Simulizi: Tabasamu langu sehemu ya sita (06)
SIMULIZI ZA MAPENZI
Baada ya muda tulikuwa zetu chumbani huku Salome akiwa anapanga nguo vizuri.
"Jacob Ndo kaenda kutushtaki? kwanza wale watu umewatambua?" Aliniambia
"Eee ni wale jambazi waliyotuteka"
"tunafanyaje?"
"hata sijui"
Muda Huo Huo dalali alifika nakubisha hodi kwenye chumba chetu, nilimfungulia mlango akaingia na kuniuliza.
"ninyi ni watu wa wapi?"
"una maana gani?"
"Mpo hatarini, muda wowote mnapelekwa jela na nimesikia proscuter Han anataka aje kuwakamateni"
Nilishtuka mno kwa sauti ya Chini nikamuambia.
"tunashukuru"
Baada ya muda dalali akiwa ameondoka, Tulianza kuchungulia kule gorofa ya nne kama watakuwa wameondoka. ndipo Salome akaniuliza.
" hivi una Hisi unaweza kuingia?"
"kama hatujafanya hivyo sichochote kwasababu muda wowote tunaenda jela afadhali nikatafute Labda naweza kuona"
"Achana na hiyo pochi, huwezi kuipata"
"kwahiyo twende jela?"
"jela tena! Nenda basi"
Baada ya muda vijana wale walitoka nje na kuondoka, nilipoona wametoka tu sikuweza kupoteza muda niliingia moja kwa moja ndani ya chumba kile.
Salome alipoona Nimeingia alirudi nyuma kwa uoga.
Nikiwa nipo ndani ya chumba cha majambazi, niliona picha za sura tofauti ukutani Ila sikuweza kuelewa, bila kupoteza muda nikaanza kutafuta kipochi changu kama ntakiona, nilipekua kila kona lakini sikuweza kupata, ile Hali ya kutafuta kwa harakaharaka Jasho Ilikuwa imenifumuka mwili mzima, mwishowe Nilikata tamaa nikahisi Labda alikitupa baada ya kuona kilikuwa hakina vitu vya thamani, moyo ulinisukuma nikaangalia kwenye dro iliyokuwa wazi kwa muda ule, taratibu nikasogea na kuvuta, aisee nilishangaa kuona kipochi changu kikiwa kipo mule, nilifurahi mno nikakibusu kwa furaha kisha nikageuka ili kuweza kuondoka, mbele yangu nilikutana na mdomo wa bastola, presha ikapanda nilipomuangalia alieishikilia nilichoka maana alikuwa ni Yule jambazi alieninyankua kipochi changu na muda Huo alikuwa ameficha uso wake kama kawaida yake.
Kutokana na uoga mwingi nilianza kulia huku nikimuelezea magumu niliyopitia nyumbani, Ila hakutaka kunisikiliza bali aliniuliza.
"kwanini ulienda kutoa taarifa kwa ma proscuter?"
"na! Na! Na! Na....." hakika nilikosa cha kujitetea.
Nikiwa naendelea kuongea maneno yasiyoeleweka, huwezi kuamini mkaka huyo alinitwanga risasi ya begani ikanipelekea kukosa nguvu na hapo hapo kudondoka Chini.
Jambazi huyo bila huruma alitoka zake nje na kuniacha pale nikiwa na hangaika.
Mdogo mdogo nilianza kujivuta ili basi ikiwezekana nimfikishie Salome.
Salome akiwa anachungulia chungulia kwa uoga alikuwa anasema mwenyewe.
" jamani Mbona umekawa proscuter Han yupo nje amekuja kutukamata Fanya haraka"
Muda Huo Huo nilitokea nikiwa nipo hoi bini taabani, Salome baada ya kuniona kwanza hakuamini, bila kupoteza muda aliniwahi na kunishika huku akiwa ananiuliza Hali yangu.
Nguvu zilizidi kuniishia nikazimia bila kuongea chochote.
Muda Huo proscuter Han aliingia akiongozana na wenzie, walipotuona walitunyooshea bastola ndipo Han akasema.
"kwasasa Mpo Chini ya ulinzi"
"dada yangu anakufa jamani" aliongea salome kwa kulalamika.
Baada ya kugundua nimepigwa risasi, waliniwahi moja kwa moja na kunipeleka hospital.
Siku hiyo Salome alikamatwa akapelekwa sero kwa upelelezi zaidi.
Baada ya Siku nne kupita, nilizinduka Nakujikuta nikoo mwenyewe hospitalini, nesi muda Huo aliingia na kuniambia.
"Hongera kwasasa Upo Salama"
"kuna nini kinaendelea?" Nilimhoji kinyonge
*usijali pia usitumie Muda mwingi kufikiria"
Nilikubali na muda Huo proscuter Han alifika, nilipomuona nilikumbuka kila kitu Ndo nikajuwa Kumbe Nipo hapa kwasababu Nilipigwa risasi.
