Header Ads

Header ADS

Simulizi: Rama sehemu ya kumi (10) MWISHOOO

 


Nimefanya nini…” niliwaza huku nikikaa chini, nilikua nikisubiria kelele za watoto kutokana na kuwamwagia maji ya moto. Lakini kimya kidogo kilipita, sikusikia kelele, nilinyanyuka na kuwasha taa. Vitanda vilikua tupu, hakukua na mtoto. Kama mtu aliyechanganyikiwa nilienda kukagua vitanda, nilitoa mpapa magodoro lakini hakukua na kitu. nilitoka mpaka sebulani, nikaenda mpaka jikoni kuona kama walikua kule. Hawakuakule, nilipata wazo kwenda chumbani kwa binti wa kazi kuona kama walilala huko. Mlango ulikua umefungwa nikaanza kugonga kwa nguvu.


“Watoto wako wapi? Mbona hawajalala chumbani kwao?” Nilimuuliza binti wa kazi baada ya kuniitikia.


“Mama akisafiri huwa wanaogopa kulala wenyewe, wanakuja kulala kwangu, sijui kwanini….” Binti wa kazi aliniambia huku akitaka kufungua mlango.


“Basi nilikua nawaangalia tu.” Nilimjibu huku nikitoka, moyoni kuna kitu kilikua kinaniambia warudie uwamaliza si damu yako, ukiwamaliza ndiyo utamuumiza yule mwanamke. Lakini kuna kitu kilikua kikiniambia kuwa hapana hawanakosa lolote, shukuru Mungu umeiepuka dhambi hii. Nilirudi chumbani na kutoa magodoro yote mawili, maji hayakua mengi sana hivyo ilikausha chini kidogo, niakchukua magodoro na kuyapeleka chumbani kwetu. Nilijua asubuhi kama wangeona kuwa yemeloa wangejiuliza maswa, ilikua ni bora kuona kama hayapo nikawaambia nimeamua kuyabadilisha.


Asubuhi niliamka mapema na kuondoka nayo, nilienda kuyatupa nikanunua mengine na kurudisha kama zawadi nikiwaambia kuwa nimeamua kubadilisha magodoro kwani yalikua yamechakaa. Nilishinda kutwa nzima nikiwa na mawazo sana, kila daikika nilikua nikiangalia siomu yangu kuona kama mke wangu atanipigia lakini hakunipiga. Nilikua na hasira sana lakini cha ajabu sikua na hasira na mke wangu, nilikua na hasira na watoto wake, niliona kama wao ndiyo walikua wamenikosea na si mke wangu.


Mpaka jioni mke wangu alikua hajanipigia simu na nikipiga simu yake ilikua haipokelewi. Nikiwa chumbani mtoto wake mkubwa alikuja, aligonga chumbani kwangu nikamruhusu aingie, lakini nilipomuona tu sura ya yule mbaba ilinijia. Ilipandwa na hasira na kujikuta naanza kumtukana, nilimtukana sana nikimuambia ni kwanini alikua akiingia chumbani kwangu bila hodi. Kumbuka aligonga na mimi ndiyo nilimuambia aingie, aliniomba msamaha huku akilia lakini sikujali, nilimuambia anitokee.


“Mama anapiga anasema simu yako haipatikani…” Aliongea huku akilia, alikua kashikilia simu ya Dada yake mkononi. Nilinyanyuka harakaharaka na kumkimbilia, nilimnyang’anya ile simu na kuanza kusema.


“Haloo! Haloo!”


“We mshenzi nini, kwanini unawatukana watoto wangu, kama una hasira na mimi malizia kwangu!” Mke wangu alianza kwa kunitukana.


“Hapana, sijafanya hivyo, nilikua namuonya ameingia chumbani bila kugonga.” Sijui kwanini lakini baada tau ya kusikia sauti ya mke wangu nilinywea kabisa, nilijikuta naomba msamaha huku nikidanganya ili tu kumridhisha mke wangu. Mke wangu hakukubaliana  na majibu yangu, alitukana sana mpaka kunikatia simu, hakuniambia chochote kilichomfanya kunmipigia.


