Simulizi: Tabasamu langu sehemu ya Tano (05)
"naumwa"
"unaumwa nini?"
"ukweli Madina Nampenda pack jin kufa mtu"
"Unasemaje wewe!"
Pack jin ni mtoto wa Mr Choi hivyo yeye ndiye aliotupokea na mpaka muda huo tulikuwa bado tunaishi kwao.
"nafikiria namna ya kumtongoza" aliongea Salome.
"Hata Kama tupo huku, hatupaswi kuacha mila na destuli ya kiafrika"
"nikweli Ila mtu kumueleza Hisia zako Sioni kama kuna ubaya wowote"
Nilimuwahi nikamtekenya kiutani kisha nikamuacha huku nikimuambia.
"amka Fanya usafi, naenda kuomba kazi"
Nilivuta begi yangu nikavaa kisha nikatoka chumbani, kabla sijafika sebuleni nilimsikia mama pack jin akimwambia pack jin.
"sitaki kuwaona tena Hawa Mabinti humu ndani, naomba warudishe ulikowatoa Sina uwezo wakulea watu nisiyo wafahamu"
Moyo wangu uliuma mno, nikatafakari nikagundua hata hivyo ilibidi tujiongeze kama watu wazima, ndipo nilirudi chumbani nakuanza kupanga mizigo, Salome akiwa ananishangaa aliniuliza.
"unafanya nini?"
"amka, panga nguo zako"
"eti?"
"nimeongea kikorea?"
"kiswahili"
"Basi Fanya ulichoambiwa"
"OK! tunaelekea wapi?"
"mama yake pack jin hataki kutuona humu ndani, kwahiyo kilichobaki Sisi ni kujiongeza tuondoke tu. maana pack jin tunampa wakati mgumu Sana"
"ntaweza kuishi bila yeye?"
Sikumjibu Niliendelea kupanga nguo zangu.
Baada ya dakika kadhaa Tulitoka chumbani huku kila mmoja akiwa na mzigo wake wa nguo.
Sebuleni alikuwepo mama yake pack jin peke yake, tulipomfikia nilimsalimia na kusema.
"Sisi Tunaondoka"
Hakutujibu bali Aligeuza shingo ishara tunamsumbua, nilipoona hivyo nilimuambia.
"Ahsante Sana kwa kutuhifadhi kwa kipindi kirefu kama hichi, Sisi Tunaondoka"
Baada ya hapo tuliondoka zetu.
Tukiwa tupo njiani tunaelekea tusikokujua, tulikaa kwenye kiti kilichoko barabarani kwa ajili ya watu kujipumzisha pindi wakichoka.
Tukiwa tumekaa Salome aliniuliza.
" tunaelekea wapi?"
Nilichomoa simu mfukoni kisha nikatafuta namba za kijana flani dalali kisha nikampigia.
"Leo tupate dinner kwa Pamoja" aliniambia baada ya kupokea simu, ndipo nilitabasamu kinyonge.
"Potezea kuhusu hilo, vipi kwanza ntapata chumba?"
"vyumba vipo ni wewe tu"
"nitafutie chumba cha bei ndogo sana si Unajua bado sijapata kazi"
Alicheka kisha akakata simu ishara atanitafutia.
"Mbona kama vile anazingua" salome aliniambia.
"ndivuo alivyo"
"Ulimfahamu vipi?"
"Kuna siku Nilimpaga dili ya kunitafutia nyumba...... ila Salome moyo wangu Hauna amani nikimkumbuka Jacob nahisi lipo Jambo atatufanyiaga hata ipite miaka 50"
"sitaki kusikia habari zake kwanza kwanini Mr Choi Hapatikani mpaka sasa?"
Muda huo dalali alinipigia simu na kuniambia.
"chumba kimepatikana tena bei nafuu kabisa"
"dala Mia ngapi?"
" mia moja tu"
Nilifurahi mno maana ndani ya mji wa Seoul kupata chumba kwa dala mia moja tu, si jambo rahisi.
ndipo Alinipatia address wapi tukutane.
