Header Ads

Header ADS

Chombezo; Dunga dunga sehemu ya tatu (03)

 


“Duuuh..! Hiyo kali.”

Mariamu ndiye alikuwa msichana ambaye nilikuwa nikimuamini sana katika mtaa wetu, sikuwa na hamu ya wasichana wengine ambao kwa kuwatazama tu walionekana kutokuwa na kile ambacho nilikuwa nikikihitaji, bikira. Kitu nilichokifanya ni kuamua kwenda katika mitaa mingine kwa ajili ya kuzitafuta bikira tu.

Sikuwa nikishinda mtaani kwetu, mara kwa mara nilikuwa nikitoka na kwenda katika mitaa mingine. Huko nilikutana na wasichana wengi lakini kutokana na uzoefu ambao nilikuwa nao katika mambo ya wasichana, niligundua kwamba hawakuwa na bikira ambazo nilikuwa nikizihitaji.

Katika mitaa ambayo nilikuwa nikienda nikaanza kutengeneza urafiki na watu wengine ambao nilikuwa nikiwakuta huko. Kila siku nilikuwa nikiwatembelea na kuwapa kampani mbalimbali huku nikijaribu kuwaonyeshea uchangamfu mkubwa.

Huko ndiko ambako nikaanza kupata mambo mengi ya wasichana mbalimbali. Msichana Judith ndiye ambaye alikuwa akiogopeka katika mtaa wote wa Mapipa.

Msichana huyu hakuwa kama wasichana wengine. Kila siku alikuwa mkimya kupita kawaida. Kuitikia salamu ilikuwa ni kawaida yake lakini maongezi mengine baada ya salamu, hayakuwa yakipata nafasi yoyote kwake. Kila mvulana alikuwa akimuogopa msichana huyu ambaye mara kwa mara alikuwa akikaa ndani ya nyumba yao tu.

Alionekana kama kuwachukia wavulana bila sababu yoyote ile. Alionekana kutokupenda wavulana kabisa. Muda wote mavazi yake yalikuwa ya kiheshima kuliko msichana yeyote ambaye alikuwa akiishi mahali hapo. Kila siku alikuwa akielekea kanisani, hasa katika siku ambazo alikuwa akihitajika huko.

Toka ahamie katika mtaa huo. Hakuwahi kuwa na skendo za kutembea na mvulana yeyote katika kipindi chote ambacho alikuwa akiishi katika mtaa huo wa Mapipa. Ilipotoke kuguswa na mvulana yeyote, Judith alikuwa akishtuka kana kwamba alikuwa ameguswa na kitu ambacho hakikuwa cha kawaida.

Kwa mara ya kwanza ambayo nilikuwa nimeambiwa mengi kuhusiana na Judith, nilibaki nikimwangalia tu. Ni kweli alinitamanisha sana lakini uzuri wake pamoja na utulivu wake vilikuwa vitu ambavyo vilikuwa vikinivutia kuliko kawaida.

Sikuwa na shaka na Judith. Alionekana kuwa mgeni kabisa katika mambo ya mapenzi. Hali ambayo alikuwa akijiweka kila siku mbele ya wavulana ilinifanya kuwa na uhakika kabisa kwamba Judith alikuwa msichana bikira na si kama Mariamu ambaye alinifanya kushangaa.

“Haumuwezi yule. Judith ni msichana wa tofauti sana” Ezekiel ainiambia.

“Najua simuwezi...ila ninamtaka, ninataka kuwa nae na kufanya nae japo mara moja” Nilimwambia Ezekiel ambaye alionekana kushtuka kupita kiasi.

“Hapo ndio pabaya zaidi. Hivi unajua kama Judith hajawahi kuwa na mwanaume yeyote katika maisha yake?” Ezekiel aliniuliza.

“Hapana”

“Habari ndio hiyo. Judith bado msichana mbichi kabisa” Ezekiel aliniambia.

Nilibaki nikitabasamu tu, maneno ambayo alikuwa ameniambia yalionekana kunifurahisha kupita kawaida. Maishani mwangu nilikuwa nikihitaji bikira tu, sasa kitendo cha kuniambia kwamba Judith hakuwahi kufanya mapenzi na mvulana yeyote, nilifurahia sana.

