Simulizi: kijiji cha wachawi sehemu ya sita (06)
Makongoro alizitazama zile nyama..ambazo zilikuwa zikitoka dam wakati wote..Hakika alijutia kwanini aliamua kwenda kumtembelea babu yake kijijini..maana laiti kama ningebaki zake mjini,basi hayo mambo yote yasingemkuta...Hivyo Makongoro akiwa ameyafumba macho yake..alikula zile nyama mbichi moja baada ya nyingine..na baada kumaliza alishushia na damu nzito iliyokuwa kwenye kikombe..wakati huo huo kwa mbali zilisikika sauti za watoto wakishangilia,,,sauti ambazo Makongoro hakuweza kutambua mahali zinapotokea.
Na Makongoro alipokuwa akiendelea kustajabishwa na zile sauti za watoto..mala ghafla mbele yake alitokea mkuu wa kichawi huku akiwa na jungu kubwa lililokuwa likifuka moshi mweusi...mkuu yule alitabasam baada kumwona Makongoro kafuzu mtihani wa kula nyama mbichi..hivyo moja kwa moja alimwamlisha anyooshe mkono wake,,nae Makongoro alifanya hivyo hivyo...ambapo mkuu yule wa wachawi alimshika mkono,kisha akasema
"Unaitwa nani..??"
"Makongoro.."
"Anhaa jina nzuri sana kijana..pia nikupe pongezi ya kufaulu huu mtihani mzito,,kwa Hakika wewe ni jasiri kupita kipimo na nakutabilia kwa siku za usoni wewe utatisha bala nzima la Africa....Lakini yote kwa yote..napenda Nikuulize maswali tofauti tofauti..na katika kujibu tamka neno..ng'onilo sawa kijana??.."
"Sawa" Aliitikia Makongoro hivyo huku akijifuta baadhi ya mabaki ya damu katika mdomo wake.
Na hapo ndipo mkuu yule wa wachawi alipo anza kumuuliza maswali mbalimbali Makongoro...na kati ya maswali hayo aligusia jinsi gani kijana ataweza kuilinda na kuiheshim kazi yake ya kichawi...nae kwa kujiamini Makongoro alijibu "Ndio nitailinda na kuiheshim"...Baada Makongoro kujiibu vizuri,ghafla kilitokea kitabu kikubwa kwa mkuu yule wa wachawi..na muda huo huo ulitokea msukule..msukule ule ulizipiga hatua mpaka kwa mkuu wa wachawi kisha akainama chini..ambapo uliweza kugeuka kuwa meza.
Hivyo mkuu yule wa wachawi akawa amekiweka kitabu juu ya mgongo wa msukule ambao umegeuka kuwa meza..kisha akamwita Makongoro ili asaini..Makongoro nae kwa kua kila kitu kigumu alikuwa ameshakivuka,,Hakika hakusita kwenda kusaini..alisaini kwa kujiamini kabisa..kwani baada kuinywa damu ile ya binadam nafsi yake iliingia dosari kidogo..dosari ya kutokuogopa kitu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na wakati hayo yakiendelea..upande mwingine nako..alionekana mchawi albino na mchawi gwimo wakizozana...badala ya kufanya kazi waliyopewa ya kulisha misukule kama moja ya adhabu waliyopewa na mkuu wao wa wachawi,,baada kuonekana wamegombana kinyume na sheria ya gambosh...hatimae walijikuta wakirudia kupigana..ambapo mchokozi alikuwa ni mchawi albino ambae hapo awali alionekana kuzidiwa uwezo na gwimo licha ya yeye kusifika kwa uhodari wa kupigana kichawi zaidi...hivyo lengo la mchawi albino ni kutaka kumnyoosha gwimo ili atunze heshima yake katika kijiji kile cha gambosh.
