Simulizi: Tabasamu langu sehemu ya tatu (03)
Muda mdogo askari waliyoko nje baada ya kusikia miparangano ndani ya monchwali, Waliingia ili kujuwa nikipi kinaendelea, walipofika walimkuta Jack akiwa amemlaza Chini Jacob huku akimpiga ngumi.
Ndipo Waliamua Ugomvi Jack akapelekwa kituoni.
Nikiwa nipo njiani narudi nyumbani niliona kweli siku zote mwenye pesa ndiye mwenye kauli ya mwisho, njia nzima nilikuwa nalia.
Baada ya muda, nilielekea mahakamani nikawaeleza kuhusu Kifo cha baba yangu kuwa hajajinyonga bali ameuwawa. Ila kila niliyekuwa nikimueleza aliniambia nirudi nyuma watafanya upelelezi wakina.
Siku hiyo Jack aliachiwa akaja kuniona nyumbani, alipofika mama alimwambia toka asubuhi hajaniona hivyo ajitahidi anitafute huwenda kuna jambo nataka kufanya.
Upande wangu nilitembelea Ofisi mbali mbali zinazohusika na haki za binadamu ila kila niliyekuwa namwambia, jibu lilikuwa ni lile lile *nenda nyumbani tutalifuatilia kwa kina*
Siku iliyofuata, asubuhi na mapema nilichukuwa bango kubwa kiasi nikaandika maelezo kuhusu Kifo cha baba kuwa aliuwawa hakujiua nahitaji waalifu waweze kukamatwa. moja kwa moja nilielekea mahakamani, nilipofika nje ya jengo kubwa la mahakama nilisimama Huku nikiwa nimeshikilia bango hilo.
Wafanyakazi kama Kawaida saa 2 kuingia kazini walianza Kuja, kila mmoja alikuwa ananishangaa Sana huku wakiingia kwenye jumba hilo.
Nilibaki pale Mpaka muda wa kazi kuisha saa 8, baadhi ya watu Wema walitamani kesi ya baba yangu ifuatiliwe kwa Kina ila walishindwa maana suala lile lilikuwa juu ya uwezo wao. njaa, kiu Pamoja na uchovu vilinitesa Muda ule ila nilifanya Yale nikihitaji Shelia ishike mkondo wake.
Muda huo mzee flani anaefanya kazi ndani ya jengo la mahakama, alinisogelea na kuninong'oneza kitu masikioni "Usijisumbue, rudi tu nyumbani ukatulie... ukinihitaji kwa maelezo zaidi Chukuwa namba yangu"
Alinipa namba yake ya simu kisha akaondoka.
Muda Huo Jack naye alifika.
"hiyo siyo suruhisho madina" aliniambia kwa msisitizo mkali.
"kwahiyo?" nilimhoji kijasiri.
Jack hakutaka kunijibu, alinishika mkono na kunitoa eneo hilo, moja kwa moja tulienda mgahawani.
Tukiwa tumekaa mgahawani, mbele yetu chakula kilikuwa kimetengwa huku kila mmoja akishindwa kula.
"tafadhali kula" Jack alinisisitiza kana kwamba yeye yupo anakula.
"binadamu ni wabaya kuliko wanyama, siku ile mdogo wangu anafariki Watangazaji wengi walinifuata kuniuliza kuhusu baba kumuua mdogo wangu... ila Leo hii nimeshangaa Hakuna aliyetaka hata kunisogelea, kwanini wasingechukuwa tukio lile Labda mheshimiwa Raisi angeona na akatoa ruhusa nikasikilizwa, Naumia Sana Jack" niliongea kwa uchungu huku machozi yakinibubujika Kama mvua.
'Naelewa ila please kula kwanza"
'Na wewe je! "
"Kula please na Mimi ntakula"
Nilianza kula huku nikilia mno hata chakula Hakikuweza kupita, nikanyanyuka na kuondoka.
