Header Ads

Header ADS

Simulizi: kijiji cha wachawi sehemu ya tano (05)



Baada Mzee baluguza kupotea maeneo Yale..muda huo huo alitua Mzee kinono akiwa sambamba na ungo wake..Mzee kinono alionekana kumfukuzia Mzee baluguza lakini kwa bahati mbaya hakumkuta.."Daah huyu Mzee baluguza anauchawi wa nchi gani!? ila ipo siku tutakutana tu"


Alisema Mzee kinono...Mzee ambae alikuwa na bifu kali na baluguza...hivyo kwisha kusema hatimae,nae alipotea.




**********


Asubuhi ilipopambazuka ngoma ya kuashilia msiba iliskika kijijini bhonde...Masikio ya wanakijiji yalitega vizuri ili waweze kuskia jina la mtu aliefariki kutoka kwa mtoa tangazo...nae mtoa tangazo la msiba hakuweza kusita kumtaja...nae hakuwa mwingine ni mama chiku.


Hakika wanakijiji walio isikia hiyo taarifa walionekana kustaajabu lakini kwa wale ambao walikuwa wachawi hawakuweza kushangazwa na kifo cha mama chiku kwani walijua sababu iliyomsababishia umauti.


Wanakijiji walijazana nyumbani kwa mama chiku kwa niaba ya mazishi..lakini kabla mwili wa mama chiku haujapelekwa kuzikwa,,mala ghafla alitokea Bi kileleganya ambae ni kiongozi...Na kitu ambacho alikifanya Bi kileleganya ni kuuzuia ile mwili wa mama. chiku usizikwe badala yake ukawe kitoweo kwa familia ya kichawi pamoja na misukule.


Hivyo Bi kileleganya kwa nguvu kubwa ya kichawi aliunyakua ule mwili wa mama chiku,,kisha akaweka mti wa mgomba..mti ambao kama huna macho ya kichawi huwezi kuugundua.


Mazashi yalifanyika..wanakijiji baadhi wakijua wamemzika mama chiku na wengine ambao walikuwa wachawi walijua dhahili shahili wamefukia mgomba wa ndizi.


Hivyo baada ya mazishi kumalizika...walionekana vijana watano wakikaa kikao cha muda mfupi..kikao hicho ambacho walijadili kufanya upelelezi ili kumpata mtu aliehusika na mauaji ya mama chiku...Hakika vijana wale ambao nao kiuchawi walikuwa si haba walikubaliana kulifanyia kazi hilo suala..na kisha wakashikana mikono wote kwa pamoja,wakawa wamepotea mfano wa taa izimikapo gizani.


Wakati vijana wale watano wakipanga kufanya upelelezi wa mauaji ya mama chiku...upande mwingine,,Wazee wateule wakishirikiana na serikali yakijiji walikaa pamoja kujadili mauaji ya kikatili yaliyofanyika kijijini kwao..ambapo walikubaliana kumuunguza ndani ya nyumba mtu atakae bainika kuhusuka na mauaji ya mama chiku.


Taarifa hiyo iliweza kumfikia chinichini Mzee baluguza ambae ndio muhusika...cha ajabu baluguza alicheka kwa dharau kisha akasema.."hii tayali imeshakuwa VITA ..sikutaka kumfundisha uchawi mjukuu wangu Makongoro lakini imebidi la sivyo Nitamkosa...ngoja leo usiku nimpeleke gambosh...hakuna namna"


Alijisemea maneno hayo Mzee baluguza huku akiungojea usiku kwa ham ili ampeleke mjukuu wake gambosh nchin Nigeria ili nae aweze kujilinda katika kijiji kile kilicho sheheni wachawi.




Hatimae usiku uliingia...ambapo siku hiyo familia ya Mzee baluguza...yaani Bi Mazoea ambae ni mke wa Mzee baluguza na mjukuu wao ambae ni Makongoro walilala mapema kwa sababu kijiji kilionekana kuchafuka baada kifo kile cha mama chiku ambae alikatwa shingo na Mzee Baluguza.


Hivyo saa Sita usiku ilipotimia..Mzee Baluguza alinyanyuka kutoka kitandani kwake,kisha akaingia uvunguni ambako alitoka na chungu chake alichokuwa akihifadhia mazagazaga ya kichawi...alikikamata kile chungu kwa mikono yake miwili..kisha akizipiga hatua kuelekea chumbani kwa mjukuu wake ambae ni Makongoro ,,wakati huo Makongoro alikuwa amelala fofofo.


