Simulizi: kijiji cha wachawi sehemu ya tatu (03)
Ilikuwa ni vita ya maneno kati ya Mzee kinono na Mzee baluguza,chanzo akiwa ni Makongoro ambae jana yake usiku alimpiga paka jiwe pasipo kujuwa kwamba alimpga binadam.
Hivyo mala baada Mzee kinono kuondoka zake na kijana wake,Mzee baluguza alirudi ndani akiwa na mawazo chungu nzima..kwani tayali alijikuta akibeba mzogo mzito wa kumlinda mjukuu wake ambae alikuwa akiwendwa na wachawi wawili tofauti,mmoja ambae ni Mzee mwakipesile,yeye alikuwa akimuwinda Makongoro kwa niaba ya kumwingiza kwenye familia ya kichawi,wakati huo Mzee kinono yeye alikuwa akimuwinda kwa niaba ya kumwondoa kabisa duniani..yote hayo akiwa ameyataka Mzee balu baada kutoa kauli mbaya kwake.
Basi mapigo ya moyo yalimwenda mbio Mzee baluguza huku kijasho chembamba kikizidi kumtilika katika mwili wake...Akiwaza atafanya nini ili kumlinda mjukuu wake ambae anaandamwa na wachawi..Hivyo wakati akiendelea kutafakari,ghafla Bi mazoae aliamka ambapo alishtuka baada kumwona mume wake kakaa kitandani huku akiwa amejiinamia.
"Babu makongoro...kulikoni mbona asubuhi mapema umejiinamia?.."
Bi mazoea alimuuliza hivyo mume wake baada kumwona kajiinamia..Lakini Mzee baluguza hakujibu chochote..aliinama uvunguni,akatoka na jungu kubwa kukuu ambalo alitoka nalo mpaka nje..kisha akachukuwa vibuyu vyake vidogo pamoja na hirizi..wakati huo Bi mazoea nae alitoka ndani..alishangaa baada kumwona mume wake akihangaika na Uchawi asubuhi,badala ya kwenda shamba kulima.Hivyo maswali mengi alijiuliza kichwani mwake ambayo alishindwa kuyapatia majibu.
"Babu makongoro,ebu nenda shamba bwanaa hayo mengine utayafanya ukitoka shamba.."
Bi mazoea alimwambia hivyo mume wake kwa msisitizo.
"Aaaah Bi mazoea..staki uniharibie siku sawa kama namnagani vipi nenda mwenyewe kwani huwezi?.."
Kwa hasira kali..akiwa amemkazia macho Bi mzoea,mzee baluguza alijibu hivyo..Ambapo Ili mbidi Bi mzoea kukaa kimya huku akimtazama mumewe alichokuwa akikifanya..lakini mwishowe aliishia kuguna kisha akarudi ndani kumwamsha Makongoro ili anawe..anywe chai.
Punde si punde Makongoro aliamka,akilalama viungo vya mwili wake kuchoka bila kufanya kazi..ghafla alitaharuki baada kujikuta akinukia harufu pumba iliyo chemshwa..Alijiuliza wapi alipoitoa ile harafu lakini hakupata jibu..asijue kuwa asiku alipelekwa na Mzee mwakipesile kuilisha misukule chakula ambacho kilikuwa ni pumba za mahindi iliyochemshwa..
"Mmh hii harufu nimeitowa wapi sasa??...Ee mbona sielewi?."
Alijiuliza Makongoro huku akijinusa mikono yake mala mbili mbili..Wakati huo Mzee baluguza akiwa amesha changanya dawa ya kutoonekana kwa macho ya kawaida,kwani alifanya vile ili afanye mambo yake kwa uhuru bila kuonwa na Mjukuu wake ambae ni Makongoro.
Hivyo kwisha kufanya kila kitu kilicho wezekana,hatimae Mzee baluguza alijirudisha katika hali yake ya kawida..ambapo aliweza kujumuika na Makongoro kunywa chai na magimbi.
"Shkamoo babu.."
"Malakhabaa umeamkaje mjukuu wangu"
"Daah salama tu babu..ila najiskia kucho...." kabla Makongoro hajamaliza sentensi yake,ghafla Bibi yake alidakia "Makongoro magimbi yakiisha njoo uongeza.."