Tulifika kwenye kituo cha mabasi, kama dakika mbili basi ilifika tukapanda na kukaa karibu na mlango maana watu walikuwa wamejaa.
Tukiwa tupo bize na safari, niligeuka nyuma kama Kawaida ya binadamu kuangalia angalia kona zote, ndipo nilishangaa kumuona kijana mweusi kama Sisi Jambo ambalo Korea kumuona mtu mweusi siyo Jambo la Kawaida, nilijiuliza maswali mengi kuhusu kijana huyo hakika Nikajikuta Natamani kumjua zaidi ili ikiwezekana tujuwane kiundani, taratibu nikageuza shingo na kumuambia Salome.
"kuna mtu nimemuona, muafrika mwenzetu natamani kumjua huwenda tukasaidizana ndani ya mji huu"
Ndipo Salome aligeuka nyuma ili kuweza kumtazama kijana huyo, alipoiona sura ya kijana huyo alishtuka mno na kuangalia mbele, ghafla Salome akaanza kutetemeka kwa Hofu, Jasho ikaanza kumfumuka mwilini ishara kuna Jambo ameona ambalo limeulaluwa moyo wake.
Nilipoona hivyo sikutaka kumuuliza kuna nini, niligeuka nakumwangalia kijana huyo kwa mara nyingine, huwezi kuamini baada ya kumtazama kwa sekunde kadhaa niligundua ni Jacob mdogo wake marehemu mr Robert, nikashangaa kumuona akionyesha picha baria wenzake kama vile kuna mtu anamtafuta, haraka niligeuka mbele huku nikipumua kwa kasi kama mtoto aliyekamatwa na mama yake baada ya kudokoa nyama kwenye sufuria.
Upande wa Salome machozi yalianza kumbubujika kwa uchungu baada ya kukumbuka tukio mbaya aliyofanyiwa na Jacob.
Kushuka ndani ya basi ni kitu hakiwezekaniki kutokana kituo kinachofuata kilikuwa mbali kidogo.
Nilipoona Salome hali yake inazidi kuwa mbaya nilimshika mkono huku nikimpa moyo asijali Allah yupo Pamoja na Sisi.
Tukiwa tupo hapo huku tukiendelea kutetemeka, huwezi kuamini sauti ya Jacob ilipenyeza vyema kunako masikio yetu akiuliza watu waliyokaa kwenye siti ya nyuma yetu.
"Hawa Madada mnawafahamu?"
baada ya kuambiwa hawawafahamu watu hao waliyopo kwenye picha alianza kupiga hatua akitufuata ili kutuuliza na Sisi kuhusu watu hao waliyopo kwenye picha tunawafahamu.
Hapo ndipo tulishikilia myoyo yetu mkononi.
Kabla Jacob hajatufikia, huwezi kuamini mama flani Aliyekuwa amekaa nyuma kabisa Alimuita na kusema.
"kama vile nawafahamu, embu leta nione tena"
Hapo ndipo tulipata kupumua, ndipo Jacob aliarudi nyuma fasta ikawa Pona Pona yetu, na muda Huo tulikuwa tumefika kwenye kituo hivyo tulitoka nje kama Wenda wazimu.
Baada ya muda tukiwa tupo njiani nilipata ujumbe nakuufungua.
Ilikuwa ni video hivyo niliifungua.
kumuona Mr Choi akiwa anapigwa na watu wasioonekana nyuso zao maana walikuwa wamezifunika ili wasitambulike, presha ilinipanda nikaendelea kuangalia huku nikiwa najiuliza Nani kanitumia video hiyo, na hapo hapo Mr Choi alipoteza maisha, kabla sijakaa sawa voice message iliingia nikaifungua Ilikuwa ni sauti ya Jacob mtu ambaye anatutafuta kwa udi na uvumba na muda mfupi Tulimuona ndani ya basi.
