Header Ads

Header ADS

Simulizi: Tabasamu langu sehemu ya nane(08)

 SIMULIZI ZA MAPENZI

 




"sikumkuta mtu yeyote, nilichukuwa mizido yetu nikaondoka zangu"


 


"ondoweni wasiwasi mtaishi hapa"


 


Salome alimshukuru Ila Mimi nilendelea kumtazama huku nikiwa najiuliza nawezaje kuishi hapa hali ya kuwa ana mke.


 


Salome aliponiona Kama vile sioneshi furaha aliniuliza kwa kiswahili ili wasisikie.


 


"Ndo nini sasa?"


 


"Han ni Mume wa mtu"


 


"Mume wa mtu?"


 


"Eee na haka katoto ni kabinti kake"


 


"Usiniambie"


 


Han na binti yake wakiwa wanatushangaa, tuligeuka kuwatazama kwa hasira mpaka wenyewe wakashindwa kuelewa.


 


Muda Huo sauti ya mschana ilisikika akisema.


 


"sweet upo wapi?"


 


Tulishtuka mno huku kila mmoja akiwa ameanza kuwaza wapi tutaelekea baada ya kufukuzwa kama mbwa, maana wanawake tunajuana.


 


 


 


Binti mrembo aliingia, baada ya kutuona alitabasamu na kumuuliza Han.


 


"kuna ugeni?"


 


Han alinyanyuka bila kuongea chochote na kumtoa nje. Tukabaki watatu. nikiwa namtazama Nana nilitabasamu na kusema.


 


" huyu mtoto Ananifanya nimkumbuke Munira wetu"


 


"Nikweli kabisa"


 


"Ninyi mtaishi hapa?" Nana alituhoji.


 


"Ndiyo! Yule ndo mama yako?"


 


"nijibu kwanza mtaishi hapa kama kina nani?"


 


"wee tutakutia viboko"


 


Nilicheka na kusema. "Mwaya Nana akikupiga nampiga"


 


"nimekupenda wewe Huyu simpendi"


 


Muda Huo proscuter Han aliingia akamuomba mwanae ampeleke Salome chumbani atakapokuwa analala.


 


Baada ya wao kutoka, Han alikaa na kuniuliza.


 


"unaendeleaje sasa hivi?"


 


"nipo sawa sema tu huyu Jacob akitoka sero afadhali nijinyonge kabla hajaniua"


 


"usiogope ntahakikisha anaozea huko.... Halafu Nana ni binti yangu, mama yake ameshaatangulia mbele ya haki"


 


"Maskini kwani Yule binti nae ni Nani?"


 


"ni Rafiki yake Nana"


 


"Rafiki yake Nana?"


 


Han alinishangaa baada ya kusikia Swali langu maana nilimuuliza kama vile simuamini anachokiongea, hata mwenyewe Nilishindwa kujielewa nikaamua kutabasamu.


 


"mtaishi hapa na mdogo wako"


 


Nilimshukuru Sana maana niliamini balaa zinaenda kuisha.


 


Baada ya siku mbili kupita, Mazingira ya nyumbani kwa proscuter Han tuliyazowea mpaka wao wenyewe tukazoweana.


 


Siku hiyo tulikuwa tumekaa Mimi na proscuter Han huku tukipiga stori mbili tatu, muda Huo Nana alifika na kumuuliza baba yake.


 


"eti baba Salome niwe namuita nani?"


 


"muite dada"


 


"huyu naye?"


 


"muite dada na yeye"


 


"Hapana"


 


"ulitakaje?"


 


"ntamuita mama"


 


Tulishtuka mimi na Han, kabla hatujaongea chochote Nana alikimbia huku akiwa anacheka.


 


Tulibaki hapo na aibu kubwa Mpaka maongezi hayakuendelea tena.


 


Upande wa pili Salome alikuwa na Nana jikoni.


 


"ulimuambia?"


 


"Eee nimemuambia ntamuita mama"


 


"haya Gonga tano sasa"


 


Waligonga tano kwa furaha.


 


Upande wetu kila mmoja alijifanya bize kusoma kitabu huku tukiangaliana jicho la wizi wizi.