Proscuter Han alimuomba nesi ampe muda ili aweze kuniuliza maswali kadhaa Ila nesi alimjibu.
"kwasasa hali yake siyo nzuri hauwezi kumuuliza maswali yoyote utakuwa unahitaji kumfanya apoteze Kumbukumbu"
Ndipo Proscuter Han alinitakia siku njema kisha akaondoka.
Baada ya siku tano kupita Kidogo Hali yangu ilikuwa imeanza kuwa vizuri maana nilikuwa na uwezo wa kuzunguka zunguka maeneo ya pale, nikiwa nipo chumbani huku nikiwa najiuliza kwa nini mtu wangu wa karibu Salome haji kuniona au Jacob atakuwa amemfanyia Kibaya? Muda Huo aliingia Han akisema.
"Upo Salama kwasasa"
Nilipomuona nilishtuka nikajuwa hapa naenda jela Hamna mjadala.
Han aliponifikia alitabasamu na kuniambia.
"tutoke tukazunguke zunguke kwanza"
Nilikataa kwa kutikisa kichwa na kumfanya aniwekee mashaka zaidi.
"Unaogopa?"
"mdogo wangu Salome yupo wapi?"
"yuko sero tunasubiri wewe upone uje utoe maelezo zaidi"
"Hana hatia lakini"
"nikweli lakini ungekubali tukatoka nje dakika mbili"
"na Mimi unataka unipeleke sero?"
"Hapana"
Baada ya muda tulikuwa tupo nje tumekaa kwenye kiti huku Han akiwa anaendelea kuniuliza maswali mengi kuhusu Sisi.
"unaweza kunipa Hadithi ya maisha yako hata kwa ufupi?"
Nilianza kumsimulia nilivyowapoteza wazazi wangu Pamoja na wadogo zangu mpaka kufikia muda huo tunavyohangaika.
Hadithi ya maisha yangu ilimsikitisha mno na kunishika begani huku akinipoza maana nilianza kulia.
"Nipo Chini ya miguu yako, ukweli mtu niliyebaki naye hapa duniani, ni huyo Salome mliemfunga, maisha yangu kwasasa yamefika ukingoni, please proscuter Han.... muachieni huyo binti aishi maisha huru Mimi nipelekeni jela" niliongea kwa huzuni.
"pole Sana, na aliyeleta kesi hajajitokeza mpaka sasa, by the way aliyekupiga risasi ni nani?"
Moyo ulishtuka nikasita kumtaja maana muonekano wake alikuwa Hana huruma kabisa.
"Usiogope ongea Nani huyo alikupiga risasi?"
Kusema Ukweli Mimi Madina kuficha ukweli hali ya kuwa naujua nikitu ambacho hakiwezekaniki hivyo nilimwambia.
"pale gorofa ya nne wapo majambazi wanaishi"
Han alishtuka na kuniuliza.
"una uhakika"
" majambazi hao ni wale waliotuteka siku ileeee"
"Kwahiyo wanaishi pale?"
"ndiyo, mmoja wao alinipiga risasi baada ya Mimi kuingia chumbani kwao"
"ulienda kufanya nini?"
"kutafuta pochi yangu kwasababu siku wanatuteka jambazi mmoja alininyang'anya pochi na humo ndiko kulikuwa passport zetu"
"nimeelewa"
Proscuter Han alinishika begani na kuniambia huku akiwa ananitazama machoni.
"pole Sana yataisha na kuhusu mdogo wako naenda kumtoa sero"
Ukweli Korea walijaaliwa wanaume wenye sura nzuri mno.
"vipi kuhusu Sisi tutaendelea kuishi pale?"
"mnahitaji kuhama?"
"tusaidie tu, kwasasa hatuna chochote tutaandikiana mkataba ntakulipa taratibu taratibu"
"Haina shida ntawasaidia"
Siku iliyofuata, Salome aliachiwa nami nikaruhusiwa kurudi nyumbani.
Tulipofika nyumbani tulisika kuingia kutokana na hofu.
"tuishie hapa kabisa?" Salome alinihoji.
"tunaishi na minyama siyo watu hawa"
"kwahiyo tunafanyaje?"
"proscuter Han Amesema atatusaidia tuhame"
"afadhali"
Siku iliyofuata Majira ya usiku nilikuwa nimetoka Kidogo kwa ajili ya kutafuta chochote cha kula usiku huo, nikiwa natembea tembea zangu, simu iliita ndipo nilipokea na kuuliza.
"Nani mwenzangu?"
Ndipo Sauti ya kiume ilisikika akisema.
" unaongea na Jacob"
Nilishtuka mno mpaka kumjibu nikashindwa.