" mwisho kabisa nimewapata, kumbe Mpo hapa Seoul! OK! naomba pangeni siku tukutane kabla sijawatafuta Mimi maana nikiwatafuta ntawaua Kifo Kibaya nahisi mumemuona mwenzenu nilichomfanyia"
Nilishusha pumzi nikiwa nimefumba macho kwa hasira nyingi mno ndipo Salome aliniuliza huku akiwa ameanza kulia.
"tunafanyaje Madina?"
"tuondoke Seoul"
"tunaelekea wapi?"
"popote"
"kama wapi?"
"twende mkowani"
"kwa Nani?"
"nielewe Salome kwasasa hatuna chaguo"
Hapo hapo tulibeba mizigo yetu na kuanza mchaka mchaka.
Tulifanikiwa kupata basi, tulikata tickets tukapata siti nakuingia na safari ikaanza.
Tukiwa tupo njiani nilizidi kumpa moyo Salome asijali maana Yeye baada ya kuiona sura ya Jacob homa ilipanda, dalali wangu alinipigia kama Mara tano sikuweza kupokea ndipo akanitumia ujumbe akisema.
"Mpo wapi?"
Sikuweza kumjibu maana nguvu zilikuwa zimeniishia mwilini vile vile hata sauti ya kumjibu nilikuwa Sina.
Safari Ikiwa inaendelea tulishtushwa na mlio wa risasi Ukiongozana na damu mbichi iliyotumwagikia usoni kwa baadhi ya abilia ambayo tulikuwa tumekaa nyuma ya dereva. Maswali katika Vichwa vyetu yalikuwa mengi, ile Hali ya kuweweseka huku kila mmoja akiwa anahangaika Kutaka kujuwa nikipi kimetokea huwezi kuamini tulikuja kugundua dereva amepigwa risasi ya kwenye komwe na watu waliyo kwenye bodaboda wakiwa wamevalia koti nyeusi na wakiwa wamezuia nyuso zao zisionekane huku wakiwa wanatokea kwa mbele.
Kelele za watu wakiomba msaada zilikuwa zikisikika ndani ya basi hilo.
Dereva ile Hali ya kuona mawenge ndani ya macho yake aliisimamisha gari pembeni kisha akaulalia uskani na kukata moto hapo hapo.
Tukiwa tunaweweseka bila kujuwa hili wala lile Nilimkumbatia Salome nikizidi kumpa moyo asijali, Muda Huo Huo watu wale ambao idadi yao sikuweza kuitambua kwa haraka haraka walikuwa zaidi ya nane, moja kwa moja baadhi yao Waliingia ndani ya basi na wengine wakabaki nje wakiwa wanadumisha ulinzi zaidi.
Watu wote walilaliana ili kujikinga maana uoga na Hofu vilikuwa vimetutawala ndani ya Nyoyo zetu.
Sauti ya jambazi mmoja Aliyekuwa ameshikilia bastola mkononi ilisikika akisema.
"Nyote shukeni"
Kwa presha nyingi tulijikuta tukiangukiana Sisi kwa Sisi,
Ile Hali ya kufokewa tulijikuta tunapoteza hakili ghafla, kijana mmoja akiwa anatafuta njia ya kupita ili aweze kutoka nje, kwa bahati mbaya alimgonga baba huyo mwenye roho mbaya.
Huwezi kuamini kijana huyo alipigwa risasi bila huruma.
majambazi waliyoko nje walituelekeza wapi tukae huku wakizidi kutupa vitisho vingi.
Baada ya muda sote tulikuwa tumekaa Chini huku tukiwa tumeweka mikono juu.
Jambazi wote walisogea tuipo kisha mkuu wao akatoa amri sote tutoe simu zetu na atakaegundulika Amebaki na simu atauwawa.
Wote walitoa simu zao huku wakitetemeka mno Ila Mimi nilitulia na simu yangu nikiamini itakuwa Salama.