 


Tukiwa tupo kimya, aliingia Yule binti ambaye yupo karibu sana na mtoto wa Han huku akisema.


 


"my Nana yupo wapi?"


 


Alipotufikia alitusalimia kisha akazunguka alipo Han nakukaa.


 


"Mbona Leo Nana hajafika shule?"


 


"hajafika?"


 


"yeah sijamuona kabisa"


 


"Mbona aliniaga eti anakuja?"


 


Muda wote mimi nilijifanya kuto kuwajali licha moyo wangu ulikuwa unaniuma.


 


"kesho kabla ya kwenda kazini ntamleta"


 


"please Leo nimeandaa kimchi Naomba twende nyumbani kwangu Pamoja na nana"


 


"Sawa"


 


Ritha alinyanyuka na kuanza kumuita Nana. Nana baada ya kumsikia mwalimu wake, alikuja huku akiwa akikimbia kwa kasi, alipomfikia alimkumbatia kwa furaha.


 


"haukuja shuleni kwanini?"


 


"niliumwa"


 


"Oohh my Gosh sorry"


 


"Kumbe madame unajuwa kingereza"


 


"eeee niliishi Marekani, Nana twende nyumbani kwangu nimewaandalia kimchi wewe na baba"


 


"wow Napenda Sana"


 


Anna alimfuata baba yake akaanza kumtikisa huku akimwambia.


 


"please baba twende"


 


"twende?"


 


"eee"


 


"sawa"


 


Ritha aliposikia kuwa Han yupo Tayari, alimuwahi na kuanza kumuinua ili waweze kuondoka, Han alisimama na kuniaga kisha wakaondoka.


 


Baada ya muda tukiwa tumekaa Mimi na Salome story zilikuwa zinaendelea.


 


"Yaani kirahisi rahisi Han anakubali kwenda na huyu binti tena kwake?"


 


"nahisi wapo kwenye mahusiano"


 


"siyo wewe tu hata mimi pia nahisi hivyo"


 


"Hivi ulivyoondokaga kule, yule jambazi ulimuonaga?"


 


"Hapana"


 


"Labda alikufa maana siku ile nilivyomshona sina imani kama angeweza kupona"


 


"usimhofie hata afe ni sawa tu"


 


"Nimeuliza tu. Kwalipi namhofia?"


 


"Hali yangu kila kukicha inakuwa mbaya hata sielewi na Pack Jin Ndo Hana hata habari na Mimi"


 


Muda Huo mlango uligongwa Salome akaenda kufungua, dakika mbili alikuja huku akiwa yupo Pamoja na Pack Jin, nilipomuona Nilinyanyuka nikamkumbatia kwa furaha maana muda umeenda na Hatuonani.


 


"mumenihangaisha sana" alinituambia.


 


"kwanini?" Nilimhoji


 


"Mlivyoondoka hamkuacha adress wapi mnaelekea. aisee nimewatafuta mpaka basi. "


 


" I'm sorry" Ndipo nilimgeukia salome na kumwambia.


 


"utapumua sasa?"


 


Salome kwa aibu alianza kunipiga Piga kwa aibu.


 


Majira ya jioni tulipomaliza kupiga story Pack Jin aliomba kutoka out na Salome, sikuwa na kipingamizi niliwaacha wakaenda.


 


Nilibaki hapo nikiwa mwenye upweke, nikaamua kutoka nje ili kupunga hewa, nikiwa nimetulia zangu, nilianza kuziangalia picha za familia yangu, taratibu machozi yakaanza kuniteremka.


 


Nikiwa nalia Han na binti yake walifika, waliponiona nalia walinifuata wakaniuliza kuna nini. Ila nilitabasamu na kuwajibu.


 


"ntakuwa Sawa msijali"


 


Han alimuomba Nana akalale, ndipo Nana alinibusu shavuni na kuingia ndani.


 


Tukiwa tumebaki wawili Han aliniambia.


 


"usijali yakupasa upunguze mawazo"


 


"ningumu sana mara nyingi nikiwa mwenyewe lazima niwe kwenye Hali hii"


 


Muda Huo upande wa pili Salome Pamoja na Pack Jin walikuwa wanakimbizana kwa furaha, huku wakiwa wanacheza michezo mbali mbali.


