Simulizi: kijiji cha wachawis sehemu ya kumi (10) MWISHOOO
Kwa kweli baada ya kuona Maimuna kachomwa kisu na Yusira nilijikuta nachanganyikiwa mbaya. Nilishindwa nifanyaje nilibaki nikiwa nimedua yani hata akili za kusema nimkimbize hospitalini nilikuwa sina. "Mume wangu Vaa nguo alafu njoo nikwambie kitu kabla Sijafa. Nakupenda sana Mume wangu na najua usingeweza kunisaliti ila ni tamaa za mdogo wangu Yusira"Aliongea Maimuna huku akionekana Mtu ambayo alikuwa anasikia Maumivu makali sana. Bado ile Kisu ambayo alikuwa Amechomwa Maimuna ilikuwa bado Ipo Tumboni mwake. Maimuna aliponiambia vile ndio nilikumbuka kama Bado nilikuwa nipo uchi. Nilienda kuchukua Suruali yangu na kuvaa haraka haraka bila hata kuvaa boksa wala bukta kwa ndani. Nilivaa suruali tupu kwa Jinsi nilivyochanganyikiwa. Nikiwa navaa Suruali Yangu kumbukumbu ya Maneno ya Mzee Hijirafu aliponiambia kuwa natakiwa kuwa makini ilianza kunijia kichwani Mwangu. Baada ya kumaliza kuvaa Suruali yangu nilisogea hadi sehemu ambayo alikuwa Amekaa maimuna huku kisu bado kilikuwa Tumboni kwake. "Mume wangu Usiwe na wasiwasi huwezi kugeuka mbwa hata siku moja. Mimi nakupenda sana na nilijua Udhaifu wa Wanaume ndio maana sikukufanyia hivyo. Ila Nashukuru sana Mume wangu kwani wewe nimegundua ulikuwa Mwaminifu kwangu na kamwe hukunisaliti. Najua kabsa kama Mdogo wangu Yusira ndio amekulazimisha. Mume wangu kabla Sijafa nataka nikwambie kitu kimmoja"Aliongea Maimuna huku Machozi kabsa yakiwa yanamtoka. Yale Maneno ya Maimuna aliyoongea kuwa kabla ya kufa anataka kuniambia neno moja ndio yalinifanya nizidi kuchanganyikiwa zaidi. "Hapana Maimuna huwezi kufa hata siku moja, Utapona Mke wangu ngoja nikupeleke Hospitalini. Utakufaje sasa wakati mimi nakupenda Maimuna. Huwezi kufa kabsa Mpenzi wanguCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Maimuna maana nakupenda sana hilo Hata Mungu analijua"Nilimwambia Maimuna huku Machozi yakiwa yananitoka. "Kapopo naomba usilie pia kaza moyo nisikilize kile ambacho mimi nitakwambia. Kufa Mimi lazima nife yani hiyo ipo wazi. Hichi kisu ambacho nimechomwa siyo kisu cha kawaida. Yani hiki kisu ukichomwa lazima ufe hata kama watakupeleka hospitali gani lazima nife. Sina Ujanja kwa hiki siwezi kumaliza saa moja nitakuwa nimeshakufa hivyo nisikilize kwa makini mume wangu"Aliongea Maimuna maneno ambayo yalizidi kuninishutua zaidi. Ilibidi niangalie kile kisu ni aina gani hadi Maimuna kuniambia kuwa hicho siyo kisu cha kawaida. Nilipokiangalia kile kisu nilibaki nashangaa kile kisu kilikuwa kinatoa kama miale mikali ya Mwanga. "Kapopo kwanza pole sana kwa kumpoteza Mwanao tumboni pia kwa kunipoteza na Mimi. Najua kama tutakuacha wakati mgumu ila sina ujanja zaidi. Nilikuwa nakupenda sana Mume wangu muda wote nilikuwa natamani sana kuendelea kuwa na wewe. Kapopo kwanza nitakapo kufa hutaweza tena kuendelea kuwa kwenye kisiwa cha majini watakutoa. Pia mali zote watakuondolea ingawa sina uhakika. Ila nahisi baba yangu anaweza kukuachia baadhi ya mali maana anakupenda sana. Pia nataka kukwambia kuwa mama yako hajafa, mama yako mimi sikumtoa kafala ila yupo na mzima kabsa. Nikifa tu mimi mama yako utaanza kumuona kabsa maana mimi ndie nilikuwa kivuli chake ili asionekane. Maneno ambayo alikuwa anakwambia Mdete ni Maneno ya ukweli kabsaa. Na yule ambae ulikuwa unamuona kama mama yako mara anabadilika kuwa mama yako mdogo ndio mama yako. Unakumbuka kuwa mimi nilikwambia kuwa ni Jini yauma ambae hatuna kafala ya damu. Tulifanya tu kiini macho kwako ili usiwe unamuona mama yako hiyo pia ilikuwa ni faidi kubwa kwako maana kila ulipokuwa unamuwaza mama yako pamoja na kumuona ona ndio ulikuwa unazidi kuwa tajiri"Aliongea Maimuna maneno ambayo yalizidi kunifanya kuchanganyikiwa zaidi. Kumbe kweli mama yangu alikuwa yupo mzima. Swala la mama yangu mimi kwa kweli halikusumbua kichwa changu ambacho nilikuwa nataka ni kumuoa Maimuna wangu anakuwa mzima. Bado kichwa kilikiwa kinazidi kuchanganyikiwa zaidi hasa Maimuna aliposema hata zile mali zitarudi na mimi kurudia kwenye ukapuku wangu. Kwa kweli hasira ambazo nilikuwa nazo kwa Yusira kama angekuwa karibu na Mimi angeniua kabsa. "Maimuna nimesema huwezi kufa hata siku moja huwezi kufa mimi nakwambia huwezi kufa. Kwani Hadi wewe ufe Mungu hajuia kama bado nakuhitaji kwanza Maimuna acha utani utakufaje wakati Mwanangu yuko tumboni kwako"Niliongea Maneno haya kwa sauti na machozi yakizidi kunitoka. "Hayo ndio Mawazo yako kapopo nikichomoa hiki kisu tumboni ndio Mwisho wa maisha yangu. Sasa kabla sijafa naomba kaniitie mfanyakazi wetu wa ndani"Aliongea Maimuna. Sikutaka kubisha Niliondoka kwa kasi na kwenda kwa mfanyakazi wangu wa ndani na kumuita. Tulipoenda chumbani tena kwa kweli sikuamini macho yangu nilipokuta Maimuna amelala chini na ametulia kimya. Nilimfuata Maimuna na kumuangalia cha ajabu sikuona kile kisu tumboni hali iliyonifanya kubaini kama alishachomoa kisu. Niliangalia pembeni vizuri alipolala ndio macho yangu yalikiona kisu. Kwa kweli nilizidi kuchanganyikiwa na kuamua kwenda kuchukua kile kisu ili nijue kisu cha Namna gani ambacho kimemuua mke wangu. Cha ajabu nilipopiga hatua moja kwenda kwenye kile kisu nilishangaa kinapotea. Ile hali kwa kweli ilizidi kuniogopesha. Nilienda hadi sehemu ambayo alikuwa amelala Maimuna na kumuangalia kwa Umakini kweli nilikuta maimuna Ameukataaa.