Nilijaribu kumpigia tena lakini simu yake haikupokelewa. Nilijikuta napandwa na hasira, nilitaoka nnje na kuanza kutukana, sijui nilikua natukana nini, lakini nilitukana, nikaenda mezani na kumwaga chakula, watoto walibaki kimya hata yule mdogo. Dada wa kazi alishangaa kuniona katika hali ile, nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa. Baada ya kutukana sana tena matusi ambayo hawayahusu nilirudi chumbani nakuanza kulia. Nilikua na hasira sana, baada ya kama nusu saa hivi simu yangu ilianza kuita, alikua ni mke wangu, nilijua lazima watoto wamemuambia kila kitu hivyo sikupokea.


Nilipoona anazidi kunisumbua ilizima simu na kulala mpaka asubuhi. Siku iliyofuata sikutoaka kabisa, hata kazini sikwenda, nilijifungia ndani huku nimezima simu. Mara kadhaa binti wa kazi alikuja kugonga lakini sikufungua mlango. Nilikua na hasira sana na niliogopa kutoka nnje kwani nilihisi kabisa kuwa naweza kufanya kitu kibaya. Jioni mke wangu alirudi. Alikua ashaambiwa kilichotokea hivyoa liahirisha safari zake na kurudi, alijaribu kuongea na mimi kuniuliza tatizo nini lakini sikua na majibu, nilimuambia kuwa niko sawa.


Kwa mara ya kwanza aliniomba msamaha akiniambia kuwa mtoto mmoja ni wangu na wale wawili kweli si wangu, aliniambia kuhusu mtoto wake wakwanza akaniambia kuwa ni mtoto wake kweli na alishawahi kuolewa. Nilimsamehe tukaendelea kuishi, ingawa nilijaribu kusahau na kulazimisha furaha lakini bado nilijikuta nina hasira. Nilikua nimewakasirikia watoto wa mke wangu, niliwaona wao kama sababu ya mimi kukosana na mke wangu.


Siku moja nilikua nimetoka kazini, mke wangua liniambia nimpitie mtoto wake mkubwa shuleni, nilimpitia nikarudi naye nyumbani. Lakini baadaye kulikuja wageni, nikawa nimwasindikiza na Gari, wakawa wamembeba mtoto mdogo wa mke wangu na yule mkubwa naye akaingia kwenye gari.


Niliwafikisha wageni lakini wakati narudi mke wangu alinipigia simu, kuna kitu alikua ananiulizia baada ya kumaliza akidhani kuwa kakata simu aliendelea kuongea, nilimsikia akiongea na simu.


“Hawezi kuondoka pale ananisaidia nyumbani yule ni binamu yangu, unaona sasa sipo kaenda kumchukua mtoto shule…” mke wangu aliongea.


“Mimi hata siwaelewagi, mtu mzima kama yule hana familia anaishi kwako tu….” Ilikua ni sauiti ambayo nilikua naifaham, aliokua ni yule Baba. Waliendelea kuongea mara nikasikia mabusu. Hasira zilinipanda, nilianza kuendesha gari pembeni, nilikua nikilielekeza kwenye nguzo ya taa ya barabarani, mtoto mkubwa wa mke wangu alikua kakaa mbele huku kampakata mdogo wake.


“watu watajua ni ajali!” Nilijisemea huku nikitaka kugongesha gari kwenye mlingoti wa taa za barabarani. Nilikua nataka kutengeneza ajali, nilikanyaga mafuta kwa nguvu lakini kabla ya kufikia ule mlingoti kuna gari nyingine ilikua inakuja kwa kasi mbele yangu, ilikua inakuja upande wangu hivyo nililazimika kuikwepa, nikajikuta narudi kulia na kuparamia gari nyingine ndogo. Niliikwaruza ile gari ndogo upande wangu na ile nyingine uiliyokuja kwa kasi ikapita. Nililazimika kusimama, tukaanza kutukanana kila mtu akimlaumu mwenzake, kwakua aliyekua anakuja mbele yangu ndiyo alionekana ana makosa na alishakimbia tuligombana na kila mtua kaondoka zake.


