Header Ads

Header ADS

Simulizi: Tabasamu langu sehemu ya nne (04)



 "maa! Tuchukulie haya yote ni kama movie, embu amka taratibu futa damu hiyo iliopo kichwani Ukimaliza tabasamu uniambie kuwa movie Ilikuwa nzuri sana"

 

Madada wote waliangua kilio baada ya kusikia maneno yangu, muda Huo Munira alikuja huku akiita mama "mamy! Mamy!"

 

Aliponifikia alinishika begani na kuniuliza "dada mbona mamy amelala pale? Ameniambia nimsubiri anakuja tulale mbona amelala pale"

 

Nilimvuta mdogo wangu kipenzi ambaye ndiye nimebaki naye, nikamkumbatia kwa nguvu huku nikisema kwa uchungu.

"Munira hatuna siku nyingi tunaenda kumuona baba pamoja na kaka. mama na yeye ametangulia"

 

"tutamuona baba na kaka?" Munira aliniuliza kwa furaha.

 

"ndiyo"

 

"twende sasa hivi"

 

Nilimuachia, taratibu nikaanza kujisogeza alipo mama, nilipomfikia Nilimuinua kichwa taratibu nikamlaza mapajani kwangu.

Munira naye alisogea akakaa karibu yangu.

 

"hukuwahi kufumbua macho kwa Muda mrefu kama hivi"

 

Nilimfumba macho kisha nikambusu na kumwambia Munira "mkiss mama umwambie bye"

 

Munira alimkiss kisha akaanza kumuasha. Baada ya kuona ukimya umezidi alianza kulia.

 

"hautaki kwenda kumuona baba na kaka?"

 

"sitaki muamshe mama"

 

Niliangua kilio kwa uchungu bila kujua nini kitafuata baadaye.

 

Muda Huo huwezi kuamini Mr Robert mwenyewe na watu wake walitia timu, nilipoangalia uso wa mzee Robert Ilikuwa ishara Tosha kuwa hajaja kwa wema, moyo uliraruka nikamwambia Munira kwa sauti ya chini.

"Kimbia chumbani"

 

Munira aliponyanyuka tu, sauti ya Mr Robert ilisikika akisema "subiri"

 

 

 

 

Munira alirudi kwangu kwa Hofu kisha akanikumbatia, pembeni ya Mr Robert alikuwepo baba flani mkorea.

 

"mama yako amekufa?" niswali lilitola kwa Mr Robert.

 

"Huyu ni mzoga tu " aliongea baada ya kuniona namtazama kwa hasira.

 

Aliwaamulu watu wake waje wautoe mwili wa marehemu mama eti unamtia karaha.

 

Walinzi hawakuwa wabishi Wakasogea pale wakanisukumia pembeni kisha wakaupeleka mwili wa mama.

 

Mr Robert kwa dharau akamwambia mtu wake wa pembeni "pulizia pafiumu haraka, pia na Nyie huko hakikisheni mmefuta ushahidi wote"

 

Kijana Yule alianza kupuliza pafiumu.

 

Robert aliomba kiti akae, akaletewa kisha akakaa huku akiwa anamueleza mkorea huyo kuhusu Mimi.

 

Baada ya kumaliza kumueleza alinigeukia na kuniambia.

 

"wewe Upo kama baba yako, na utakufa Kifo Kibaya sana, unajuwa kwa hii dunia Sipendi kuona watu vimbele mbele Kama wewe? Kwanza wewe mlete Yule mtoto hapa" Mr Robert Alimuamulu kijana wake aje kumchukuwa Munira, aliponifikia Nilimkumbatia Munira kwa nguvu huku nikimwambia mkaka Yule "tafadhali nisaidie"

 

Mkaka Yule kwa sauti ya Chini Akaniambia "I'm sorry Jambo hili lipo Juu ya uwezo wangu"

 

Alimchukuwa Munira akampeleka kwa boss wake.

 

" nileteeni friji hapa"

 

Nilijiuliza anataka afanye nini na friji ila sikupata jibu.

