Header Ads

Header ADS

18 - SITASAHAU YALYONIPATA WAKATI NAFANYA KAZI YA KUNUNUA SALAMA ZLZOKWSHA TUMIKA


Sehemu ya Kumi na Nane ( 18 )
********
Nilikata smu haraka na kuelekea La vede Hoteli.
Nyumba ya saba kutoka nyumbani, nilikutana na rafiki yangu wa utotoni aitwae John! Huyu jamaa nilisoma nae shule ya msing na secondary, ni jamaa yangu sana. Utoto wetu wote tulicheza wote.Tulitengana baada ya kumaliza Sekondary. Yeye alienda dar kusimamia lodge ya ndugu yake .
Ndani ya miaka mitatu baada ya kuanza ile kazi maisha yake yalibadilika sana. Alinunua kiwanja pale mtaani na kujenga nyumba, pia nasikia kule dar alijenga lodge yake na kuacha kufanya kazi kwenye lodge ya ndugu yake.
Licha ya kutajirika kwa haraka na kusaidia ndugu zake, mpaka sasa utajiri wake hakuna aliyekuwa anajua chanzo chake na wala haieleweki hela za kufanya yale yote alipata wapi.
“ John…john..” Nilimwita.
“ rich..’ Alitamka kwa mshangao baada ya kuniona. Tulisogeleana na kukumbatiana kwa nguvu sana.
“ Nimekutafuta sana ndugu yangu!” Nilimwambia.
“ Acha utani… “
“ Kweli sitaniii..nimekutafuta sana.” Nilimwambia.
“ Mmmmh! basi umenipata ndugu yangu..niambie..”
“ Mwanangu mwenzio maisha yamenipiga… tena sio kidogo yamenipiga hadi sio poa.. hapa unaponiona sina mbele wala nyumaaa.. kifupi sina kazi inayoeleweka..”
“ Inamaana hata mdogo wako yule genius kashindwa kukutafutia mchongo?’
‘ Aaaah! yule hapana. ALinipa kazi lakini ilinishinda! Kwanza ile haikuwa kazi.. ni matatizo..” Nilimwambia. John hakuongea neno, alinishka mkono na kunivutia pembeni. Tulipiga hatua kadhaa tukaingia kwenye grocery jirani yetu.
“ Nipe kaz hata kwenye lodge yako john..”
“ Mmmh! siwez kukupa kazi kwenye lodge yangu..itakuwa sio poa kabisa. Nitakufundisha mishe niliyokuwa naifanya mimi! Ukiwa makini nawe utatajirika baada ya muda mfupi sana.” Aliniambia. Nilikaaa vizuri kwenye kiti changu na kutega sikio vizuri.
“ Kabla sijakuambia kitu chenyewe, kwanza naomba nisaidie nikutane na kaka yako! Nasikia yuko hapa.”
‘ inamaana safar yako kutoka dar ni kwa ajili ya kaka?’
“ Ndio nina jambo nae kubwa sana..” Aliniambia. Twiiiii. Simu yake iliiitana kwenye kioo cha simu likatokea jina la mchungaji. John alipokea na kusogea pembeni. Aliongea kwa dakika kadhaa kisha akarudi nilipokuwa mimi.
“ Unadeal na wachungaji siku hizi?” Nilimuuliza.
“ Huyu niliyeongea nae ni mchungaji mkubwa sana dar! Tena anakanisa lake kubwa sana..na yeye ndo chanzo cha mimi kutajirika haraka.”
“ Alikuombea?’
“ Hapana..kuna bidhaa nilikuwa namtafutia na kumpelekea. Sasa hizo bidhaa nasikia kaka yako nae alikuwa anazinunua..hivyo nilitaka kuongea nae, ikiwezekana tufanye biashara.” Aliniambia
Mmmmh! nilguna kimoyo moyo. Akilni niliwaza kaka hakuna bidhaa nyingine aliyokuwa ananunua zaidi ya kondomu. Nilijaribu kuunganisha matukio lakin haikuingia akilini.
“ Kama alikuwa anamkusanyia mchungaji bidhaa aliyokuwa anaitaka kaka inamaana huyo mchungaji alikuwa anataka salama zilizokwisha tumika?” Nlijiuliza pasipo majibu.Nikiwaza hayo, John alipokea simu nyingine. Alisogea pembe kuongea kisha akarudi na kuniambia inabidi aende dar muda ule ule.
“ Tutaongeaa..inabidi niende dar sasa hivi.” ALiniambia na kuondoka pale grocery.
Nami sikukaaa, muda ule ule nilismama na kuelekea la vede hoteli kukutana na kaka.
……………………..
Nilifika.
“ Kuna nni kimetokea? imekuwaje baba, mtu ambaye alikupenda kupita maelezo akakufukuza nyumbani .” Nilmuulza.
“ Ni elmu na kutojielewa.” Alinijibu kifupi.
“ Broo acha utan! Kutojielewa ndio kumfanye hadi mama awe vile?”
Hakunjibu, badala yake alimgeukia mwenzake na kumpa ishara atoke nje.
Altoka
Alinishika mkono kisha akanitazama machoni.
“ Unakifua?”
“ Ninacho.”
Mkiwa wavivu kucoment namimi nakuwa mvivu kupost hivyo comment kwa wingi jamani ili mnie mizuka
# PIA USISAHAU KUNI FOLLOW ILI USIWE UNAPITWA NA STORY ZANGU FAIDA YA KUNI FOLLOW NI KUWA WA KWANZA KUPATA STORY KILA NINAPO POST
May be an image of 1 person and text that says "18 2 SITASAHAU NILIVYOFANYA ΚΑΖΙ YA KUNUNUA KONDOMU ZILIZOTUMIKA."
All

No comments

Powered by Blogger.