Mzee Baluguza baada kuingia chumbani kwa Makongoro...alimwamsha nae Makongoro aliamka.


Baada Makongoro kuamka..Mzee Baluguza akimtazama mjukuu wake usoni kisha akasema "Nakuomba ufumbe macho yako..usifumbue mpaka nikuruhusu" Alisema Mzee Baluguza ,,wakati huo akimfunga hirizi mjukuu wake. Mara baada kumalizika zoezi lile,hatimaye Mzee Baluguza alimwambia Makongoro asimame.Makongoro alisimama huku akijiuliza babu yake anamaana gani kumkatisha usingizi na kisha kumfanyia Mambo Yale.


"nakuomba usifumbue macho...ukifumbua kabla sijakuruhu shauli yako..." Alisisitiza Mzee Baluguza akimwambia mjukuu wake.


Hivyo baada kumaliza hayo,,Mzee Baluguza alimwambia Makongoro amkumbatie..Makongoro alimkumbatia,ambapo punde si punde alijikuta wapo nje ya nyumba.


Mzee Baluguza alinyoosha mkono wake wa kulia,,ghafla kikatokea kibuyu chake kidogo ambacho ndani yake kilikuwa na damu, alikunywa damu ile iliyo kuwomo ndani ya kile kibuyu...Kisha akarudia kumwambia Makongoro "usifumbue macho macho,pia nikumbatie vizuri usiniachie" Makongoro alifanya hivyo.


Kwisha kusema hayo,walipaa angani...safari ya kuelekea gambosh ikawa imeanza.


Wakati walipokuwa angani...Makongoro alihisi baridi Kali pamoja na upepo mkali,,kitu ambacho kilimfanya kutaka kufumbua macho ili angalie yupo katika mazingira gani...lakini kabla Makongoro hajaifkia macho yake...ghafla alijikuta wametua aridhini...na hivyo Mzee baluguza alimruhusu Makongoro kuyafumbua macho yake.


Makongoro alishtuka baada kufumbua macho yake..kwani aliwashudia wachawi wapatao therathini ambao mavazi yao yalifanana na mavazi aliyoyavaa babu yake.


"Babu kwani hapa wapi" Alihoji Makongoro akimuuliza babu yake...Lakini cha kushangaza Mzee baluguza hakumjibu chochote mjukuu wake. Wakati huo ilisikika sauti kutoka ndani ya wachawi wale therathini ikisema "Jamani tuondokeni tayali tumetimia"


Ilisikika ikisema hivyo ile sauti,,ambapo iliweza kuungwa mkono na wachawi wote waliokuwa wamekusanyika pale rukwa kwa niaba ya safari y kuelekea gambosh.


Hivyo baada wazo hilo kuungwa mkono na jopo lile la wachawi...punde si punde alitokea mtokea Mzee mmoja ambae aliitwa mahulubila...ambapo baada kutokea Mzee yule..haraka sana alichukua kisu kidogo ambacho muda wote alikuwa nacho mfukoni...kisha akatia dam kile kisu,,,wakati huo huo akawaambia wachawi wenzake wafumbe macho.


Baada kumalizika Mambo yake,aliwaambia wafumbe macho..


"waoooo....ndege?.." Alisema Makongoro huku akitabasam baada kuiona ndege..


Ruksa ilitoka kwa Mzee Mahulubila..akiwaambia wachawi wenzake waingie ndani ya ndege ile ya kichawi,kwa niaba ya kuelekea gambosh kwenye chimi chimi ya uchawi.......Mzee baluguza alimshika mkono mjukuu wake,,wakazipiga hatua kuelekea ndani ya ndege..wakati huo Makongoro akionekana kuwa na shauku kubwa ya kuipanda ndege ile ambayo ilitokea kimazingala.


Hatimae ndege ile ya kichawi ilipaa angani..wakati huo ikiwa haina sauti yoyote......Na wakati ndege ile ilipokuwa bado ipo angani..Mzee baluguza alimgeukia mjukuu wake ambae msamaha wote alikuwa akitabasam kupanda...Mzee baluguza akasema "huku tunakokwenda...nakuomba uwe makini sana!! ukiona kitu usikikodolee macho sana pia maswali yako ya kipuuzi siyataki..vilevile chakula chochote au kinywaji ukipewa tumia..tofauti na havyo utafia huku huku"


Aliongea hivyo Mzee baluguza..maneno ambayo yalimnyong'onyesha Makongoro akiwa haelewi babu yake anampeleka wapi na pia kufanya nini na japo lile la wachawi..