Kwa kweli kitendo cha kumuona Maimuna tayari kabsa asilimia tisini na tisa point tisa tisa ameshakufa nilitokea kuchanganyikiwa sana. Muda ule nilikuwa natemeka Mwili wote huku jasho likiwa linanitoka. Makamasi puani yalianza kunitoka huku sikuwa na Mafua kabsa. Kichwani kwangu nilikuwa nahisi kizungu zungu kikali huku machoni mwangu kimiminika kisichozuilika kilikuwa kinatiririka. "Maimuna tafadhari naomba usife, maimuna utakufaje na kuniacha mimi katika hali kama hii. Maimuna kumbuka uliniambia hadi shule niache ili nikuoe wewe. Sasa mbona unaniacha mimi nitaishi na nani. Hebu acha utani wako amka jifungue hata mtoto wangu ili wewe ufe"Niliongea kwa hazuni huku nikiwa nimemkaba Maimuna utafikilia nilikuwa nimegombana nae. "Shemeji Umemfanya nini dada Maimuna, Dada amka basi mimi mdogo wako nimekuja. Dada kumbuka wewe ndio ulinichukua na kuanza kunilea baada ya kutambua kama mimi ni mtoto yatima. Sasa kama utakufa na wewe nani ambae atanilea mimi. Hapana Dada nasema hapana huwezi kufa hata siku moja"Aliongea Mfanyakazi wangu Wa Ndani Adele huku akiwa analia. Wakati tunaendelea kulia pale Ghafla nilianza kuona Kitu kama Mvua hivi ikianza kunyesha huku ikiwa imeambatana na miale mikali na ngurumo za radi. Kwa kweli ile mvua ilinishangaza sana na kunifanya kuashilia kulikuwa na hatari. Maana ile Mvua ilikuwa inanyesha dani tu tena chumbani kwangu, sasa nilishindwa kuelewa ile mvua itanyeshaje ndani wakati juu kulikuwa na bati. Ile hali hata Mfanyakazi wangu alianza kushangaa maana haikuwa hali ya kawaida. Ilibidi Ninyanyue Macho yangu juu kuangalia huenda bati zilikuwa zimeezuliwa nini. Nilipotazama Juu kwa kweli nilibaki nikiwa nimeshangaa maama mazingira ya kisiwa cha Majini hasa kwa Mzee Hijirafu yalikuwa yanaonekana huku kulikuwa na Mrudikano wa watu wengi sana wakiwa wanalia. Ile hali kwa kweli ilinishitua sana kitendo cha kuona mazingira ya kisiwani Juu ya Nyumba ile kwangu ilikuwa kitu cha ajabu. Bado mvua ilikuwa imeendelea kunyesha ndani na muda ule ilikuwa Imeambatana na Upepo mkali sana. Yani Ukiangalia kupitia Dirishani Nje kulikuwa Na hali ya kawaida tu tena Jua lilikuwa limewaka kulikuwa hakuna mvua yeyote ambayo ilikuwa inanyesha. Ile hali Mimi sikutaka kushangaa sana maana nilikuwa najua kinachoendelea. Mshangao mkubwa ulikuwa kwa Mfanyakazi wangu Adela maana yeye alikuwa anashanga sana. Wakati tukiwa tunashangaa ile hali ghafla mvua ilikata na Mwanga mkali wa Jua uliangaza ndani. Ile hali tena ilinishitua sana na kuangalia tena juu ya bati. Nilipoangalia sikuamini tena Macho yangu nilipoona Juu ya ile Nyumba hasa chumba ambacho tulikuwa tupo kulikuwa hakuna bati wala gymsang board yeyote ile kulikuwa wazi kabsa na Mwanga wa Jua ulikuwa unaonekana. "Shemeji kuna nini mbona Mimi sielewi dada anapaa" Yalikuwa ni Maneno ya Mfanyakazi wetu Adela yaliyonifanya kuacha kuangalia Juu na kuangalia ile sehemu ambayo alikuwepo mpenzi wangu Maimuna. Kweli nilipoangalia nilishangaa Kumuona Maimuna akiacha Usawa wa ardhi huku akienda juu kwa mwendo wa polepole sana. Ile hali ilinishangaza sana maana Maimuna Muda ule alikuwa kwenye mavazi meupe yote tofauti na yale ambayo alikuwa amevaa CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mwanzo. Kwa kweli sikuwa tayari kuona Maimuna anaondoka machoni Mwangu kwa namna Ile maana bado sikuamini kama amekufa niliamua kwenda kumfuata ili kumzuia. Nilipoenda kumshika cha ajabu nilipigwa na kitu kama shoti ya Umeme ambacho kilinirusha na kwenda kunipigiza chini. Ule mshituko kwa kweli ulikuwa wa hatari maana hata kuamka tena nilishindwa nilibaki nikiwa nimelala pale chini chali huku nikiangalia Mwili wa Maimuna ukipaa taratibu. Muda ule Mfanyakazi wangu alibaki akiwa anatetemeka tena mbaya zaidi. Binti wa watu pamoja na umri wake kuwa mkubwa lakini muda ule hadi mikojo ilikuwa inamtoka. Sikuwa na jinsi nilimwangalia Maimuna akipaa huku machozi yakiwa yananitoka maana sikuamini kama ule ulikuwa Mwisho wa kuonana na Maimuna. Baada ya Maimuna kupaa na kuvuka usawa wa nyuma ghafla hali ya nyumba ilirudi kama kawaida. Tena cha ajabu kulikuwa kupo vile vile hata ile mvua iliyokuwa inanyesha ndani hatukuona hata maji wala Unyevu wa aina yeyote. "Shemeji kuna nini mbona haya Mambo yanayotokea