Header Ads

Header ADS

NIPUNGUZE NYEGE SEHEMU YA 02



By Steve
WhatsApp 0765 441 971
Umri🔞
_____ ILIPOISHIA_____
"" yule kijana paschal yule!""
"" enhee! Kawaje tena Rafiki yangu?""
"" naomba awe ananiletea siku nikishindwa kuja huko!""
"" ahahaha! Shoga yangu hilo nalo neno?,niwewe tuuuu! Mmh! Usiniambie umemuelewa shoga?""
""Hahaha halooo!! Kwani mi sifai kua na mpenzi?""
Basi huo ulikua ni utani baina ya marafiki wawili waliozoeana sana..
______SONGA NAYO_____
Basi kama maagizo yalivyokwisha kuachwa kesho yake asubuhi na mapema mama Halima aliandaa chai mapema ili aweze kuwahi kazini kwake,kutokana na ujasiliamali alokua nao aliweza kumiliki makampuni ya magari,sheli za mafuta pamoja na baadhi ya maduka,.hivyo angehitaji kuwajibika kupata hesabu za mauzo pamoja na kujua ni mizigo kiasi gani angehitaji kuingiza kwa ajili ya wateja wake,..
Aliweza kuzitembelea ofisi zake zote na ndipo aliweza kurudi jioni nyumbani kwa ajili ya mapumziko,,
Haikua Mara ya kwanza kwa mama Halima kuwa na ratiba kama hii iliyobananika pamoja na urembo wake alokua nao hakuona tabu kujibidisha na ndio maana alijikuta akiwa bize kupitiliza ye alichowaza zaidi ni maisha yake..huku biashara na huku malezi ya binti yake hivyo basi jioni anaporudi nyumbani hua amechoka sana hata muda wa ku starehe au wa kumfikiria mwanamme unadhani ungetoka wapi,haya ndio maisha aliyoyazoea na bila shaka kama alivyoweza kukiri mbele ya marafiki zake,,wanaume wangempotezea muda na malengo yake yote aliyokua nayo.
Hatimae ilikua siku ya tatu tangu achukue mahitaji yake kule supermarket kwa mama Ruth, na hivyo alitamani apate mahitaji mengine.
Aliwaza je aende ama aagize,lakini kutokana na kule kummisi kijana paschal moyoni mwake aliwaza akaona kua supermarket ndio oangekua mahali sahihi zaidi kumuona,na pia angeweza kumzoea kidogo kidogo pasipo yeye kushtukiwa na paschal,. Na pia angeweza kumwona shoga yake (mama Ruth)
hatimae aliafikia kwenda tu supermarket! Japo alikua kachoka kutokana na mizunguko ya Jana lakini aliamua kujikakamua kwani hata hivyo hakua akitumia miguu kwamba atachoka zaidi! Lahasha! Alitumia gari lake LA siku zote LA mizunguko aina ya range rover na kuingia mtaani!!..
Hatimae aliweza kufika supermarket, na baada ya manunuzi Yale alishangaa siku hii kutokuiona kabisa sura ya yule kijana mpya paschal kitu ambacho kiliufanya moyo wake udunde kwa kasi,,
Alimsogelea Rafiki yake mama Ruth na kuanzaa mazungumzo yao ya utani na kweli
"" shosti,vipi uko poa?""
"" Niko poa mama Halima, sijui wewe?""
"" mmmh! Shoga yangu Niko poa kiasi!""
"" mhh! Kiasi hicho vipi ndugu yangu na uzuri wote huo?"'
""Hahahahaa!! Eti uzuri!! Mama Ruth usinichekeshe!""
"" nakuchekeshaje tena shosti? Mmh! Ebu nambie kimekusibu nini hadi useme uko poa kiasi maana we ndugu yangu navyokujua hujuagi kukasirika au kukosa raha kirahisi!!""
'"Kwani hujui shosti??""
""Nijue halafu nikuulize kweli shosti??""
"" hahahahaa!! We daktari WANGU wa moyo Leo simuoni Rafiki yangu umempeleka wapi? ""
"'Hmmh!! Daktari gani au unamaanisha paschal?""
"" ndio kwa hujui daktari WANGU??'"
"" mmh shosti hivi uko siriazi,!!""
"" akia Mungu tena ,Yule kijana mi nimempenda sana yaani uuuwi sijui hata nifanyeje ili nimpate!!""
"" mmmh! Makubwa! Paschal hayupo shosti!""
"" kaenda wapi tena huyo kipenzi cha roho ya mie?""
"" paschal yuko hospitalini!""
"" what???(nini?),anaumwa??""
"" hapana,,kaenda kumwona mama yake ni mgonjwa kalazwa!""
Baada ya taarifa ile mama Halima aliwaza sana kwani alijua kua kama paschal kaenda kumuuguza mama yake,isingekua rahisi kurudi siku hiyo hiyo hivyo alijua kua atakaa huko kwa siku kadhaa ndo aweze kurejea!
"" Mungu wangu! Kwa hiyo paschal sitaweza kumuona kwa siku mbili tatu hizi? Mmmh!! Moyo wangu hauwezi vumilia lazima nikamuone,,lazima,kwanza najihisi kuchelewa asijependwa na mwanamke mwingine nikaipoteza tamu yangu!""yalikua na mawazo ya mama Halima
Kisha alimwomgelesha mama Ruth aliyekua bize na wateja
"" mama Ruth, kwani,wapo hospitali gani? ""
"" vipi unataka uende shoga yangu?""
"" ndio ngoja hata nikamjulie hali mgonjwa!""
"" wapo hospitali ya rufaa yetu hii,!!"
Hata kabla hajamaliza mama Halima alikurupuka haraka na kutoka nje huku mizigo yake akiidondosha chini na kuingia ndani ya gari bila hata kujali aliungurumisha mashine na kuelekea moja kwa moja mpaka hospitalini
Amefika hata wodi ama chumba alicholazwa mama paschal hakijui ikabidi amwombe mama Ruth namba ya paschal ili iwe rahisi kujua alikokua mama paschal
"" shikamoo mama Halima "" ilikua ni sauti ya Rose aliyekua amemshika bega paschal ishara ile ilionyesha kwamba wawili hawa wana mahusiano ya karibu sana kutokana na pozi walilokua wamekaa
""Marahaba ! Rose mbona uko huku!!""
"" mm mm..nam aaa nimekuja kumwona mama yake paschal!'"
"Shikamoo mama!" Alikua paschal
"" marahaba paschal we mzima!""mama halima alijikuta akiachia tabasamu lililonona huku kawivu kakimpanda kwa mbali kutokana na pozi walilokalia vijana wale wawili na hii ilionekana dhahiri baada ya Rose kuupitisha mkono wake kiunoni kwa paschal walipokua wakitembea kuelekea chumba alicholazwa mama paschal!!
"" ina maana paschal tayari ana mpenzi?? "".. Mama Halima alijiongelea kimoyomoyo
"" sikubali,mie ndo nishazimika hivyo lazima awe Wangu! ""
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Story hii pia unaweza kuipata kupitia group la Tamthilia tamu ama Whatsapp kupitia namba hizo happy juu!

No comments

Powered by Blogger.