 

Robert alimtabasamia Munira na kumwambia "usijali Eee"

 

"namtaka baba, mama na kaka" Munira aliongea Huku akivuta kamasi.

 

"usijali unaenda kuwaona Muda huu huu"

 

Niliposikia hivo aisee sijui nguvu zilitoka wapi, Nilinyanyuka kwa hasira ili kumfuata Ila walinzi walinizuwia, maneno mengi niliongea ila nikama nilikuwa namwagia maji kwenye mgongo wa bata.

 

Muda mdogo friji ililetwa, Robert akanyanyuka na kufungua mlango wa friji kisha akamwambia Munira.

 

" Ingia ndani ukawaone wazazi wako "

 

"Munira Hapana usiingie" niliongea kwa sauti ya juu na kumfanya munira aongeze kilio. Baada ya munira kugoma. Mr Robert kwa mikono yake alimnyanyua na kumuingiza ndani ya friji kisha akafunga mlango.

 

Sauti yangu haikuweza kutoka tena, nililegea mwili mzima na kukaa Chini, sauti ya Munira akiwa Analia kwa kupaza sauti huku akiniita niende kumpa Msaada, niliisikia vizuri ikavuruga Ubongo wangu.

 

Taratibu nilipiga magoti na kumuambia Mr Robert "Nipo chini ya miguu yako tafadhali mtoe mdogo wangu anateseka huko"

 

"dada baridi" ilikuwa ni sauti ya mdogo wangu iliyozidi kunipagawisha.

 

"nisubiri mdogo wangu nakuja sasa hivi" niliongea kwa sauti ya juu ili kuweza kumfariji.

 

"Oohh Nikweli subiri nikutoe" Mr Robert aliongea kiutani na kutaka kufungua mlango. Kabla hajafungua,

simu yake iliita na kumpelekea asitishe kufungua kisha akapokea simu na kuanza kuongea.

 

kilio changu, kelele zangu hazikuweza kusaidia chochote, kwa sauti ya maumivu nikasema "Nani ananisikia aje kumsaidia kipenzi changu, tafadhali jamani Munira bado mdogo anateseka huko embu sikieni halii tena"

 

Baada ya muda nikiwa nimekata tamaa Robert alimaliza kuongea kwenye simu kisha akafungua mlango na kumtoa Munira, alipomuweka Chini aliinua kichwa chake na kuniambia "kama vile amekufa!"

 

Niliendelea kumtazama huku nikiwa nimeduwaa.

 

Mr Robert na wenzie waliamua kuondoka.

 

Taratibu nilijikongoja Nikamsogelea Munira alipolala, nilipomgusa mwili wake ulikuwa wabaridi mno, kwa sauti ya Chini nikamwambia "I'm sorry nimechelewa kuja kukutoa Ila kwasasa Nipo hapa"

 

Nilianza kumpa joto kwa kumpulizia pumzi.

 

Mama mmoja alisogea pale nilipo akavua kitenge ili kumfunika Munira maana Alihisi atakuwa anapigwa na baridi, akiwa anamfunika alishtuka na kuniangalia usoni, nilipoona kama vile kuna Jambo lipo tofauti nikamuuliza "nini?"

 

Mama huyo aliangua kilio na kusema "samahani Munira hatupo naye tena"

 

Nilimsukuma mama huyo huku nikamfunika vizuri Munira.

 

Sikutaka kumsikiliza tena nilimuuliza Munira "hauwezi kuamka?"

 

Ukimya ulitawala mwenyewe nikajidhihirishia kuwa tayari ameshafariki licha nilikuwa najifariji fariji tu, nilimvuta nikamkumbatia huku nikilia mno, Nilipaza sauti nikisema "amka Munira"

 

Baada ya muda Nilijikatia tamaa kabisa nikawa najiuliza Mimi ni Nani kwa hii dunia na Kwa nini awe Mimi tu, sauti ya mwisho ya Munira ilijirudi kwenye ubongo wangu alivyokuwa akiniita akinitaka nikamsaidie kumtoa ndani ya friji kwasababu baridi ni nyingi, uzalendo ulinishinda nikapoteza fahamu hapo papo.