Nilimpigia simu mzee Yule akanipa maelezo, bila kupoteza muda nikaelekea kwake.
Nilipofika tulikaa kibarazani nikamueleza chanzo cha mdogo wangu kuuwawa Mpaka Kifo cha baba.
"hili Jambo huwezi kuliacha likaenda taratibu?" aliniuliza.
"siyo kwa mtu aliyefiwa kama Mimi"
"sawa, Naelewa, sasa ngoja nikwambie... kufanya Yale siyo suluhisho, ukija kuangalia vibaya utapewa kesi kuwa unataka kuleta machafuko ndani ya nchi.. mjukuu wangu haya mambo nimeyaona na kuyasikia kwa Muda mrefu Sana toka Nipo kijana, mimi ni wakili kwa watu mbali mbali Labda Kiufupi niseme huwezi kupigana vita na tajiri hali ya kuwa wewe ni masikini"
"kwahiyo nafanyaje?"
"wewe ni kijana na damu yako inachemka sana, kila litakalokuja kichwani utataka kufanya Ila ni hatari Sana upande wako"
"nafanyaje sasa?"
"Achana nayo Mungu atakulipizia"
"siyo kirahisi kwa mtu mwenye uchungu kama Mimi, hivi unajua mwili wa marehemu baba yangu Ulivyokuwa? Baba alihangaika sana alitamani msaada akaukosa nahisi alipokuwa anapigwa alikuwa akiniita niende kumsaidia..... Labda nikuahidi kitu kimoja, Mimi naenda kufanya kitu ambacho kitashangaza ulimwengu mzima" baada ya kuongea kijasiri, Sikutaka kusikia marefu kutoka kwake bali niliondoka zangu.
Siku iliyofuata, nilitia timu nje ya kampuni kubwa ya kusafirisha abiria ambayo mmiliki wake ni nusu shetani mr Robert, nikiwa nipo nje huku ndani ya mfuko nimejaza mayai yaliooza nilijisemea moyoni "Utalipa kwa kile ulichokifanya, si unajidai Kisa una hela, ningoje taratibu"
Ghafla mr Robert alitoka ndani akiongozana na baunsa wake wawili huku akiwa anaongea kwenye simu na hali yake alionekana amefurahi mno kutokana alikuwa anacheka cheka.
Ile kumuona tu, aisee uzalendo ulinishinda, nilivuta mayai manne kwa Pamoja bila kuchelewa nikamrushia kwenye shati yake ya bei chafu aliyokuwa amevaa, yakampasukia na kutoa harufu mbaya. baunsa wake na Yeye pia waligeuka kuniangalia kwa mshangao, kwa sauti ya Juu nikasema.
" Kwanini baba yangu ulimuua?"
Baunsa wale walinifuata, nilipoona wanataka kunifikia, niliachia mayai Sita mfululizo yakampata yote Mr Robert, baadhi yalimpata kichwani mengine usoni na mengine kifuani.
Kabla baunsa wale hawajanifikia askari polisi kama Kawaida yao kuimalisha ulinzi, walifika wakanikamata na kunipeleka kituoni kwa ajili ya maelezo zaidi.
Baada ya siku nne kupita nikiwa bado nipo sero, Robert alinifuata, nilipomwona Nilinyanyuka kwa hasira nikasogea kwenye nondo na kuyashika kwa nguvu huku nikipumua Kama mlusi mjamzito.
"Yu hali gani binti yangu?" Mr Robert bila hiyana aliniuliza huku akiachia tabasamu kwa mbali.
Kwa hasira nilivuta kikohozi na kumtemea usoni.