 


Siku iliyofuata niliamka mapema nikamuandaa Nana ili kumpeleka shule. Nilipomaliza kumuandaa alimuaga baba yake kisha tukaondoka.


 


Tulipokuwa njiani, nilianza kukumbuka siku ile nilivyowapelekaga wadogo zangu shule na nikaja kumpoteza mdogo wangu Abdallah.


 


Nana akiwa amenishika mkono aliniambia.


 


"mama angalia kule"


 


Baada ya kuniita mama nilichuchumaa na kumuuliza.


 


"nani alikuambia uwe unaniita mama?"


 


"Kwani haupendi?"


 


"usiniite hivyo baba yako hapendi"


 


"mi nataka wewe uolewe na baba yangu"


 


"baba yako anamchumba mwingine"


 


"ndiyo ana madame Ritha"


 


"si unasikia sasa! Kwa taarifa yako ukiniita tena mama sintokupatia tena chocolate"


 


"Salome Ndo aliniambia"


 


"Salome Ndo alikuambia uanze kuniita mama?"


 


"ndiyo"


 


"ataniona"


 


Nilimshika mkono tukaendelea na safari.


 


Tulipofika karibu na shule lao nilimuaga na kumwambia ntamfuata Baadaye kumchukuwa. Nana akiwa ananipungia mkono, kuna mtu alikuja na pikipiki kisha akasimamisha pembeni yangu na kunishika mkono kwa nguvu, moyo ulidunda haraka nikageuka kumtazama atakuwa nani kanishika mkono, nilipomtazama Sikuamini kumuona jambazi ambaye toka nimuone Ananifanya niyaone maisha kuwa magumu, presha ilinipanda huku nikiwa najiuliza moyoni.


 


"Wakati namfanyia upasuaji kuna vyuma niliachana mwilini mwake au?"


 


 


 


 


Kabla sijaongea chochote aliniambia kwa sauti ya Chini.


 


"panda pikipiki"


 


Muda Huo Nana alikuwa bado hajaingia shuleni kwao hivyo alikuwa anaangalia kinachoendelea.


 


Nikiwa nahanya hanya kama vile sipo tayari, alichomoa bastola mfukoni na kuninyooshea kimya kimya bila watu kuelewa chochote. sikuwa na namna nilipanda na safari kuanza.


 


Nana alitusindikiza kwa macho na kuamua kuingia shuleni kwao maana alikuwa bado mdogo hangeweza kuelewa chochote.


 


Upande wetu safari iliendelea huku Mimi moyo wangu ukiwa na mashaka ya hali ya juu


Kilichonishangaza ni kwamba, Tulianza kuuacha mji na kuelekea maporini. Ndipo niliamua kujitoa muhanga na kumhoji.


 


"tunaelekea wapi?"


 


Jambazi huyo aliongeza mwendo kiasi kwamba mbele nikawa sioni chochote kutokana na upepo kuwa mwingi, nikaamua kufumba macho.


 


Safari iliendelea mpaka Majira ya saa 7.


Sikuwa na budi Nilikubaliana na kila Jambo licha mkono wangu ulikuwa bado haujapona vizuri.


 


Tulifika eneo ambalo pikipiki haiwezi kupita, hivyo alisimamisha na kuniambia nishuke, nilishuka kwa hofu maana niliamini naenda kufanyiwa kitu Kibaya.


 


Jambazi huyo aliposhuka alianza kutembea bila kunijali, nilipoona anazidi kwenda moyo Ulianza kunisukuma nichukuwe pikipiki niondoke zangu, hapo hapo nilipanda, kabla sijawasha jambazi huyo Alinionyesha ufunguo wa pikipiki ishara siwezi kwenda sehemu yoyote.


 


"twende" aliniambia.


 


"nahitaji kurudi nyumbani kwani unanipeleka wapi mbona sina hatia"


 


Alichomoa bastola Kama Kawaida yake na kuninyooshea.


 


Tulitembea kiasi kwamba viatu nilivyokuwa nimevaa nikahisi vinawaka moto, mpaka Majira ya usiku tulikuwa bado tunatembea, nililia sana mpaka nikatamani aniue tu maana kama ni mateso nilikuwa nimeyapata.