"Sawa bibi" Alijibu makongoro haraka,huku akitaka kumwambia babu yake,vile anavyojiskia mwili.
"Eeh ulikuwa unataka kusema!?.."
"Nilitaka kusema kwamba najiskia kuchoka mwili mzima..harafu istoshe mikono yangu inatoa harufu ya pumba iliyo chemshwa..yaani hapo nilipo hata sielewi kwanini"
Makongoro alimwambia hivyo babu yake,lakini cha ajabu mzee baluguza alimtazama Bi mazoea jicho ngebe huku akiaahirisha kula magimbi..moja kwa moja alisogea mpaka mahali alipokuwa amekaa Bi mazoea akila magimbi.
"Nadhani umemskia mjukuu wako jinsi anavyo lalamika..sasa nakwambia wewe,ili ukawaambie Wenzako kwamba staki michezo yenu kwa mjukuu wangu...Chezeeni vijana wa hapa hapa kijijini sio huyu sawaaa"
Kwa sauti ya upole Bi mazoea aliitikia "Sawa"
Wakati huo Mzee baluguza akijiandaa kuelekea shamba..hivyo kufumba na kufumbua alipotea pale nyumbani kwake,akatokea shambani ambako aliendelea na Shughuli zake.
***************
Naam!mchana shwari usiku shali katika kijiji kile bhonde..hatimae usiku uliingia ambapo ilipotimia saa nne usiku,iliskika mbiyu ya kichawi ..Mbiyu ambayo iliwafanya wachawi wote wa kijiji bhonde kufaham kuwa usiku wa manane kutakuwa na kikao.. kasoro mzee baluguza hatokuwemo kwa sababu alikuwa na uchawi wa kujitegemea.. Kweli saa saba usiku ilipotimia,wachawi wote walikusanyika chini ya ule mti mkubwa kuliko yote kijiji kizama..Na punde si punde Bi kileleganya ambae ndio mkuu wa wachawi alifungua kikao ambacho kilijadili mstkabali wa kumwangamiza Mzee baluguza ambae kwa namna moja ama nyingine alionekana kikwazo kwao..Hoja ambayo iliungwa mkono na wachawi wengi haswa walipokumbuka lile shambulizi la nyuki wa kufungwa..ila Bi mazoe ambae nae alikuwemo kwenye kikao hakuiafiki hiyo hoja,lakini alishindwa kuzungumza kwa sababu asilimia tisi na nane walilipendekeza hilo suala..
Na wakati hayo yakijili....Nyumbani kwa baluguza..Alitokea Mzee kinono baba wa kijana aliepigwa jiwe na Makongoro,mzee ambae alikuwa na uchawi wa kujitegemea kama ilivyokuwa kwa Mzee baluguza.
Hivyo basi mzee kinono alitua nje ya nyumba akiwa katika mavazi ya kichawi...na nakabla hajafanya jambo lolote alikunjua kiganja chake akatazama usalama wa eneo alilo simama..Alicheka baada kujikuta yuko salama,hivyo kazi ikawa imebaki moja tu ya kumwangamiza makongoro ambae alikuwa amebaki ndani peke yake..Wakati huo Mzee baluguza nae alikuwa amekwenda nyumbani kwa mzee kinono kumwangamiza kabla hajammaliza mjukuu wake..hivyo wakawa wamepishana angani..pasipo wao kujuwa.
"Lazima niondoke na kichwa chake"
Alisema Mzee kinono.
Baada Mzee kinono kusema kuwa anaondoka na kichwa na makongoro,mwishowe aliamua kumfanyia vituko kwanza kabla hajamfanya jambo baya...ambapo alichukua hirizi yake kisha akaanza kuisugua sugua huku akiongea maneno ya kirugha,punde si punde Makongoro alinyanyuka kutoka kitandani..akatoka nje.
Mzee kinono alitabasam baada kumwona Makongoro,haraka sana alimmwagia maji ya kichawi ambayo yalimfanya Makongoro kurudi katika hali ya kujitambua...wakati huo tayali amesha pelekwa kando kando ya mto maragagalasi,,ambapo huko alikutana na yule kijana wa Mzee kinono..kijana ambae alipigwa jiwe na Makongoro.