Salome baada ya kutoa simu yake aligeuka kunitazama ishara na Mimi ni toe yangu, ila moyo ulininsunta nikazidi kujiaminisha kuwa sintopata tatizo lolote.
Jambazi Watatu walikuwa wanatuzunguka zunguka ili kutuwekea ulinzi zaidi na wengine walikuwa wameifuata gari huku wakiwa wanapakuwa vitu ambavyo hatukuvigundua kwa muda huo.
Tukiwa tumetulia huku kila mmoja akiwa anaomba Dua kwa Muumba wake huwezi kuamini miongoni mwetu simu yake iliita tena kwa sauti ya Juu iliyotufanya sote Hofu izidi Mara Elfu moja maana tuliambiwa simu zote tukabidhi.
Sote tuligeuka kuangalia itakuwa ni simu ya Nani, aisee simu ile Ilikuwa ni ya bibi flani ambaye kwa Muda Huo alikuwa anatetemeka kwa uoga.
Baba mkatili ambaye ni mkuu wa kikosi hicho, alisogea tulipo na kuuliza.
"kuna nini?"
Hakuna aliyeweza kujibu bali sote tulielekeza macho chini, tatizo simu ya Yule bibi iliendelea kuita ndipo akamuuliza.
"una kichaa?"
Bibi wawatu masikini alimjibu huku akitetemeka mno.
"Nisamehe mjukuu wangu"
baba huyo alimtwanga risasi bila kufikiria huyu mtu nimempiga risasi je kuna kosa gani kalifanya mpaka nimuadhibu kiasi hiki, baada ya kumtwanga risasi alipiga hatua akisema.
"watu viherehere wanaojifanya kutokusikia siwaamini kabisa"
Muda Huo upande wa dalali wangu akiwa yupo na mwenzie alisema.
" namtumia ujumbe hajibu"
"Mpigie"
Ndipo Dalali alinipigia.
Upande wangu nikiwa nimesahau kuwa Nina simu baada ya kuona mauwaji ya bibi Yule, Huwezi kuamini simu yangu iliita tena kwa sauti ya Juu.
Moyo wangu ulishuka fasta nikawa kama sijitambui vile, huwezi kuamini miongoni mwahao jambazi mmoja wao aliwahi pochi yangu ndogo iliyokuwemo simu kisha akaichukuwa huku akatoa sim, muda Huo Huo mkuu wao alirudi kwa jazba nyingi akisema.
"Nani huyo mshenzi?"
Nilitetemeka mno huku nikiamini muda siyo mrefu naenda kuonana na vipenzi vyangu baba, mama, Munira, Abdallah Pamoja na teacher Jack.
Ndipo baba huyo alisogea karibu yangu na kuniuliza.
"ni wewe?"
Nilitikisa kichwa ishara siyo Mimi ndipo alimfuata kijana ambaye alichukuwa pochi yangu na kumuuliza.
" Nani alikuwa nayo?"
Kijana huyo hakumjibu kitu bali alimuacha na kuwafuata wenzie.
Ikawa PonaPona yangu, Walipomaliza kupakua kuna kikosi kingine cha majambazi kilitokea muda Huo Huo Wakaanza kushambuliana na risasi.
Sisi tulipokuwa tumekaa tulilala Chini kwa usalama zaidi.
Kikosi cha kwanza cha watu wale waliotuteka walipanda haraka bodaboda zao na safari ikaanza wakiwa na vile vifurushi vya vitu walivyovichukuwa.
Jambazi wale Waliendelea kukimbizana ikawa PonaPona yetu tukatoka hapo nduki.
Tukiwa tunakimbia barabarani tukirudi mjini Seoul gari za police zilifika zikatupatia msaada, miili ya wale waliopoteza maisha ikachukuliwa kisha tukarudi mjini.
Baada ya muda tukiwa tupo police station walianza kutuuliza maswali kuhusu kile kilichotokea, watu wote tuliokuwa nao hawakuweza kutoa taarifa yoyote kwasababu waliogopa.
