Header Ads

Header ADS

Simulizi: Safari sehemu ya tatu (03)



Basi vijana kazi waliitupa kando, dhana za kufanyia kazi, na kufanya


juhudi za kushibisha matumbo yao, kwani bila nguvu huwezi kufanya shuguri ya


kuchochea JAHAZI,ili kuweza kusonga mbele, walifakamia misosi kwafujo sana,


huku kauli yao pindi walipo pata nafasi ilikuwa ni "Nguvu Afya ndipo


Tuwajibike". misosi hiyo iliwafanya wapotoke, na kuto zingatia mda wakula,


walitumia mda mlefusana, kiasi mkuu wao akahisi kuna kuchelewa, kwani vyombo


vilianza kupunguza speed, huku kijana YOROBI akiwaita vijana wenzake kuja


kusaidia kuongoza, kwani aliona yakiwa na speed chache, lakini vijana hawa


kutaka kusikia licha ya kiongozi wao kutoa tamko kali juu yao, Baadhi ya


vijana waliitika wito lakini hawakuwa wote, wengine waliendelea na kunywa na


kula mikate, huku mabaki ya vyakula na makopo ya vinywaji, wakitupa kwenye


bahari hiyo. Waliijua kutupa kitu ndani ya bahari hiyo, kutaleta madhara,


lakini siku zote hakuna binadamu hasiye na kasoro, basi wengine walitupa chupa


za soda na bia, na mikate iliyobaki, hawakutazama kuwa kuna watumwa hawakupata


hata hicho walicho tupa, lakini siku zote mtumwa athaminiki, hata kuwe na kitu


gani, wafanya kazi wale watukutu, waliendelea hivyo hivyo, huku hawakujua


kama, vile vyakula na alufu ya pombe vina wavuta samaki PAPA ambao nao kwa


wingi sana, walianza kujaa kutapakaa chini ya vyombo vyao vya usafiri, ndani


ya ma jahazi hawakuwa na habari, kama wamesha nusa harufu na wako chini yao.


wao Waliendelea hivyo hivyo, huku PAPA wa bahari hiyo ijulikanayo (BAHARI


NYEUSI) walianza kuwa na hasira, kwani wengi wao siku hiyo hawakuwa wameona


chakula,kwamaana ile arufu ilizidi kuwatia hamsha hamsha, kwa namna vile


walivyo kuwa wakitupa baadhi ya mabaki ya chakula, ambayo hayakuwa mengi sana


kiasi chakuwatosheleza, papa wale, papa waligombeana chakula huku wakipigana,


mwisho PAPA walianza kukosa uvumilivu, na kuanza kuchomoza juu nakuludi chini,


huku vijana hao wakifurahia jinsi PAPA walivyokuwa wakiruka na kudumbukia tena


ndani ya maji.


Basi huruma iliwaingia vijana hao na ndipo kila mfungwa alipatiwa kipande cha


mkate, ili nao wapunguze njaa, kwani walionekana,hata chakula hawakupata kule


waliko toka, na huku matazamio yao kuwapelekaa tena kufanya kazi katika ngome


yao.


Kila mmoja alipata na wengine wali pewa nusu nusu, mikate hiyo kwani


haikuwatoshereza kwa wote, bila kulingana na vijana hao walitoa upendeleo, na


kuanza kuwagawia mabinti waliokuwepo, huku wakifatiwa na vijana walionekana


kuwa na vurugu mpaka wengine walikosaa, kipande hicho cha mkate.


Basi fujo ilipoonekana kuwa kubwa, kijana hodari YOROBI, alifika na kuituliza,


kwani nae alionekana kuwa katili hatari hasiye penda masihara, nae?... hao


papa vipiiiii watamwacha mtu salama ebu




 Fujo hizo zilipotulia , baada ya kijana YOROBI, alikuwa ametumia jitihada na akili mingi, japokuwa kichapo kilitembea


kidogo, kwa kila mtu aliyekuwa akileta jeuli, basi aliwatenga kwa makundi ambayo aliona kuwa yanaweza kutulia kwa mda mrefu,


na kuliko kuwaweka pamoja watumwa hao.


