimama kwa mbali huku akinitazama, hofu ilinitawala nikajua huwenda amesikia nilichomwambia Han hivyo niliita taxi na kupanda haraka.


 


Baada ya muda nilifika nyumbani na kumkuta Salome kanuna.


 


"Vipi tena?" Nilimhoji.


 


"Umefanya nini Madina?"


 


"Kwani ulitaka nikae na siri ya maovu rohoni? Nimemwambie Han kila kitu na Hivi ameenda kuwakamata"


 


"Haaaa Madina jamani, mbona unajitaftia matatizo hivyo? Hata siri hiyo umesema?"


 


"Mbona hatuelewani"


 


"Ndo umeamua kumwambia pack jin kwamba nampenda?"


 


"Tatizo iko wapi? Unashindwa kumuambia na yeye mwenyewe domo zege, nakosaje kuwaunganisha?"


 


Wakati huo upande wa Hyun Joong alikuwa kwenye pikipiki na Eun chae huku wakielelea kwenye makao yao.


 


"Walikuwa wanaongea nini?" Hyun Joong aliendelea kujiuliza maswali bila majibu.


 


Upande wa Han alikuwa pamoja na maproscuter wenzie huku wakielekea nilikowaelekeza. Gari zilikuwa na spidi ya kufa mtu. Wakati wako njiani Hyun Joong pamoja na Eun chae walikuwa nyuma yao bila kuelewa.


 


"Oppah, endesha taratibu naumwa"


 


"Unaumwa nini?"


 


"Kichwa"


 


"Basi nishike"


 


Eun chae alishtuka kwa hofu, Ndipo Hyun Joong alimshika mkono na kuupenyeza ubavuni kwake. Taratibu Eun chae aliupenyeza na mwingine na kumkumbatia, Ndipo Hyun Joong aliachia tabadamu.


 


Upande wetu nilikuwa bize kumpigia Han ila simu yangu hakushika.


 


"Unawaza nini?" Salome alinihoji.


 


"Ngoja nikamlete Nana"


 


Upande wa maproscuter walichanja mbunga wakaamua kujigawa baadhi kulia wengine kushoto.


 


Upande wangu, wakati natoka kumchukua Nana huku tukiwa kituo cha daladala, Basi lilifika na abiria wachache, na miongoni mwao alikuwa Jacob, moyo ulishtuka haraka nikageuza mgongo kabla hajaniona.


 


"Huyu mpuuzi ametoka sero?" Nilijisemea moyoni haraka nikambemba Nana mgongoni tayari kukimbia.


 


Baada ya masaa kadhaa kupita, maproscuter walipokaribia walipaki gari zao na kushuka wakiwa wamejikoki vizuri, walijigawa kwa mara nyingine na kuanza kutembea kwa makini.


 


"Nimemuona Jacob" nilimuambia Salome baada ya kufika nyumbani.


 


"Unasemaje Madina?"


 


Upande wa ma proscuter walifika kwenye pango lile, cha kwanza walitulia huku wakiangalia ramani. Ghafla vijana wawili walitoka na kuondoka, hapo hapo Han alituma vijana wake wakawakamate, wengine walizama ndani. Kilichotokea risasi zilianza kurindima ndani ya pango hilo, walipigana vya kutosha baadhi wakakamatwa ila Chief na wengine walifanikisha kukimbia.


 


Maproscuter wawili walifariki wengine 6 wakajeruhiwa. Walipotoka tu, Hyun Joong alifika, mazingira yalimshangaza mno Ndipo alitokea dogo jambazi na kumueleza kilichotokea.


 


"Wewe ulikuwa wapi?"


 


"Sikuwepo, wakati narudi Ndipo nilikuta tukio"


 


Hapo Ndipo Hyun Joong alijua nimewauza.


 


Majira ya usiku Upande wetu tukiwa bize kucheza gemu, hauwezi kuamini ilipigwa risasi ikapasua kioo cha tv, wakati tunahanya Hanya nilishangaa kumuona Chief anaingia kwa kishindo kikali, haraka nilinyanyuka na kuanza kurudi nyuma, aliponifikia alinishika shingo na kunipeleka ukutani, alinibamiza kwa hasira kisha akaanza kuninyonga kwa hasira. Salome alipiga kelele na muda huo Nana aliamka. Alipofika sebuleni na kukuta Hali hiyo, alikumbuka baba yake huwa anamuambia endapo akiona uvamizi asije kujitokeza, hivyo alianza kurudi nyuma huku akifuata maelekezo ya baba yake. Moja kwa moja alielekea kwenye sanduku lililoko mbele ya mlango kisha akaingia na kujifungia.