"nimefurahi Sana kukutana na wewe maeneo hayahaya, Halafu Siku hizi naona mmenisahau Nyie Watoto"
Jasho ilianza kunifumuka mwili mzima nikaanza kuangazaangaza kona zote maana aliniambia amefurahi kukutana na Mimi eneo hilo nikihisi Labda atakuwa maeneo hayo.
Ile kuangalia angalia, niligeuka nyuma nikamuona mwanaume akiwa amesimama huku akinitazama Ila sikuweza kumtambua kutokana na giza kuwepo maeneo Yale, huwezi kuamini mtu huyo alinipungia mkono ndo nikajua ni Jacob.
Jacob alipoona nimemtambua aliachia kicheko kikali, sikutaka yawe marefu nilianza kukimbia ili kama ataniua aniuwie mbele ya watu, nikiwa nakimbia kwa kasi ya kufa mtu, nyuma yangu Jacob naye alianza kunifukuzia.
Tulikimbia makilometa ya kutosha Ila huwezi kuamini watu hawakujali walihisi Sisi ni wapenzi bila kujua mwenzao naenda kuuliwa.
Nilikimbia mpaka nikahisi pumzi inaenda kukata, moja kwa moja nilitokezea sehemu ambayo watu wanasubiligi daladala yaani kituo cha usafiri, nilipofika niliwakuta watu wengi wakiwa wamesimama, moja kwa moja nikajichanganya nao, Jacob alivyokichaa hakukoma kunifuatilia aliingia naye katikati ya watu na kuanza kunitafuta, nilipokuwa nimejificha karibu na mzee flani alishuka Chini na kukaa akidai amechoka ikapelekea Mimi kuonekana Ila Jacob hakuweza kuniona kwa muda ule, haraka nilimfuata mkaka flani ambaye nilikuwa simtambui nikasimama nyuma yake nakumshika koti aliyokuwa amevaa.
"tafadhali oppa wanataka kuniua nisaidie unifiche mwenzio ntauwawa" nilimwambia kwa hofu.
Mkaka huyo aliendelea kusimama bila kugeuka kunitazama wala kuniuliza kuna nini, na Mimi nilipoona amekaushia nikafurahi nakuendelea kujificha, muda Huo Jacob alifika maeneo hayo na kumuuliza kijana huyo.
*mke wangu ameingia hapa je umemuona? Ni binti mweusi kama mimi yaana siyo mkorea, je umemuona?"
Mkaka huyo alibaki kimya licha Jacob alimuuliza kwa kikorea.
Baada ya muda Jacob sikuweza kumuona tena na muda Huo usafiri ulifika watu Wakaanza kupanda, nilijitokeza nakusimama pembeni ya mkaka huyo.
"Asante Sana kwa msaada wako"
Kilichonishangaza ni kwamba, hata kunipa muda wa kuniangalia hakuweza kuniangalia, nikamtazama kwa mshangao maana alikuwa amevaa kofia nyeusi na kuishusha usoni. Nilimkagua kwa muonekano wake alikuwa ni more handsome.
Ndipo Mkaka huyo alivuta barakoa inayoziba mdomo na pua kisha akavaa na kunipita kuifuata basi, nilijiuliza maswala mengi kuhusu kijana huyo ila sikupata jibu, niliamini ndiyo tabia za vijana wakorea yaani wanazarau, taratibu nikageuza kumuangalia mgongoni aisee nembo ya koti ya yule jambazi aliyenitwanga risasi ilikuwa kwenye koti aloivaa kijana huyo, hapo ndipo nikajuwa kumbe muda wote nachezea mgongo wa mambo baada ya kukoswa na simba.
Niliona poletea Kote hata nikisusa kuingia kwenye usafiri halafu Jacob akanikuta hapo ntakuwa nimeokoa nini, moja kwa moja nikaingia kwenye usafiri.
Tukiwa tupo njiani macho yangu yote yalikuwa kwa huyo kijana, hofu yangu huwenda amenikumbuka. Tulifika kwenye kituo maalum na wa kwanza kushuka alikuwa mimi.
Baada ya muda nikiwa nipo chumbani nilimuambia Salome.
"Kumbe wapo majambazi wenye sura nzuri"
"kama nani?"
"nimemuona huyu mkaka anaeishi gorofa ya nne aisee ni more handsome"
"Weeeeee"
"Ila shetani ni shetani tu"
"Mbona hujaniambia kuhusu Hali yako maana ulivyorudi ulikuwa tofauti Sana"
"Hamna kitu Mbona"
Niliamuwa kumficha maana nilijuwa nikimuambia kuwa nimemuona Jacob sijui Angelala vipi.
"proscuter Han atakuja kutuchukuwa saa ngapi?"
"unahisi utaishi kwake?"