"yote unayoyafanya mama yako na mdogo wako watayalipa, kitu naenda kukufanyia utajuta maishani mwako mazima....Halafu wewe utakufa mapema maana unahasira hasira Kama baba yako, hivi unahisi baba yako asingejifanya kufuatilia kuhusu mdogo wako angekufa Kifo Kibaya Kama kile? Narudia kusema, nitafanya Kibaya kwa mama yako na mdogo wako Mpaka mwenyewe hutokaa ukaamini, Labda nikuhabarishe, kuanzia sasa hivi wewe ni binti yangu maana mama yako yupo ndani kwangu, nimemuoa" Mr Robert aliongea kwa hasira huku akiwa amebananisha meno ishara anatamani kunitafuna tafuna sema kaheshimu jumba la serikali. Maneno yake niliyapuuza, kwa kibri na zarau nikatabasamu.
"kelele za Chura, hazimzuwii tembo kunywa maji" niliongea kijasiri.
Ndipo mr Robert alichomoa simu yake na kupiga simu.
"baby Upo nyumbani? Ongea na binti yetu"
Aliweka raundispika. kwa masikio yangu nikasikia sauti ya mama akiniuliza "Upo Salama mwanangu?"
Aisee hapo ndipo Nilichanganyikiwa mno, mr Robert akamwambia mama.
" mwambie binti yetu kuwa nimekuoa"
"Madina, Baba yako yupo hapo kwa ajili ya kukutoa sero, usijali utakuja naye nyumbani mtakuta nimewaandalia chakula"
Sauti ya kumjibu niliikosa nikaishia kushangaa, Robert akakata simu na kuniambia
" karibu ndani kasri yangu"
Kisha Akaondoka na kuniacha nikiwa namsindikiza kwa macho, taratibu niligeuka nikashuka Chini na kukaa huku nikiwa nimejikunja, nilijaribu kukumbuka maneno aliyoniambia muda si mrefu kupita, pia nikakumbuka sauti ya mama alivyokuwa anaongea. aisee nilijikuta naangua kicheko cha maumivu kikiambatana na machozi kama Mvua.
Baada ya muda huwezi kuamini nilitolewa sero bila adhabu yoyote nikapandishwa gari kiubabe na kupelekwa sehemu nisiyoitambua.
Moja kwa moja kwenye mjengo mkubwa uliyopo nje ya mji Kidogo, kiukweli nyumba hiyo, ilikuwa kubwa mno, maana kwa mtazamo tu, nusu mtaa wanaweza kuishi na wasibughudhiani. ni jinsi gani mjengo ulivyo mkubwa mno.
Tulizama ndani, wafanyakazi wa ndani kama kumi wakaja kunipokea nikapelekwa aliko mama na mdogo wangu Munira.
Munira aliponiona alinikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu tofauti na siku zote.
"mbona Munira anaogopa sana?" nilimhoji mama ambaye nilimpelekea kuanza kulia.
Taratibu nilichuchumaa na kumwangalia usoni Munira, uso wake ulikuwa umejaa mangeu mpaka mwenyewe nikapata Hofu na mashaka.
"wamekufanya nini mrembo wetu?" nilimhoji kiupole.
"dada wamepiga Mimi, namtaka kaka"
Nilimsogelea mama alipokuwa amekaa kitandani kisha Nikamuuliza.
"mama nini kimesababisha Mpo hapa? kwasababu mi nakujuwa vizuri huwezi kufanya haya embu niambie"
"I'm sorry my daughter"
"mbona Munira yupo hivi?"
"mwanangu chanzo cha Mimi kuwa hapa ni Munira na wewe, walimteka Munira wakanirushia video wapo wanamtesa nikaambiwa ili asiuwawe kama pacha wake nikubali kuolewa na mshenzi huyu, na Mimi sikuwa na jinsi niliona Nifanye hivi ili kumuokoa Munira wangu" mama aliongea kwa uchungu mkali ndipo nilianza kumfuta machozi huku nikimpa moyo wa ujasiri.
"usijali niko Pamoja na wewe, katika wakati mgumu Kama huu, yakupasa uvae viatu vya baba na uhakikishe vimekutosha ili tuweze kushinda vita hii.... Kumbuka Hakuna atakaeishi milele kwenye ulimwengu huu... baba, Abdallah wametangulia ila nasi twawafuata"
Baada ya muda nilitoka chumbani nikamuona mfanyakazi mmoja akiwa Analia kwa uchungu, taratibu Nilimsogelea na kumuuliza.