 


Tulipigwa na salome ila mimi nilipigwa kisawasawa mpaka nikakoma kuropoka.


 


"Hakikisha mtoto wa Han analetwa" aliongea Chief kwa msisitizo.


 


Nana alitafutwa kona zote lakini hakuonekana Hali ya kuwa kijiboxi walikuwa wanakipita kwa zarau kwasababu kilikuwa mlangoni hivyo hakuna angeweza kukiwekea mashaka.


 


Baada ya kumtafuta na kumkosa, waliondoka na sisi. Wakati tunatoka Jacob alifika akiwa na bastola kwa ajili ya kutumalizia, Aliangaza nyumba nzima hakuona mtu.


 


Upande wetu tulipelekwa sehemu flani tukapigwa vipoko vya maana mpaka tukasema yes, kilichofuata tulifungwa kamba tukakunjwa kama mpira kisha tukaning'inizwa juu kwa juu huku tukiwa tumezibwa midomo. Pipa zililetwa mbili zikajazwa maji, hauwezi kuamini kamba ziliachiwa kila mmoja akazama ndani ya pipa. Hakika usiombe ikakukuta na Hali ya kuwa umezibwa mdomo. Tulihangaika bila kurusha miguu Wala mikono mwisho tukavutwa, imagine unatoka sehemu ya hatari then ukajisaidia kuvuta pumzi kupitia puani. Yaani nimateso kuliko kitu chochote, ndani ya moyo wangu nilijua endapo tutarudishwa Basi ntakufa.


 


Hyun Joong pamoja dogo yule walifika akanitazama jicho la hasira kweli, kidogo tumaini ilirudi nikajua lazma atanisaidia kama siku ile, Ndipo kijana mmoja alimgeuka na kuanza kumfokea.


 


"Ungeacha tukamuua siku ile, ona sasa wenzetu wameuwawa wengine wamekamatwa. Unahisi nini kitafuata kuhusu sisi? Si kukamatwa?"


 


Chief kwa hasira alimnyooshea bastola Hyun Joong. Wote wakamgeuka mwenzao kutokana siku ile alinitetea na ilitakiwa niuwawe kwasababu nimejua siri zao.


 


Ndipo Hyun Joong alichukia na kuchomoa bastola moja kwa moja akanitwanga risasi ya tumbo. Ukimya ulitawala, damu mbichi ikaruka.


 


 


SONGA NAYO!


 


Damu iliruka ukimya ukatawala kwa sekunde kadhaa kila mmoja akitafakari kwa anachokiona. Salome hakuamini alibaki kutoa macho.


 


Upande wa Han alipofika nyumbani Nana alitoka ndani ya box akilia.


 


"Nana" Han alimuwahi na kumtoa haraka.


 


Upande wetu Hyun Joong alisepa zake bila kujali, Ndipo Chief alimuachia agizo dogo flani ya kutulinda kisha akasepa na wengine, dogo huyo alitutazama Sana hofu ikamtawala akihisi huwenda mapolisi wanaweza kutokea ikawa shida kwake, hivyo alimfungua salome na kuondoka zake.


 


Salome alihangaika huku akilia mno, alichofanya alitafuta mawasiliano na Han hivyo wakanipeleka hospitalini, madokta walihangaika kwa ajili ya kuokoa maisha yangu. Mwenyezimungu alisaidia risasi ikatolewa.


 


Niiliingizwa ICY matibabu mengine yakaendelea.


 


"Vipi doctor!" Han alimhoji doctor baada ya kumuona akitoka chumba nilipo.


 


"Kwasasa afadhali kidogo"


 


Siku zilisonga sikuweza kupata fahamu, wiki na mawiki nikiwa ICY mpaka mwezi na nusu bado sijarejesha famu. Walikata tamaa juu yangu ila hawakuchoka kunitembelea.


 


"Kama unaumwa ni muhimu kwenda kupima" Han alimuambia Salome.


 


"Ntafanya hivyo"


 


"Siyo ntafanya, hebu Nenda sasa Hivi"


 


Muda huo walikuwa pembeni yangu,Ndipo salome alitii kishingo upande na kutoka. Wakati anafungua mlango alishangaa kuona mtu anaondoka akiwa amevaa koti yenye chata mgongoni na hapo Ndipo aligundua ni Hyun Joong. Haraka alirudi ndani na kumuambia proscuter Han.


