26 SITASAHAU YALYONIPATA WAKATI NAFANYA KAZI YA KUNUNUA SALAMA ZLZOKWSHA TUMIKA
Sehemu ya Ishilini na Sita ( 26 )
********
“ Toka nje hapo kisha fata hio kordo had mwsho utakiona choo.’ Aliniambia. Haraka nilisimama nikiwa naenda choon, njiani,nilikiona kisu kikiwa jikoni, haraka nilikiwahi na kukificha mgongoni.
Nilitembea taratibu kuelekea kwenye kile chumba.
“ Nimuue kwanza huyu kisha nikamuue kaka?” Nilijiulza.
“ Hapana! Atapiga kelee kisha kaka atashtuka. Dawa ni kufanya kimya kimya, naenda kumuua kaka kisha nammalizia huyu kuondoa ushahidi.” Niliwaza. Nilimpita kwa tahadhar kubwa pasipo yeye kukiona kisu changu.
Niliingia kwenye kile chumba alichokuwa kaka.
Nilimkuta yuko bize na laptop yake.
“ Kwahiyo mdogo wangu nazani tumeelewana. Mzigo ni huu hapa, Kesho utaondoka kwenda dar es salaam na Kuhusu usalama wa hizi pesa na utafanyaje kuzipata hizo salama, hio ni kazi yako.” Aliniambia.
“ Sawa..sawa…” Nilijibu nikiwa natetemeka, Mkono wangu ulioshika kisu ulicheza kwa hofu. Nilitaman kumchoma lakin sikuwa na ujasir wa kufanya hivyo.
“ Mbona unatetemeka? Umechukua kisu unataka kuniua?’ Aliniuliza kaka.
‘ A…a….aaa’
“ huwez niua mdogo wangu! Huwezi…” Aliniambia
Alinigeuzia laptop nikaona video wakati nikiwa naenda choon hadi nachukua kisu.
“ Hiii nyumba ina kamera kila sehemu! Hata ungefanikwa kuniua bado ungekuwa ni uamuz wa kijinga sana! Kama baba na mama wameshakufa, la msing hapa ni kufanya kile ninachokuambia ili uweze kubadilisha maisha yako! Hiv unazan utaish kimasikini hivi hadi lini?’ ALiniuliza.
“ Hela sio kitu kaka. MUNGU hapendi unayoyafanya?”
“ MUNGU?’
“ Ndio MUNGU! Unayofanya ni kinyume na amri zake.’
“ Ahahaha..ahahaha..ahahaha..ahahaha..’ Alicheka kaka. Ksha kwa dharau sana aligeukia akaniuliza ni mungu gani ninayemzungumzia.
“ Unajua namzungumzia yupi?’
“ Kwahiyo huyo MUNGU wako anaupendo? Hatend mabaya?’
“ Ndio yeye ni mwema na anaupendo! Kupitia yeye sisi tunaishi. Katupa hewa safi na vngi vingne bure.”
“ Acha kujidanganya mdogo wangu! Huyo MUNGU unayemzungumzia anaroho mbaya na anamaovu meng kulko mimi! Hebu fikiria bila huruma aliwaua wamama wajawazito na watoto wachanga.”
“Aliwaua wapi?’
“ Hivi hujasoma kuhusu sodoma na gomora?’
“ Nimesoma , ule mji ulijaa dhambi ndio mana aliamua kuuteketeza kwa moto.”
“ Basi katka kuuchoma ule mji bila huruma huyo MUNGU wako aliwachoma moto wanawake wajawazito na watoto wachanga wasiokuwa na makosa! Halafu huyo MUNGU mnasema anajua mambo hata kabla hayajatokea, na kama ni hvyo kwanin asingewazuia watu wa ule mj wasitende dhambi?’
“ Dhambi n kaz ya shetani , shetan ndio anawashawsh watu?’
“ Huyo shetan alumbwa na nani?’
“ Aliumbwa na MUNGU kama malaika, ila alipohas ndio akatupwa duniani kama shetani.”
“ kwahio huyu MUNGU wako wakati anamuumba huyo malaika aliyehasi hakujua kama atahasi? Kama alijua kwanini alimuumba?”
“ Broo, hizi kauli zako ni kufuru.. utalaaniwa kwa hili…” Nilimuambia na kuelekea nje, lakin kabla sijafika popote kaka aliropoka.
“ Ukitaka kupambana na mimi kwanza tafuta hela! Kwenye dunia ya sasa hakuna masikini anayesikilizwa, si uliona mwenyewe kwenye msiba! Nani alikusikiliza pale! Licha ya kuwa ulkuwa unaongea mambo lakin hakuna alyekusiklza.’
“..Hata polis pia! Hakuna aliyekusikiliza, ulienda na hoja ya msing sana, lakni hawakukusikiliza, ila mimi bia hoja bila nini nilimtumia mpelelez milioni tatu kisha nikamwambia wewe ni muuaji, bila hata kuulza alikuja kukukamata. Na hiv ndivyo dunia inavyoenda, hvyo mdogo wangu tafuta hela.. hata kama unataka kulipa kisasi kwangu..tafuta helaaaaaa..” ALiniambia.
Maneno yake yaliniingia.
“ ni kweli, inanipasa niungane nae kwanza ili nipate pesa.” Niliwaza.
Mkiwa wavivu kucoment namimi nakuwa mvivu kupost hivyo comment kwa wingi jamani ili mnie mizuka
# PIA USISAHAU KUNI FOLLOW ILI USIWE UNAPITWA NA STORY ZANGU FAIDA YA KUNI FOLLOW NI KUWA WA KWANZA KUPATA STORY KILA NINAPO POST

No comments