 

Baada ya siku moja kupita nilikuwa bado sijakurupuka, ndipo nikazinduka nikamuona Salome pembeni yangu Pamoja na Yule baba mkorea Aliekuwa yupo Pamoja na Mr Robert.

 

Salome aliponiona nimezinduka alifurahi na kuniuliza "Upo Salama?"

 

Nilikaa kitako kisha nikamuuliza "Huyu mtu amefuata nini hapa?"

 

"amekuja kutusaidia"

 

Nilipokumbuka yaliyopita, nilianza kulia upya, ndipo mkorea Yule Akaniambia kwa kingereza.

 

"usijali nipo hapa Kwa ajili ya kukusaidia, kitendo cha Jana hakikunifurahisha hata Kidogo, kwahiyo nikuondoe wasi wasi lazma ulipize kisasi"

 

Nilimtazama kwa muda mrefu kisha Nikamuuliza.

 

"wewe haujatumwa na Mr Robert?"

 

"Hapana"

 

"please Madina muamini yupo hapa kwa ajili ya kutusaidia"

 

"kitendo cha kumuua mtoto mdogo kikatili namna ile, siwezi kumsamehe lazma niwasaidie" aliongea Mkorea na kunifanya nianze kumuamini.

 

Ndipo Tulianza kupanga Plani.

 

Baada ya muda Nilipokuwa nasoma ramani vizuri, Salome alikuja na kuniambia "Jacob eti amesafiri"

 

"eti?" nilimhoji kwa mshangao.

 

"ninavyomtamani aisee ntakata kiungo kimoja kimoja baada ya kingine"

 

Baada ya muda tuliambiwa Mr Robert anakuja, Mimi na Salome tukakonyezana maana ndivyo tulikuwa tumepanga.

 

 

Tulitoka eneo hilo huku tukipanda ngazi kwa mashaka, njiani Tulikutana na Yule Kijana Mlinzi wa Mr Robert siku Ile nikamuomba anisaidie asimpeleke Munira kwa Mr Robert la akaniambia nimuiwie radhi siyo Yeye, alisimama mbele yetu na kusema.

 

"I'm sorry siku ile sikuweza kukusaidia Ila nakuahidi Leo ubaya wa mtu huyu utaishia humu ndani, siyo Siri walinzi wenzangu wote wamesema watakusaidia maana Kifo cha mdogo wako kilimgusa kila mmoja"

 

Tulitabasamu Mimi na Salome kisha tukaendelea kupanda Juu.

 

Tulipofika juu kabisa kunako chumba cha Mr Robert, tuliwakuta walinzi wawili wakiwa mbele ya mlango wa chumba kile huku wakiimalisha ulinzi zaidi, ndipo Salome akaniuliza.

" Mbona hivi?"

 

Makaka wale walituonyesha kupitia ishara tuingie ndani Hamna shida. Ndipo nilitabasamu na kusema "tupo nao hawa"

 

"Asante Mungu"

 

Tulipiga hatua tukaingia moja kwa moja ndani ya chumba cha Mr Robert, nilipoiona sura yake, hasira ilinipanda nikatamani kumrukia ila Salome akanituliza kwa kunishika mkono.

 

Mr Robert Baada ya kusikia kuna mtu kaingia chumbani Bila kubisha hodi, aliamka na kuuliza "Nani?"

 

Alipotuona alitabasamu na kuniuliza "Oohh ni wewe uliefiwa na wazazi wote Pamoja na wadogo zako mapacha ?"

 

Moyo uliniuma mno. ile nataka kumfuata nyuma yangu alitokea yule baba mkorea nakunituliza kwa kunishika begani.

 

Mr Robert bila kuelewa chochote alitoka kitandani huku akimwambia Rafiki yake bila kujua ni msaliti.

 

"Mr Choi! Huyu binti anasikia harufu ya Kifo nikizani"

 

Mr Choi alitabasamu na kusema "Labda ni wewe?"

 

"una maana gani?" alimhoji kwa mshtuko.