“Nitataka kuwa wa kwanza kwake” Nilimwambia Ezekiel.

“Utakuwa unajisumbua tu. Kwanza utaanza vipi?”

“Hilo si suala la kuwa na wasiwasi, cha msingi ni kuwa wa kwanza kufanya nae tu” Nilimwambia Ezekiel.

Ezekile aliniangalia mara mbili mbili, uso wake haukuishiwa tabasamu hata kidogo, alikuwa akiniangalia huku macho yake yakinionyeshea kutokuwa na matumaini ya mimi kumpata Judith. Nilitamani kumwambia ni kwa kiasi gani nilikuwamkali hasa kwa wasichana lakini nikajikuta nikibaki kimya.

“Acha niwasafishie njia. Nikitoka mimi, nafikiri hatowakataa” Nilimwambia Ezekiel.

“Jaribu...ila sidhani kama utafanikiwa. Abdul amechemka, Michael amechemka, achana na hao, hadi Barnabas Sallu amechemka. Unafikiri utaweza wewe?” Ezekiel aliniambia.

“Sawa. Ila ni lazima nijaribu. Msichana hawezi kunishinda hata mara moja. Wote wameumbwa kwa ajili yetu....hasa mimi” Nilimwambia Ezekiel.

“Sawa bwana. Jaribu bahati yako” Aliniambia.





Kila siku nilikuwa nikielekea katika mtaa ule wa Mapipa kumtembelea Ezekiel huku lengo langu kubwa likiwa ni kukutana na Judith. Ingawa niliambiwa kwamba Judith alikuwa msichana mgumu sana lakini wala sikuonekana kujali, katika maisha yangu niliwaona wasichana wote kuwa wepesi ila kitu ambacho kilikuwa kikihitajika ni kwenda kwa uangalifu.

Niliendelea kwenda kwenye mtaa ule kwa mwezi mzima lakini wala sikuweza kumuona Judith zaidi ya ile siku ya kwanza. Sikukata tamaa, bado niliendelea kuelekea katika mtaa ule huku lengo langu likiwa lile lile, kuonana na Judith na kumwambia kile ambacho kilikuwa kikiusibu moyo wangu.

Sikutaka kuisahau siku hii, siku ambayo kwa mara ya pili kuonana na Judith tena baada ya mwezi kupita. Nakumbuka siku hiyo nilikuwa nimekaa nyumbani kwa kina Ezekiel huku nikifikiria ni kwa jinsi gani ningeweza kuonana na Judith.

Nikayainua macho yangu, sikuamini kabisa mara baada ya kumuona Judith mbele yangu akija kwa mwendo wa madaha. Nilijihisi kupigwa na mshtuko, mapigo yangu ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi huku mzunguo wangu wa damu ukiwa mkubwa mwilini mwangu.

Nilikuwa nikimwangalia Judith kwa makini, mwendo wake tu ulikuwa ukiniacha hoi, Gauni ambalo alikuwa amelivaa lilikuwa likiuchora vilivyo mwili wake. Mimi nilikuwa miongoni mwa wavulana ambao walikuwa wakimwangalia Judith.

Kila mvulana ambaye alikuwa akimwangalia Judith alikuwa akiogopa kumfuata. Kwa sababu mdomo wangu ulikuwa na uzoefu sana kuongea na wasichana, nikasimama na moja kwa moja kuanza kumfuata Judith ambaye alikuwa ameshika kidumu kidogo akielekea katika kituo cha mafuta kununua mafuta ya taa.

Nilipokuwanikipiga hatua kumfuata, tukagonganisha macho. Mapigo yangu ya moyo yakaanza kudunda zaidi, uzui wa Judith ukanilegeza kupita kawaida. Huku nikiendelea kupiga hatua kumfuata, mawazo yangu yakaanza kuvuta picha ya chumbani. Nikajiona kuwa pamoja na Judith kitandani, nikaanza kumvua nguo zake na kisha kuanza mchezo ule ule ambao katika vitabu vyote vya dini duniani vilikuwa vimekataza, MAPENZI.