Hakika patashika nguo kuchanika mapigano ya nguvu yakiendelea katika nyumba ile ya kutunzia misukule..wakati huo misukule nayo ikilia njaa kiasi kwamba ilivunja milango na madirisha..kisha ikasambaa sehem mbalimbali..Huku ugomvi wa mchawi albino na gwimo bado ukiendelea kupamba moto,pasipo kujuwa kuwa wamesababisha balaa la misukule kutoroka.
Na ugomvi ule ilipokuwa ukiendelea...Kwingineko nako..mkuu wa wachawi alionekana kumkabidhi Makongoro hirizi tisa zenye ukubwa tofauti tofauti kisha akaondoka nae moja kwa moja mpaka kwenye Mkutano..ambapo alikuta maongezi mbalimbali yakiendelea katika ukumbi ule wa wachawi..na hivyo baada mkuu kutokea,hatimae kimya kizito kilitawala huku wachawi wale wakijiuliza chipkizi wengine wako wapi mpaka mkuu arudi na chipkizi mmoja ambae ni Makongoro..lakini maswali yao kabla hawajayapatia majibu,,mala ghafla mkuu yule wa wachawi alipasa sauti akisema "Kwanza kabla ya yote,,ebu mpongezeni kijana huyu Mdogo kwa kile alicho kifanya..kwa Hakika huyu ni kijana jasiri natumai siku za karibuni atatisha sana" Alisema mkuu yule wa wachawi..ambapo hapo kelele za wachawi wakimpongeza Makongoro zililindima kila kona ya ukumbi..ila kasoro mtu mmoja tu hakuweza kumpongeza Makongoro..ambae nae si mwingine ni mwalimu shija...
Hivyo mala baada pongezi kumfikia Makongoro..hatimae mkuu yule wa wachawi alielezea aina ya chakula alichopewa Makongoro kama moja ya mtihani.. Hakika wachawi wote walibaki midomo wazi...wakati huo Mzee baluguza akimtazama mjukuu wake na kisha kusema "Inaamna supu ya macho mbaya..ila nyama mbichi tena ya sehem ya Siri ndio tamu??...Hahahaaaaa kweli mjukuu ninae..pole yao Mzee mwakipesile" Hakika Mzee baluguza alisema hivyo huku akiachia tabasam pana.
Hivyo baada ya hayo mkuu wa wachawi..alitaka kufunga kikao..lakini kabla hajafunga,ghafla Bibi mmoja alietokea nchini Congo ambae nae alimpeleka mjukuu wake gambosh ili apewe uchawi..alisimama na kisha kuhoji mahali alipo mjukuu wake pamoja na wenzake..
"Wameshindwa mtihani..kwahiyo sheria yetu inasema mtu yeyote akiferi mtuhani..hastahili kurudi katika jamii ya watu wa kawaida kwa maana atavujisha Siri" Kwa sauti Kali...mkuu yule wa wachawi alimjibu bibi kizee...ambapo nae baada kusikia maneno hayo aliangua kilio kikubwa huku akilitaja jina lamjukuu wake..
Wakati huo huo mkuu yule alifunga kikao kisha akatoweka..