Safari iliendelea, njaa kiu vilinitesa Sana kwa wakati ule.


 


Tulielekea moja kwa moja kwenye nyumba flani, Tulipofika tulipokelewa na binti mrembo Sana, jambazi huyo baada ya kumuona alitabasamu Jambo ambalo upande wangu lilinishangaza sana.


 


"oppa Hyun Joong"


 


Hapo Ndo nikajua Kumbe mwamba Anaitwa Hyun Joong.


 


"Eun chae" hyun alimuita binti huyo.


 


Tabasamu lao lilinidhihirishia kuwa wapo kwenye mahusiano.


 


Hyun Joong alimshika begani Eun chae wakaingia zao ndani na kuniacha pekeyangu nje, moyo uliniuma kiasi kwamba nikahisi Labda Mimi niliumbwa tofauti na wenzangu, yawezekana nikajiona nipo Kama wao kumbe wakawa wananiona Kama Mnyama.


Taratibu nilishuka Chini na kukaa huku machozi yakiwa yananilenga machoni.


 


Nilivua viatu nikajiangalia miguuni hakika miguu imetapakaa damu ishara viatu viliniunguza mpaka madonda ya Katokea, mawazo yangu yalianza kuniongoza nitoroke niondoke zangu.


 


Kabla sijanyanyuka, binti Eun alinifuata na kuniomba niingie ndani, nilimtazama kwa hasira mpaka nikaanza kulia.


 


Baada ya Eun chae kuniona nalia, alirudi ndani kwa hofu na kamwambia Hyun Joong.


 


Hyun Joong aliponifikia alikunja uso Kama kawaida yake na kuniambia.


 


"Ingia ndani"


 


Muda Huo binti Eun chae alikuwa anachungulia.


 


Nilionyesha Hali ya kugoma ndipo Hyun Joong alichomoa bastola kama kawaida yake.


 


Nilinyanyuka kwa unyonge maana mwili mzima ulikuwa Umechoka, binti huyo alipoona Hyun Joong ananinyooshea bastola aliumia akaamua kuingia ndani.


 


Baada ya muda nilikuwa nimejitenga nao, nilikuwa nimekaa karibu na ukuta huku nikiwa nimejikunja kwa huzuni.


 


Upande wa Hyun Joong alimuuliza mwenzie.


 


"hali yako Ipo je kwasasa?"


 


"niambie kwanza Huyu binti amekukosea Nini Mpaka unamtesa kiasi hiki?"


 


"siyo lazma ujue, utajua Baadaye"


 


"namuonea huruma anabaki kulia muda wote"


 


"Ndiyo Hali yake"


 


"miguu yake inatoa damu"


 


Hyun Joong baada ya kusikia aligeuka na kuniangalia kwenye miguu.


 


"namuonea huruma sana"


 


Hyun Joong hakuongea chochote bali aliendelea kunitazama nilivyojikunja.


 


Eun chae alipoona nahitaji Msaada zaidi, alinyanyuka na kinifuata nilipo.


 


"twende ukaoge nikuwekee dawa kwenye miguu yako"


 


Nilikataa kwa kutikisa kichwa na kumfanya ajisikie vibaya.


 


"hali yake siyo nzuri amekataa kuoga" aliongea eun na kutoka karibu yangu.


 


Ndipo Hyun Joong alinyanyuka na kunifuata nilipo, hakuongea chochote alichomoa bastola na kuninyooshea, ukweli hali niliokuwa nimefikia hata bastola nilijikuta siiogopi tena hivyo niliendelea kukaa nikijisemea moyoni liwalo na liwe.


 


"nenda ukaoge" hyun joong aliniamrisha lakini haikusaidia kitu.


kama Kawaida yake kutokujali kitu chochote alifyatua risasi ikanikwaruza karibu na bega langu la kushoto ikazama ukutani. nilishtuka kiasi kwamba hata kupumua ikawa shida. Mwili ukapoa hadi kumtazama usoni nikashindwa.


 


 


 


 


Eun chae alivuta koti na kujifunika usoni huku akitetemeka kwa hofu kubwa.


 


"Oppa...." Aliishia kumuita kaka huku akiwa haamini kwa alichokisikia, hofu yake tayari amenimalizia.