Nikamfikia Judith na kuanza kutembea pembeni yake. Judith alibaki akinishangaa, ghafla nikamuona akianza kuelekea pembeni kabisa na mimi, nikaanza kumfuata kule kule. Judith alionekana kuogopa, hapo ndipo nikaamini kwamba Judith alikuwa akiwaogopa wavulana.

“Mbona unanikimbia Judith” Nilimuuliza swali mara baada ya kumfuata kule kule.

Judith hakujibu kitu chochote kile, akabaki kimya. Sikutaka kunyamaza, nikalirudia swali langu, Judith ado alikuwa kimya. Nilipolirudia swali langu kwa mara ya tatu, Judith akasimama na kuanza kuniangalia usoni, bado akili yangu ilikuwa ikiufikiria uzuri wake.

“Wewe mvulana vipi?” Judith aliniuliza huku akiwa amekasirika na uso wake kuukunja.

“Mbona unanikimbia? Ninanuka au?” Nilimuuliza huku nikianza kuinusa fulana yangu.

Maneno yale yalionekana kumuhuzunisha kwa kiasi fulani. Niliyatumia maneno yale makusudi kabisa kwani niliamini ni lazima angehisi kwamba ninamuona msichana mwenye maringo aliyejaa dharau.

“Nafikiri ninakuchafulia hali ya hewa. Naomba unisamehe kwa hilo Judith” Nilimwambia.

“Umelijua vipi jina langu?” Aliniuliza huku akionekana kushangaa.

Hilo lilikuwa swali ambalo kwangu nilimuona kufanya osa kubwa sana. Swali hilo lilitarajiwa kuja na maelezo mafupi ambayo kwa namna moja au nyingine basi ingenifasa kuzoeana nae. Nilimwangalia kwa makini na kuanza kutabasamu.

“Kwa nini unaniuliza hivyo?” Nilimuuliza.

“Sikufahamu na wala sifahamu kama nilikwishawahi kukuona sehemu yoyote ile” Aliniambia maneno ambayo yaliongeza tabasamu langu zaidi.

“Unanidanganya Judith” Nilimwambia

“Kweli. Yaani sikumbuki kabisa” Aliniambia huku vijana wengine wa mtaa ule wakionekana kutushangaa, hawakuamini kama kungekuwa na kijana ambaye angeweza kumsimamisha Judith na kuongea nae kama nilivyofanya.

“Umekwishawahi kuniona ila haukumbuki tu, nafikiri ni muda mrefu umepita” Nilimwambia.

“Kweli?”

“Ndio” Nilijibu huku nikionekana kuwa na uahakika juu ya kile ambach nilikuwa nikikiongea kwa wakati ule.

“Sawa” judith aliitikia na kuendelea na safari ya kuelekea kule alipokuwa ametumwa.

Sikutaka kubaki mahali pale, na mimi nikaanza kupiga hatua kumfuata na kuanza kuongozana nae. Judith alionekana kutokuwa na amani lakini wala hakuniambia kitu zaidi ya kuendelea kuwa kimya. Nilijua kwamba japokuwa tulikuwa tumeongea kwa muda mfupi sana lakini nilikwishajua kwamba Judith alikuwa ameanza kunizoea.

“Ningependa nikusindikize” Nilimwambia Judith.

“Wapi?”

“Unapoelekea. Bia shaka katika kituo cha mafuta” Nilimwambia, tabasamu likaanza kuonekana kwa mbali usoni mwake, kwa asilimia kadhaa nikaanza kujipa ushindi juu ya kile ambacho nilikuwa nikikitaka kwa wakati huo.

Nikaanza kupiga stori na Judith, kila tulipokuwa tukipita, wavulana walikuwa wakituangalia, walionekana kutokuamini kile ambacho walikuwa wakikiona. Judith alionekana kuwa mzuri kweli, uzuri ambao kila mwanaume ambay alikuwa akimtazama basi alikubaliana moja kwa moja na maneno niyasemao.