hapa ni Mageni sana kwangu. Kitu gani kimempata dada yangu Maimuna, au Shemeji wewe ni mchawi"Aliongea Adela huku akiwa anazidi kushangaa zaidi. "KAPOPO NIFATE NIFATE HARAKA NJOO KISIWANI"Ilisika sauti kutoka kwenye kioo kikubwa ambacho tulikuwa tunatumia na Maimuna kwenda kisiwani kabla hata sijamjibu swali ambalo alikuwa ameniuliza adela. Ile Sauti iliposikika ilifanya moyo wangu kulipuka na kugundua hali ya hatari sasa inaenda kutokea. Cha ajabu kile kioo kilianza kutoa na chenyewe Ngurumo na cheche hivi. Kile kio kilipoanza kutoa zile Ngurumo nilishanga na mimi naanza kuvutwa kuelekea kwenye kile kioo, hata nilipojikaza nisiende lakini ilishindikana.
Kwa kweli baada ya kujikaza kile kioo kisinivute na kunipeleka upande kilipo na kuona imeshindikana bado kinanivuta niliamua kukubali na kuamka nikaanza kusogea kuelekea kwenye kile kioo. Nilipokaribia nilishangaa kinanivuta kwa kasi ya ajabu na kuingia ndani ya kile kioo. Nilipoikigusa tu kile kioo sikujua kilichoendelea. Niliposhituka nilijikuta nipo chumba ambacho nilikuwa nimelala kwa Mara ya mwisho kisiwani. Kile chumba kilikuwa kipo kwenye nyumba ya Mzee hijirafu na ndio ilikuwa chumba cha Mwisho kulala na Maimuna kisiwani kabla hajafa. Nilipochunguza kwa makini kwenye kile chumba niliona Mwili wa Maimuna ukiwa umehifadhiwa kwa vazi jeupe na kuacha uso tu ulikuwa unaonekana. Ile hali kwa kweli ilinifanya machozi yalianza kunitoka tena. Bado sikuamini kama ule ulikuwa Mwisho wa kumuona maimuna tena. Niliamka pale kitandani na kuanza kutembea kuelekea sehemu ambao ulikuwepo mwili wa Maimuna. Nilipoifikia ile sehemu na kuinama kumshika Maimuna nilishangaa natokezea sehemu ambayo kulikuwa na watu wengi sana wa kiume ambao walikuwa wapo sehemu ambayo bila shaka ilikuwa ni makaburini. Wale watu wote walikuwa weupe wakati nikiwa nachunguza kwa makini ndipo nilimuona Mzee wangu akiwa anammbembeleza Mzee Hijirafu baba yake na Maimuna. Ile hali ndio ilinifanya Kugundua kuwa tulikuwa tupo kwenye mazishi ya Maimuna. "Jamani naombeni Msimzike Maimuna bado yupo mzima. Mzee wangu Hijirafu tafadhari waambie wasitishe hili zoezi la kumzika maimuna wangu maana hata bado sijamwaga"Niliongea kwa sauti haya maneno huku Machozi yakiwa yananitoka. Cha ajabu nilipoongea haya Maneno hakuna hata mtu mmoja ambae aligeuka kuniangalia zaidi ya watukuendelea na mambo yao. Ile hali ilifanya nianze kutembea kuelekea pale kaburini ambapo ilionekana ndipo wanamzika Maimuna. Nilipofika pale nilikuta ndio mwili wa Maimuna unatolewa kwenye kitanda unaingizwa kaburini. Ilibidi na Mimi kuingia hadi kaburini kuzuia ile hali. Cha ajabu nilipoingia kaburini wazo la kuzuia maimuna kuzikwa liliondoka kabsa zaidi ya kushirikiana na watu ambao walikuwepo kaburini kupokea mwili wa Maimuna. Tuliupokea mwili wa Maimuna tukauungiza hadi kwenye mwana andani. Mwana andani ulijengewa vizuri kisha tulitoka na kuburi lilianza kufukiwa. Kitu ambacho kilinishangaza Muda ule kwa kweli nilikuwa sina huzuni wowote zaidi ya kuona kawaida tu. Baada ya mazishi kumalizika cha ajabu watu wote walipotea na pale nilibaki mimi Mzee Hijirafu na Mtoto wake wa kiume Daudi. Daudi alinishika mkono na kuanza kunivuta kuelekea sehemu ambayo baba yake alikuwa anaenda. Tulienda hadi sehemu ambayo kulikuwa na gari nyeupe imepaki tukapanda na Safari ya kuelekea sehemu ambayo sikuijua ilianza. Kwenye gari Muda wote mzee hijirafu alikuwa analia tu. Kile kitu kilizidi kuniumiza sana ila sikuwa na huzuni sana hasa hata nilipokuwa najitaidi ili na mimi kulia nilikuwa nashindwa. "Mwanangu mimi siwezi kukulaumu wewe, namlaumu Yusira kwa kile ambacho amekifanya. Yusira kwa kweli kanifanya nimewapoteza watu watu muhimu. Nimekupoteza ww mwanangu kapopo, nimempoteza mwanangu maimuna na mjukuu wangu. Kwa kweli siamini kama Mwanangu angeniadhibu hivi lakini kwa nini Yusira anafanya hivi"Aliongea mzee huku akizidi kulia. Yale Maneno kwa kweli yalinifanya kubaini kuwa wameshafahamu kuwa yusira ndio alifanya vile. Kitu ambacho kilikuwa kinanishangaza kwa muda ule ni hali ya Mzee Hijirafu kusema kuwa na mimi amenipoteza bado sikuelewa amenipoteza kivipi. "Mzee mimi bado nipo upande wako, haijarisha maimuna kufa pamoja na mtoto wangu tumboni ila mimi bado nitakuwa Mwanao