 


Han haraka alinyanyuka ili kuondoka ila ajabu Salome alishangaa kuona natikisa kidole. Ndipo Han aligeuka kunitazama.


 


"Oooh my God" Han aliongea kwa upole haraka akamuagiza salome akaite dokta.


 


Siku zilisonga nikaanza kupata afadhali, nilipoteza kumbukumbu nikawa sikumbuki chochote Wala yeyote. Walijitahidi kunikumbusha mambo yazamani lakini haikusaidia kitu, mpaka nikaruhusiwa kuondoka bado sina kumbukumbu hata moja.


 


"Inabidi mtu ampeleke sehemu alizowahi kufika ili tuone kama atakumbuku" Han alimuambia Salome wakati huo wakinitazama nilipokaa.


 


Ndipo salome alichukua jukumu la kunizungusha mtaani.


 


"Mi naanza kusikia kizunguzungu, ila Madina acha hivyo unasahau vipi vifo vya ndugu zako" salome aliniambia.


 


"Vifo? Ndugu zangu? Walikuwaje kwani"


 


"Jitahidi kukumbuka mi nimechoka"


 


"Kwani we ninani kwangu mbona unaongea utakavyo"


 


"Hata mimi jitahidi kunikumbuka bhana, kwanza nisubirie hapo nakuja"


 


Salome aliniacha hapo na kufuata chocolate, nilimsubiri mpaka nikachoka Ndipo niliamua kuondoka bila kujua njia iliyotuleta ni ipi. Nilitembea ndani ya mji huo mpaka nikachoka, sikuwa na wakumuomba msaada Wala kumuomba anielekeze nyumbani, njaa uchovu vilinitesa nikajikuta nahangaika. Nilipita karibu na mgahawa Ndipo nilimuona kijana mweusi mwenzangu ambaye ni Jacob hata kumbukumbu juu yake sikuwa nazo nikaona bora nikamuombe msaada, niliingia mgahawani huku nikisalimia watu kwa shobo. Wakati Jacob akichezea simu nilishika meza kwa bahati mbaya kinywaji kikammiminikia Jambo ambalo lilimfanya ageuke kunitazama.


Muda huo kumbe Hyun Joong alikuwa meza ya pembeni pamoja na mwenzie, hivyo aligeuka naye kunitazama.


 


Jacob baada ya kuniona alishangaa na kukunja uso, haraka nilitoa leso kwenye mkoba na kuanza kumfuta futa huku nikimuomba msamaha.


 


Muda wote Hyun Joong alikuwa akinitazama na kutazama tisheti niliyovaa ya siku ile akanipa.


 


"Nisamehe Sana kaka yangu, naomba Sana" niliongea kwa kingereza nikizani haelewi kiswahili na hapo Ndipo nilimshangaza Jacob.


 


"Anaigiza mbele yangu?" Jacob alijisemea huku akinitazama. Ndipo nilikaa na kuanza kula chakula chake tena kwa pupa.


 


Hyun Joong alinitazama akashindwa kuelewa kwanini nakula hivyo, hata Jacob alibaki kunitazama. Ndipo nikaanza kusema huku chakula kipo mdomoni.


 


"Waliniambia naitwa Madina lakini sikumbuki, na sijui kwanini naishi kwenye nchi hii ya wakorea yaani nimehangaika kila niliyemuomba msaada ananishangaa tu, nilivyokuona mweusi mwenzangu nikasema mwenyezimungu amekushusha kwa ajili yangu"


 


Baada ya kuongea niliachia bonge la tabadamu, Jacob alikunja uso akaangaza kona zote huku akihisi huwenda ni mtego wa proscuter Han.


 


Upande wa salome alikuwa nyumbani na Han huku akilia mno.


 


"Tutampata usihofu" Han alimuambia.


 


"Tatizo mtu mwenyewe jeuri kwanini hakunisubiria"


 


Upande wetu maongezi yaliendelea.


 


"Haunijui mimi ni nani?" Jacob alinihoji kwa kiswahili na kunifanya nishangae.


 


"Wow! Unaongea kiswahili? Sikujui kwani wewe unanijua?"


 


Jacob alibaki kunitazama nami nikajua ananifahamu, nilipiga makofi kwa furaha na kuongea kwa kikorea tena kwa Sauti mpaka kila mmoja akabaki kunishangaa.