Tuliongea mengi, tukapata muda wa kuzoeana, tukawa tukiongea huku tukichekeana kana kwamba tulikuwa tumeonana katika kipindi kirefu kilichopita. Sikutaka kuongelea kitu chochote kile zaidi ya stori za kawaida sihusuyo maisha ya kawaida.

“Naomba uishie hapa” Aliniambia mara baada ya kufika karibu na kwao.

“Haina tatizo. Ila ningependa niendelee kuwasiliana nawe baada ya hapa.

“Kuwasiliana na mimi?” Aliniuliza huku akionekana kushtuka.

“Ndio. Kwani kuna tatizo lolote?”

“Hakuna. Ila si tutakuwa tukionana mara moja moja?”

“Nafahamu lakini nafikiri inaweza kuchukua muda mrefu sana”

“Yeah. Huwa ni mara chache sana napata nafasi ya kutoka nje. Nafikiri utaniona hata siku nyingine” Aliniambia.

“Sawa. Ila ningependa unipe namba yako ya simu. Ila kama hautojali”

“Sina simu”

“Hata ya rafiki yako wa karibu?”

“Sina rafiki wa karibu zaidi ya mama yangu”

“Sawa. Naomba nikupe yagu. Kama uktokea kupata muda, naomba japo uniambie usiku mwema....lunch njema na hata asubuhi njema” Nilimwambia.

Akabaki akitabasamu.




Kwa kasi ya ajabu nikaondoka mhali hapo na kukifuata kiduka kilichokuwa pemben yetu na kisha kuomba karatasi pamoja na kalamu. Judith alikuwa akinisubiri mahali pale alipokuwa. Niliporudi, nikaanza kuiandika namba yangu ya simu na kisha kumgawia.

“Tutaonana” Aliniambia na kisha kuondoka mahali pale. Nilibaki nikiendelea kumwangalia tu, vijana wote ambao walikuwa wakituangalia wakabaki wakinishangaa hawakuamini kama kweli nilipata nafasi ya kuongea na Judith na kisha kutangulizana nae.

“Taratibu ndio mwendo. Mimi ndiye simba mwenda pole bwana” Nilijisifia na kuondoka mahali hapo huku Judith akiwa amekwishaingia getini.

*****

Kila siku nilikuwa nikimfikiria Judith, akili yangu haikuwa ikitulia, Judith alikuwa akinipelekesha kupita kawaida. Katika siku zote, siku hizo ndizo ambazo nilikuwa makini sana na simu yangu. Nilikuwa nikiisubiria simu ya Judith kupita kawaida.

Kila simu yangu ilipokuwa ikiita, nilikuwa nikifikiria kuwa ni Judith na nilikuwa nikitegemea kuiona namba ngeni simuni mwangu. Nilichoka na kukasirika kila nilipokuwa nikiangalia kioo cha simu yangu na kuziona namba hizo kuwa si ngeni simuni mwangu.

Siku zilikatika wala namba ya Judith haikuingia simuni mwangu. Sikutaka kukubali, kila siku nilikuwa nikielekea katika mtaa wao huku lengo langu likiwa ni kuonana na Judith na kumuuliza sababu za kutokunipigia simu na wakati namba yangu alikuwa nayo.

Kumuona Judith halikuwa jambo rahisi, alionekana kuwa mgumu sana kupatikana mtaani. Vijana wa mtaa ule wa Mapipa bado walikuwa wakiniona kwamba mimi ni miongoni mwa watu waliokuwa na bahati sana. Kitendo cha kuongea na Judith kilionekana kuwashtua.

“Unasemaje?” Ezekiel aliniuliza huku akionekana kushtuka.

“Ndio hivyo. Niliongea nae na nikampa namba ya simu” Nilimwambia.

“Amekupigia?”

“Bado. Tena naombea hivyo hivyo aendelee kuchelewa” Nilimwambia Ezekiel.

“Kwa nini?”

“Nitamlalamikia katika hali ambayo hata yeye mwenyewe atanionea huruma” Nilimwambia Ezekiel ambaye akabaki akicheka tu.

SOMA MAKALA ZA MAFANIKIO

INAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.