tu. Pia naombeni Msameheni Yusira kwa kile alichokifanya maana hajui alitendalo"Nilimwambia Mzee Hijirafu kwa sauti ya huzuni. "Kapopo unaongea hivyo kwa kuwa Hujui kile ambacho kinaenda kutokea, mwanangu hujui kile ambacho kinaenda kunipata. Mwanangu wewe hautakuwa upande wangu tena wala sitakuona tena labda ukubali na wewe kubadilika kuwa jini. Yani ukubali wewe kubadilishwa kutoka ubinadamu wa kawaida na kuwa jini. Hata hivyo bado itakuwa vigumu kidogo maana ukoo wangu sizani kama watanielewa na sijui na wewe kama utakubali. Kumsamehe Yusira mimi kama baba yake tayari nimemsamehe ila hata yeye sitakuwa naye tena. Sisi majini hatuna Gereza la kuwafunga majini waliofanya makosa kama binadamu mnavyofanya. Sisi Majini mtu akifanya kosa la kuua huwa tunajikuzasanya tunamsomea hadi na yeye anakufa. Hivyo kwa hili kosa Yusira ambalo amelifanya hataendelea tena kuwa hai na yeye atasomewa dua hadi atakufa. Hivyo Mwanangu mimi sina kitu sasa hivi nitabaki na Daudi wangu tu"Aliongea Mzee Hijirafu maneno ambayo yalinifanya nibaki nikiwa nimemkodolea MachoCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa kweli yale Maneno ya Mzee Hijirafu yalizidi kuniumiza mbaya, Raha ambazo nilikuwa nazipata kipindi nikiwa na Maimuna ndio zilikuwa zinaenda kuyeyuka namna ile. Muda ule nilizidi kuomba yale ambayo nilikuwa nayaona iwe ndoto na Maimuna bado aendelee kuwa mzima lakini ukweli bado uliendelea kubaki vile vile. Baba yangu walikuwa na furaha huku wakiwa wanatembelea Magari kwa ajili ya mahusiano yangu na Maimuna. Rafiki yangu Mdete alikuwa tajari na kutembelea Gari kwa ajili ya uhusiano wangu na maimuna. Kama uhusiano wangu na Maimuna utakata ilikuwa inamaanisha maisha ya raha ilikuwa ndio mwisho. "Ukiacha na Masuala ya kumkosa mwanangu, mjukuu wangu na wewe pia mwanangu kila kitu ambacho ulikuwa unakimiliki kitarudi kwenye ukoo wa majini. Nilitamani sana Mwanangu uendelee kuwa na zile mali hususani zile ambazo zipo kwa baba yako, rafiki yako na zile ambazo mlikuwa mnatumia na Maimuna lakini sina jinsi. Mashariti ya Ukoo wetu wa majini unanibana maana unasema kila kitu ambacho ulimpa binadamu kama atashindwa kutimiza mashariti basi vinatakiwa kurudi"Aliongea tena Mzee Hijirafu maneno ambayo yalinishitua sana. "Mzee tafadhari naomba msifanye hivyo, jicho langu mimi nitamuangalia nani. Kumbuka mimi tayari nilikuwa ni tajiri na kama nitakuwa masikini watu wataniangaliaje. Mzee hijirafu mimi nipo tayari kubadilika kuwa hata jini ili mimi niendelee kumiliki hizi mali na kuwa mtoto wako. Mzee Kufa kwa Maimuna naomba isiwe Mwisho wa Mahusiano yangu na wewe. Bado wewe utaendelea kuwa baba yangu na nipo tayari kufanya chochote ambacho unataka ili niwe kama Mwanao tu"Nilimwambia Mzee Hijirafu huku machozi yakiwa yananitoka. Kwa kweli muda ule nilikuwa nipo tayari hata wanibadilishe kuwa jini kama alivyosema ili niendelee kumiliki mali na kuwa karibu na mzee Hijirafu. Sikuwa napata picha kama nitafilisika na kuwa mtu wa kawaida kama mwanzo watu wangenichukuliaje. Nilishazoe kila sehemu ambayo nilikuwa naenda nilikuwa natumia Gari sasa nirudi kwenye maisha ya kawaida ya kukodi baskeli ilikuwa kitu ambacho kilikuwa kinauma Sana. "Sawa twende Nyumbani tukawasikilize Ukoo wa Majini unasemaje maana mimi siyo msemaji mkuu. Kama nilivyokwambia Mwanzo natamani sana kuendelea kuwa na wewe ila mashariti ndio yananibana. Wewe tayari ni mchafu kwenye ukoo wa Majini hata kama Yusira ndio kakufanyia. Hapa tuombe Mungu ili kule wakakuelewe wazo lako la kutaka kubadilika kuwa Jini ili uendelee kuwa na mimi Mwanangu"Alinijibu Mzee Hijirafu kwa unyonge. Kwa jinsi ambavyo alikuwa anaongea Mzee Hijirafu ilikuwa inaonyesha uwezekano wa mimi kuwa na undugu na Majini ulikuwa Mdogo sana. Safari iliendelea pale kisiwani huku nikiwa naangalia ule mji mzuri kwa Uchungu zaidi maana nilihisi huenda ndio ikawa Mara yangu ya Mwisho kuona kisiwa kile. Huwezi Amini muda ule hakuna sehemu ambayo nilikuwa naipenda kama ile hata maisha yangu nilikuwa natamani kuishi hata huku Muda wote. Ndio maana nilikuwa nipo tayari hata kubadilika kuwa Jini ili niweze kuendelea kuwa kwenye sehemu nzuri kama hii na wazazi wangu waendelee kuwa tajiri. Muda wa dakika kama kumi na Saba tayari tulikuwa