Na baada mkuu wao kuondoka!?..Mzee baluguza alizipiga hatua kumfuata mjukuu wake alietunukiwa jopo la hirizi na uchawi wa kutosha...hivyo moja kwa moja walijikusanya pamoja kama walivyotua katika ardhi ya gambosh..lakini kati yao alipungua mmoja ili watimie therathini ...ambae ni gwimo..kwahiyo haraka sana harakati za kumtafuta zilifanyika..lakini hakuweza kumpata..na hivyo mkuu wa msafara alichukua kisu chake kidogo..ambapo kufumba na kufumbua kiligeuka kuwa ndege..wote walipanda hatimae safari ya kurudi Tanzania ikaanzaa baada kukaa gambosh kwa siku mbili......Hivyo ndege ile ya kichawi baada kufika sumbawanga ilitua chini..ambapo walishuka Mzee baluguza na mjukuu wake kisha kila mmoja akachukua ungo..na safari ya kurejea kijijini bhonde iliendelea,,wakati kijiji kilikuwa kimechafuka wakimtafuta Mzee baluguza kwa udi na uvumba ili wamuuwe baada kugundulika kuwa yeye ndio alie husika na kifo cha mama chiku..mama muuza pombe alieuwawa kikatili kwa kukatwa shingo na Mzee baluguza..wakati huo huo Mzee kinono nae alikuwa akimuwinda Makongoro ili amteketeze.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzee baluguza akiwa na mjukuu wake ndani ya ungo wakirudi kijijini baada kutoka gambosh..ghafla walishtuka walipoona moto ukiwaka kwa mbali katika kijiji chao cha bhonde...hivyo moja kwa moja Mzee baluguza Alimtazama mjukuu wake ambae alikuwa pembeni yake kidogo,kisha akasema "Makongoro jiandae,,maana moto ule unao uona si bure"
Alisema Mzee baluguza huku akijifunga vizuri hirizi yake kwenye mkono wake...ambapo nae Makongoro alifanya hivyo hivyo...na baada ya dakika kadhaa,walitua chini nje kidogo na nyumba yake Mzee baluguza...ambapo baluguza na mjukuu wake,kwa pamoja walichuchumaa style ya kupiga magoti mfano ya wanariadha,,punde si punde walipotea nje,wakatokea ndani.
Hakika kitendo kile kilimfrahisha sana Makongoro...akajikuta akitabasam huku akimtazama babu yake,ambapo nae Mzee baluguza aliachia tabasam kama vile alivyofanya mjukuu wake,kisha akasema "Naam Makongoro kazi nzuri...Sasa kama wanajiamini wachokoze moto huu" Alisema Mzee baluguza akionekana kujiamini kabisa.
"Hahahaaa babu bwanaa sawa mimi niko sawa kila idara" Makongoro alijibu hivyo huku akipiga kifua chake kuonyesha kuwa yupo sawa kwa lolote kwa chochote.
"Sawa mjukuu wangu nenda kalale ila kumbuka kesho pasaka,,hivyo mchana tutajumuika pamoja kufrahia sikukuu,ila usiku tutaelekea buharamulo kwenda kula chakula chetu cha kichawi"
"Sawa babu nimekuelewa..usiku mwema" Makongoro alimjibu babu yake kisha akaingia chumbani kwake.
Wakati hayo yakiendelea,upande ule ambako ilionekana moto..walionekana wachawi wa kijiji cha bhonde wakiimbana kucheza huku wakiwa uchi,,wakati huo pembeni yao likionekana jungu kubwa lililokuwa limejaaa nyama za binadam likiwa juu ya mafiga...hivyo baada kuimba na kucheza kwa muda mrefu,hatimae mkuu wa hafra ile ya kichawi alistisha ngoma kisha akasema "Jamani tumefrahi vya kutosha..tukiimba na kucheza ila kwa sasa ni muda wa kula kitoweo kilicho andaliwa mahususi kwa siku ya leo" Kwisha kusema hivyo mkuu yule wa hafra ambae aliitwa Mzee dole tupu,,ghafla kelele na moyowe ya wachawi zilisikika kila pande...huku mirunzi kadha wa kadha nayo ikifuatia...bila shaka hiyo yote ilikuwa ni furaha ya kusikia jina kitoweo.
Mkuu wa hafra alimteua Mzee sule ndio awe mgawaji wa chakula...hivyo Mzee sule aliweza kuifanya kazi ile kwa umakini zaidi..nacho chakula kile zilikuwa ni nyama za binadam.
Baada wachawi wale walipomaliza kula chakula chao,,hatimae mkuu wa hafra aliwataka waondoke majumbani mwao...lakini kabla hawajasambaa,mala ghafla alikuja popo katika sherehe ile..popo huyo alitua moja kwa moja kwenye bega la Bi kileleganya ambae muda wote mwanzo mpaka mwisho wa sherehe alikuwa kakaa pembeni akiwatazama wachawi wake jinsi wanavyo frahia sherehe..