"unatatizo gani binti?"
Baada ya kuniona alishtuka na kuanza kujifuta machozi, nilimshika mkono na kumuuliza kwa Mara nyingine.
"unanini mdogo wangu?"
"naitwa Salome, Nani mwenzangu?" alinihoji baada ya kujikaza.
"Mimi ni Madina"
"karibu sana"
"Mbona unalia?"
"nimarefu. nifuate muda mwingine"
Aliondoka huku akiyafuta machozi yake.
Baada ya muda nilimtafuta, nikamkuta chumbani kwake akiwa amelala, nilikaa kitandani na kumuuliza "unaumwa?"
Aliposkia sauti yangu aliamka na kunijibu.
"Hapana sipo vizuri kwa Leo. wewe ni mgeni hapa?"
"Ndiyo! Embu nikuulize, unamjua mmiliki wa nyumba hii?"
"ni Mr Robert"
"hivi hakuna njia yoyote ya kutoroka humu ndani?"
"sijawahi kujaribu, Kwanini Upo hapa?"
Nilimpa mkasa wote ulionipata mpaka nikaletwa hapa.
"pole Sana my dear"
"Nimeshapoa, why kila muda unalia?"
"yalioyonikuta kama yako, hata mimi Mr Robert ndiye kamuua baba yangu"
"kisa nini?" nilimuuliza kwa mshangao.
"sijui kisa, Ila nilienda kila kituo ili kutoa malalamiko yangu Haikusaidia chochote, nilipopata nafasi ya kumuona Robert nilimuuliza Akaniambia Yeye anafurahia Sana Akiona damu ya mtu ikimwagika"
"mama yako yuko wapi?"
"Muda mrefu hayupo duniani"
"pole Sana, sasa kwanini wewe Upo hapa?"
"baada ya kuniona nafuatilia sana kuhusu Kifo cha baba, alitangaza kuwa atanilie na atanisomesha, mwisho wa siku akanileta hapa"
"sasa baba yako Ilikuwa kuwaje akafa?"
"sijui kiundani Ila walimsingizia eti kajinyonga kisa kachoka maisha"
Ndipo nilipata picha nikajuwa Kumbe Mr Robert Yeye anaua kisha anafuta ushahidi kwamba marehemu mwenyewe ndiye kajiua kutokana na sababu flani.
"dada Madina, hapa ndani tunaishi kama punda, ukifanya kosa dogo bakola utakazopigwa hutokaaga ukasahau"
"vipi kuhusu Mr Robert, anaishi hapa ndani?"
"Hapana, kwanza sijui kwanini aliijenga nyumba hii, Ila wanawake wote utakaowaona humu ndani, juwa ni wake zake"
"aliwaoa?"
"Hapana wapo kama vimada"
Siku hiyo ndiyo Ilikuwa siku yangu ya kwanza kuanza kupanga mipango ya kutoroka.
Siku iliyofuata, kwa kuwa simu yangu nilikuwa nayo, nilianza kuwasiliana kupitia SMS na Jack ambae kwa siku chache nilitokea kumuelewa na kumuamini sana.
"Munira anaendeleaje?"
"yupo sawa.... ona Jack! Naomba nisaidie kitu. eleza walimwengu kuhusu Sisi tuliopo huku'
"kuhusu hilo ondoa Shaka, mimi nipo kwa ajili yenu"
"ntakutumia baadhi ya video uisambaze kila kona"
"sawa"
Siku zilisonga huku Jack akizidi kutafuta baadhi ya viongozi wanaohusika na haki za binadamu na Wengine wanaohusika na haki za wanawake.
Siku hiyo nilipata ujumbe kutoka kwa Jack akisema.