Wakati Makongoro akiendelea kujiuliza bila kupata jibu,mala ghafla ndege ile ya kichawi ilianza kuyumba yumba..Na punde si punde nyuma ulizuka moto




Moto ule ulienea kwenye ile ndege ambayo ulikua imepakia jopo la wachawi...wakati huo Makongoro alikuwa akipiga kelele kuomba msaada...lakini kelele zake Makongoro zilifikia tamati baada Mzee baluguza kumziba mdomo..wakati huo huo mmoja wa wachawi waliokuwemo ndani ya ile ndege,alionekana kuzipiga hatua kuelekea mahali alipokuwa Mzee baluguza ambae alikuwa akihaha kumziba mdomo mjukuu wake ili asipige kelele.


"Mzee mwanzangu huyu nani yako??...maana anavyo onekana ni mgeni katika safari hizi.." alisema yule mchawi ambae alionekana kuwa na cheo frani katika kazi ile ya kichawi.


"Mmh huyu bwanaaa...ni mjukuu wangu..ila kwa kua kijijini kwetu wamecharuka kutaka kumuangamiza?? hivyo nimeona heri nije nae huku ili na yeye aweze kujilinda dhidi ya maadui zake.." Alijibu Mzee baluguza.


"Anhaa jambo jema Mzee mwenzangu,sina la ziada"


Kwisha kusema hivyo,,hatimae ndege ile ya kichawi ilitua chini...ampapo mkuu wa safari aliinyoshea kidole ndege..ghafla ikageuka kuwa kisu kama ilivyokuwa awali kabla ya kugeuka kuwa ndege.


Wakati huo huo walionekana binadam wawili wa kutisha,,ambao mmoja alikuwa na jicho moja katikati,na mwingine hakuwa na maskio...wote walikuwa wamevaa koti nyeusi ambazo zilikuwa na kofia zake..hivyo watu wale walipiga hatua kuelekea mahali walipokuwa Makongoro pamoja na jopo nzima la wachawi aliotua nao.


"Babu hao ni akinanani??.."


"Shiiiiiii kaa kimya" Alijibu hivyo kwa kunong'ona Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake baada kuulizwa kuhusu wale watu waliokuwa wakiwafuata.


"Karibuni" Wale watu walisema huku wakiambaa kuelekea kwenye jengo kubwa ambalo mlangoni ilionekana nembo ya kichawi..na chini ya hiyo nembo yalionekana maneno ambayo yaliandikwa kwa rugha ya ajabu ajabu...ingawa baada kuingia ndani zaidi,Makongoro aliliona jina gambosh katika koldo moja ndani ya ile nyumba..na hapo ndipo alipo faham kuwa tayali wametua katika ardhi ya gambosh. 


Hivyo wale watu walionekana kutisha kwa upande wa Makongoro,walizidi kupiga hatua huku Makongoro na babu yake pamoja na wale wachawi wengine wakiwafuata nyuma...mwishowe walifika katika ukumbi mkubwa ambao ulikua umesheheni watu wa kila aina.


Makongoro walipigwa na butwaa baada kuwaona wachawi wale..alitamani kumuuliza babu yake kisa kilicho wafanya watu wale kufulika kiasi kile katika ile ukumbi,,lakini aliogopa kwa sababu babu yake alisha mkataza kuuliza uliza maswali....Wakati ule ule mbele yake Makongoro..alikiona kiti ambacho kilikuwa kiking'aa mfano wa almasi...Na katika kiti kile,alitokea mtu mmoja ambae kimwonekano alikuwa na jinsi mbili tofauti..kwani hata sauti aliyopasa ilisikika mala mbili,yaani ya kike na yakiume..vile vile yule mtu katika kifua chake alionekana kuvaa cheni zenye nembo ya mafuvu.


Aliogopa Makongoro baada kumwona yule mtu ...alitamani kumuuliza babu yake kuhusu yule mtu,,lakini mwendo ule ule alisita baada kukumbuka kuwa babu yake hataki maswali.




Kimya kilitawala katika ukumbi ule..na ghafla ilisikika sauti ndani ya ule ukumbi,,ukumbi ambao ilikuwa umejaza wachawi mbalimbali pamoja na binadam wa kila aina..sauti hiyo ilisema.."Wote simameni na kisha tuungame kabla hatujaanza kuyadadavua masuala yaliyotukutanisha mahali hapa.." Ilisema hivyo ile sauti..sauti ambayo ilisikika katika jinsia mbili,ya kike na ya kiume...