tumeshafika nyumbani kwa mzee Hijirafu. Tulipofika tuliingia hadi ndani, mle ndani nilikuta kuna watu wengi sana. "Karibu sana Mzee Hijirafu uje utoe nasaha za Mwisho kwa Mwanao maana Tayari yuko hapa tunamuombea ili na yeye afe. Najua itakuumiza sana Mzee ila mwanao tayari kavunja mashariti ya kijini hivyo lazima afe. Pia yule Mume wa Mtoto wako pia kuanzia sasa mkataba na Majini utaisha maana tayari ni mchafu. Haijarishi kafanyiwa kimakusudi au alikuwa na nia ya kufanya. Pia ule mpango uliotuomba kuwa Tumsamehe na tumwambia abadilike kuwa jini tumeusitisha. Yeye atarudi duniani kama kawaida na ataendelea na maisha yake maana hakuna kitu ambacho tutamzurumu zaidi ya Mwenyewe kukupotezea watoto wawili. Mali zetu zote tutarudisha kwa njia ambayo binadamu hawataona pia tutakupa laki nane kwa ajili ya kujengea nyumba ya kuishi maana kuna kitu tutakifanya ambacho kitakufanya ujenge nyumba nyingine mpya. Haya Maelezo ambayo nimeyatoa mzee wangu yanatosha hivyo mwambia kapopo hatutaki swali shukrani wala ombi la aina yeyote zaidi tunamtakia maisha mema huko duniani"Yalikuwa Maneno ya mzee mmoja ambayo yalinifanya hadi nilianza kuona kizunguzungu. Kauli ya kusema mimi nitarudi duniani na mali zote zitachukuliwa kwa kweli ilikuwa inaniuma sana. Niliangalia mbele yangu kidogo kumtazama mzee yule ili kuongea neno ingawa alisema hataki neno lolote. Nilipoangalia mbele nilishangaa kumuona Yusira akiwa kwenye Vazi jeupe huku akiwa analia sana. Tayari Yusira nae alikuwa mtu wa kufa maana ndio alikuwa anaombewa ile afe.
Kwa kweli hali ambayo alikuwa anaonesha Yusira ilikuwa ya huruma sana. Hata mimi nilipomuona huku akiwa kwenye vazi jeupe nilianza kumuonea huruma maana alikuwa anaenda kufa kifo ambacho alikuwa anakiona kabsa. "Kapopo naomba nisamehe sana kwa kukufanya kuwa katika maisha ambayo hujayapenda. Kama ningelijua ipo siku yangekuja kutokea haya kamwe nisingethubutu kufanya kitu chochote na wewe. Ambacho nataka kutoka kwako ni Msamaha wako tu kabla sijafa. Najua nimekufanyia kitu cha kinyama lakini naomba nisamehe ili nife nikiwa na amani. Kupitia tamaa zangu za kimwili nimempoteza dada yangu pamoja na mtoto wake tumboni, nimekufanya wewe kurudi katika maisha ya dhiki wakati ulishakuwa tajiri na mashariti ya Majini ulikuwa umeyaweza. Pia kupitia tamaa zangu za Mwili leo hii nakufa kapopo, siwezi kujilaumu sana maana hata mimi nilikuwa nakupenda sana. Dada yangu Maimuna nakuja huko wewe uliko ila naomba unisamehe mimi mdogo wako, sikujua kama kitu kama hiki kingetokea. Nilikuwa nafanya hiki kitu kwa mara ya mwisho ila na wewe ulitokea"Aliongea Yusira huku akizidi kulia. "Yusira siwezi kukusameheCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ hata siku moja. Hiki ambacho umenifanyia mimi ni Makusudi kabsa. Kumbuka Yusira kabla ya kufanya mapenzi nilikuwa nakusihi ila ulikuwa hutaki kabsa kunielewa. Nilikuelezea hadi madhara ambayo tutayapata mimi na wewe endapo tukifanya kitu kile ulichokuwa unahitaji lakini ulikataa na kunilazimisha kwa nguvu. Nasema siwezi kukusamehe hata siku moja leo upo huku kisiwani siwezi kukufanya kitu. Nakuacha unakufa na mimi ipo siku nitakufa, nikifa nitakukuta huko mbinguni ndipo nitakuja kukiwasha. Umeniharibia maisha yangu Yusira, kumbuka nimeacha shule na kumuoa Maimuna maana aliniambia maisha yangu yatakuwa mazuri. Leo hii wewe unaniharibia hivi. Sura yangu nitaificha wapi Yusira. Kama unataka mimi nikusamehe basi nakuomba Mrudishe Maimuna nianze kuishi nae tena, kama Kuishi nae itakuwa kazi basi naomba hata Nimuone tu kwa Mara ya mwisho"Nilimwambia Yusira huku Machozi yakiwa yananitoka na mwili wote nilikuwa natetemeka kwa Hasira. "Kapopo hicho ambacho umeniambia nauwezo wa kukifanya tena hata sasa hivi. Utamuona Maimuna sasa hivi hapa ila nomba uniambie uhakika kama utanisamehe"Aliongea Yusira. Mimi nilimwambia Yusira kama nitamsamehe maana nilikuwa na hamu sana ya kumuona Maimuna kwa mara ya mwisho. Baada ya kumwambia vile Yusira aliinamisha Uso wake chini kama mtu ambae alikuwa anaomba. Muda ule Majini wote walikuwa kimya mle ndani hakuna ambae alikuwa anaongea. Yusira aliinama kwa Muda kama wa dakika mbili hivi ghafla upepo mkali ulianza kuvuma mle ndani. Ulikuwa ni upepo mkali sana ambae