"kuna baadhi ya watu nimewapata, wamesema wapo tayari kutusaidia kwahiyo tujipange na ushahidi, hii nahisi itakuwa babukubwa"
Ujumbe wa Jack ulirejesha tabasamu langu, nikajikuta nazidisha upendo ndani ya moyo wangu maana alionyesha jitihada za kutukomboa.
"una waamini?" nilimhoji.
"saana, maana ni marafiki zake na mzee, pia yupo Mwandishi wa habari niliesomaga naye ameniambia atanisaidia kusambaza kwenye magazeti na vyombo vya habari. kwahiyo ondoa Shaka Unakuja nikuoe uwe wangu"
Nilizidisha tabasamu baada ya kuona ujumbe huo, ndipo Nikamuuliza.
"neno la mwisho eti nini?"
"sorry siyo Mimi niliaandika hapo mwisho, simu hii sijui inatutakia nini jamani "
"Nakuamini Sana Jack"
"Hata mimi pia "
Upande wetu furaha ilianza kurudi kama zamani kwasababu Mr Robert au watu wake hawakuweza kuja kutusumbua kama nilivyohisi mwanzo, pia hata Jack alizidi kunipa tumaini kubwa.
Siku nyingine, tulikuwa tunacheza Mimi, mama, Munira Pamoja na Salome, hakika siku hiyo ilikuwa ni special kwetu sisi.
Baada ya siku kadhaa kupita, Nilisubiri ujumbe kutoka kwa Jack Ila sikuweza kupata. Jambo ambalo Kidogo lilinitia wasi wasi, kila SMS niliyokuwa nikituma Ilikuwa haijibiwi maana baadhi ya wenzangu walikuwa wapo tayari kutoa ushilikiano ili tujirikodi video tukiwa tunaomba msaada waje kutuokoa, nikiwa nipo sebuleni na Salome Pamoja na Mabinti wengine, tulishangaa kumuona Jacob ambaye ni mdogo wake Mr Robert, akija kwa kasi ishara kuna Jambo limetokea, baadhi yetu walisimama ili kumpa heshima Ila Mimi na Salome Tuliendelea kukaa huku mimi nikiwa namtazama jicho mbaya.
Jacob alipotufikia alimzaba kibao Salome Na kusema "siku hizi jeuri sana Eee"
Nilinyanyuka kwa hasira na kumuambia "Nipige Mimi usimpige Huyu"
"subiri Fimbo yako inakuja Muda siyo mrefu, nawashangaa sana, Madina nilikwambia siku zote masikini Hawezi kupigana vita na tajiri... angalia sasa mwenzio umemuweka matatizoni, chunga sana domo lako na kupayuka kwako"
Yote aliyokuwa anaongea nilikuwa sielewi anamaanisha nini, ndipo akavuta sigara yake yenye thamani akanipulizia moshi kisha akaniuliza kwa kejeri.
"unamjua Huyu mtu?"
Alinirushia picha kadhaa na kuondoka zake huku akicheka kwa sauti ya Juu.
Nilijiuliza picha hizo zina maana gani, taratibu nikashuka Chini na kuokota picha moja, aisee nilipoiona sura ya mtu aliyoko kwenye picha moyo uliruka huku nikiwa kama vile siamini kwa kile ninachokiona. kwa macho yangu niliona sura ya mwalimu Jack akiwa amefariki, kijana ambaye alikuwa ananisaidia kwa baadhi ya mambo, Huwezi kuamini kwenye picha alikuwa amejinyonga kupitia kamba.
Presha ilinipanda nikatoka hapo nduki huku nikimfuata Jacob, nilipofika nje ya jengo hilo, nilimuona Jacob akiwa anataka kupanda gari, walinzi wawili wakaja kunizui ili nisote eneo hilo, kwa sauti ya Juu yenye majonzi makali nikamhoji.