Hapo akili zilinirudia kidogo. “Hivi nataka kuwafanya nini hawa watoto?” Niliwaza, nilikua nikitetemeaka, watoto nao walikua wakitetemeka. Nilirudi nyumbani nakuingia ndani, mke wangu hakurudi mpaka saa mbili usiku. Alirudi na kukuta nishamuandikia talaka tatu nakumkabidhi.


“Hii ni nini?” Aliuliza kwa mshangao, hakuamini kilichokua kimetokea, hata mimi sikuamini kuwa nilikua namuacha mke wangu.


“Talaka, nimekupa talaka tatu si mke wangu, kesho uondoke.” Nilimuambia, mke wangu alidhani ni utani, aliaza kutukana kama kawaida yake huku akiniambia kuwa ile nyumba ni yake, ina jina lake hivyo kama nikuondoka basi niondoke mimi.


“Hii ni mara ya pili na nusurika kuwaua watoto wako, mara ya kwanza niliwamwagia maji ya moto lakini hwakuepo kitandani, kama unakumbuka nilibadilisha magodoro. Leo nilitaka kuwagongesha kwenye gari wafilie mbali lakini Mungu kawaoko, kaangalie gari imekwaruza. Naamini mara ya tatu nitafanikiwa, sitaki kufanya hivyo lakini siwezi kuishi na watoto wako, sikutaki na utaondoka. Hii nyumba nimejenga kwa jasho langu utaondoka au kama uking’ang’ania inaweza kuwa ni kaburi la wanao, sikutaki wewe na wanao.”


Nilimuambia taratibu kabisa na kutoka kuondoka, sikurudi tena mpaka kesho yake, nilikuta mke wangu anafungasha vitu vyake anaondoka. Alijaribu kuniomba msamaha lakini sikua tayari kwa hilo.


“Naweza kukusamehe lakini siwezi kuishi na wanao, sina mtoto na wewe, hata yule niliyekua nadhani ni wangu sidhani kama ni wangu tena. Nitapima DNA ila kwa sasa ondoka, sikutaki, najua siwezi kukufanya chochote ila hawa watoto nitawaua.” Mke wangu aliniangalia na kujua kuwa nilikua namaanisha, aliondoka na talaka zake kurudi kwao. Sikukaa hata miezi miwili niliiuza ile nyumba, niliancha kazi na kwenda Kigoma.


Lengo langu lilikua ni kumshitukiza Joan lakini nilipofika nilikuta kashapata mwanaume mwingine, wamefunga ndoa ya kiserikali na ana mimba yake. Miezi sita nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa, nilimaliza pesa yote, sikurudi hata kupima DNA ya mtoto wangu, nilikua naogopa. Mwaka jana nilibahatika kupata kazi sehemu nyingine maisha yangu sasa hivi kidogo nimazuri lakini bado sijapata ujasiri wa kumtafuta aliyekua mke wangu na kupima DNA. Joan naye hataki kabisa mawasiliano na mimi, matumizi ya mtoto natuma lakini nikipiga simu hazipokelewi hivyo sijui hata mwanangu anaendeleaje.


Baada ya kumpa talaka mke wangu hata hakurudi kwao, kuna nyumba alikua amejengewa na yule mwanaume, alihamia na sasa hivi ni kama kawekwa kinyumba. Mara kadhaa nakutana naye mjini akiwa na wanaume tofauti lakini hatusalimiani, naona kinyaa na kuna wakati najiuliza hivi alinipa nini mpaka kuvumilia utumbo wake wote. Anaonekana kabisa hajabadilika na hata tukikutana hajali chochote. Naumia sana kumuona na sasa hivi nafuatilia kazi nyingine Dodoma kwani nataka kuanza maisha yangu upya, hii ni mara ya kwanza kutoa yaliyonikuta katika maisha yangu kwani hata ndugu zangu hawajui ni sababu gani hasa zilinifanya kuachana na mke wangu.


***MWISHO

No comments

Powered by Blogger.