Simulizi: kijiji cha wachawi sehemu ya nane (08)
Wakati hayo yakiendelea..upande mwingine nako alionekana Makongoro akizipiga hatua kuelekea kijiji jirani kwenda kutazama movie...lakini wakati Makongoro alipokuwa akitembea hana hili wala lile..mala ghafla nyuma yake alitokea Sudi mtoto wa Mzee kinono...Sudi akiwa katika mavazi yake ya kichawi,alizipiga hatua kumfuata Makongoro..Na kabla hajamfikia,Sudi alimrushia kombola Makongoro..hali ya kuwa Makongoro nae hirizi yake aliyopewa na mkuu wa wachawi gambosh ilianza kumbana,,na hapo hapo alijuwa tayali kuna tatizo hivyo kwa kuhusi tu lipotea ndani ya nusu sekunde kisha akaonekana tena live...na lile kombola la kichawi alilorusha Sudi likawa halijampata.
Makongoro aligeuka nyuma akamwona kijana mdogo mwenye makamo kama yake akiwa katika mavazi ya kichawi...Hakika Makongoro alijikuta akicheka huku akiendelea na safari yake ya kuelekea kijiji jirani.
Lakin licha ya Makongoro kumpotezea Sudi kijana wa Mzee kinono..ila Sudi bado aliendelea kumchokoza Makongoro..akasahau onyo aliyopewa na baba yake kuhusu Makongoro mjukuu wa Mzee baluguza...Na hapo ndipo Makongoro uvumilivu ulipo mshinda,hivyo kwa kutumia mkono wake uliokuwa na hirizi alimnyooshea kidole Sudi,,na punde si punde Katika kidole chake Makongoro ulitokea moto mwembamba,moto ambao ulikwenda kumpata Sudi..haikupita dakika Sudi alidondoka chini akafa.
Baada Sudi kupoteza maisha..Makongoro aliogopa sana hivyo aliamua kuahilisha safari yake akawa amerudi nyumbani..moja kwa moja alipitiliza hadi chumbani kwake huku akionekana kuwa na hofu juu ya kile alicho kifanya..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini kitendo kile cha Makongoro kupitiliza hadi chumbani kwake bila kumsalimia bibi yake ambae alikuwa sebleni akipika chakula cha usiku..kiliweza kumshtua Bi Mazoea bibi yake Makongoro..ambapo aliweza kumeita ili amwambie kilicho msibu,,ile Makongoro hakuitikia...Na wakati huo huo Mzee baluguza nae alifika nyumbani,hivyo ikabidi Bi Mazoea kumwambia mume wake akamuulize kinacho msibu Makongoro.
Mzee baluguza baada kuambiwa vile..haraka sana alizipiga hatua kuelekea chumbani kwa Makongoro..kwa sauti ya kunong'ona Mzee baluguza alimuuliza mjukuu wake kitu kinacho msumbua.
"Babu nimezusha balaa..kumbe uchawiwenu unauwa kabisa.."
Alisikika ikisema hivyo Makongoro huku kilio kifuatia,,na Mzee baluguza baada kuona hali ile,,hima aliongea maneno yake ya kirugha huku akisugua kiganja chake...Na punde si punde kwenye kiganja chake walionekana wachawi wa kijiji kile cha bhonde wakiwa wamekusanyika kwa nia kumtaka Makongoro na kisha kumuuwa Mzee baluguza ambae ndio babu yake Makongoro.
"unaona sasa mjukuu wangu??..Kwahiyo kaa ukijuwa kuwa tumezungukwa na madui wengi..Na kauli mbiyu yetu ni dawa ya moto maji..Na sio dawa ya moto moto..hahahaaaaa wao wanawasha halafu sisi tunazima..futa machozi mjukuu wangu hujakosea kumuuwa yule mtoto wa Mzee kinono kwani ukiona hivyo nae alikuwa akikuwinda ili akuue.." Alisema hivyo Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake,,hali iliyomfanya Makongoro kujiamini juu ya kile alicho kifanya.
Na giza lilipo tanda katika kijiji kile cha bhonde...Mzee mwakipesile alipanda ungo wake na kisha kutua sehem ile waliyoahidina wakutane na wazee wenzake.Hivyo punde si punde wale wazee nao walitua,ambapo walikubaliana kwenda kumuuwa Mzee chande kisha waelekee tena kwa Makongoro kwenda kujaribu tena bahati yao.
Kumbe wakati wazee wale walipokuwa wakipanga mikakati ya kumuua Mzee chande..Mzee chande nae machale yalimcheza,ambapo alichukua ungo na kibuyu chake kidogo..kisha akapaa kuelekea Congo ili kuongeza uchawi zaidi wa kuweza kujirinda dhidi ya Mzee mwakipesile na wenzake ambao wamepanga kumuuwa kabisa.
Hivyo wakati anaiacha ardhi na kuliona anga tu..mwakipesile na wenzake nao walitua nyumbani kwa kwake chande,,ambapo walijikuta wamechelewa kumuwahi Mzee chande.
Hakika roho ilimuma sana Mzee mwakipesile ambae ndio alikuwa kiongozi wa msako..Lakini yote kwa yote aliwataka wazee wenzake waelekee nyumbani kwa Mzee baluguza kwenda kumfuata Makongoro..hali ya kuwa Makongoro nae ameshaambiwa kuwa amezungukwa na maadui,,hivyo kuuwa ni jukum lake.
Kikao cha muda mfupi walikaaa Mzee mwakipesile na wachawi wenzake watatu...ambapo Mzee mwakipesile alisikika akisema. "Jamani kwa kuwa tumemkosa huyu mzee chande,,sasa safari hii tuelekee kwa Mzee baluguza,kwenda kumfuata mjukuu wake..lakini napenda kukumbusha kuwa tuwe tayali kwa mapigano maana nadhani kila mmoja hapa Kati yetu ameweza kushuhudia uwezo wa yule mtoto..je,kweli si kweli??.."
"Kweli kabisa.." waliitikia wale wachawi wengine baada Mzee mwakipesile kusema maneno hayo akiwaasa wenzake wawe makini pindi watakapo elekea nyumbani kwa Mzee baluguza.
Na mala baada kuelewana,,Mzee mwakipesile na wachawi wenzake walijifunga vizuri hirizi zao,kisha wakanywa damu ya binadam iliyokuwa kwenye kibuyu chao...Na hapo hapo safari ya kwenda kwa Mzee baluguza ilianza,,ambapo walipaa angani kwa kutumia ungo.
PATA VICHEKESHO MEMES KUPITIA SIMU YAKO BONYEZA HAPA
ITAENDELEA
.jpeg)
No comments