Basi walionekana kutulia pasipo shurutishwa, na YOROBI kwa mda mrefu aliwaangali kwa tahadhari, maana alijuwa kuwa,


matazamio yao walitaka kupata chochote, kwani wengi wao hawakula mikate hiyo, ndipo kijana mmoja aliyekosa mkate nae


alimuona binti mmoja mrembo BERALITA akiwa na mawazo mengi, amekaa kwautulivu, huku mkate akiwa kaushika tu! bila hata ya


kuula,tofauti nawenzake, ambao waliifakamia araka sana, basi mawazo yake kijana huyo ajulikanae kwa jina la MWAIPAMBA,


aliuwaza nakuutamani sana, mkate huo endapo, kwamba akiupata na kuula, atakuwa amepunguza njaa kwakiasi kikubwa, basi


alizingusha macho yake na kuwaza labda pengine wapo wengi waliokuwa, wakiupigia mahesabu mkate hule, wabinti mrembo mwenye


mawazo mengi, nikweli alimwona kijana mwingine nae akiwa anauangalia pia, na huku macho akiyapeleka zaidi mpaka kwa binti


BERALITA. YOROBI alikuwa pembeni hakujua kuwa kutakuwa na fujo itakayo tokea hivi punde, basi aliendelea kukiongoza chombo


vizuri, huku akiwasimamia wenzake na kuhakikisha chombo hakipatwi na misukosukooo yoyote.


BERALITA hakuwa akifahamu, yakuwa vijana waliokuwa pembeni yake walikuwa wakimtazama, na kuutamani mkate aliokuwa ameushika


kwaajili ya kuula. Hakuwa na hili wala lile binti BERALITA, akendelea na mawazo yake, maana alikuwa akiwaza mbali sana asa


juu ya kufika kwenye nchi yao, huku akipoteza hamu ya kula huo mkate, alivuta picha jinsi itakavyo kuwa pindi afikapo, yani


licha ya kuwa na njaa kali, lakini hakusikia kabisa njaa, na huku akiwazaaa mengi juu ya kufika walipo ambiwa wanapelekwa,


akiamini kabisa ni nyumbani kwao walipotokea miaka mingi iliyopita.


kijna MWAIPAMBA alishindwa kuvumilia kwa njaa aliyokuwa nayo, na ndipo kupatwa na kitu, na kujikuta akisimama na kuangalia


huku na kule, akaona kupo fresh akamwesabia bint huyu alie topea kwenye mawazo, huku akiludia kuangalia huku nakule, tena


kwa mara ya mwisho, asije kuwa kachelewa kufanya alichokusudia. MWAIPAMBA alinyata mpaka alipomkalibia BERALITA, na kugeuka


nyuma huku akiona wenzake wote wakim suport kwa ishala, kumbe walikuwa wana mfwatilia mipango yake, basi nae akapata nguvu


ya hajabu, kutokana na support hiyo yawenzake, huku matazamio yake ni mkate tu.Kijana MWAIPAMBA alimwangalia tena binti na


kujua basi yuko na mawazo chungu nzima, alipata nafasi ya kumwingia binti ili ampokonye mkate huo, hakuwa lahisi hivyo,hapo


hapo BERALITA alihisi kitu, na kufumbua macho na kutazama bahari, na kuona samaki wakiruka, akazani ndiyo kitu kilicho


mfanya machale yake kucheza, hapo akajinyoo sha viungo vya mwili wake, navyo vikalia kama vina vunjika,wakati akijinyoosha


viungo vyake,.


SOMA HAPA ENEO LIFAOLO KWA KUFANYIA BIASHARA


INAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.