Header Ads

Header ADS

Simulizi: Tabasamu langu sehemu ya saba (07)

 SIMULIZI ZA MAPENZI

 

 




"yule Hawezi kubisha hodi kama kichaa namna hii"


 


"Labda ni proscuter Han amekuja kuomba msaada"


 


"unamaanisha wamezidiwa na majambazi wakawa wamepigwa vibaya?"


 


"eeee nenda ukafungue"


 


Nilisogea karibu na mlango taratibu nikafungua huku nikiwa nimejawa na uoga usio wa Kawaida, ile nafungua tu nilishtukia mdomo wa bastola unawekwa kwenye komwe na Aliyekuwa ameniwekea bastola hiyo alikuwa ni Yule mkaka jambazi tunaeishi naye. huku akiwa ametapakaa damu mwili mzima kama vile kakatwa katwa na mapanga.


 


 


 


Moyo wangu ulilaluka mno ukija kuangalia kijana huyo ni mtu ambaye Hanaga huruma hata Kidogo.


Ndipo Alinionyesha ishara kupitia kichwa nitembee, sikutaka kupoteza muda nilipandisha mikono juu nakuanza kutembea.


 


Tuelekee moja kwa moja gorofa ya nne anakuoishi, Salome alitoka na kuchungulia, haraka akarudi chumbani.


 


Upande wetu tuliingia moja kwa moja chumbani kwake, jambazi huyo alinisukumia pembeni Ila sikuweza kudondoka na muda wote hakili hazikuwa zangu.


 


"kwanini umetuuza?" Alinihoji kwa sauti ya maumivu.


 


Nikiwa namuangalia kwa uoga alichomoa picha kisha akanirushia zikaenda Chini, taratibu nilishusha macho kuangalia kwenye picha zile nilishangaa baada ya kujiona Mimi nikiwa na proscuter Han, Ndipo nikajuwa Kumbe muda ule tulipokuwa tunaongea ndani ya gari wapo majambazi walikuwa wanatufuatilia.


 


"I'm sorry oppa, I'm so sorry oppa" nilianza kuomba msamaha kwasababu kaka huyo alikuwa hana mzaha kabisa. Na Oppa maana yake ni kaka hivyo nilimlalamikia vyakutosha.


 


Kijana huyo alinifuata na kunisukumia pembeni nikaanguka Chini huku nikizidi kulia, alichomoa boxi flani mlikuwa dawa za kila Aina ndani yake, baada ya kuchomoa boxi hilo alivua koti alilokuwa amevaa kisha akavua na singledi akabaki kifua wazi, ukweli nilipomuangalia jeraha alizokuwanazo nilimuonea huruma licha Yeye Hawezi kunionea huruma.


 


Baada ya kuvua alilala kitandani chali nakuniita kupitia vidole, presha ilinipanda huku nikiwa najiuliza anahitaji nini mbona ameniita hivyo.


 


Nikajifanya Sijaelewa chochote, jambazi huyo alichomoa bastola yake nakuninyooshea huku akiniita kupitia bastola.


 


Nilipoona bastola Nilinyanyuka haraka.


 


"Nifanyie upasuwaji kuna kipisi cha bomu kimeingia hapa kitoe sasa hivi" aliniambia huku akiwa amebana meno kwa maumivu.


 


Ukweli Mimi nilisomea udokta ila nilikuwa sijafikia uwezo wa kuweza kumfanyia upasuwaji mtu.


Sikuamini kwa kile alichoniambia, niliendelea kumtazama kwa mshangao, jambazi huyo baada ya kuniona nimeogopa alinishika kidevu kwa nguvu na kuniambia.


 


"Nasema Nifanyie operation kabla sijakutwanga risasi"


 


Nilikubali haraka haraka bila kupoteza muda nikavuta boxi lile nakuanza kukagua dawa ambazo naweza kuzitumia, moyo wangu uliniuma sana maana nisingeweza kumsaidia kwasababu nilikuwa sijui chochote.