"umemfanya nini we mshenzi"
Jacob alinipungia mkono kisha akaingia zake ndani ya gari, nikiwa nimeanza kulia nikamwambia "ntakuua kwa mikono yangu miwili"
Baada ya muda kupita, nilikuwa nimeikumbatia picha moja miongoni mwa picha za jack, machozi machoni mwangu yalikuwa hayakati, furaha niliyokuwa nimeipata kwa sekunde chache iliyayuka kama gesi iliyoko ndani ya mtungi usiyo na kizibo.
nilikumbuka mengi tuliyoyafanya, maneno yake ya ukarimu yalizunguka kichwani mpaka nikatamani kupiga kelele huwenda ningepunguza hasira.
Nikiwa hapo Salome alifika na kuniambia " nimepata Wazo"
"wazo gani? " nilimuuliza huku nijifuta machozi.
"nahitaji tujirikodi ile video. tutairusha wenyewe"
"hatuwezi kufanya hivyo mdogo wangu, sitaki kumuweka mtu mwingine matatizoni"
"unahofu na Mimi?"
"ndiyo"
"Labda nikwambie.... tayari Mimi maisha yangu nimeshayatia matatizoni. au unahisi mimi sina uchungu na mzazi wangu? Lazma Nifanye kitu"
Nilipenda ujasiri wa Salome, bila kupoteza muda, tuliwashilikisha wenzetu ila wakakataa na kudai tupambane sisi ikitokea tukafanikisha basi na wao pia watanusurika.
Tulijiandaa, tukaanza kujirikodi video, niliongea maneno mengi yenye huzuni ndani yake tukizungumzia vifo vya watu wasiyo na hatia na yote msababishaji ni Mr Robert.
Tulipomaliza tuliiposti sehemu mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii.
"hii simu uliiletaje huku?" Salome alinihoji baada ya kupumzika.
"nilikabidhiwa kituoni baada ya kuachiliwa"
Upande wa katikati ya mji, video ile ilianza kuvuma kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Mr Robert akiwa yupo ofisini kwake wapambe wake walimletea video ile.
Baadhi ya viongozi ambao wanashirikiana naye kwa mambo madogo madogo walianza kumpigia simu wakimlaumu, kabla hajakaa sawa alipewa taarifa kwamba watangazi na waandishi Wa habari wapo nje wanamsubiri.
Kwa kuwa Mr Robert anajiamini sana, alitoka ndani ya kampuni yake bila wasiwasi, alipofika mbele ya mlango wa kampuni yake, Watangazaji walianza kumuuliza maswali mengi kuhusu video ile, Huwezi kuamini Mr Robert alianza kufuta machozi kwa huzuni huku watu wakimuangalia kwenye TV mbali mbali.
"Nasikitika Sana kusikia mambo haya yakiendelea, Mimi ni mtu mwema sana, nasaidia Yatima, nasaidia baadhi ya wasiojiweza Mpaka Yapo mabasi nimejitolea nimegaia serikali kwa ajili ya kuwasafirisha Watoto Yatima kwenda mashuleni, Ila Leo hii nimegeuka muuwaji? Hivi hamuwezi kujiuliza kuhusu video hiyo kuwa ni watu wanataka kunichafulia Jina? Kidhibitisho gani walichokionyesha kinachonionyesha Mimi nikiwa naua? tafadhali Naomba sana serekali ishike mkondo wake kuhusu Jambo hili" Mr Robert aliongea Kwa uchungu mpaka kupelekea kila aliyekuwa ameanza kutuamini na kutuona wajinga.
Kisha Aliondoka huku akiendelea kufuta machozi, baadhi ya waandishi wa habari na Watangazaji hawakupata maswali mengine ya kumuuliza.
Mr Robert alipofika ndani ya gari lake alitabasamu ishara ya Ushindi.
Tukiwa tupo nyumbani tulishangaa kwenye comments watu wanatuchamba tofauti na mwanzo, ndipo Nikamuuliza Salome "kuna nini mbona sielewi?"
