Header Ads

Header ADS

Chombezo: Dunga Dunga sehemu ya nne (04)



 “Wewe mkali. Nimeamini kwamba wewe mkali” Aliniambia.

Bado nilikuwa nikiendelea kumfuatilia Judith mtaani kwao lakini bado hakuonekana. Nilikuwa sina raha kabisa, Judith akaonekana kuanza kuuteka moyo wangu kupita kawaida. Siku bado zilikuwa zikiendelea kwenda mbele, Judith hakuonekana machoni mwangu na wala simu yake haikuingia simuni mwangu.

Naikumbuka siku hii. Nilikuwa nimetoka kucheza mpira. Uchovu mwingi ulikuwa umenipata kiasi ambacho baada ya kuoga nikaamua kutulia kitandan huku nikiangalia televisheni. Simu yangu ambayo ilikuwa pembeni kabisa ya kitanda ikaanza kuita.

Niliiangalia simu ile, nilionekana kukasirika, sikutaka kabisa kupokea simu katika wakati huo. Kwa kutotaka kelele nikaunyoosha mkono wangu na kuivutia kwangu. Macho yangu yakaelekea katika kioo cha simu, namba ilikuwa ngeni simuni mwangu. Kwa haraka haraka nikaipeleka sikioni.

“Halloooo....!!” Sauti ya kike ilisikika simuni.

Niliuhisi mwili wangu ukipigwa na ganzi, sikutegemea kupokea simu kwa wakati ile kutoka kwa msichana ambaye sauti yake ilikuwa ikivutia namna ile. Jina la Judih likaanza kujiandika kichwani mwangu, kwa mbali nikaanza kutabasamu huku ule uchovu ukionekana kunitoka.

“Hallooo...!” Niliitikia huku tabasamu likionekana usoni mwangu.

“Naomba unisamehe kwa kuchelewa kukupigia” Judith aliniambia.

Kichwani mwangu sikuona sababu yoyote ya msichana mrembo kama Judith kunimba msamaha, nilina kwamba alikuwa na sababu zote za kuchelewa kunipigia simu kutkana na urembo wake.

“Usijali. Kawaida tu japokuwa ulinifanya kutokujisikia fresh” Nilimwambia.

“Nafahamu na ndio maana nimekuomba msamaha. Nyumbani wananibania sana yaani hata sipati muda wa kutoka nje” Aliniambia.

“Urembo wako ndio unasababisha yote hayo Judith. Kama ungekuwa msichana wa kawaida....nafikiri wala usingezuiliwa kutoka nje” Nilimwambia Judith ambaye nilikisikia kicheko chake cha chini.

“Usinidanganye”

“Kweli Judith. U msichana mrembo sana, nafikiri kama sitoweza kukuaminisha hili, moyo wayo wangu ungesikia hukumu” Nilimwambia.

“Ila si mrembo kama msichana wako”

“Msichana wangu! Msichana yupi?”

“Huyo uliye nae”

“Yupi?”

“Kwa hiyo unataka kunidanganya kwamba hauna msichana?”

“Nitamtoa wapi? Bado sijamuona msichana wa kuwa nami” Nilimdanganya kama kawaida yangu.

“Aahahah...unanidanganya”

“Huo ndio ukweli Judy. Nahitaji msichana aliyetulia kama ulivyo. Sitaki kuchukua msichana atakayenifanya nijute” Niliendelea kumdanganya.




“Sawa. Tafuta, unaweza kumpata”

“Natarajia kumpata. Niko kwenye harakati za kumwambia ukweli”

“Safi sana. Nani huyo? Unaweza kunionyeshea ili nimjue wifi yangu?”

“Sawa. Unataka lini nikuonyeshee?” Nilimuuliza.

“Hata kesho”

“Utapata muda wa kuonana nami?”

“Nafikiri”

“Utaaga vipi nyumbani?”

“Niachie mimi ila ningependa uniambie utakuwa wapi na wifi yangu huyo”

“Kama itawezekana njoo Manchester Bar”

“Bar?” Aliniuliza huku akionekana kushtuka.

“Ndio”

“Sijazoea kuingia bar”

“Sawa. Basi njoo katika frmu zile za kutengeneza mikate katika msikiti wa Kichangani”

“Saa ngapi?”

“Muda wowote ule”

“Sawa. Basi tufanye saa nane. Nafikiri nitapitia huko nikitoka kumtembelea shangazi”

“Sawa. Utanikuta”

“Ila uwe nae mahali hapo”

“Sawa. Nitamwambia. Ila hii ndio simu yako?”

“Hapana. Hii ni simu ya mama. Usijaribu kupiga hata simu moja” Aliniambia.

SOMA HAPA MEMES KUPITIA SIMU YAKO

ITAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.