 


Nilichukuwa dawa flani ya maji maji nikamimina kwenye pamba kisha Nikaanza kumuosha kabla ya kumfanyia upasuwaji huku nikiwa naendelea kulia.


 


Baada ya kumaliza kusafisha kidonda nilichukuwa kisu huku nikiwa natetemeka mno, nilipokifikisha kisu kile karibu na kidonda niliangua kilio na kumwambia


 


" please sijui chochote"


 


Jambazi huyo alinipiga kichwani na bastola akanifanya niingiwe na ujasili, kupumua kwake kulikuwa ni kwa shida mno.


 


Kabla sijafanya chochote nilikumbuka kuna sindano inapaswa nimdonge ili asiskie maumivu, nilichukuwa sindano nikavuta dawa Ila kabla sijamdunga aliushika mkono wangu ulioshikilia sindano na kuniuliza.


 


"unataka kuniua?"


 


Nilitikisa kichwa ishara siyo kweli.


 


"siyo hivyo ni ya kukufanya usisikie maumivu"


 


"acha, Fanya hivyo hivyo"


 


"utaumia jamani"


 


Ndipo aliniwekea tena bastola nikaamuwa kufanya nilichoambiwa.


 


Nilipambana kadri ya uwezo wangu mpaka nikafanikisha kutoa kipisi kile cha bomu licha kazi ilikuwa ngumu mno. baada ya kukitoa Alihisi maumivu makali mpaka mwenyewe nikamuonea huruma.


 


Muda Huo damu zilianza kumbumbujika kama Mvua, nikaanza Kuhangaika kutafuta cha kuweza kuzuia, haraka nilileta nguo yake nikamuwekea.


 


Upande wa Salome akiwa yupo dilishani anachungulia nje aliona gari ya ma proscuter inaipaki nje na muda Huo proscuter Han alitoka ndani ya gari hilo huku akiwa ametapakaa damu nyingi Pamoja na wenzie.


 


Upande wetu kuna dude flani lililia moja kwa moja jambazi huyo akagunduwa tayari mapolisi wapo nje na wanaingia ndani.


 


sijui nguvu alizitoa wapi alivuta bandeji akajifunga freshi kunako kidonda kisha akanishika na kuniwekea bastola tukatoka naye nje.


 


Moja kwa moja tulielekea chumbani kwetu tukamkuta Salome akiwa amekaa kitandani, baada ya kutuona alishtuka mno ndipo jambazi yule akamuambia.


 


" ukiongea kuhusu Mimi ntamuua dada yako"


 


"tafadhali usimuue Madina"


 


Ndipo Jambazi huyo alinipeleka moja kwa moja bafuni kisha akabana mlango.


 


Proscuter Han na wenzie Waliingia chumbani gorofa ya nne wakakuta damu nyingi Pamoja na vifaa vya matibabu Ndipo wakagundua kuna mtu alikuwa anatibiwa, bila kupoteza muda walianza kumtafuta kona zote ila hawakuweza kumuona.


 


Moja kwa moja walielekea chumbani kwetu, proscuter Han na wenzie walipofika walimkuta Salome akiwa amejifunika shuka mwili mzima kwa uoga.


 


"dada yako yuko wapi?"


 


Salome baada ya kusikia sauti ya Han alitoa shuka fasta na kumuangalia, alipotaka kujaribu kusema kuwa jambazi yupo humu ndani alisita maana alijuwa na Mimi atanipoteza.


 


"sijui"


 


"hujui?"


 


Muda Huo Huo walishangaa kuona damu binchi Ikitoka bafuni Jambo ambalo Salome lilimshtua mno.


 


Han baada ya kuona hivyo, alisogea taratibu kwa makini huku akiwa amenyoosha bastola yake kuelekeza kunako mlango wa bafu.