"hata sijui"
Muda huo Jacob alifika Pamoja na baunsa wake kama kumi, Tulimtazama kwa Hofu huku kila mmoja akiwa anajiuliza je ameiona video.
Jacob aliponifikia alininyang'anya simu na kuitupa pembeni kisha ikapasuka pasuka kioo, sikuweza kuleta vurugu tena maana niliona hali Ipo tofauti Sana.
Jacob kwa hasira alimshika mkono Salome kisha akamwambia.
"nataka nikufanyie kitu ambacho hutokaaga ukakisahau maishani mwako mazima, pia nahisi hicho kitamfanya kiherehere mwenzio awe anajutia pindi akikuona"
Alianza kumvuta akimtoa eneo tulipo, nilipoona mwenzangu anateswa Nilinyanyuka ili kuweza kumsaidia Ila Huwezi kuamini baunsa wale, walivuta rungu na kuanza kunipiga.
Jacob moja kwa moja alimpeleka Salome kwenye chumba flani ili kumbaka.
Nikiwa napigwa bakola maumivu sikuweza kuyasikia bali nilikuwa namuomba Jacob asifanye chochote kwa Salome.
Mama akiwa yupo chumbani aliposikia kelele zinazidi sebuleni alimuomba Munira alale anakuja, Munira alilala kisha mama akatoka chumbani.
Mabinti wenzetu Pamoja na kina mama walikuwa pembeni wanalia huku wakichungulia kwa hofu.
Mama alipofika sebuleni alitaka kunisaidia Ila alipewa bakola Za kutosha akatulia.
Baada ya muda Jacob alimtoa chumbani Salome Kisha akamrusha pembeni na kusema.
" jifunze kukaa kimya"
Kitendo kile mama kilimuudhi sana akanyanyuka na kumfuata Jacob, alipomfikia alianza kumpiga Piga huku Jacob akiwa anaendelea kutabasamu kwa dharau, mama aliendelea kumpiga kwa hasira mwishowe Jacob alimsukumia pembeni ili kuondoka zake.
Jacob akiwa anapiga hatua huku akitafuna bigijii mdomoni, alisimama baada ya kushikwa mguu. Kwa hasira aligeuka kutazama atakuwa Nani kamshika.
"unatafuta Kifo?" Jacob alimhoji mama maana ndiye alikuwa amemshika kwa hasira.
"we mshenzi usie kuwa na moyo, mmeniulia Mume wangu na mwanangu, kwa ukatili wenu unakuja kuharibu maisha ya binti mdogo Kama huyu, Leo lazma nikuonyeshe" mama aliongea kwa uchungu, haraka alimng'ata meno kwenye mkuu ikampelekea Jacob kuchukia sana baada ya kupiga kelele kwa maumivu, bila kupoteza muda Alichomoa bastola na kumshuti lisasi ya kwenye komwe maskini mama taratibu akaenda Chini.
Sauti ya kuita mama ilikata nikaendelea kushangaa shangaa huku nikijiuliza Nikweli au naota.
Jacob kwa jeuri akasema.
"Oohh masikini! eti Madina nimefanikiwa kumuua aduwi yangu? Aaahhh kumbe mama yako huyu Eee.... I'm sorry lisasi imetoka kwa bahati mbaya embu Njoo ujaribu kumuamsha huwenda akaamka"
Aliachia kicheko kama Kawaida yake kisha akaondoka, kabla hajatoka kijana mmoja Kati ya baunsa wake alimuuliza.
"boss vipi kuhusu mwili huu?"
"acheni kwanza Labda Madina atamuamsha"
Ndipo waliondoka zao.
Nikiwa Nimelala Chini huku mwili wangu ukiwa umetapakaa damu, maumivu niliyokuwa nayo ndani na nje yalikuwa siyo ya Kawaida, nilijitahidi taratibu nikaamka na kukaa kitako, pembeni Salome alikuwa Analia kwa sauti ya Chini mno.
Nilimuangalia mama alipo kisha nikamwambia huku nikilia.

No comments