uliambatana na Ngurumo za hapa na pale ambazo zilikuwa hazieleweki kabsa. Upepo ule ulitumia kama Muda wa dakika tano hivi kisha ulitulia. Ulipotulia ule upepo nilibaki nikiwa nashangaa nilipomuona Maimuna akiwa amesimama sehemu ambayo alikuwa amesimama Yusira. Kitu kilichozidi kunishangaza Maimuna alikuwa anatabasamu tu hali iliyonifanya kugundua alikuwa na furaha sana. Niliondoka pale kwa kasi ili kwenda kumkumbatia maimuna. Nilipomfikia na kutaka kumkumbatia cha ajabu nilikumbatia hewa na Maimuna hakuwepo. "Kapopo naomba umsamehe mdogo wangu kwa kile ambacho amekufanyia. Hata Mimi tayari nimemsamehe. Usiwe na wasiwasi kabsa mimi nakupenda sana huenda mwisho wa kuwa na mimi ulitakiwa kuishia hapa. Usiwaze kuhusu utajiri maana ulizaliwa hauna kitu cha muhimu ukitoka kisiwani nenda ukapambane nahisi Mungu atakusaidia tu. Huwezi kunikumbatia kapopo maana mimi sasa hivi nimeshakufa na nimekuja kimzimu kuja kukwambia kuwa umsamehe mdogo wangu kwa heli mpenzi wangu kapopo"Ilisikika sauti tu bila kumuona Maimuna. Baada ya Maimuna kupotea kwa kweli sikuwa na jinsi zaidi ya Kumwambia Yusira kuwa nimekusamehe. Kitendo cha Kumwambia Yusira tu kuwa nimemsamehe nilishangaa Kuona naishiwa na Nguvu na kuanguka chini kisha usingizi mzito ulinipitia sikujua kile ambacho kiliendelea. Nilipokuja kushitu nilijikuta nimelala nje ya nyumba yangu huku kelele za watu wakisema moto zilikuwa zimetawala. Niliamka pale chini na kuangalia ile sehemu ambayo kelele zilikuwa zinatokea sikuamini macho yangu nilipokuta nyumba yangu ilikuwa imewaka yote moto.
Kwa kweli sikuamini macho yangu niliposhituka na kukuta nyumba yangu ikiwa inawaka moto. Niliamka kwa kasi pale chini huku nikiwa nimechanganyikiwa na kuanza kutembea kwa kasi kuelekea karibu na nyumba yangu. Ili kuweza kufanya chochote kuhakikisha ule moto unazimwa. Nilitembea kama hatua mbili tu kwa mbele nilishangaa kumuona Baba yake na Maimuna anatokea kwa mbele yangu. "Mwanangu kapopo nini sasa ambacho unakishangaa wakati nilishakwambia hii siyo mali yako tena. Hii nyumba inaonekana inaungua ila haiungui. Sawa kwa macho yenu binadamu hii nyumba imeungua ila upande wa majini bado ipo vile vile. Ila hii nyumba inavyoungua ni kama inshara ya wewe kutokuimiliki tena. Inamaana kuanzia sasa hapa siyo kwako kabsa. Baada ya hii nyumba kuonekana inaungua baadae itaonekana kama inajengwa kumbe hakuna kitu chochote ambacho kimefanywa wala nyumba haijaungua. Ninachokuomba ondoka hapa nenda nyumbani kwenu ukamuelezee mzee wako uhalisia wa mambo yote. Pia siku ya Juma tano ambao ni kesho kutwa saa saba mchana mnatakiwa wote msiwepo mle ndani nyumbani kwa baba yako maana ile nyumba itapigwa na Radi ya kutumwa. Pia kwenye ile nyumba ile siku usichukue kitu chochote ambacho ni mali yetu. Yani Gari na vitu vyote vya thamani kwenye hiyo nyumba msichukue. Kama utachukua moja ya mali ya Majini basi hata wewe utapigwa radi siku ya nyumba yenu kupigwa Radi. Kesho kutwa saa sita kamili mvua ya upepo mkali itakuwa inanyesha na saa saba kamili ndio nyumba yenu itapigwa Radi. Pia nakuomba kuanzia leo kwenye nyumba hii ambayo imewaka moto usirudi tena hata kama itajengwa hurusiwi kuja kuingia humu. Kama ukija kuingia ndani ya hii nyumba basi ndio utakuwa Mwisho wa maisha yako. Kule kwa baba yako nyumba yenu itapigwa radi kabsa na itaanguka. Kwa kuwa kile ni kiwanja chenu unarusiwa kwenda kujenga nyumba nyingine mpya. Mwanangu kapopo nafanya hivi siyo kwa roho mbaya bali nahitaji uendelee kuwa salama maana sina jinsi mwanangu"Aliongea Mzee Hijirafu huku hadi machozi yalikuwa yanamtoka. Kwa kweli yale Maneno ya Mzee Hijirafu yalinifanya hadi niliishiwa nguvu na kukaa chini. Mtu ambae nilikuwa namiliki magari na maduka mbalimbali pale singida leo hii nilikuwa nafilisika taratibu. "Mzee kwa kweli naomba usinifanyie hivyo, mle ndani ya nyumba kuna pesa kama milioni tatu tulikuwa tunaweka na mpenzi wangu Maimuna. Hivyo tafadhari nakuomba niingie angalau nichukue zile pesa. Pia nahitaji kujua Yusira ameshakufa au bado"Nilimwambia Mzee Hijirafu huku nikiwa nimechanganyikiwa mbaya. "Kapopo huhitajiki kuingia humu ndani tena. Hata zile pesa miliona tatu siyo za kwako bali za majini. Yusira ameshakufa na hata Mazishi yake tayari yalikuwa