Hivyo baada popo yule kutua kwenye bega la Bi kileleganya....hima alisimama kisha akasema "Natumain wote kwa pamoja mmefurahi sana..lakini furaha yenu hii isiwafanye mjisahau kujilinda.." Alisema Bi kileleganya kisha akameza mate..lakini kabla hajaendelea,mala ghafla ilisikika sauti ya mmoja ya wachawi,,sauti hiyo ilisikika ikisema " Unamaana gani mkuu" Kwisha kusema hivyo yule mchawi..wachawi wenzake walimtazama kwa jicho baya..huku kwa kunong'ona ilisikika sauti nyingine ikimjibu "We kaa kimya..usirudie tena kuongea wakati mkuu hajamaliza kuongea" Alionywa hivyo yule mtu..ambapo nae aliomba radhi huku akionekana kuwa na hofu..lakini Bi kileleganya,licha ya kuisikia ile sauti..ila hakuweza kudili nayo kwani alijuwa ni presha iliyomkamata mchawi wake...hivyo aliendelea na kitu alichotaka kuongea.." Jamani naombeni nisiwachoshe...ila ninacho wataka ni nyinyi kuwa makini..maana Mzee Baluguza karudi..." Alisema kwa msisitizo Bi kileleganya huku akiwakodolea macho wachawi wake..ambao nao walionekana kupigwa na butwaa baada kusikia jina Baluguza.
Na wakati wachawi wale wakiwa katika dimbwi la wasiwasi...mala ghafla Bi kileleganya alimwita Mzee mwakipesile,kisha akamwambia " Mwakipesile fanya kazi yako sasa ya kutuletea yule mjukuu wa Mzee baluguza kwenye familia yetu..Sawa sawaa??.."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sawa mkuu..." Kizee mwakipesile alijibu kwa heshima..
"Haya mnaweza kurudi majumbani kwenu" Aliongeza kwa kusema hivyo mkuu yule wa wachawi kijijini bhonde..ambapo yeye ndio alikuwa wa kwanza kupotea maeneo yale,,kisha wengine wakafuatia..punde si punde wote walipotea.
Usiku uleule kabla hapajakucha...Gambosh nchini Nigeria..Mchawi albino na mchawi gwimo..walijukuta wakiwa katika wakati mgumu baada kukutwa wakigombana...wakati huo wakisababisha misukule kutoroka.
Katika chumba mahususi kwa niaba ya mateso..walipelekwa wachawi wale..lakini kwa kuwa mchawi albino alikuwa akijiamini kwa sababu ya kuwa na nguvu nyingi za giza,hatimae alipinga mateso ambayo angeyapata..kitendo kilicho mkera mkuu wa kitengo cha mateso..ambapo aliamulu kuwa mchawi albino abebe naaadhabu ya gwimo....hivyo gwimo nae alibadishiwa adhabu..ambapo alipelekwa shambani kulima.
Hakika gwimo alilima sana siku hiyo...istoshe alipokonywa nguvu zake za kichawi...hivyo akawa analima yeye kama yeye..