"Mwanangu huyu hapa mshenzi aliekupiga jiwe jana usiku,kwahiyo mfanyie jambo lolote unalo litaka..alafu mimi nimmalize kabisa"
Kijana yule wa mzee kinono alicheka baada baba yake kumwambia hivyo,hima alichukua bakora kisha akamcharaza..
*********
Wakati Makongoro alipokuwa akipigwa fimbo,upande mwingine alionekana Mzee baluguza akihaha kumtafuta Mzee kinono ili amuue..lakini juhudi zake ziligonga mwamba,na hapo ndipo alipokumbuka kuwa Mzee kinono aliahidi kumfanyia kitu kibaya Mjukuu wake...kwahiyo baada Mzee balu kulikumbuka hilo suala,haraka sana alikaa kwenye ungo wake kisha akarudi nyumbani kwake ambapo moja kwa moja alipitiliza Chumbani kwa mjukuu wake...ghafla alishtuka baada kumkosa mjukuu,hivyo alijuwa dhahili shahili Mzee kinono atakuwa amekuja kumchukuwa...Naam!bila kupoteza muda,mzee balu aliingia uvunguni mwa kitanda chake,akatoka na jungu lake kukuu lilokuwa likitunza vikolokolo vya kichawi..kisha akatoa filimbi yake ambayo alitoka nayo nje ya nyumba..hivyo akaipuliza kwa sauti kali,sauti ambayo iliwaita nyuki wake pamoja na bundi..ambapo Mzee kinono alimtuma yule bundi akamtafute Makongoro alipo ili aje atoe taarifa.
Kweli baada yule bundi kuondoka,ndani ya nusu saa alirudi moja kwa moja alitua kwenye bega la Mzee balu..hivyo nae mzee balu alimchukua kisha akamtazama kwenye mboni..Alishtuka baada kumwona Mjukuu wake akichapwa bakora na kijana wa Mzee kinono.
Haraka sana Mzee baluguza alipanda kwenye ungo wake huku jopo la nyuki likimfuata nyuma..punde si punde alitua pale pale kando ya mto maragarasi,ambako ndiko alipokuwa Makongoro akichezea kichapo kutoka kwa kijana wa Mzee kinono alihali Mzee kinono nae akiwa pembeni aktazama.
Lakini wakati yule kijana alipokuwa akiendelea kumchapa Makongoro,ghafla alistisha baada kuskia kuumwa na nyuki...Alitazama juu huku akiskia sauti ya kundi la nyuki likija mahali walipokua na baba yake wakimwadhibu Makongoro..na hapo ndipo walipoamua kutimua mbio wakimwacha makongoro,wakati huo mzee kinono akiamini kuwa kitendo cha makongoro kushambuliwa na nyuki ni adhabu tosha,kumbe asijue kuwa wale nyuki ni wa babu yake Makongoro ambae ni Mzee baluguza.
Baada Mzee kinono na kijana wake kutimka,mzee balu alifanya mambo yake ya kichawi ambayo yalimfanya Makongoro kutojitambua.Kisha akarudi nae nyumbani kwak...wakati huo Bi mazoea nae alirejea kutoka kweny mkutano wa kichawi,ambao ulikuwa ukijadili jinsi ya kumwangammiza mzee baluguza ambae alionekana kuwa kikwazo kwao.
**************
Asubuhi ilipopambazuka,wa pili kuamka alikuwa ni Makongoro ambapo alishangaa kujikuta mwili umevimba bila kusjia maumivu..Lakini yote kwa yote alisubili babu yake bibi yake aamke ili amuulize tatizo nini,wakati huo akitafuta kibiriti ili akoke moto kwa sababu asubuhi ile palikuwa na baridi kali.
Hivyo mala baada moto kukolea vizuri..ghafla Makongoro aliitwa na bibi yake chumbani.
"Umeamkajekipenzi changu"..Bibi yake makongoro alimsalimia Makongoro huku akijifunga vizuri kitenge chake kifuani.
Hivyo makongoro nae alishusha pumzi kidogo huku akijiuliza atumie nafasi ile kumwambia bibi yake mambo yanamkuta kila siku au la!..lakini mwisho makongoro aliamua kunyamanza kimya,zaidi alimjibu bibi tu salam bibi yake.