 


 


 


 


Proscuter Han alipoufikia mlango alishika kitasa taratibu akafungua na moja kwa moja akaninyooshea bastola maana muda Huo nilikuwa nimekaa Chini.


 


Han baada ya kugundua ni Mimi, aliingia haraka kisha akanishika huku akiniuliza kuhusu hali yangu.


Proscuter Han aliangaza kona zote ila hakuweza kuona mtu.


Nikiwa nimekaa huku damu zikinibubujika begani, Han aliniuliza.


 


" imekuaje?"


 


Muda Huo Salome naye aliingia.


Salome baada ya kuniona na kutokumuona jambazi yule, alishindwa kuelewa nini kinaendelea, na muda Huo ndani ya bafu mwanga ulikuwa hafifu hivyo ilikuwa ngumu kumuona.


 


"Madina unaMatatizo gani?" Han alinihoji.


 


"jambazi, amenichoma kisu baada ya kugundua kuwa nimewatolea


Siri kwenu" niliongea kwa shida.


 


Muda Huo jambazi yule alikuwa Juu akiwa amening'inia huku mikono na miguu akiwa ameisambua.


 


Salome akiwa bado haelewi alishangaa Toni la maji linamdondokea kichwani, taratibu akagusa kichwani ili kusikiliza ni nini, alipoangalia mkononi alishangaa kuona damu, taratibu akaangalia juu. hakuamini kumuona jambazi yule.


 


Bila kupoteza muda Salome alishusha kichwa Chini kwa uoga, proscuter Han alimgeukia Salome Na kumuuliza.


 


" imekuwaje kwa dada yako?"


 


"a a a alikuja a a akiwa a a a ametapakaa damu sasa sijui ni nini kinaendelea, na ndo maana ulivyoniuliza dada yako yuko wapi nimekujibu sijui maana nilikuwa naogopa"


 


Proscuter Han bila kujua kuwa mbaya wake yupo hapo aliwaita wenzake wakanitoa mule na kunipeleka hospital.


 


Baada ya Sisi wote kutoka nje jambazi yule alishuka fasta huku akiwa ameshikilia jeraha yake kwa maumivu makali.


 


Siku moja kupita nilizinduka na kujikuta hospito huku nikiwa nimewekewa dripu ya maji, pembeni yangu alikuwepo Salome akiwa amelala, taratibu nilimtikisa kichwani akaamka na kuniangalia, hakika alifurahi mno akisema.


 


"afadhali"


 


"proscuter Han Hali yake vipi?" Nilimhoji.


 


"kwasasa yupo vizuri na ametoka hapa muda huu huu embu niambie Unajuwa mpaka sasa sielewi Nini kinaendelea?"


 


Nilimpa mkasa kwa ufupi.


 


"bafuni ilikuweje?" Alinihoji.


 


"ile damu yote iliyokuwa Chini ilikuwa ni yake, sasa akaona atagundulika Ndo akanitonesha kwenye kidonda kisha akaniambia nikisema chochote atanizika nikiwa mzima mzima ndo ilivyokuwa hivyo"


 


"na Mimi nilimuona alivyokuwa ananing'inia Juu, Unaonaje tuhame?"


 


"nahitaji hata Muda huu huu tuweze kuhama"


 


"Ngoja niende nikachukue nguo zetu zote tukatafute eneo lingine.... aisee Ndo maana nyumba nzuri bei yake ndogo Kumbe wanajuwa ndani wanaishi wanyama"


 


"Kuwa makini huko uendako"


 


Salome alitoka, akaniacha nikiwa nafikiria kuhusu jambazi yule namna alivyo mkakamavu kiasi kwamba anauwezo wa kuvumilia maumivu makali kama Yale.


 


Baada ya muda nikiwa nimetulia zangu, aliingia nesi mmoja muonekano wake alikuwa ni wa kiume licha alikuwa ameuficha uso wake, nesi Yule baada ya kufika aliweka sahani Chini iliokuwemo baadhi ya dawa Pamoja na sindano, ndipo alichukuwa sindano akaingiza ndani ya kichupa Kidogo sana kilichokuwemo dawa ambayo nilikuwa siitambui maana masuala ya udaktari ndiyo nilisomeaga, baada ya kumaliza alinisogelea ili kuweza kunidunga.