Wakati huo katika chumba kile cha mateso ilikuwa patashika nguo kuchanika,,ugomvi Kati ya mchawi yule albino na mkuu wa kitengo cha mateso...kwani mchawi albino alionekana kupinga mateso,,na hivyo ikawa imefikia hatua ya kupigana.....Lakini wakati wakiwa katika mapigano,,mala ghafla alitokea mkuu wa wachawi Africa nzima...Mkuu yule alionekana mifupa tu bila ngozi wala nyama za mwili..ambapo mkuu yule wa wachawi kwa kutumia rupia yake aliyokuwa nayo mkononi...aliizungusha kwa kuipitisha katikati ya vidole vyake...wakati huo mchawi albino alikuwa akiishiwa nguvu kila sekunde zilivyozidi kwenda...mwishowe kabisa akinyong'onyea kabisa..ambapo alifungwa nyororo kisha akavuliwa nguo mwili mzima..na punde si punde baada kufungwa mnyororo,ghafla alitokea mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitano..mtoto yule alizipiga hatua kuelekea mahali alipokuwa mchawi albino akiwa katika fundo za nyororo..Hivyo baada kumfikia...mtoto yule alinyoosha mkono wake juu..punde si punde Katika mkono wa yule mtoto ilitokea bakuli kubwa na mkasi mdogo mkali.....mtoto yule alicheka kwa sauti Kali iliyoambatana na mwangwi mkali,,na mala baada kumaliza kucheka,aliuchukua mkasi kisha akaanza kukata kiungo kimoja baada ya kingine kwenye mwili wa mchawi albino,,ambae nae alipasa sauti Kali ya kuhisi maumivu.
Wakati huo kijiji bhonde..wachawi wote waliingiwa na hofu baada kusikia habari za Mzee baluguza...lakini hali hiyo ilikuwa tofauti kwa Mzee kinono..kwani baada kusikia kuwa Mzee baluguza karudi,haraka sana alichukua ungo wake,kisha akapaa kumfuata nyumbani kwake kwa lengo la kwenda kumuuwa Makongoro..mjukuu wa Mzee baluguza..pasipo kujuwa kuwa Makongoro nae kapewa uchawi.
Angani saa za usiku..alionekana Mzee kinono akiwa ndani ya ungo akisafiri kumfuata Makongoro kwa nia ya kulipa kisasi...kwani ikumbukwe kuwa Makongoro alimpa paka jiwe,,pasipo kujuwa kuwa paka yule alikuwa ni mtoto wa Mzee kinono..Na Hivyo kitendo kile kilimkela sana Mzee kinono,,mpaka akaamuwa kujenga chuki dhidi ya Mzee baluguza ambae ni babu yake Makongoro.
Lakini kabla Mzee kinono hajatua kwenye nyumba ya Mzee baluguza,,mala ghafla ungo wake uliyumbishwa..Mzee kinono alishtuka baada kuona hali ile..Hivyo alichukua kibuyu chake kidogo alichosafiri nacho,pia akachukua na kipisi cha mkia wa ng'ombe..ambapo mkia ule aliuchovya kwenye kile kibuyu chake kilichokuwa na damu kisha akanyunyuzia kila pande kuu ya dunia.
Na mala baada Mzee kinono kufanya hicho kitendo...haraka sana alifungua mkoba wake chakavu,kisha akatoa hirizi kubwa,,hirizi hiyo alijifunga kwenye mkono wake huku akiongea maneno ya kichawi....ambapo punde si punde ungo ulitulia.
"Mimi ndio mfalme wenu pumbafu zenu" Alijigamba hivyo Mzee kinono baada kufanikisha kuutuliza ungo wake kwenye ramani sahihi..wakati huo kwa mbali walionekana wachawi wengine wakielekea kule alikitoka Mzee kinono,,lakini cha ajabu wale wachawi waligeuka na kisha kumfuata Mzee kinono kwa kasi ya ajabu..
Kwa hakika Mzee kinono nae baada kujishtukia kuwa anafuatwa na wachawi nyuma yake..hima nae aliongeza kasi ili kuwakimbia wale wachawi ambao walionekana kuwa na uwezo mkubwa kuliko yeye.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hivyo wakati hayo yakiendelea...upande mwingine nako Makongoro nae alipokuwa amelala kitandani..mala ghafla alishtuka kutoka usingizi baada kusikia sauti ikimwita.....sauti hiyo haikuwa ya mtu mwingine bali ilikuwa sauti ya mkuu wa wachawi..ambapo Makongoro baada kuifaham ile sauti aliondoa hofu mwili,alisimama kando ya kitanda chake kisha akakaa tayali kumsikiliza mkuu wake anasemaje,,
Na wakati Makongoro alipokuwa kimya,,akimsikiza mkuu wake ili aseme neno..ghafla chumbani kwake ulitokea mwanga mkali...mwanga huo kabla haujatoweka mle chumbani..ulitokea mkono bila kiwiliwili,mkono huo ulikuwa umeshikilia hirizi ukimpatia kijana Makongoro.
