Chombezo: Dunga dunga sehemu ya nane (08)
Kila siku Christina alitamani sana mazoea na mimi kama ambavyo alivyokuwa nayo kwa wavulana wengine. Nilikuwa nikimkwepa, sikutaka kumpa hata dakika tano za kukaa nami. Nilikuwa nikijipa ubize mkubwa kila nilipokuwa nikikaa nae.
Akili yangu kwa wakat huo ilikuwa imezama sana kwa Nilfat. Kiukweli sikutaka kumuacha msichana huyu, akili yangu ilikuwa ikiniambia kwamba Nilfat alikuwa na bikira asilimia mia moja. Kila siku nilikuwa nikimpigia simu na kujifanya mtu mkarimu sana kwake.
Nilfat akaonekana kuanza kuvutiwa nami japokuwa mara kwa mara alikuwa akiogpa kuja kunitembelea nymbani. Wala sikujali sana kwamni moyo wangu ulikwishajua kwamba Nilfat aligundua ni kitu gani kingetokea kama tu angediriki kuja nyumbani.
Nikaamua kuwa mvumilivu. Mwezi mmoja ulipita huku katika siku zote za mwezi huo nikiwa nikimpigia simu Nilfat. Christina nae alikuwa akija kwa moto wa kasi kiasi ambacho akaanza mazoea na wanawake ambao walikuwa wakikaa katika nyumba ile niliyokuwa nimepanga huku lengo lake ikiwa ni kunipata kwa karibu zaidi.
Judith na wasichana wengine hawakuwa akilini mwangu tena, na hii ilitokana na kukikosa kile ambacho nilikuwa nikikitaka kutoka kwao. Nilipataka pale kwa Nilfat kwani niliamini kwa jinsi alivyokuwa basi ingekuwa ni rahisi sana kuikuta bikira ambayo ilikuwa ikinisumbua sana maishani mwangu.
“Unanipenda?” Nilfat aliniuliza kwa lafudhi ya kiarabu simuni.
“Mbona umeshtuka sana?” Nami nilimuuliza.
“Hapana. Sijashtuka”
“Au kuna watu maalumu wa kukuambia neno hili?”
“Hapana”
“Basi ndio hivyo Nilfat. Umetokea kuuteka moyo wangu vilivyo” Nilimwambia.
“Hapana. Haiwezekani kutokea kitu kama hicho kwa muda mchache namna hii. Unanidanganya” Aliniambia.
“Kwa nini isiwezekane? Mwezi mmoja ni muda mchache kwa mimi kukupenda kwa mapenzi ya dhati?”
“Ndio. Ni muda mchache sana. Mapenzi uhitaji muda mrefu”
“Usijidanganye. Umekwishaiona muvi ya Titanic?” Nilimuuliza.
“Ndio. Huwa ninapenda kuiangalia mara kwa mara” Alinijibu.
“Mpaka meli inazama ilikuwa ni siku ya ngapi?”
“Siku ya pili au ya tatu nafikiri”
“Unajua kwamba Jack na Rose walipendana sana?”
“Hilo ninalifahamu, ningependa nami nipende na kupendwa kama vile”
“Sawa. Hebu jifikirie. Ndani ya siku tatu ambazo ni chache sana walipenda namna ile, unafikiri itakuwa ngumu kwangu kukupenda kama vile au zaidi ya vile ndani ya siku thelathini?” Nilimuuliza, alibaki kimya kwa muda.
“Siku thelathini ni nyingi mno Nilfat. Naomba uamini kwamba ninakupenda sana”
“Sitakiwi kufanya uamuzi wa haraka juu ya mahusiano. Ningependa unipe siku kadhaa” Aliniambia.
“Mpaka lini?”
“Labda keshokutwa”
“Mhh! Sawa”
“Mbona umeguna?”
“Siku nyingi sana. Ila haina budi kusubiri”
“Usijali. Mvumilivu hula mbivu” Aliniambia.
“Nafahamu. Hata ngoja ngoja nayo huumiza matumbo” Nilimwambia methali ambayo ilimfanya kutoa icheko cha chini.
“Sawa. Tutawasilina”
“Usijali” Nilimwambia na kukata simu.
Nikashusha pumzi ndefu kama mtu aliyekimbia umbali mrefu.
ITAENDELEA

No comments