 


"samahani dawa ya nini hiyo"


 


Nesi Yule alikaa kimya akataka kulazimishia kunichoma. kabla sindano haijaufikia mwili wangu, nilimshika mkono ambao kwa muda Huo ulikuwa umeshikilia sindano kwa nguvu nyingi huku nikiwa nazidi kumuuliza dawa ile anayotaka kunidunga ni ya nini, naye pia aliendelea kukaa kimya.


 


Nilipoona mtu huyo huwenda siyo nesi, niliingiwa na nguvu nikakata kanyola waliyokuwa wameniwekea kisha nikamsukumia pembeni akaangukia ukutani, nikiwa sielewi elewi nilianza kujipanga ili kuweza kutoka nje, kabla sijafanya chochote mtu Yule alitoa mavazi yake ya kinesi akabaki kwenye mavazi yake ya Kawaida, pia akavua na kile kitambaa alichokuwa amevaa usoni ili asiweze kuonekana.


 


Nilipoiona sura yake nilishtuka mno maana alikuwa ni Jacob aduwi yangu wa kila siku, sikutaka kusubiri aniue Kiurahisi, niliona bora nife nikiwa najitetea, bila kupoteza muda nilitoka kitandani na moja kwa moja nikatoka chumbani na kuelekea nje huku nikiwa nakimbia kwa kasi ya kufa mtu.


 


Jacob kama Kawaida yake huwa ni mtu asiyeogopa macho ya watu, alianza kunikimbiza huku akiwa ananiambia kwa kiswahili.


 


"Simama hapo hapo"


 


Tulikimbia, nikafanikiwa kutoka ndani ya hospitali akiwa bado hajanikamata, ile kukimbia Kimbia bila kuangalia mbele, tuligongana na proscuter Han maana muda huo alikuwa anakuja kuniangalia.


 


Tulipogongana alinikumbatia ili nisiweze kudondoka, hakili zangu zikiwa bado hazijakaa sawa.


 


"una Matatizo gani Madina?" Alinihoji.


 


Niliposikia sauti ya Han niliinua macho nakumtazama usoni huku Jasho Ikiwa inazidi kunibubujika usoni.


 


Muda Huo Jacob alifika, nilipomuona nilimzunguka Han nikajificha nyuma yake huku nikiwa napumua kwa kasi.


 


Jacob akiwa anapumua kwa hasira alijishika mfukoni akaanza kusogea tulipo, kwa nguvu nyingi niliishika tisheti ya Han Mpaka han akaanza kupata mashaka.


 


Jacob kama Kawaida yake kujiamini, alimuambia Han.


 


"namhitaji mke wangu"


 


"nani?" Han alimhoji.


 


"huyo ni mke wangu amenitoroka Kenya akaja kukimbilia huku"


 


Han alishangaa, akawa kama ameanza kumuamini vile, maana alipomuangalia Jacob alivyo mweusi kama Mimi alijikuta anaanza kuamini, nikiwa nipo nyuma yake alinishika mkono na kunitoa nyuma yake huku akiwa ananiambia.


 


"utakuwa sawa"


 


"Ni mumeo?" Alinihoji nikabaki kumtazama kwa hofu.


 


"Kama ni mumeo nenda tu"


 


Moyo ulishtuka mno kiasi kwamba hata kuongea Nilishindwa, kifua changu kikaanza kupanda na kushuka, hapo hapo nikaishiwa nguvu mwilini taratibu nikalazakichwa changu kifuani kwa proscuter Han na hapo hapo nikazimia.


 


Jacob alipata muda wa kumueleza uongo Han Mpaka akaamini.


 


"Kwahiyo hautomfanya aliye tena?" Han alimhoji.