Makongoro bila wasiwasi aliizipiga hatua kuifuta ile hirizi...Na mala tu alipo ishika ..sauti ya mkuu wa wachawi ilirudia kusikika ikisema "Makongoro hiyo ndio kila kitu kwako..Sema kitu chochote cha kichawi utakipata...Hivyo itunze itakusaidia" Kwisha kusema hivyo..ile sauti ilipotea,na mwanga ule mkali nao ulizimika..ambapo Makongoro nae alijifunga vizuri ile hirizi kwenye mkono wake kisha akarudia kitandani kulala..
Ils la kabla usingizi haujamkamata..ghafla ile hirizi aliyokuwa ameivaa mkononi ilianza kumbana kiasi kwamba akashindwa kulala..akawa amekaa kitandani tu....Na wakati huo huo. Mzee kinono tayali alikuwa ameshatua kwenye nyumba ya Mzee baluguza..ambapo baada kutua..Makongoro akiwa chumbani kwake alisikia mshindo,hivyo alisimama kutoka kitandani kisha akachukuwa nguo yake nyeusi ambayo alijifunga kiunoni..na moja kwa moja alizipiga hatua kuelekea kwenye kona ya chumba chake kisha..punde akawa amepotea akatokea nje.
Mzee kinono baada kumwona Makongoro alicheka sana kwa dharau na kejeli,,na baada kumalizika kucheka alisema "Eti na wewe unatuiga sisi??..sasa acha nikionyeshe ili utambue kuwa uchawi na ugolo ni vitu viwili tofauti" Alisema Mzee kinono akimaanisha kuwa Makongoro hana uchawi,bali anaugolo kwa sababu ugolo na uchawi vinafanana.
Hivyo Mzee kinono baada kusema hayo alirusha kombola moja la kichawi kuelekea mahali alipokuwa Makongoro..lakini cha ajabu Makongoro alipotea akatokea nyuma yake Mzee kinono..kitendo ambacho kilimshangaza sana Mzee kinono kwa uwezo ule aliouonyesha kijana Makongoro.
Ila licha ya Mzee kinono kushangazwa na uwezo ule wa Makongoro..kwa Hakika hakutaka kushindwa,,zaidi aligeuka nyuma yake alipokuwa amesimama Makongoro ambae nae alikuwa akicheka mfano wa mtu anaetekenywa.
Na mala baada Mzee kinono kumgeukia Makongoro..safari hiyo hakumrushia kombola,bali alimrushia moto wa kichawi..lakini moto ule kabla haujampata Makongoro..ghafla Makongoro aliunyoosha mkono wake wa kushoto uliokuwa na hirizi aliyopewa gambosh...punde si punde moto ule alio urusha Mzee kinono uliganda kisha ugeuzwa ukawa maji.
"Mmmh" Mzee kinono aliguna asiamini kama kweli Makongoro ndio anaeyafanya Mambo yale..wakati huo akijiandaa kumkimbia kabla kijana hajajibu mashambulizi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na haikuchukuwa muda Mzee kinono alipotea akatokea nyumbani kwake. ..ambapo baada kufika,moja kwa moja alichukua jungu lake lililokuwa na makorokoro ya kichawi kisha akaenda nalo mpaka sebleni kwake huku akijiuliza "mtoto yule uchawi mkali vile kautoa wapi??..Daah hapana mimi kinono bwana miaka dahali nipo kwenye uchawi,sasa iweje mtoto mdogo kabisa anishinde??...
ITAENDELEA
.jpeg)
No comments