Muda Huo alikuja mkaka mzuri (handsome boy) akajitambulisha kuwa Yeye ni proscuter Anaitwa Han jan.
Baada ya kujitambulisha alianza kutuuliza maswali Ila Hakuna aliemjibu.
Nilipoona watu wanaogopa kusema ukweli hali ya kuwa wapo wenzetu wameweza kupoteza maisha bila hatia Nilinyanyuka na kusema.
"ntasema kila kitu"
Wote waligeuka kunitazama mpaka proscuter Han mwenyewe, ndipo nikasema.
"kuna mizigo walikuwa wamekuja kuchukuwa"
"ilikuwaje?" Alinihoji.
Nilianza kumpa mkasa wote mpaka walivyokimbia.
Proscuter Han alinishika begani na kuniambia.
"Asante kwa maelezo yako tafadhali tupe Muda zaidi kuna interview itafanyika Naomba uwepo"
Ukweli kwa maovu niliofanyiwa nchini kwetu Kenya niliona lazma nishilikiane na serikali ya Korea mpaka jambazi wale wakamatwe ili marehemu wale wapumzike Salama.
Baada ya muda mimi na Salome tulikuwa tupo ndani ya gari ya proscuter Han huku tukielekea kwenye kitengo cha ma proscuter.
Tulipofika tuliingia ndani ya mjengo mrefu, Tulipofika juu tulipewa kiti tukakaa ili kusubiri Kidogo, tukiwa tumetulia kuna maproscuter wawili walisimama mbele yetu huku wakiwa wanajadiri Jambo flani huku mmoja akiwa ameshikilia picha mkononi, niliwapa masikio kwa umakini mmoja alisema.
"Hawa Mabinti wanaishi humu ndani ya Korea bila vitambulisho maalumu na inasadikika walikimbia nchini kwao Kenya baada ya kusababisha kesi ya mauwaji"
Mwenzie akamuuliza.
"kesi hii Sisi ndo tutaifuatilia?"
"Han nahisi inamuhusu hii"
Muda wote nilikuwa nimeanza kutetemeka, vijana wale bila kujuwa kuwa Sisi ndiyo wanatafuta walitupita na kuondoka zao na Mimi nilijuwa ni Sisi tu Hakuna wengine licha nilikuwa sijaona picha, ndipo nikamuambia salome.
"kimenuka tuondoke"
Salome akiwa haelewi chochote aliniuliza.
"kuna nini Kwani?"
Nilimshika mkono na kutokanaye nje baada ya kuona Hawezi kunielewa.
Tukiwa tupo mtaani Pamoja na mabegi yetu nilisema.
"wapo watu ambao tupo kwa hii dunia ili kukimbia Kimbia kila Mara"
"kunanini mbona sikuelewi?"
"nahisi Jacob ameenda kutoa taarifa kituoni kuwa Sisi tupo hapa Seoul kwasababu tumekimbia kesi ya mauwaji, pia hatuna passport"
"si tuna passport kwani. tutajieleza ilimladi serikali yetu Inajuwa yote"
Tukiwa tunazidi kusonga mbele nilishtuka na kusimama, ndipo Salome akageuka kunitazama na kuniuliza.
" kuna nini?"
"kwenye ile pochi Ndo kulikuwemo passport zetu"
"Weeeeeee"
"Oooh my God yule jambazi aliondoka nayo, tunafanyaje sasa?"
"hakika bora nife tu maana nimechoka haya majanga ya kila Mara, na yote haya umeyataka mwenyewe maana Haiwezekani watuambie tutoe simu zetu wewe uweke jeuri. kwanza nikuulize.... kwenye ile simu kuna kitu chako cha thamani?"
"hata sijui ila ndani ya simu ile mna picha za ndugu zangu na ni Kumbukumbu ya pekee niliyobaki nayo"
"haya! Tunaelekea wapi? Ndo hivyo passport hatuna na tumepewa kesi ya mauwaji"
Sikuweza kumjibu chochote Niliendelea na safari taratibu.