yameshamalizika. Ambacho mimi nitakusaidia nitakupa zile laki saba ambazo majini walisema watakupa kujengea nyumba maana wakati ile nyumba inajengwa walibomoa nyumba yenu. Pia mimi nitakuongezea Milion moja maana laki saba hazitatosha kujengea hata nyumba ndogo. Ningekuwa na uwezo wa kutoa pesa hata milioni mia ningekupa ila sisi majini kimo cha mwisho kumpa mtu pesa ambae huna uhusiano wowote hususani binadamu huwa miliona moja. Nazani sina kitu chochote cha kuendelea kukwambia zaidi ya kukuaga na kukutakia maisha mema. Baada ya nusu saa hivi pesa ambazo nimekuhaidi kukupa utazikutaka kwenye mfuko wako wa suruali. Pia vitambulisho vyote vya bank ambayo uliifungua na kuifadhi pesa tayari tumesha vichukua"Aliongea Mzee Hijirafu na kupotea ghafla. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/"Mwanangu kuna nini mmefanya kwenye hii nyumba hadi moto umewaka. Lakini mzima mwanangu hujaungua na moto"Ilikuwa ni sauti ya mama yangu iliposikika nyuma yangu baada ya Mzee Hijirafu kupotea. Nilipogeuka kuangalia kwa kweli Sikuamini macho yangu nilipomuona mama yangu wakiwa na baba yangu pamoja na Mama yangu mdogo. Yani muda ule wote wawili mama yangu mdogo na mama yangu mzazi ambae nilikuwa najua nimemuua kwa kumtoa kafala. Nilipomuona mama yangu nilikumbuka usemi wa Maimuna kuwa akifa tu na mama yangu atakuwa anaonekana. Nilimkimbilia mama yangu na kwenda kumkumbatia kwa furaha. "Pole sana Mwanangu naona mabalaa yamewakabiri sana. Haya ni majaribu tu endelea kumuomba Mungu siyo muda hali yako itakuwa vizuri. Maana Mke wako kufa ni kama amefungulia na balaa nyingine maana hata rafiki yako mdete gari yake imepotea mazingira ya kutatanisha. Kinachozidi kushangaza zaidi baada ya Gari yake kupotea tu kesho yake tena Duka lake alikuta limeibiwa kila kitu. Yani huwezi amini Duka la vifaa vya simu kibao na simu kibao vyote vimekombwa. Maisha ya Rafiki yako kwa kweli ndio yameharibika maana amechanganyikiwa hata kufatilia ni nani wanaomfanyia hivi ameshindwa amekuwa mtu wa pombe tu"Aliongea baba yangu maneno ambayo yalinishitua na kugundua hata mali za mdete majini tayari walikuwa wameshachukua.
************************************************ Kwa kweli yale Maneno ya mama yangu ndio yalizidi kunichanganya zaidi. Ilikuwa vigumu sana kuweza kuamini kwa maneno ilibidi niondoke kasi kuelekea hadi dukani kwa Mdete. Kweli nilipofika Dukani nilikuta Duka lake ndio watu wanakarabati mlango. Yani mle ndani kulikuwa kweupe hata ule mlango aliyekuwa anakarabati alikuwa mtu mwingine ambae alitakakufungua biashara yake. "Unajua huyu kijana alijiamini sana kupita kiasi. Mtu duka linathamani ya Milioni kumi na tano alafu hakuna mlinzi unafikilia nini. Mimi nahisi hadi kufikia kuibiwa alikuwa amejitakia mwenyewe"Nilimsikia Fundi Mmoja akiwa anaongea. Baada ya kuhakikisha kweli Mdete alikuwa hana kitu ilibidi niondoke na mimi kuelekea kwenye Maduka yangu kwenda kuangalia na huko kitu gani kinaendelea. Maana hata huko niliambiwa kuwa ni mali za majini. Nilikuwa nahitaji kwenda kujua huko kitu gani kilikuwa kinaendelea au huko majini walikuwa wamejisahau. kutoka pale dukani kwa Mdete hadi sokoni ambako ndio duka langu kubwa lilikuwepo haikuwa mbali sana. Hivyo mwendo kama wa dakika kumi hivi tayari nilikuwa nimeshafika dukani. Watu njiani walikuwa wananishangaa sana maana haikuwa kawaida yangu kutembea bila Gari. Nilipofika pale dukani wafanyakazi wangu wote walikuwepo. Kabla Sijaingia hata Dukani kuulizia kitu kinachoendelea mfanyakazi mmoja ambae alikuwa anaitwa mzee Suma aliniita pembeni. Yule mzee mimi nilikuwa namwamini sana na ndio mzee ambayo mawazo yake tulikuwa tunayasikiliza pale. Tena uwepo wa yule mzee pale dukani kulikuwa kunaongezeka hata wateja maana moja alikuwa anafahamika kwa watu wengi sana pia uaminifu wake na Ucheshi ndio ulikuwa unawavutia watu. "Boss lakini kitu gani kimekufanya hadi kufikia kuliuza hili Duka lako. Unajua jana wakati umekuja hapa kuandikishana nakumuuzi duka mtu mwingine mimi sikuamini. Mbona Duka lilikuwa linakulipa sana kuna matatizo gani umeyapata hadi ufikie kuuza Duka. Maana nahitaji kupata ukweli bado sijaamini kabisa kama hili duka umeliuza"Aliongea Mzee maneno ambayo yalinifanya kushituka Kidogo. Maana jana mimi sikuwepo