"Nimeamka salama bibi..daah ila leo kuna bonge la baridi"
"Mmh kumbe ilikua hujui kama bhonde kuna baridi?..sasa nadhani umelijua hilo.."
"Kabisa bibi mimi siku zote nilikuwa sijui.."
"Sawa lakini si umkoka moto??.."
"ndio "
"Haya nenda kaote"
Makongoro alitoka ndani akimwacha bibi yake kitandani...wakati huo kule nje alipita Mzee mwakipesile akiwa na swala aliemnasa kwnye mtego wake..Hivyo baada mzee mwakipesile kumwona Makongoro,alimuuliza "Rafiki babu yako yupo?
Makongoro akiachia tabasam pana alijibu"Hayupo"
"Anhaaa haya twende nyumbani kwangu sasa tukale nyama ya swala"
Alisema hivyo Mwakipesile huku akipiga hatua za kuondoka...ambapo Makongoro aliweza kumfuata.
Kwa hakika Mzee mwakipesile alifrahi sana baada kuona makongoro kakubali kwenda nyumbani kwake,hivyo alijuwa tayali anaenda kukamilisha kazi aliyopewa na mkuu wake wa kichawi ambae alimkabidhi kazi ya kumvuta Makongoro kwenye familia ya kichawi.
Upande mwingine taarifa za kumuua Mzee baluguza zilienea kila club cha pombe pale kijijini ..kwani waliamua kutumia njia hiyo kwa sababu waliona hawataweza kumuua mzee balu kwa nguvu za Kichawi...bali pombe pekee kwa maana Mzee baluguza alipenda sana pombe .
Kweli ilipotimia saa nane ya Mchana...Mzee baluguza alirudi kutoka shamba,hivyo kwa kuwa alikuwa na kiu ya pombe aliamua kupita kwenye banda la pombe kabla ya kufika nyumbani kwake...Ambapo baada mpimaji wa pombe kumwona mzee balu,,alikumbuka taarifa zilizo sambaa za kumuua huyo mzee..hivyo kabla ya kumpimia alizunguka nyuma ya banda akafungua fundo la uchawi aliokuwa nao kwenye khanga,kisha akarudi kwenye kitengo chake..wakati huo Mzee balu alikuwa nje akiweka oda ya nyama ya mbuzi ya kuchomwa ili achachue mdomo...Kitendo ambacho kilimfanya yule mama mpimaji wa pombe kuweza kutia uchawi kwenye pombe ya mzee balu bila wasiwasi wowote.
"Mmmh...aaaa....naaam leo nimekubali pombe yako iko vizuri....!!..karibu nyama au huli nyama ya mbuzi?.."
"Apana we kula tu mi nikila natokwa na vipele mwili mzima" Alijibu mama muuza pombe..ambapo mmzee baluguza aliachia cheko kubwa kisha akasema
"Tatizo lenu uchawi mwingi hiki kijiji...ona sasa wanakuroga hadi kula nyuma ya mbuzi??..Daah"
Aliongea hivyo Mzee baluguza wakati huo akiendelea kunywa pombe yake....Na baada kumaliza alilipa kisha akaondoka zake nyumbani huku mkono akiwa na nyama choma kidogo aliyobakisha,,akimpelekea mjukuu wake ambae nae alikuwa kwa Mzee mwakipesile akila nyama.
Lakini wakati mzee balu alipokuwa njiani akirudi nyumbani kwake ,ghafla alihisi tumbo kumuuma..ambapo alishindwa hata kutembea,na punde si punde alianguka chini huku mapovu yakimtoka mdomoni na mkono wake wa kushoto ukionekana kukamitia hirizi kwanguvu.
Basi baada kuikamatia hirizi yake vizuri mkononi..mwishowe Mzee baluguza aliiachia baada maumivu ya tumbo kuzidi...hivyo akawa ameshika tumbo lake kwa mikono yake,wakati huo nguvu polepole zikizidi kumwishia.