 

Choi alianza kuzunguka zunguka ndani ya chumba hiko huku akimwambia.

 

"wewe ni Rafiki yangu nimekujuwa kwa Muda mchache Sana, sikujuwa kuwa wewe ni katili kiasi hiki, biashara yetu, mkataba wetu, Naomba uishie hapa maana unaenda kulipa kwa kile ulichomfanyia mtoto Yatima asiyekuwa na hatia"

 

Mr Robert Jasho taratibu ikaanza kumtiririka.

 

"umeamua kunisaliti kisa jambo dogo kama hili?"

 

"aaahhh kumbe kuua unachukulia Jambo dogo sana eeee" aliongea Mr Choi.

 

"mbona Kawaida sana"

 

Hasira ilinipanda nikamrukia Mr Robert na kumpiga ngumi ya shavuni, Mr Choi alinifuata akanizuwia nisiendekee kufanya chochote huku akiwa anazidi kunipunguza jazba.

 

Mr Robert Baada ya kuona yupo hatarini, alianza kuita walinzi wake waje kumsaidia Ila Hakuna aliejitokeza, ndipo Mr Choi akamwambia.

 

"Hakuna mtu anaehitaji kuendelea kuona ushenzi wako, wote wamekutema"

 

Presha ilianza Kumpanda taratibu, ndipo akaanza kutafuta simu Ili aweze kumpigia mdogo wake amjuze taarifa hizo.

 

Mr Choi hakupoteza Muda alimuwahi kabla hujachukuwa simu akamshika mkono kisha akamgusa shingoni kunako mshipa mkuu unaosafirika damu na kumzimisha.

 

Mr Choi alisogea tulipo kisha akatuambia.

 

"Huyu mtu kumpiga au kumuua sasa hivi siyo suruhisho kilichopo nataka tumfanye asikie maumivu ya kuitwa masikini"

 

Niliendelea kumtazama bila kujuwa ana plan gani.

 

Muda mdogo Waliingia kina baba wa wili ndipo Nikamuuliza Mr Choi.

 

"Kina Nani Hawa?"

 

"Huyu ni mwanashelia wake"

 

"mwanashelia wa Mr Robert?"

 

"Ndiyo"

 

Nilimpa mkono na kumuuliza.

"Upo Pamoja na Sisi?"

 

Alikubali kwa kutikisa kichwa, nilifurahi mno maana nilikuwa nimejikatia tamaa kabisa.

 

Mr Choi alichomoa sindano flani akamdunga begani Mr Robert kisha akasogeza kichwa chake karibu na sikio la kushoto la Mr Robert, kisha akasema.

 

"Mimi Robert nimekubali kwa ulimi wangu na hakili zangu timamu kuwa Mimi ndiye niliemuua bwana Musa Pamoja na mke wake Pamoja na Watoto zake wawili mapacha, na si huyo tu! Nimeua masikini wengi maana nikiona damu ya maskini ikimwagika Ndiyo furaha yangu, ukweli Mimi kwa kuua nikimuua mtu huwa nafuta ushahidi kuwa amejiua .....sasa kutokana na makosa hayo Naomba serikali ya nchi yetu Kenya muweze kuniadhibu adhabu yoyote nipo tayari kwasababu niliua watu takribani 100 na zaidi na Kifo cha mtu wa mwisho kumuua ni mtoto mdogo binti wa mfanyakazi wangu Mussa ambaye nilimuua kwa kumuweka ndani ya friji kwa lisaa limoja, kwahiyo Kifo chake kinazunguka katika Ubongo wangu Mpaka Sina amani. na video ya tukio nikiwa namuua huyo mtoto ntawaonyesha, kwahiyo Nipo tayari kuingia jela miaka yangu yote, pili kampuni yangu kubwa ambayo mmiliki ni Mimi nimeamua niwagaie serikali ili wawasaidia masikini na wajane, Na nyumba zangu tatu moja iliyopo Mombasa na zingine mbili zilizopo hapa Nairobi nazo pia serikali Naomba mzisimamie wawekeni Watoto Yatima wote, nikizani ndiyo ntasamehewa.