hata duniani alafu naambiwa nilikuwa nimeuza duka langu. Hadi hapo niliamini kama tayari hata hili Duka lipo kwenye mikono ya Majini. Nilichomwambia Mzee Suma kuna pesa nyingi sana Maimuna alikuwa anadaiwa bank alikuwa amekopa. Hivyo baada ya kufa ndipo bank walianza kufatilia kuchukua nyumba ndio nikaamua kuuza duka ili kuokoa nyumba yangu. Kupitia yale maneno mzee sumu hakuwa na swali tena zaidi ya kunionea huruma na kunipa pole. Baada Ya maongezi ya hapa na Pale hatimae niliondoka nakumuacha mzee Suma. Njia kila nilipokuwa nakumbuka mambo ambayo mzee Hijirafu aliyoniambia ndio nilizidi kulia zaidi maana pale ndio nilikuwa naenda kuwa masikini hivyo. Nilipeleka Mkono mfukoni baada ya kukumbuka kuwa Mzee Hijirafu aliniambia niangalie mfukoni baada ya nusu saa nitakuta pesa. Kweli nilipopeleka Mkono mfukoni nilikutana napesa. Hata nilipohesabu kweli nilikuta milioni moja na laki saba. Sikutaka kurudi tena kwenye ile nyumba iliyoungua moto. Niliondoka Moja kwa Moja hadi Nyumbani kwa wazazi wangu. Nilipofika nyumbani niliingia na kwenda kukaa kwenye sofa na kutulia. Kila nilipokuwa naangalia muundo mzuri wa ile nyumba na vitu vya thamani ambavyo vilikuwepo mle sikuamini kama kesho kutwa hii nyumba itapigwa na radi kisha tunakosa kila kitu. Nilikaa mle ndani kwa Muda kama wa dakika kumi hivi ndio nilisikia mlango wa nyumba ukiwa unagongwa. Nilipoenda kufungua nilikutana na Mdete huku mkononi akiwa amebeba chupa ya bia. mdete aliponiangalia cha ajabu hadi machozi yalianza kumtoka. Pamoja na kulewa pombe lakini bado alionekana alikuwa na huzuni wa kupitiliza. "Umeona kapopo kitu ambacho umekifanya hadi nimefirisika. Kapopo wazazi wangu walikuwa wananitegemea mimi nisome ili nije kuwasaidia. Sasa hata shule nilikuwa nimeacha sasa itakuwaje. Nitakuwa mgeni wa nani mimi sasa, kapopo Duka langu siyo kwamba limevamiwa ila Daudi kaka yake na Maimuna ndio ambae alikuja kuchukua vitu vyote pamoja na Gari. Kwenye macho ya watu wanajua duka limevamiwa na Gari imeibiwa lakini ukweli mimi ndio naujua. Kwanini sasa ulikubari kufanya mapenzi na Yusira amboa sasa hivi katufanya kuwa hivi"Aliongea Mdete kwa sauti ya kilevi yenye huzuni na machozi yalikuwa yanamtoka. Mdete alikuwa anaongea tu ila hakujua Ugumu wa maisha ya kumkwepa Yusira nilivyotumia lakini ilishindika. Ilibidi kumuelezea Mdete kwa ufupi hali iliyopo na kumwambia haya ndio maisha kuna kupanda na kushuka cha muhimu tusibweteke. Usiku wa siku ile kwangu ulikuwa mgumu sana maana ndio muda ambao niliwaelezea wazee wangu kila kitu. Niliwaeleza hadi nilipoishi zaidi ya Mwaka nikiamini mama yangu nimemtoa kafala. Hadi sababu ya kifo cha Maimuna niliwaambia. Wazee kwa kweli walibaki wakiwa wanashangaa tu maana ilikuwa vigumu kuamini kama nilikuwa naishi na Jini. Wazazi wangu ni waelewa sana hivyo baada ya kuwaeleza hawakuwa na nguvu za kung'ang'ania zile mali. Siku hiyo tuliongea mambo mengi sana. Siku ya tatu ambapo tuliambiwa ile nyumba itapigwa radi tuliamka asubuhi na kuondoka. Kweli Muda wa saa sita mvua ilianza kunyesha huku kukiwa na ngurumo za hapa na pale. Mvua ilipoisha na kwendaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Nyumbani kweli tulikuta nyumba yetu ilikuwa imesambalatishwa mbaya. Kwa kweli watu walikuwa wanatuonea huruma sana na wengine walianza kuhisi huenda mimi nilikuwa nimejiunga na Freemason nimeshindwa mashariti na mali zilikuwa zinarudi. Maana matukio yangu ya nyumba kuungua na Moto huku nyingine kupigwa radi ilikuwa inajenga picha tofauti kwenye vichwa vya watu. Baada ya nyumba kupigwa radi tulitafuta nyumba tukapanga kwa muda wa mwezi mmoja huku nikifanya mpango wa kujenga kinyumba kingine kupitia ile laki saba. Baada ya mwezi mmoja tayali nilikuwa nimekamilisha nyumba ya vyumba viliwi na sebure. Muda ule maisha nyumbani kwa kweli yalikuwa Magumu sana kuliko hata Mwanzo. Tulihamia kwenye kile kinyumba na Maisha yaliendelea. Niliendelea kuishi maisha ya shida huku nikipambana kutafuta pesa ili kuweza kufanikiwa. Hadi muda wa Mwaka mmoja unaisha maisha yaliendelea kuwa Magumu vile vile na niliyazoe na kuishi maisha kama ya watu wengine wenye kipato cha chini. Hadi muda ule sikuwahi kumuona mzee Hijirafu wala jini wa Aina yeyote.
MWISHO
.jpeg)
No comments