 


"thamani ya mke wangu mimi pekee ndiye naijua, nimetoka huko Africa nikaja huku kwa ajili yake, tumepitia Matatizo makubwa kwenye familia yetu. ikampelekea mke wangu kuchanganyikiwa akaamua kukimbilia huku, mimi...... "


 


Jacob alishindwa kumalizia ndipo aliinamisha kichwa Chini ishara anamaumivu makali ndani ya kifua chake.


 


"pole Sana Rafiki yangu, Naomba twende nyumbani kwangu akipata afadhali bila Shaka utaenda na mkeo"


 


Tulipanda gari ya proscuter Han, nyuma nilikuwa Mimi nikiwa bado sijajitambui huku Jacob akiwa yupo pembeni yangu, maana aliomba akae karibu yangu ili kuniwekea ulinzi.


 


Safari Ikiwa inazidi kusonga mbele Han alimuambia Jacob.


 


"mlaze begani kwako asiumie shingo"


 


Jacob alijilazimisha kutabasamu kisha akanishika na kunilaza begani kwake, hasira ilimpanda baada ya kuiangalia sura yangu kwa makini.


 


"umemlalia simba kweli?" Alijisemea moyoni.


 


 


 


Baada ya masaa kadhaa kupita nilizinduka nikajikuta eneo tofauti kabisa na nyumbani, nilianza kutafakari huku nikijiuliza *nimefika fikaje eneo hili* Ndipo Nikakumbuka mwisho kabisa nilikuwa mikononi mwa proscuter Han.


 


Mawazo yakanijia nikahisi huwenda Nipo kwa Jacob Ila moyo mwingine ukaniambia Jacob Hawezi kukuweka kwenye kitanda kizuri namna hii.


 


Nilichokifanya nilitoka kitandani taratibu kwa mwendo wa kunyata, nikaanza kutoka nje huku moyo wangu ukiwa haujatulia kabisa.


Nilipofika sebuleni niliona picha ya proscuter Han Hapo nikajuwa Nipo kwa Han, moyo wangu ukawa huru nikaanza kutembea huku nikiwa najinyoosha nyoosha Kama nimefika kwangu vile.


 


Upande wa nje proscuter Han alikuwa amekaa Pamoja na Jacob huku wakiendelea kupiga story.


 


"Nampenda sana mke wangu"


 


"Vumilia utaondoka naye Kikubwa umemkuta ni mzima"


 


"nimetoka naye mbali sana, ningempata na mdogo wake ningefurahi mno yaani familia ya mke wangu wote walifariki wakabaki wawili tu"


 


"usijali wote utaondoka nao, Ngoja nakuja naenda kumchukuwa mtu flani muhimu kwangu"


 


"mkeo?"


 


Han alitabasamu na kumjibu.


 


" utamuona"


 


Han alimuacha Jacob akiwa amekaa nje kisha akaifuata gari yake na kuondoka.


 


Ndani ya nyumba tukabaki wawili tu, Mimi nilikuwa sijui kuwa Jacob yupo hapo, nilikuwa zangu nimekaa sebuleni huku nikiwa naangalia movie kwa uhuru.


 


Nikiwa naendelea kuangalia movie, karibu na sikio langu nilisikia sauti ya kiume ikiniambia.


 


"nakuhitaji"


 


Haraka niligeuza shingo ili Kutaka kujuwa atakuwa Nani, aisee uso kwa uso na adui yangu wa siku zote Jacob, mapigo yangu ya moyo yalinienda mbio kiasi kwamba Jasho mwilini ikaanza kunifumuka kama vile nimekaa karibu na fulu ya mkaa.


 


Jacob uso wake ukiwa upo karibu na uso wangu huku tukiwa tunatazamana, alitabasamu na kuniuliza.