"Naelewa atatukodishia, vipi atakuja lini?"
"Sijajua pia kesho nahitajika kwenda hospitalini"
"kufanya nini?"
"kuomba kazi"
"Halafu sijui kwanini Pack Jin hatutafuti au ameanza kunisahau"
"kwanza nikuulize, wewe na Pack Jin mlikubaliana kuwa namahusiano au wewe ndo Unampenda?"
"Nampenda Mimi"
"kamuambie ukweli basi"
"I'm African women"
Nilicheka kwa furaha kisha nikalala maana nilikuwa nimeanza kujisikia vibaya.
Asubuhi ya siku nyingine niliamka mapema na kuelekea hospitalini kwa ajili ya kuomba kazi. nilipofika nilionana na mkuu wa pale akaniambia ili kupewa kazi lazma nirudi chuo licha nimesoma Kenya miaka kadhaa niliambiwa mpaka nisome chuo cha korea.
Baada ya muda nilitoka nikiwa nimenyong'onyea, nilipofika mbele ya mlango Kumbe muda wote proscuter Han alikuwa amenisubiri nje, nilipomuona nilimfuata nakumsalimia.
"unaumwa Mbona upo hapa?" Nilimhoji.
"no! nimekufuata wewe"
"Oohh.... Nipo hapa kwa ajili ya kuomba kazi"
"umepata?"
"Hapana"
"pole Sana but tuingie ndani ya gari kuna kitu nahitaji kukuuliza"
Tuliingia ndani ya gari yake kisha tukatoka maeneo Yale akaenda kupaki sehemu yenye ukimya.
Tukiwa tumetulia Proscuter Han alitoa picha flani akanionesha, nilipoangalia nilimuuliza.
" Nini hii?"
"haya ni mabox ambayo yalikuwa na madawa ya kulevya siku ile mnavamiwa walikuwa wameyafuata"
"Ndio maana! sasa yalikuwa ni yao?"
"yalikuwa ni ya kile kikosi cha majambazi kilichokuja kuwafukuzia wale jambazi waliokuwa wamewateka"
"inaonekana na wao walitaka kuyavusha?"
"yeah! sasa hiki kikosi cha nyuki...."
"nyuki?" Nilimkatisha.
"wanajiita nyuki"
"Ndo Hawa tunaoishi nao?"
"kwanza Naomba tufanye dili, wewe nahitaji uwe mpelelezi wangu ujuwe wapi kesho wataenda kufanya tukio maana kila siku kama ya kesho lazma wafanye tukio"
"Mmmmmh! ntaweza kweli na ninavyowaogopa?"
"jipe moyo utaweza Kikubwa nikujiamini, please Nifanyie upelelezi"
"sawa ila siku ile ningekufa kisa kuongea ukweli"
"nipo bega kwa bega na wewe, hii ndio namba yangu ukinihitaji ntaruka fasta. ukweli Hawa majambazi ni hatari Sana hawajali kitu chochote"
"Ndo maana walimuua bibi asiyekuwa na hatia maskini"
"please nisaidie"
"usijali ntajitahidi"
Siku iliyofuata Majira ya saa sita Mchana nilikuwa nje ya mjengo wetu huku nikifanya usafi, nikiwa naendelea kufanya usafi nilisikia mtu akiongea na simu, taratibu nilisogea alipo kisha nikabana karibu ya ukuta nakuanza kumsikiliza kwa makini na alikuwa ni miongoni mwamajambazi wale.
" Eee!!...... Ndiyo!.......Hapana, Leo itafanyika kwenye ile kampuni ya ujenzi. Ndiyo...Sawa sawa"
Baada ya kuongea aliingia ndani nikachomoa simu moja kwa moja nikamtumia ujumbe proscuter Han.
Majira ya usiku kilichotokea sikuweza kufahamu, Ila proscuter Han aliniahidi asubuhi atakuja kutuchukuwa kilichopo tufungashe mizigo yetu.
Tukiwa tumemaliza kufungasha mizigo yetu, Salome aliniuliza.
"haiwezi kuwa tatizo kwa Han?"
"una hofia atakuwa ameauwawa?"
"Eee maana kama vile tumewachonganisha"
Tukiwa tunazidi kujadili mlango uligongwa, Nyoyo zikatuchomoka tukasikilizia kwa makini.
Mtu yule aliendelea kugonga kwa fujo mpaka wenyewe tukashindwa kuelewa ni Nani na anatafuta nini.
Salome kwa sauti ya Chini akaniuliza.
"ni nani?"
"sijui"
"siyo Jacob?"
"atakuwa amejuaje tunapoishi"
"kafungue basi Labda ni dalali wako"
BONYEZA HAPA KUPATA SMS NZURI ZA MAPENZI
ITAENDELEA

No comments