Tukiwa tupo njiani tulikumbana na dalali wangu akiwa anaendesha beskeli yake ndogo, alipotuona Alitufuata huku akisema kikwao.
"mnazingua Ndo nini sasa"
Salome kwa sauti ya Chini akaniuliza.
" Nani Huyu?"
"dalali"
Dalali alipofika alisimamisha beskeli yake mbele yetu na kuniuliza.
"Mbona unazingua Sana Madina?"
Nilijilazimisha kutabasamu kisha nikamjibu kwa sauti ya unyonge.
"I'm sorry kwani chumba tunaweza kupata kwasasa?"
" Ninyi sasa"
Tuliongozana huko alikotuelekeza, Tulipofika kwenye mtaa huo, watu walikuwa wachache mno licha maisha yalikuwa ya Kawaida ndipo Nikamuuliza dalali.
"Mbona watu Hamna hapa?"
Dalali alitabasamu na kuniuliza.
" unatafuta chumba au watu?"
Nilimpiga kijikofi cha Utani kisha tukaingia ndani ya nyumba hiyo, Tulipofika ndani mwenye nyumba alianza kutuzungusha ndani ya vyumba tofauti ili kutuonyesha Mazingira, Ila kilichotushangaza na ukubwa wote wa nyumba wapangaji walikuwa Hamna Kiufupi gorofa ya floo nne yote Ilikuwa Haina watu tena Ilikuwa ni nyumba nzuri ya gharama kikawaida Korea chumba dala Mia tatu kuendelea Ila Yeye akatuambia dala Mia moja tu.
Kama Kawaida yangu nikiwa sielewi kitu lazma Niulize, nilimsimamisha mwenye nyumba nikataka kumuuliza ila dalali aliniwahi na kuniziba mdomo.
Sikuongea tena Tuliendelea kuelekezwa.
Tulipofika juu gorofa ya tatu nilimuomba tukaangaliana Juu zaidi ila aliniambia.
"juu Hapana kwasababu kule wapo watu wanaishi"
Aliposema hivyo, moyo wangu Kidogo ulitulia nikamtazama Salome Na kumpa tano.
Tuliandikiana mkataba baada ya muda tukabaki wawili Mimi na Salome huku tukiwa tunafanya usafi gorofa ya pili maana tuliambiwa ya tatu na ya nne Hapana licha ya tatu Ilikuwa Haina mtu.
Tukiwa tunazidi kufanya usafi kwenye ngazi, tuliona wanaume wa tatu wakiwa wamevaa koti nyeusi, mikononi gloves nyeusi vile vile na kofia nyeusi.
Tuliacha kile tulichokuwa tunafanya tukawashangaa maana walikuwa wanaelekea tulipo.
Kijana wa Katikati sura yake haikuweza kuonekana maana alikuwa amefunika uso wake, wenzie wawili sura zao zilikuwa zinatisha mno ukija kuangalia walikuwa wamechora tattoo mpaka kwenye komwe.
Walipotufikia tulisogea pembeni wakatupita bila kuongea chochote.
Baada ya kuwaona moyo wangu ulilaluka nikataka kujuwa kina nani Hawa wanaingia kwenye nyumba ya watu bila kuongea, taratibu nikageuka kuwaangalia wanavyotembea. aisee kijana wa katikati alikuwa ametapakaa damu mgongoni kama vile katoka machinjioni, nilipomuangalia vizuri mgongoni nilishtuka mno Baada ya kuona koti aliyovaa inanembo kama ya yule jambazi aliyeninyang'anya pochi yangu baada ya simu kulia.
Makaka hao wakaelekea gorofa ya tatu, Mimi na Salome tulitaka kujuwa wanaelekea wapi hivyo tukaanza kuwafuata nyuma, Tulipofika juu kabisa tuliwaona wanaingia kwenye chumba kilichopo gorofa ya nne, hapo nikapata picha.

No comments