 

Mr Choi alipomaliza kuongea akamwambia "kila utakachoulizwa kubali pia kubali kusaini"

 

Alipomaliza alimlaza chali kisha akasogea pale tulipo, muda wote mimi nilikuwa mwenye kushangaa tu.

 

"tumsubiri Kama dakika mbili ataamka" aliongea Choi.

 

Muda Huo aliingia mkaka flani na camera ndipo Nikamuuliza Mr Choi.

" Huyu naye vipi? "

 

"usijali utaona mwenyewe"

 

Dakika mbili hazikupita Mr Robert akaamka, ile kuamka tu mwanashelia wake alisogea karibu yake na cameraman akaanza kuchukuwa tukio.

 

Mr Robert bila kujielewa akaanza kunukuu maneno yote aliyoambiwa na Mr Choi, ukweli hakuacha hata nukta vyote aliongea, alipomaliza kuongea mwanashelia wake alimuuliza.

 

"kwahiyo boss tufanyeje?"

 

"Nipe ni saini"

 

Mwanashelia wa Mr Robert alivuta documents akampa asaini, pembeni baba Yule aliyekuja na mwanashelia alikuwa pembeni kama shahidi, Mr Robert alipomaliza kusaini, mwanaShelia wake akasaini naye pia huku shahidi akiwa anashudia.

 

Baada ya hapo Mr Robert akiwa hajitambui alivuta simu akaingia gallery akaplay ile video alipokuwa amekaa huku mdogo wangu Munira akiwa yupo ndani ya friji Analia akiomba asaidiwe.

 

Niliposikia sauti ya marehemu mdogo wangu uzalendo ulinishinda nikatoka hraka huku nikilia.

 

Baada ya muda video waliyomrikodi Mr Robert akiwa anakili makosa yake, ilisambaa kona zote kwa dakika kadhaa mpaka serikalini video ilifika, kilichowaumiza zaidi wananchi na serikali ni ile video ya kumfungia mtoto mdogo ndani ya friji mpaka akakata roho.

 

Baada ya masaa kadhaa Mr Robert aliamka akajihisi mchovu Sana tofauti na siku zote, kila muda alikuwa anapiga mhayo Kama mwenye njaa, taratibu aliamka akawasha TV kisha akaanza kupiga mswaki bila kujuwa kinachoendelea.

 

Akiwa anaendelea kupiga mswaki, alishtuka kuskia sauti yake ikisema "Mimi ndi5e nilimuua Mussa na...." taratibu akageuka kuangalia TV je ni kweli kwa kile anachokisikia?

 

Aisee hakuamini kuona sura yake pia na kusikia sauti yake akiwa anaongea Siri zake hadharani.

 

Presha ilimpanda bila kujielewa alidondosha mswaki Chini kwa sauti ya Juu akasema "Nani kafanya haya?"

 

Mwisho kabisa alikumbuka Sisi ndiyo tulikuwa ndani ya chumba chake na akakumbuka Mr Choi walikuwa wameanza kugombezana. kila alichokuwa anakishika kilikuwa hakishikiki kwa wakati huo, Haswa alipofikiria kampuni yake anayoipenda kufa na kupona eti Leo hii siyo yake kaikabidhi mikononi mwa serikali, hapo ndipo alipatwa na ukichaa.

 

Taratibu akasogea dirishani akafungua pazia akaona polisi wengi wamezunguka nyumba yake.

 

Kulia alishindwa machozi ndiyo yalianza kumbubujika.

 

Kila kiungo cha mwili wake kilikuwa kinatetemeka kwa uoga, taratibu alivuta simu yake akakuta missedcall za marafiki zake vigogo kama sita wakiwa wamempigia kama Mara stini, missedcall za wafanya biashara waliyo na hisa zao ndani ya kampuni yake, walimpigia kama Mara 40 na hapo voice whatsapp zilikuwa zinazidi kipimo, muda Huo mdago wake Jacob alipiga simu akajikuta anamkatia simu bila kujielewa. Ndipo Mr Robert akaona yeye ampigie.