 


Hyun Joong alinitazama kwa sekunde kadhaa na kutoka nje haraka, nilichokifanya nilimfuata Eun chae na kumuomba maji nikaoge, binti huyo alinishangaa kwa masikitiko na kunyanyuka haraka.


 


Usiku huo ulikuwa usiku mzito upande wangu, hakika sikuweza hata kufumba macho kwa kuyahofia maisha yangu, Hyun Joong alikuwa pembeni kakaa huku Eun chae akiwa tayari kasinzia.


 


Asubuhi na mapema niliamka na kutoka nje, nilianza kuangaza kona zote ila kilichonishangaza hakuna nyumba nyingine iliyokuwepo maeneo hayo.


 


"Umeamka jamani" nilishtushwa na ssuti ya Eun chae haraka nikageuka kumtazama, uso wa binti huyo ulikuwa mzuri haswaa pale alipoachia tabadamu.


 


"Naomba nikuandalie uji" aliniambia na kunifanya nitabasamu, wakati natabasamu Hyun Joong alitoka ndani na kunitazama, macho yetu yalipogongangana nilishtuka na kuacha kutabasamu.


 


"Oppa umeamka?" Eun chae alimhoji na kumuwahi Hyun Joong.


Huwezi kuamini kijana huyo hakumjibu zaidi ya kumpita.


 


"Hamuwezi kuondoka muda huu" aliongea Eun chae na kuzama ndani kwa hasira.


 


Baada ya muda tulikaa na kuanza kunywa chai, mkono wangu ulikuwa mzito mpaka kila mmoja akanitazama.


 


"Uko salama?" Eun chae alinihoji.


 


Majonzi yalinitawala kifuani na kunifanya nishindwe kujibu, Ndipo Eun chae alimgeukia oppa wake na kumwambia.


 


"Muulize jamani"


 


Hyun Joong alinitazama kwa sekunde huku Eun chae akimsisitizia aniuliza nini kinanisibu.


 


"Mbona haunywi uji?" Alinihoji kibabe.


 


"M m mkono umekufa gazi kwasaba..." Nilishindwa kumalizia maana machozi yalitoka haraka. Eun chae alisikitika mno na kuchota uji kwenye kijiko kisha akaniomba ninywe.


 


Majira ya jioni tulikuwa nje tayari kwa ajili ya safari.


 


"Oppa usikae Sana huko, ujue huwa nakumiss Sana" Aliongea Eun chae kwa huzuni na kumfanya Hyun Joong amkumbatie. Niliwatazama nikagundua wanapendana Sana.


 


"Oppa ukirudi uje ukae na Mimi" aliongea Eun chae mwisho akatuaga safari yetu ikaendelea.


 


Haikuchukua muda Sana, tulifika kwenye pango kubwa na kuingia ndani. Kiukweli mazingira hayo yalinishangaza mno nikagundua kuna watu wanaishi humo, ghafla tulianza kukutana na vijana mionekano yao ni majambazi nguli. Tulifika sehemu iliyotengenezwa vizuri wanawake makahaba wakiwa wanakunywa pombe na kucheza vilevile baadhi ya majambazi wakiwa wametulia,wote macho yao yalikuwa kwangu mpaka nikapatwa na hofu. Moja kwa moja Hyun Joong alinipeleka kwa mkuu wao ambaye alikuwa amekaa pamoja na wanawake wawili vilevile na vijana wake kama sita, macho yao niliyaogopa mno na kujificha nyuma ya mgongo wa Hyun Joong.


 


"Karibu naitwa Chief" mkuu wao alinikaribisha ila nilionyesha hofu hata hivyo sikumjibu.


 


Majira ya usiku nikiwa nimejikunja sehemu bila kujua wapi alipo aliyenileta, alikuja kijana flani na kuonyesha kunitamani. Alinitazama juu chini na kulamba mdomo wake kimatamanio.


 


"Mungu wangu, mambo gani haya" nilijisemea na muda huo Hyun Joong alifika, baada ya kufika kijana huyo aliondoka.


"Nyanyuka" aliniambia.





INAENDELEA


 


 



No comments

Powered by Blogger.