 


" hivi ni wewe kweli ambaye unanifanya mpaka sasa siwezi kuingia ndani ya nchi yangu? maisha yangu kwasasa yamekuwa yakuhangaika kama kunguru kisa wewe kahaba? Kifo chako kitakuwa kizuri zaidi ya kile cha mama yako"


 


Kwa vitisho nilivyopewa na Jacob kwa muda ule nilipiga kelele nikiomba msaada kwa proscuter Han, bila kujuwa kuwa Han hayupo.


 


Jacob alipoona nahangaika huku nikiomba msaada alicheka Sana, nikaendelea kumuita Han bila mafanikio.


 


"unaemlalamikia sasa hivi hayupo" aliongea han.


 


Haraka niligeuka kumtazama Jacob kwa Hofu kubwa, moyoni nikiwa najiuliza amemuua aidha, sikuweza kupata majibu yake bali niliona niitetee nafsi yangu kwanza.


 


Haraka Nilinyanyuka ili Kutaka kukimbia, kwa bahati mbaya Jacob aliushika mkono wangu maana nilikuwa nimechelewa kusimama, nilianza kujitoa kwake, Ila alinirudisha kwenye sofa kisha akasogea pale nilipo nakunikwida shingoni, alianza kunininyonga kwa nguvu nyingi kiasi kwamba misuli ya mwili wake ilijilanda misili ya simba ambaye kamuona swala.


 


Sauti yangu ilikata, nikaanza kurusha miguu huku mikono yangu Ikiwa inajaribu kumzuia Aache.


 


Tuliendelea kuparangana, mpaka ikafikia hatua Nikaona Kifo kipo mbele yangu.


 


Kama bahati muda Huo proscuter Han aliingia na kusema kwa sauti ya ukali.


 


" achaaaaaaa!!"


 


Jacob baada ya kumsikia Han aliniachia huku macho yake yakiwa yamegeuka kuwa mekundu, proscuter Han kitendo hicho kilimpa picha mbaya na kuanza kumtilia mashaka Jacob.


 


Upande wangu nilikuwa nakohoa kiasi kwamba nguvu zikaniishia nikashuka Chini Nakukaa huku nikiwa naendelea kukohoa.


 


Proscuter Han akiwa amekunja uso alimuuliza.


 


"unahitaji nini?"


 


"ninachokihitaji ni Huyu binti kuwa mikononi mwangu" aliongea Jacob.


 


"Mbona ulikuwa unamnyonga Hali ya kuwa uliniambia ni mkeo?"


 


"iwezi kuwa na mwanamke mchafu kama huyu"


 


"bali?"


 


"nipo kwa ajili ya kumuua"


 


Kiukweli Jacob alikuwa ni kijana ambae ukimtazama muonekano wake alikuwa anatisha kisura, kutokana madawa ya kulevya aliokuwa akipenda kuyatumia, vile vile na ile Hali ya roho mbaya iliifanya sura yake iogopeke.


 


Han hakutaka marefu alitoa pingu na kusema.


 


"jisalimishe upo Chini ya ulinzi"


 


Jacob baada ya kuambiwa ajisalimishe alitabasamu kisha akamuwahi Han na kumpiga teke ya tumboni.


 


Han alipoona kizaa zaa kimeanza alijipanga freshi ngumi zikaanza.


 


Upande wangu nilikuwa natetemeka mno kiasi kwamba hata kile walichokuwa wanakifanya nilikuwa sikiona, picha nzima ya kifo cha mdogo wangu Munira ilinirudia hakilini mwangu Nikajikuta Naanza kupiga kelele kwa sauti ndogo huku nikiwa kama vile nimepoteza hakili.


 


Jacob na Han Waliendelea kuviringishana.


 


Muda Huo kama bahati Waliingia ma proscuter wawili ambao walikuwa ni marafiki zake Han wakamnyooshea bastola Jacob ili ajisalimishe, kiulaini walimkamata nakumpeleka kituoni.


 


Han akiwa anajiuliza Hawa wenzie wamejuwaje kuwa yupo hatarini aliingia binti mdogo mwenye umri wa miaka 6 akisema.