 

Jacob alipokea na kumuuliza akiwa na jazba kali "kuna nini kinaendelea kaka?"

 

Mr Robert kuongea alishindwa akaishia kuachama tu.

 

Jacob akaendelea kumuuliza.

 

" Nani kakufanyia upumbavu huu? Au wewe mwenyewe Umefanya haya kwa hakili zako?"

 

Jacob hakuweza kupata majibu yoyote kutoka kwa Mr Robert ambaye ni kaka yake ya wadanu.

 

Muda Huo askari kwa nje walisikika wakimgongea mlango wa chumba aliko Mr Robert ili waweze kumkamata, Mr Robert Baada ya kusikia askari. sauti yake ilirudi akamwambia mdogo wake huku akipumua kwa kasi kubwa.

 

" ni ni ni Mr Choi amenizunguka na ameungana na Madina, nisaidie mdogo...."

 

Kabla hajamalizia police walivunja mlango na muda Huo simu ya Mr Robert ikadondoka Chini kwa presha Kali.

 

Jacob Muda Huo Yeye alikuwa yupo zake Korea kwa ajili ya biashara zake haramu.

 

Jacob Akiwa yupo ndani ya hotel ya kifahari alikunja uso na kusema. "mtalipa kwa hili"

 

 

 

Upande wa huku Kenya Mr Robert aliwekwa ndani ya mikono ya police na tayari kupelekwa mahabusu ili kusubiri kesi yake ipelekwe mahakamani.

 

Baada ya siku kumi kupita nilikuwa Mimi na Salome ambaye kwa Muda mchache tulijuwana nikamfanya kuwa mdogo wangu.

 

"muda mwingine nikijaribu kukumbuka kitu alichonifanyia Jacob Natamani kujinyonga" aliongea Salome.

 

"usiongee hivyo Kikubwa Nikumuomba Mwenyezi Mungu atupiganie kwenye kesi hii"

 

"na nasikia watu wengi wanasema wanatuunga mkono mpaka ahukumiwe Kifo"

 

"na Mimi nipo imara kusimama kizimbani sijali chochote"

 

"hapa ulikuwa unaishi na wazazi wako?"

 

"Ndiyo Kwani pabaya?"

 

"pazuri sana"

 

"kweli sometimes nahisi ntakuja kuwa chizi one day maana sitaki kuomba tena kazi nataka kuendelea kuishi hivi hivi mpaka nafsi yangu itakapotengana na mwili ili niwafuate wazazi wangu na wadogo zangu"

 

"pole kwa upweke vipi Huna boyfriend?"

 

"mtu ambaye moyo wangu ulikuwa umeenza kudunda Kwake ni Jack. Naye hayupo tena"

 

"pole"

 

Muda Huo Mr Choi ambaye alikuwa mwema kwetu kwa siku chache alifika na kusema "are you there"

 

Tulitabasamu tukamkaribisha akakaa kwenye sofa.

" mnaendeleje!"

 

"tupo vizuri huko mambo yapoje?" nilimhoji.

 

"wiki ijayo Mr Robert atasimama kizimbani, vipi utaweza?"

 

"ntalazimika kuweza maana kama sijafanya hivyo ntauwawa"

 

"inatakiwa mkimaliza Mwende Korea kwa ajili ya usalama zaidi maana Jacob atakuwa na kisasi Kikubwa juu yenu"

 

"yupo wapi huyo mshezi" Salome aliuliza.

 

"unamzungumzia Jacob?"

 

"ndiyo"

 

"Yeye yupo Wingereza"

 

"Kama yupo huko yatupasa tufanye haraka. ila tatizo viza hatuna yakutufikisha Korea" niliongea.

 

"Msijali"

 

Imani yetu Jacob yupo wingereza Kumbe Yeye alikuwa yupo Korea huko tunakotaka kukimbilia.

 

"naamini lazma Robert atakatiwa kifungo cha maisha, Ikiwa hivyo passport ntawatafutia na tickets pia"

 

Nilitabasamu na kumjibu kikwao. "kumawo"

 

"unakijua?"

