SITASAHAU NILIVYOFANYA KAZI YA KUNUNUA KONDOMU ZILIZOTUMIKA.
Sehemu ya Kumi ( 10 )
***********
Tulipoishia
“ hakuna babu anayelinda hapa. Hili ni lindo langu, huu mwaka wote niko mm hapa.” Alniambia.
Hakika nilishangaaa. Yalikuwa ni maajabu, macho yalinitoka isivyo kawaida na kichwa kilizid kuniuma. Maumivu yalkuwa makal isivyo kawaida. Nilinyongonyea nikawa nimekishika kichwa na pale pale nilianguka chini mzima mzima.
……………………..
Nilizinduka nikajikuta nipo hospital, mbaya zaidi sikuwa kwenye wodi ya kawaida, nilikuwa kwenye wodi ya vichaa.
“ Kwanini nipo hapa?” Nliwaulza wenzangu.
“ Hakuna alyenijibu. Kila mmoja alikuwa bize na yake. Haraka haraka nlshuka ktandani. Niliangaza kushoto na kulia nikamuona mama na baba wakiwa wanakuja nilpokuwa mimi.
“ Mwanangu pole sana.” Aliniambia mama.
“ imekuwaje nipo hapa?” Niliwauliza.
“ Inamaana haukumbuki yaliyotokea?” Aliniuliza baba.
“ Nakumbuka mara ya mwisho nilikuwa naongea na mlnz wa lodge! Baada ya hapo sjui nni kilitokea.” Niliwaambia. Baba na mama waliangaliana kisha baba akanishika mkono.
Aliniambia siku naongea na mlinzi wa lodge, wiki moja nyuma nilianguka na kupoteza fahamu, aliniambia baada ya kuzinduka nilianza kufanya vitu vya ajabu! Anasema eti nilianza kufukuza watu hovyo na pia nilikuwa naokota makopo.
“ Aaaah”
“ Hivyo ndvyo ilivyokuwa mwanangu.Baadhi ya watu wanaokujua walitupigia simu ndio tukaja. Tulikukamata kwa nguvu na kukuleta hapa hosptali. Hii ni hospital ya vchaaa.”
“ Inamaana nimekuwa kichaaa?”
“ Kwa matendo yako inaonesha hvyo! Moja ulkuwa unafanya vitu visivyoeleweka! Hebu fikiria nyumba unayao lakin ulikuwa unalala mtaani.” Aliongea baba. Maneno yake yalinivunja nguvu kabisa.
“ Laakin naanzaje kuwa kchaaa?”
“ Ukiuliza hivyo unakosea! Kla mwanadamu anaweza kuwa kichaaa, lakn pamoja na hilo bnafsi niliamua kufatilia. Licha ya kukuleta hapa hosptali, pia nilienda kwa mganga kumuuliza kuhusu hili. Alipoangalia alsema unavita na majini. Kuna mambo ulkuwa unayafanya ambayo yalikuwa yanawakera na kuharibu mipango yao, hvyo waliamua kukunyeshwa dawa ndio mana ukawa hiv.”
“ inamaana mzee sudy alkuwa ni jinni?” Niljuliza.
“ Hapana..hapana..” Nilijiambia, haraka nlimuomba baba aende kwa mzee sudy. Nilmpa ramani kama alvyonpa mzee sudy. Baba muda ule ule aliondoka na kuniacha na mama.
“ sasa nipo sawa. Nazani naweza kuruhuswa kurudi nyumbani.” Nlimweleza mama.
“ Subir tupate majibu kutoka kwa waataalamu.” ALiniambia.
…………
Masaa mawli mbele, baba alirudi na majibu yaliyonichanganya .
“ Ulposema niende hakuna nyumba zaidi ya shule. Pia mtaa wote ule hakuna mtu anayeitwa mzee sudy.” Aliniambia.
“ Hapana..hapana..” Nlmwambia nikiwa nataka kushuka kitandani.
“ Unataka kwenda wapi?”
“ Kwa mzee sudy, bila shaka umekosea. Umeenda sehemu ambayo sio.’ Nilmwambia, lakini kabla hajanijbu nilikumbuka kaul ya mlinz wa kwenye ile lodge kuwa mlnz wa pale ni yeye wala sio mzee sudy.
“ Ulkuwa mchezo.” Nilijkuta nmetamka.
“ Ni kweli ulkuwa mchezo! Na kama sisi tungekuleta hospital haraka haraka pasipo kwenda kwa mganga bila shaka had sasa ungekuwa kchaaa.” ALiniambia baba. Licha ya maelezo hayo walinisihi niendelee kukaa hospitali.
Nilikubali.
Siku ya tatu niliamua kuomba ruhusa, licha ya hali yangu kutokuwa nzuri nilimtaka daktar aniruhusu nirudi nyumban! Nilimuahidi kurudi siku ya pili kwa uangalizi zaidi.
Alkubali.
Nlitoka hosptali na kuelekea nyumban! Majirani na baadh ya watu wengine walinishangaa. Wengi wao walinikwepa. Nadhani waliamni mimi ni kchaaa. Sikuwajali. Nilienda hadi nyumbani kwangu. Niliingia ndani na kuangalia mazingira ya chumba changu.
Yalikuwa yapo vile vile.
Nilitoka nje na kuelekea nyumban kwakina ashura.
“ Kwanni nikutane njiani na Ashura akiwa na kwato? Na kwanin alkuja kunilaumu kwa yeye kukosa mtoto.” Nlijiulza nikiwa naelekea nyumban kwake. Mitaa kadhaaa kufika, kauwoga fulan kaliniingia! Nilkumbuka ilivyokuwa ile siku usiku.
‘ Akiwa mchawi si anaweza kuniua huyu mshenzi?” Nilijiulza.
“ Potelea mbali! Liwalo na liwe. Haiwezekani anifanyie ujinga ! Leo atanieleza kwanin alisema mmi ni chanzo cha yeye kukosa ujauzito! Pia atanieleza sababu ya kunitokea usiku akiwa na makwato yake.” Niljiambia.
Nilijitutumua bila woga nikaenda kugonga mlango wao.
‘ Karibuuu.” Nilisikia sauti ya alex ndani.
‘ Ahsante” Niljibu.
Alex alkuja kufungua mlango.
“ Rich..” ALinshangaaa.
“ Usinishangae..namtaka mkeo sasa hivi.” Nilimwambia.
“ Aaaah! na ukichaa wako unataka kumfanya nin mke wangu?”
“ Mim sio kichaa aiseee.. mlete mkeo nje hapa..” Nilimwambia. Mabishano yetu yaliwafanya watu waliokuwa ndan waje. Tukiwa tunabishana nilimsiia ashura akimwambia babu yake abaki ndani yeye anatoka kuangalia kuna nini.
“ Siwez kukuacha uende huko nje peke yako.” Babu yake alijbu, nae almfata mwanae kwa nje. Wote walitoka nje.
“ Aaaah!” Nliduwaa baada ya kuwaona. Babu yake ashura alikuwa mzee sudy.
Mkiwa wavivu kucoment namimi nakuwa mvivu kupost hivyo comment kwa wingi jamani ili mnie mizuka
# PIA USISAHAU KUNI FOLLOW ILI USIWE UNAPITWA NA STORY ZANGU FAIDA YA KUNI FOLLOW NI KUWA WA KWANZA KUPATA STORY KILA NINAPO POST
No comments