Simulizi: kijiji cha wachawi sehemu ya pili (02)
Khaa uchawi huu kautoa wapi huyu mzee!..hakika leo nimeumbuka...ila ngoja nijitahidi la sivyo huyu mzee atamzoea mjukuu wangu"
Ni mzee baluguza alikuwa akiyaongea hayo maneno,wakati bado akiwa chini akiendelea kuugulia maumivu...ila mwishowe alisimama kisha akarusha moto kwa kutumia mkono wake wa kulia ghafla Mzee mwakipesile akaunasisha pamoja na moto wake,haraka sana Mzee balu alirusha tena moto kwa kutumia wa kushoto...hivyo kwa kuwa nguvu zote za mzee mwakipesile zilikuwa zikitumika upande mmoja ambao ni kuugandisha moto pamoja na mokono wa kulia wa buluguza...Hatimae ule moto uliorushwa na mkono wa kushoto ulifkia Mzee mwakipeslile......Alilalama kwa sauti kali kali huku akigagaa chini..Sauti hiyo iliweza kumfikia mkuu wake wa kichawi kule milimani ambako ndiko kulikokuwa na makazi maalum ya kulisha chakula misukule pia na wachawi kulia chakula.Hivyo mkuu yule baada kuiskia hiyo sauti ya Mzee mwakipesile alishtuka..hima alimwita mchawi mmoja kisha akamwagiza amletee chungu,kweli punde si punde yule mchawi alikileta..ambapo mkuu yule ambae jina lake ni Bi kileleganya alifanya mambo yake ya kichawi...ghafla ndani ya kile chungu kilichokuwa na mkojo wa mama mjamzito,walionekana Mzee baluguza na mzee mwakipesile wakipigana.Wakati huo Mwamipesile akionekana kushambuliwa sana.
"nyote kimyaaaa" Bi kileleganya ambae ndio mkuu wa wachawi pale kijijini bhonde,aliutuliza umati wa wachawi ulikuwepo pale milimani...kweli wote walikaa kimya
"Mnaongea ongea tuuuu...mnajuwa kinachoendelea muda hu?.."
Aliongeza kwa kusema hivyo mkuu yule wa wachawi..ghafla wote walianza kutazamana.
"sijawaambia mtazamane...pumbafu zenu..haya haraka sana kila mmoja ajiandae,safari moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Bi mazoea tukamwokoe mwenzetu..."
Amri ilimtoka kwa mkuu wa wachawi huku akionekana kukasilika...hivyo punde si punde wachawi wote walikuwa wameshakaa kwenye nyungo zao tayali kwa safari ya kwenda kumwokoa Mzee mwakipesile ambae alikuwa akipigwa vibaya na Mzee baluguza.
*************
Mfano wa mbayuwayu warukavyo angani ndivyo ilivyokuwa kwa wale wachawi jinsi walivyopaa angani na nyungo zao...naam!punde si punde wachawi wale wakawa wanefika,ila walitua pembeni kidogo kisha wakapanga mikakati jinsi ya kumwokoa mwenzao..Hivyo wote kwa pamoja walikubaliana kumvamia Mzee baluguza kasoro Bi mazoea ambae ni mke wa mzee baluguza..Hakika patishika nguo kuchanika, ugomvi uliendelea pale lakini mwishowe wale wachawi walimvamia wote kwa pamoja baluguza..na kwa kuwa baluguza alikuwa ameshachoka alishindwa kujitete kwa kutumia mikono yake,hivyo aliita nyuki wa kichawi ambao alikuwa amewafuga...kweli punde si punde sauti za nyuki ziliskika wakija kwa kasi,kitendo ambacho kiliwafanya wale wachawi kutimka lakini hawakumwacha Mzee mwakipesile ambae alikuwa kapigika vibaya.
Baada ya hayo kupita,Mzee baluguza alirudi ndani kulala akiwa hoi bi taabani..wakati huo kabla hapajakucha Makongoro nae aliamka ili aende chooni kujisaidia..Alistaajabu baada kujikuta mwili umechoka bila kufanya kazi yoyote ngum,lakini hakutaka kujaji sana zaidi alishuka kitandani kisha akaelekea chooni kujisaidia...hakuna asiejuwa vyoo vya kijijini jinsi vilivyo..makongoro wakati anatembea kuelekea chooni ghafla alimwona paka mkubwa mweusi mbele yake,,alimfkuza lakini hakutoka.....Hivyo Makongoro akaamua kuchukua jiwe kisha akampiga yule paka mbae nae alilia kwa sauti kali kama mtoto huku akimfuata mbio makongoro.
"Bibi nakufaaaa"...Sauti ya makelele iliskika kutoka kwa Makongoro huku akikimbilia ndani..waakati huo yule paka aliepigwa jiwe alikuwa akimfukuzia nyuma..Lakini kabla yule paka hajamkalibia,ghafla alipotea...Hivyo hata mzee baluguza alipotoka nje kuangalia kilichomkuta mjukuu wake,hakuona chochote...Na hapo ndipo alipo mtuliza kumwondoa hofu,wakati ho tayali haja ya kwenda chooni kujisaidia ilikuwa imeshapotea kwa Makongoro.
Asubuhi ilipo ingia kabla Mzee baluguza na familia yake hawajaamka,ghafla mlango wa nyumba yake uligongwa...hivyo Mzee balu baada kuiskia hodi aliamka ili akamsikilize huyo mtu aliedamkia kwake..Baada kufungua mlango,alikutana uso kwa uso na Mzee mmoja ambae aliitwa kinono Mzee ambae pembeni yake alikuwa na kijana wake mdogo mwenye umri kama miaka kumi na nne...kijana huyo alikuwa ameshika kichwa chake ambacho kilikuwa kikitilisha dam.
"Habali za hasubui mzee baluguza"
"Salama tu sijui kwako!?.."
"Kwangu sio salama kiukweli...Kama unavyomwona kijana wangu jinsi alivyojileruhiwa na mjukuu wako.."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mjukuu wangu??..embu acha utani basi kinono..mjukuu wangu hajawahi kugombana na mtu yoyote hapa kijijini,kwahiyo wewe unapo niletea hizo tarifa zako naona kama unanichefua"
"Nakuchefua?..jana wakati kijana wangu alipokuwa kwenye matembezi yake,alipigwa jiwe na mjukuu wako,halafu leo hii unaniambia nakuchefua?..aaah wapi Mzee baluguza siku zote mimi huwa mstarabu lakini ukiniudhi na mimi ntakuudhi mala mbili ya ulivyo niudhi...hivyo basi mimi naondoka lakini nakuomba umkanye mjukuu wako,awe makini hapa kijijini la sivyo utamkosa..."
"Aaah mkwala huo..wewe mzee kinono huwezi kunitisha mimi wala mjukuu wangu,na kwa taarifa yako endapo kama mjukuu wangu akikutwa na tatizo lolote..hakika ntadili na wewe mpaka mwisho..mpumbaffu wewe"
SOMA MAKALA ZA MAFANIKIO
ITAENDELEA
.jpeg)
No comments