 


"Yeeeee nimempata mtu wa kwetu"


 


Hapo Ndipo Jacob alianza kuamini amini huwenda nikweli sina kumbukumbu. Hyun Joong na mwenzie waliamua kuondoka zao.


 


Ndipo Jacob Alitabasamu na kupindisha mdomo huku akijisemea.


 


"Kiu yangu inaenda kukata, now sitoota njozi za ajabu tena"


 


"Kwani kaka kiswahili ni cha nchi gani?" Nilimhoji.


 


"Wewe ni mkenya ndo maana unaongea kiswahili"


 


"Aaaaa kenya! Natamani kupaona"


 


"Twende nyumbani kwangu" Jacob aliniambia kwa umakini akitazama mapokezi yangu.


 


"Wow! Twende"


 


 


 


Jocob alitabasamu kwa mara nyingine na kunyanyuka, nilinuuka haraka kisha tukatoka. Moja kwa moja tulielekea nyumbani kwake.


 


"Wow nyumba nzuri" niliongea na kuanza kuzunguka zunguka. Jocob alinitazama kwa muda kisha akajisemea.


 


"Endapo ntachelewa ntajikuta njozi zikiendelea"


 


Wakati huo nilipita karibu yake na kumtabasamia huku nikiendelea kuzunguka.


 


"Mbona karembo kidogo, nimbake kisha nimuue"


 


Ndipo aliniambia niende chumba cha pili kuna zawaidi yangu, haraka nilienda nikikimbia. Nilipofika nilianza kuangaza na muda huo Jacob aliingia akiwa kifua wazi huku akivuta bangi kwa hasira. Nilimshangaa Sana na kumuuliza.


 


"Uko sawa kweli?"


 


Jacob alinirushia bangi usoni ikaniunguza kidogo, hofu ikaanza kunitawala.


 


"Unajifanya haunikumbuki we malaya"


Aliongea kwa jazba haraka akanifuata na kunishika, alinitikisa kwa nguvu huku akiendelea kunilalamikia kuhusu kifo cha kaka yake, kisha akanirusha kitandani. Nilianza kupiga kelele nikawahi kusimama kabla hajanishika, Jacob hakukoma alinifuata kwa bahati mbaya akavuta tisheti ikachanika mgongoni. Kwa ukicha wa Jacob alianza kunipigiza ukutani mpaka nikawa mwekundu ghafla.


 


Kama bahati Hyun Joong aliingia na kusema.


 


"Muache huyo mwanamke"


 


Jacob aliniachia nikadondoka kama mzigo.


 


"We ni nani?"


 


"Mimi ni mimi"


 


Walijibizana kibabe Ndipo Jacob alishuka kitandani na kumsogelea Hyun Joong, wakati anamkaguakagua kwa zarau alipigwa ngumi moja akaenda chini na Wala hakuamka.


 


"Jamani jamani mimi" niliongea huku nikilia Ndipo Hyun Joong aligeuza mgongo na kuondoka.


 


Alipofika nje nilitoka na kumuwahi kumshika mkono.


 


"Mi naogopa we kaka, ona alitaka kunibaka nisaidie sijui naishi wapi? Sijijui mimi nani, kuna kabinti kadogo dogo keusi kanajifanya kunijua kameniuza kwa huyu mjinga ndo kaliniambia naitwa Madina kumbe katapeli"


 


Maneno yangu yalimfanya Hyun Joong abaki kushangaa, Ndipo alianza kuunganisha baadhi ya matukio. Alikumbuka mara ya mwisho alinipiga risasi ya tumbo na hata alivyokuwa akija kuniangalia hospitalini nilikuwa kwenye chumba cha maututi na hata alivyoniona mgahawani nikama nimebadilika Sana, Ndipo alinigeukia na kunihoji.


 


"Unanifahamu?"


 


"Heee! Kwani we nani?"


 


Hyun Joong aliona nampotezea akapanda pikipiki na kuondoka, niliangua kilio kwa Sauti na kuanza kumkimbilia ili asiniache. Hyun Joong akiwa ananitazama kwenye kioo alijiuliza maswali mengi Ndipo aliamua kusimama. Haraka nilikuja mbio mpaka nikamfikia.




BONYEZA HAPA KUSOMA MAKALA MBALIMBALI ZA MAFANIKIO


 INAENDELEA




No comments

Powered by Blogger.