 

Tulicheka kwa Pamoja.

 

Baada ya siku nne kesi ya Mr Robert iliwekwa mezani serikali ya Kenya haikutaka kesi yake ipelekwe mahakamani ingawa baadhi ya viongozi walitaka iwe hivyo ila serikali ilikataa ikatangaza kuwa atafungwa kifungo cha maisha kwa muujibu Wa Shelia maana vidhibitisho vya kuonyesha kuwa Yeye ni muuwaji vilikuwepo, vile vile hata Yeye alijisemea mwenyewe kwenye video japo alikuwa anadai anasingiziwa siyo yeye na video Ilikuwa yakutengenezwa.

 

Nilifurahi mno ndani ya mahakama, tukakumbatiana na Salome kwa furaha isiyo ya kifiki.

 

Mr Robert Baada ya kusikia maneno kutoka kwa mheshimiwa hakimu alipaza sauti akidai asikilizwe hata kwa dakika mbili, ila askari magereza walimfuata na kumshika kisha kumtoa eneo hilo.

 

Furaha kwangu ilizidi mpaka nikaanza kulia huku nikimshukuru mwenyeziMungu kwa miujiza amenionesha kwa dakika za mwisho.

 

Tulitoka eneo hilo Mimi na Salome tukapanda ndani gari ya Mr Choi kisha tukaelekea sehemu flani ili kutuliza hakili zetu.

 

Tulielekea nje ya mji Kidogo, tulipofika tuliweka makazi yetu ya muda mchache Sana kwenye nyumba flani nzuri kiasi.

 

Tukiwa tupo ndani ya nyumba hiyo. Mr Choi alikuwa anatuandalia tambi maana ndiyo chakula chao pendwa.

 

"kwetu chakula hiki ndo kinapendwa sana" aliongea Choi.

 

"vipi kuhusu ubwabwa?" nilimhoji.

 

"Sisi hatuuandai kama Ninyi. Mkifika kule yupo kijana wangu atawapokea Anaitwa pack jin"

 

"vipi kuhusu wewe hatuendi wote?"

 

'Hapana. naenda marekani kwanza maana kuna mzigo naufuatia"

 

"aaahhh" nilijibu kinyonge.

 

"nyumbani kwetu Korea ukipewa zawadi na mwanaume usiempenda usichukuwe" Mr Choi alianza utani na kutufanya tucheke.

 

"kwanini nisiichukue?" Salome aliuliza.

 

"kwasababu ukichukuwa utakuwa umemkubali"

 

Tulicheka Mimi na Salome kisha nikasema "mi naichukuwa kisha nione sasa atafanya nini"

 

Mr Choi alipakuwa tambi akaleta na miti sita kwa ajili ya kutumia kulia tambi, alitukabidhi kisha akatuonesha namna ya kututumia.

 

Tulijaribu ila tulishindwa tukaamua kutumia mikono.

 

Upande wa Mr Robert Alikuwa yupo ndani ya chumba cha magereza huku akiwa amejikunja kama mtoto Yatima, mdomo wake ulikuwa umekauka kwasababu ya kukosa chakula kwa muda, maana kila walipokuwa wanamletea chakula alikuwa akizarau na kudai wamletee chakula kizuri tofauti na kile ila haikuwezekana, kila akikumbuka Mali zake, walinzi wake, wafanyakazi wake wa ndani Pamoja na vimada wake pia akakumbuka alivyokuwa akipita barabarani kama msafara wa Raisi ndipo akaunganisha alivyoambiwa Mali siyo zake tena na anahukumiwa Kifungo cha maisha aisee hapo ndipo alizidi kuchanganyikiwa zaidi.

 

Upande wetu tukiwa tunatumia msosi nilimuuliza Mr Choi "muda ule nipo mahakamani niliangaza kama ntaona mtoto wa Mr Robert au hata mke sikuweza kumuona, je wapo wapi?"

 

"Huyu mzee hanaga mtoto wala mke"

 

"kwahiyo hakuwahi kuoa?"