Hivyo wachawi wale walifanya kama amli ilivyosikika...kasolo Makongoro ambae hakusimama ingawa nae alishikwa mkono na babu yake akimtaka asimame kama wengine walivyo fanya...


Baada kumalizika kuungama..wot kwa pamoja walikaa chini..na hiyo ikawa nafasi pekee ya Makongoro kutazama kila pande katika ukumbi..akiwa bado katika kutazama tazama,,mala ghafla alishtuka baada kumwona mwalimu wake wa hisabati ambae aliitwa shija..nae akiwa miongoni mwa wachawi waliokuwemo ndani ya ule ukumbi..Makongoro alijiuliza ni vipi mwalimu wake atoke Dar es salaam ambako anafanya kazi,moja kwa moja aonekane gambosh?? Na hapo ndipo Makongoro alipokumbuka kuwa mwalimu huyo alishahusishwa na tuhuma za kichawi,,ila zikawa zimeishia chini chini....na hivyo Makongoro akawa amefaham kuwa mwalimu shija ni mchawi kama alivyokuwa akituhumiwa na wanafunzi wa shule mwenge..shule ambayo mwalimu hiyo alikuwa akifundisha pia Makongoro nae akiwa miongoni mwa wanafunzi wa shule hiyo.


Makongoro aliduwaa huku akimtazama vizuri mwalimu yule...wakati huo huo shija nae aligeuka upande aliokuwa Makongoro...na hivyo wakawa wamekutana uso kwa uso...kitendo ambacho kilimfanya shija kurudisha uso wake kama awali baada kumwona Makongoro ambae alikuwa ni mwanafunzi wake "Mmh huyu Makongoro kafikaje fikaje huku??.. na bila shaka atakuwa kanijua...na kama kweli kanijuwa,,hakika nitafanya juu chini ili nimwangamize kabla unga haujazidi maji" Alisema shija baada kuingiwa na hofu kuhusu Makongoro.




Na wakati hayo ya Makongoro pamoja na mwalimu wake ambae ni shija...alipokuwa yakiendelea,upande wa pili nako yule mtu mwenye jinsi mbili tofauti...aliendelea kuzungumza Mambo mbalimbali kadha wa kadha..na katika mambo hayo ilikuwemo suala nzima la kugawa uchawi kwa watakao hitaji..kisha akaomba majina ya watu wanao hitaji na aina gani ya uchawi unaotakiwa.


Kwisha kusema hayo kengere ililia,,kuashilia kuwa umefika muda wa kula chakula...hivyo mtu yule ambae alikuwa akiendesha Mkutano ule wa kichawi..aliwaruhusu wachawi wake wakale Kwanzaa chakula kisha waendelee na Mkutano..ambapo Mzee baluguza alimshika mkono mjukuu wake,moja kwa moja walielekea kwenye chumba mahususi kwa kulia chakula..Chumba ambacho kila kona ilisikika harufu ya dam za binadam.


"Chochote utakacho letewa kula wala usiohope...na pia ukienda kuchukuwa uchawi kwa yule kiumbe,,Naomba uchukuwe uchawi wa kujilinda na kuua..Sarawak??.." Mzee baluguza alimwambia hivyo mjukuu wake kwa msisitizo... huku wakiwa tayali wameketi kwenye viti ambavyo vilitengenezwa kwa kutumia mifupa binadam pamoja na ngozi ya Chui..


Hivyo Makongoro baada kuambiwa vile na babu yake,aliitikia kwa kichwa..wakati huo huo alionekana binti mzuri ambae miguu yake ilikuwa kama mbuzi..binti yule akiwa na bakuli mbili mkononi,,alizipiga hatua kuelekea kwenye meza ambayo walikuwa wapo Mzee baluguza pamoja na Makongoro.


Hivyo binti yule baada kuifikia meza ile..aliwapa zile bakuli baluguza na mjukuu wake...ampako Mzee baluguza aliufakamia kwa pupa mchuzi uliokuwemo ndani ya bakuli yake....wakati huo Makongoro nae alipo ingiza kijiko chake kwenye mchuzi katika bakuli lake...ghafla alistisha baada kuona kiganja cha macho ya binadam yakielea kwenye ule mchuzi.