 


"baba Upo Salama?"


 


Binti huyo mdogo alikuwa ni binti wa proscuter Han.


Upande wangu Niliendelea kujificha huku nikiita Jina la Munira.


 


Han alimkumbatia binti yake na kumuuliza.


 


"umekujaje mbona haukunisubiri?"


 


"Kwanini haukuja kunichukuwa shule?"


 


"sorry!"


 


"baba Nimekuja hapa nikakuona unapigana nikaenda kumuambia Babu akanipa simu nikampigia Tae so akaja"


 


Han alifurahi mno na kumnyanyua binti yake huku akimtaja kwa jina.


 


" wow binti yangu Nana"


 


Nana aliponiona alininyooshea kidole huku akimuuliza baba yake.


 


"nani yule"


 


Han aliponiona alishtuka mno kama vile alikuwa amenisahau, haraka alimuweka Chini binti yake kisha akanifuata nilipo.


 


Akiwa ananiuliza najisikiaje, Nana kimoyo moyo alikuwa anajisemea.


 


" umenitupilia mbali kisa Huyu mwanamke sawa"


 


Baada ya muda nilipelekwa kitandani kwa ajili ya kupumzisha hakili.


nikiwa Nimelala huku Han na binti yake wakiwa wapo karibu yangu, nilimtazama Nana huku nikijiuliza kimoyo moyo.


 


"Inawezekana vipi mtoto yupo karibu na Han kiasi hiko? au atakuwa binti yake? ila mbona kama vile Han bado kijana mdogo Sana"


 


Nana alimsogelea baba yake akamnong'oneza vitu masikioni kisha akapandisha mdomo kama vile hajafurahia uwepo wangu.


 


Han alitabasamu na kumuambia.


 


"Muulize mwenyewe"


 


"baba"


 


Alipomuita Han baba Ndipo nikajuwa Kumbe Han tayari ni Mume wa mtu.


 


Han alinitazama na kuniuliza.


 


"naweza nikakuhoji sasa?"


 


Nilitikisa kichwa ishara ya kukataa nikaamua kujifunika uso mzima maana niliamini tayari Han ni Mali ya mtu mwingine kabisa hivyo sitakiwi kuweka mazoea.


 


Nana alimuonyesha ishara baba yake kuwa Nina zarau aachane na Mimi.


 


Muda Huo mlango uligongwa ikabidi Nana aende kufungua mlango, alipofungua mlango alishangaa kumuona Salome akiwa ameshikilia mabegi, ndipo alimuuliza.


 


"unamfuata nani?"


 


"baba yako"


 


Salome aliingia ndani na mabegi yake mkononi huku akiwa anaangaza angaza pande zote akiangalia Mazingira ya ndani.


 


Upande wetu Han aliniambia.


 


"najua Hali yako siyo nzuri ila ungejitahidi kuamka nikufanyie matibabu kwenye mkono wako"


 


Hasira niliokuwa nayo sikujua inatokana na nini.


 


Muda Huo Salome aliletwa na Nana tulipo.


Salome alimsalimia Han kisha akimuuliza kuhusu Hali yangu, nilipoisikia sauti ya Salome niliamka na kukaa kitako.


 


"vipi Hali yako?"


 


Nilimpa mkasa mzima kuhusu Jacob, ndipo Han akatuambia.


 


"ukweli sikujuwa kuwa Yule kijana ni Yule uliyeniambia. nilomkaribisha ndani akidai wewe ni mke wake"


 


"Hapana Naomba jamani asitoke sero atatuua Sisi" nilimjibu.


 


"usijali! Salome kule ulitoka tokaje?"


 


"Salome?" Binti yake aliita kwa mshangao"


 


"yeah Huyu naye ni Madina"


 


Nana aliangalia pembeni ishara hajafurahishwa na ujio wetu.




INAENDELEA....


 



No comments

Powered by Blogger.