Hakika Mzee baluguza alipasa sauti ya kuhisi maumivu...ila mwisho aliamua kukaa kimya kisha akajikaza kiume,ambapo alinyoosha mkono wake kuifuata hirizi yake aliyokuwa ameiachia...Baada kuikamata kamata,hatimae aliitemea mate mala tatu huku akiongea kirugha...Ghafla alitokea bundi wake wa kichawi ambae alikuwa amemfuga..Ambapo mzee baluguza alimshika kisha akamtazama kwenye mboni...Cha ajabu ulitokea mwanga mkali kwenye macho ya Mzee baluguza.Mwanga ambao ulienda kugonga kwenye macho ya yule bundi..Hivyo punde si punde yule bundi akawa amepotea akimwacha Mzee baluguza akiendelea kuvuja jasho jembemba la maumivu ya sumu aliyowekewa kwenye pombe pasipo yeye kujuwa.
Kweli baada ya nusu saa yule bundi alitua mbele ya Mzee baluguza huku akiwa na mkoba mdogo.Mkoba ambao ndani yake ulikuwa na dawa za miti shamba pamoja na hirizi mbalimbali..Hivyo Mzee baluguza alitabasam kwa mbali baada kumwona bundi wake kafanya kama alivyomwelekeza,na hapo sasa kazi ikawa imebaki moja tu ambayo ni yeye mwenyewe kuyaokoa maisha yake...
Lakini kabla Mzee baluguza hajafanya jambo lolote la kuweza kuyaokoa maisha yake kwa kutumia dawa zake..ghafla alitokea Mzee kinono..Mzee ambae alikuwa akimuwinda Makongoro mjukuu wa mzee baluguza ili amuue..wakati huo Mzee baluguza nae alikuwa akimuwinda kinono ili amuue kabla hajamuua mjukuu wake..Hivyo kile kitendo cha Mzee kinono kumkuta Baluguza hoi bitaabani..ilikuwa ni neema kwake kwani aliachia cheko kubwa kisha akasema.
"Mzee baluguza wewe mkubwa kiumri ila kiuchawi wewe bado mtoto sana...tazama sasa unakufa hivi hivi unajiona"
Aliongea maneno hayo Mzee kinono ambae alionekana kuvamilia mavazi ya kichawi..huku akimzunguka Mzee baluguza alielala chini akiwa hajiwezi.
Basi baada Mzee kinono kusema maneno hayo alichuchumaa chini kisha akauchukuwa ule mkoba ulioletwa na Bundi wa Mzee baluguza...akatwa mikononi mwake kisha akaongeza kwa kusema.
"Baluguza usijifu unambio bila kumwangalia anae kukimbiza...hivyo labda niseme neno juu yako..sihitaji lingi kutoka kwako huna viwango vya kupambana na mimi ambae nina uwezo wa kusafiri kila sehem hapa duniani...sio wewe mwisho wako sumbawanga ukienda mbali Congo halafu unajiaifu..."
Aliongeza kwa kujingamba hivyo Mzee kinono juu ya baluguza ambae tayali alionekana kukubali kifo...Na baada kusema hayo hatimae Mzee kinono alikunjua kiganja chake,ambacho kilitoa taswila jinsi Makongoro alivyokuwa akila nyama na Mzee mwakipesile...Hivyo alimwonyesha Mzee baluguza,,kisha kinono akasema "nilipanga nimmalize mjukuu wako..ila nabadilisha maamuzi ngoja nianze na wewe kwanza kisha nidili na mjukuu wako.."
Alisema hivyo Mzee kinono..wakati huo Mzee bulu akihusi kupata nguvu baada kumwona Mjukuu wake yupo kwa mwakipesile ambae nae alikuwa ni Mchawi.
********************
Basi upande wa pili nako kule klabuni..yule mama aliemfanyia unyama Mzee baluguza kwa kumuwekea uchawi kwenye pombe ili amuue..hatimae aliweza kuwatangazia baadhi ya walevi waliokuwepo pale klabuni..
"Jamani nitoboe ni sitoboe..?
Alisema hivyo kwa furaha yule mama muuza pombe ambae alifahamika kwa jina la Mama chiku.
"Duuuh naona leo umeuza sana mpaka unaonekana kuwa na furaha kiasi hicho??? .." Mmoja ya walevi alidakika kwa kusema hivyo..Lakini Mama chiku aliendelea ...
"Mimi nauliza nitoboe nisitoboe.."