"Lazima ule la sivyo hutoki huku..."


Alisema Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake...baada kumwona akiogopa kuyala yale macho ambayo ni chakula maalum kilicho andaliwa kwa niaba ya wachawi watakao hudhulia Mkutano gambosh.




Makongoro aliyatazama yale macho yaliyokuwa yakielea kwenye mchuzi ndani ya bakuli..kisha akamtazama na babu yake ambae alionekana kula chakula kile bila wasiwasi...ghafla mate yalimjaa Makongoro mdoni,,akahisi kichefuchefu....na punde si punde alitapika..kitendo ambacho kiliwafanya wachawi wote waliokuwemo ndani ya chumba kile kusimama huku wakikodele macho meza ambayo alikuwa kakaa Mzee baluguza na mjukuu wake ambae ni Makongoro.


"Nani huyo ambae anafanya ujinga hum ndani??.." Mchawi mmoja mwenye ulemavu wa ngozi yaani albino..alisikika akisema hivyo kwa sauti kali..ambapo hapo hapo,alionekana mchawi mwingine alinyoosha kidole kuelekea kwenye meza ambayo aliketi Mzee baluguza nammjukuu wake.


Hivyo baada mchawi yule albino kuonyeshwa ,,haraka sana alizipiga hatua kuelekea kule alikokuwa Mzee baluguza...wakati huo Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake kwa sauti ya kunong'ona..akisema "Unaona sasa tayali umeshavuruga...tangu awali nilikwambia chochote utakacho letewa we kula tu hata kwa kujikaza ili ufuzu zoezi la kupata uchawi !! Lakini wewe unajifanya mtoto wa mjini,,haya sasa kazi kwako..huyooo albino anakuja"


Alisema hivyo Mzee baluguza huku akiangalia jicho ngembe kule anakutokea mchawi albino.. Makongoro aliogopa,hima alinyanyuka kutoka kwenye kiti akitaka kumkimbia mchawi albino..lakini Mzee baluguza alimtuliza kwa kumwambia kuwa "endapo ukikimbia basi utakufa" Makongoro baada kusikia neno hilo kutoka kwa babu yake..woga ulizidi maladufu..akajikuta yupo Kati kwa Kati,kukaa alishindwa pia kukimbia alishindwa...Hivyo alisimama huku akitetemeka,na macho yake yakimtazama mchawi albino ambae nae alizidi kuzipiga hatua kuelekea mahali alipokuwa Mzee baluguza na Makongoro.


Baada mchawi albino kufika katika meza ile ya Mzee baluguza..ghafla alimshika Makongoro kisha akavuta kwake kwa nguvu...huku akiongea rugha ambayo Makongoro na babu yake hawakuweza kuielewa...


Hakika Makongoro alipasa sauti ya kilio..akiomba msaada asaidiwe..lakini cha ajabu wachawi wote waliokuwemo ndani ya kile chumba akiwemo Mzee baluguza..hakuna aliejitolea kumng'atua Makongoro katika mikono ya yule mchawi albino ambae alionekana kutaka kumuua Makongoro.


Hivyo wachawi wote waliishia kutazama tu..wakati huo minong'ono mbili mbili ikisikika kwa chini chini..minong'ono ambayo ilisikika ikimsifu mchawi yule albino kwa uhodari aliokuwa nao wa kupigana kichawi....wakati huo Mzee baluguza yeye alikuwa ameweka mikono kichwani akitazama jinsi mjukuu wake alivyokabwa na mchawi albino...kwa hakika alimwonea huruma sana,,alitamani kwenda kumwokoa..lakini Mzee baluguza akajikuta kuwa nguvu alizo nazo hawezi kupigana na mchawi albino..mchawi ambae alibarikiwa nguvu aina Saba za giza.


Lakini wakati mchawi yule albino,alipokuwa akiendelea kukazana kutaka kumtoa roho Makongoro..mala ghafla katika wachawi wale therathini waliosafiri na Makongoro kutoka sumbawanga mpaka gambosh..alijitikoze mmoja ambae alifahamika kwa jina gwimo..ambapo gwimo kwa kutumia kiganja chake aliunyoosha mkono wake kisha akampiga moto mchawi albino..nae baada ule moto kumpata,haraka sana alimwachia Makongoro..kisha akamgeukia yule aliempiga moto wa kichawi.