 

"kila akioa anafukuza na wengine alikuwa anauwa"

 

"hakubahatika kuwa hata na mtoto hata mmoja?"

 

"alisema wanawake mbele yake ni uchafu na Hawezi kuzaa na uchafu ndomaana Mara nyingi alikuwa anawachukuwa wanawake wa wafanyakazi wenzie ili kuwachezea tu na yote aliafanya ili kuonesha ulimwengu kuwa siku zote mwenye pesa anaweza kufanya chochote"

 

Nilishusha pumzi na kusema "Natamani kumuona kwa sasa hivi kabla sijaenda Korea"

 

Tukiwa tupo hapo television ilipeperusha habari ikisema "mzee ambaye alikuwa kwasasa ameichukuwa nafasi ya pili ya utajiri mkubwa hapa nchini Kenya, ajulikanae kwa Jina la Mr Robert cha-cha mmiliki wa hotel kubwa mbili zilizopo Mombasa na....

 

Akiwa anaendelea kusema Mr Choi alituuliza "kumbe alikuwa na hotel?"

 

"nashangaa kusikia" nilimjibu.

 

Tuliendelea kumsikiliza Mtangazaji yule wa kike alivyokuwa akitangaza: ....... Masaa matano kupita baada ya kumkatia hukumu ya kifungo cha maisha bila kesi yake kusikilizwa kutokana na Kifo alichokisababisha kwa mtoto mdogo wa miaka 6 ajulikanae kwa Jina la Munira Mussa kumuweka ndani ya friji kwa lisaa limoja, chanzo kwasababu ya tukio ya dada yake ajulikanae kwa Jina la madima Mussa kuweza kuungana na Rafiki yake ambaye hajatambulika vizuri nakurusha clip ya video huku wakiomba msaada ili kuokolewa ndani ya nyumba kubwa ya Mr Robert iliyopo hapa jijini Nairobi.... Mr Robert ameamua kujinyonga mwenyewe baada ya hukumu hiyo, mlikuwa na Mtangazaji wenu...

 

Aliendelea kuongea huku tukiwa tunashangaa bila kuamini.

 

Mr Choi kwa sauti ya Chini akasema.

 

" Malipo ni hapa hapa duniani, angalia alikuwa anapenda kuwafanya watu wajinyonge kupitia kamba, Leo hii yeye huyo huyo imemrudia"

 

"lala mahala pema Mr Robert mwisho wako umekuwa mzuri zaidi"

 

Siku zilisonga tukajipanga na safari ya kuelekea Korea.

 

Moyo wangu ulitulia kila Mara nilikuwa nikimshukuru mwenyeziMungu kuona alinilipizia kisasi.

 

Tuliendelea kujipanga Mimi na Salome mwishowe tulielekea airport tukaagana na Mr Choi kwa furaha kisha tukapanda ndege ili kuelekea Korea, naye akarudi ili kujipanga na safari ya kuelekea wingereza.

 

Kidogo Tabasamu yangu ilirudi Licha vipenzi vyangu wote waliangamizwa na Mr Robert.

 

 

 

SONGA NAYO!

 

Baada ya Miezi mitatu kupita, Mimi na Rafiki yangu Salome baada ya kutoka nchini kwetu Kenya nakuelekea Korea kwa ajili ya usalama zaidi, tulizoea maisha ya hapo vile vile na rugha ya kikorea.

 

Miezi yote hiyo hatukuweza tena kupata mawasiliano na Mr Choi ambaye ndiye alitusaidia kulipiza kisasi kwa aduwi yetu Mr Robert.

 

Maisha ya Korea upande wetu yalikuwa mazuri zaidi kutokana na kuishi bila kubugudhiwa, licha sehemu tuliyokuwa tunaishi walikuwa wakitubagua muda mwingine.

 

Siku moja natoka mahangaikoni, nilimkuta Salome akiwa amelala na siyo kawaida yake

 

"Nini shida?" Nilimhoji.

 BONYEZA HAPA KUPATA MAKALA ZA MAFANIKIO KUPITIA SIMU YAKO

 

ITAENDELEA

 

 

No comments

Powered by Blogger.