"Mmh huwenda leo kuna pombe ya bure hapa maana wewe mwenyewe si unamwona jinsi alivyokuwa na furaha.."
"Eeh kweli...ngoja tumwitikie.."
Zilikuwa ni sauti za walevi zilizokuwa zikiskika kwa kunon'gona...Na hatimae mmoja kati ya wale waliokuwa wakinong'ona alinyanyuka kisha akapasa sauti akisema..
"Jamani tusiwe na viburi...Hatuwezi juwa huwenda mama chiku leo anatoa zawadi ya pombe kwa hiyo tumwitikie jamaniii"
Hakika kicheko kikubwa na vikohozi vya kubanja...Vilisikika kutoka kwa walevi waliokuwepo pale klabuni...Na hapo ndipo sauti ya pamoja ilipo fuata ikisema "Toboaaaaaaa"
"Aaanhaaa habari njema ni kwa..aambaa yule Mzee anaejifanya anaujuwa sana Uchawi kuliko wengine,leo nimemnasa.."
Baada kusema hivyo yule mama muuza pombe..Ghafla walevi wote walipigwa na butwaa huku wakihoji "Nani huyo?.."Embu tuambie basi"
"Si huyu Mzee mwenye kijukuu kilichoka mjini"
Alijibu hivyo Mama muuza pombe.
"Anhaa kumbe huyu Mzee baluguza!.."
"Eenhee huyo huyo...kwa uchawi huu wa jumlajumla niliomuwekea,sijui kama kwake kafika"
Hakika yule mama chiku alionge kwa kujiamini...kwa maana alitimiza agizo la mkuu wa wachawi..agizo alilotoa la kumwondoa Mzee baluguza duniani kwa sababu alikuwa ni kikwazo kwao.
--------
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hivyo upande mwingine nao alionekana Mzee mwakipesile akiwa na Makongoro,huku wakila nyama choma ya swala..wakati huo story mbali mbali zikiendelea.
"Mmh nyama hii tam sio Mchezo.."
Aliongea Makongoro huku akiwa ameshikilia nyama kubwa isoyokuwa na mfupa.
"Ee ukiskia swala ndio huyu bwana...hivi huko mjini kuna swala kweli??.." Mzee mwakipesile nae aliongeza kwa kusema hivyo..Kitendo ambacho kilimfanya Makongoro kucheka kwanza kabla ya kumjibu Mwakipesile.
"Daaah.. babu unachekesha sana..we umeshasema Mjini,sasa mjini mapori ya kuishi swala yanatoka wapi??.."
"Duh kwahiyo huko mjini hakuna hata pori la kuwinda sungura au kanga"
"Babuuu kule hakuna vitu kama hivyo...yani kule unapishana na magari tu.."
"Kha yani sehem kama hiyo me siwezi kuishi..kwa sababu sitoweza kuka siku mbili bila ku..."..Kabla Mzee mwakipesile hajamalizia Sentensi yake,ghafla Makongoro alidakia kwa kusema. "Babu geuza kwanza hiyo nyama inaungua"
"Aah kiukweli rafiki uko vizuri" Alijibu Mzee mwakipesile..na hivyo wote wakawa wamecheka.
"Enhe malizia sentensi yako sasa maana nilikukatisha..Sijui ulitaka kuongea nini"
"Anhaa sawa subiri niende chooni kwanza kujisaidia"
Mzee mwakipesile alimjibu hivyo Makongoro,kisha akaelekea nyuma ya nyumba yake ambako huko alinyoosha Mkono wake juu huku akiongea maneno ya kirugha..Ghafla kwenye ule mkono wake aliounyoosha ilitokea hirizi kubwa kiasi ambayo nayo aliifumua..kisha ukatoka unga mweusi ambao ndio uchawi.
Hivyo baada kuuchukuwa ule uchawi..Uchawi ambao ulikuwa mahususi kwa niaba ya kumvuta mtu kwenye familia ya kichawi..Hatimae Mzee mwakipesile alirudi ndani kwa niaba ya kumaliza agizo alilopewa na mkuu wa kichawi.
SOMA HAPA MSJ ZA MAPENZI>>>BONYEZA HAPA
INAENDELEA
.jpeg)
No comments