Hivyo akionekana kughadhibishwa na kitendo kile..mchawi albino aliongea tena maneno yasiyoeleweka..lakini hakujibiwa na mtu..zaidi gwimo alijitokeza na kisha kusemama "Mimi hapa gwimo mwana wa gwimo" Kwa kauli ya kishujaa kabisa mchawi gwimo alijigamba mbele ya mchawi albino..ambae alikuwa si mchezo katika shunghuli nzima ya kupigana kichawi.


Wakati Mzee baluguza akimnyoosha mjukuu wake shingo baada kutoka kwenye imaya ya mchawi albino...upande mwingine nako walionekana wachawi baadhi wakisogeza meza kando ili kuwaachia nafasi mchawi gwimo na mchawi albino..ambae tayali alikuwa amesha badilika uso kutoka katika umbile la kibinadam..na kuingia katika umbile lingine tofauti..maskio yake yalipotea huku macho yake nayo yakionekana kuwa kama ya nyoka.


Wakati huo gwimo yeye hakubadilika kitu chochote..zaidi aliikaza vizuri kiunoni vazi lake nyeusi..kisha akasimama katikati ya uwanja..ambapo mchawi yule albino aliasama mdomo wake..ghafla ulitoka moto mkali uliomfuata gwimo ..lakini kwa kuwa gwimo nae hakuwa haba..hivyo aliweza kuukwepa moto ule.


Hakika shangwe za kumshangilia gwimo..zilisikika baada kupangua moto ule .na pia ziliongezeka maladufu baada gwimo kujibu shambulizi ambalo moja kwa moja lilimkuta mchawi albino..ambapo alianguka chini mfano wa mzigo wa kuni utokapo kichwani.


Kwa hasira kali mchawi albino alinyanyuka akata kujibu shambulizi..lakini ghafla kengere ililia kuashilia kuwa muda wa kurudi ukumbini umewadia..na hivyo mchawi yule albino alirudi katika hali yake ya ubinadam..kisha wakaelekea ukumbini..wakati huo Mzee baluguza akiwa sambamba kabisa na mjukuu wake Makongoro..ambae nae baada kunusurika kifo kutoka kwa mchawi yule katili albino,alitamani akalipe kisasi kwanza pindi atakapo pewa uchawi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


Hivyo mala baada kufika ukumbini..ghafla ilisikika sauti ya mkuu wa wachawi ikiwata wale wachawi waliokuwa wakipigana watoke nje wakalishe misukule..mpaka pale kikao kitakapo kitakapo malizika..ambao watu hao ni mchawi albino pamoja na mchawi gwimo.


Wote walinyanyuka kila mmoja akimtamani mwenzie,,kisha wakapotea pale kwenye kikao..ambapo baada kupotea kwa hao wachawi..punde punde mkuu yule wa wachawi gambosh..aliwataka chipkizi wanao hitaji uchawi.......Hivyo haraka sana Mzee baluguza alirudia kumkubusha Makongoro..akisema "Tafadhali nakuomba uchague uchawi wa kuua na kujirinda dhidi ya maadui sawa sawaa" Aliaisitiza Mzee baluguza..wakati huo Makongoro akiwa tayali kanyuka..hivyo alizipiga hatua kuelekea kwa mkuu wa wachawi,,hakuwa peke yake bali alikuwa na chipkizi wengine mbalimbali wiliotoka mataifa tofauti tofauti ndani na nje ya bara la Africa.


Na baada Makongoro na wenzake kufika kwa mkuu yule wa wachawi..hatimae aliondoka nao moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha kiapo..ambapo katika chumba hicho zilisikika sauti mbalimbali za wafu pamoja na harufu mbaya iliyoenea chumba kizima..Hakika Makongoro aliogopa sana,,ila aliamua kupiga moyo konde,na hivyo punde si punde ilisikika sauti nzito ndani ya kile chumba cha kiapo..saut ambayo ilisikika ikisema "kabla ya kuapa..lazima ule kwanza nyama mbichi ya binadam pamoja na kikombe cha damu..kwani hicho ndicho chakula chetu stahiki kama ilivyo wali kwa mwanadam wa kawaida"


Kwisha kusema hivyo..ghafla mbele yake Makongoro alitokea mtu alievaa koti jeusi kuanzia juu mpaka chini,,,,akamkabidhi Makongoro bilauli kubwa lililokuwa limejaaa ulimi na sehem ya Siri ya mwaume pamoja na moyo bila kusahau kikombe kikubwa kilicho sheheni damu nzito ya binadam.


INAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.