Chombezo; Dunga dunga sehemu ya saba (07)
Nani? Mimi?” Aliniuliza japokuwa alijua fika kwamba nilikuwa naongea na yeye.
“Ndio. Unaonekana kama una wasiwasi. Tatizo nini?”
“Hapana. Mambo ya kawaida tu kaka yangu” Aliniambia huku kwa mbalia akiliachia tabasamu ambalo lilionekana kunichanganya.
“Mambo ya kawaida ambayo siruhusiwi hata kuyafahamu?”
“Ndio. Yangu binafsi”
“Sawa. Ila nafikiri hata kama ni yako binafsi ninaweza kukusaidia pia”
“Kunisaidia?”
“Ndio” “Kivipi?”
“Mmmmmhhh! Hapana kaka yangu, we acha tu” Aliniambia.
Hapo ndipo uipokuwa mwanzo wangu kuanza kuongea na yeye. Sikutaka kumuachia nafasi ya kupumua kwani nilikuwa na uzoefu mkubwa wa kutambua udhaifu wa wasichana wa kiarabu. Kila nilipotoa neno hili, niliingiza lile kiasi ambacho akaanza kuvutiwa nami kimaongezi.
Muda wote huo nilikuwa nikisali kimoyo moyo. Nilitamani sana nikute foleni maeneo ya Jangwani ili nipate muda mwingi wa kuongea na mtoto yule ambaye alionekana kuniteka ghafla sana. Sijui kama Mungu alikisikia kilio changu au la kwani tulipofika maeneo ya Fire, magari yakazuiliwa kwa kuwa msafara wa magari ya Waziri mkuu uikuwa ukipita katika barabara hiyo.
“Nimefurahi sana kuongea nawe mchana wa leo” Nilimwambia.
“Hata mimi”
“Ila samahani kama nitakuwa nimevuka mipaka. Hivi unaitwa nani rafiki yangu?” Nilimuuliza huku lengo langu likiwa ni kumuomba namba ya simu tu.
“Nani? Mimi?” Aliniuliza.
“Najua kwa kuuliza hivyo tu unataka kunipa jina la uongo. Sawa, nipe hata hilo la uongo, nadhani nitafurahi tu” Nilimwambia maneno ambayo yalimfanya kuanza kucheka kwa kicheko cha chini.
“Hakuna. Siwezi kukudanganya. Mimi naitwa Nilifat” Aliniambia.
“Nashukuru. Kuna umuhimu wa kukuambia jina langu?” Nilimuuliza.
“Utakavyoamua” “Sawa. Mimi naitwa Gideon”
“Nashukuru kwa kukufahamu”
“Usijali. Ila mimi nashukuru kwa kufahamiana” Nilimwambia.
Mara baada ya msafara ule kuruhusiwa baada ya dakika kadhaa, tuliendelea na safari yetu kama kawaida. Bado nilikuwa nikiendelea kuongea nae. Tulionekana kuwa marafiki wa muda mrefu sana hata zaidi ya watu waliokuwa wametoka safari pamoja.
Ingawa safari yangu ilikuwa ikiishia Manzese lakini nikaamua kuendelea na safari mpaka pale ambapo Nusrat angeishia. Kama kawaida ya wanaume, mimi ndiye nilikuwa mlipaji nauli na hata mnunuaji maji ya baridi njiani.
“Unaishi wapi Nusrat?”
“Sinza Legho”
“Sawa. Nafikiri haitokuwa na tatizo kama tukiendelea kuwasiliana baada ya hapa” Nilimwambia kauli ambayo kwa kiasi fulani alionekana kushtuka.
“Unamaanisha nini?”
“Namba ya simu. Au kuna ubaya wowote ule?”
“Hapana”
Alichokifanya ni kunipa simu yake na kisha kuandika namba yangu ya simu. Hakutaka kunipa namba yake ya simu kwa kuniambia kwamba angeweza kunipigia siku ambayo angehitajika kufanya hivyo, wala sikujali na wala sikuwa na wasiwasi.
Alipofika Shekilango, akateremka na mimi kuelekea mpaka Ubungo ambako nikachukua daladala ya Posta na kuanza kurudi Manzese ambapo ndipo nilipokuwa nikielekea.
Akili yangu ilikuwa imekwishatekwa na wasichana. Kila wakati nilipokuwa nikikaa chini na kutulia, nilikuwa nikifikiria wasichana tu. Nilitamani mapenzi kuliko kitu chochote kile, ilikuwa ni bora uninyime chakula lakini si kuninyima mapenzi.
Jina la msichana wa kiarabu, Nilfat ndilo ambalo lilikuwa kichwani mwangu kwa wakati huo. Sikuwa na shaka nae, alionekana kuwa msichana mdogo ambaye moja kwa moja niliamini kwamba alikuwa bikira. Sikuwa nikifikiria kama Nilfat alikuwa ameucheza mchezo huo kabla au la.
Siku nzima toka niachane nae pale Sinza, masikio yangu na macho yangu yalikuwa katika simu yangu ya mkononi. Nilikuwa na uhakika kwa ucheshi ambao nilimuonyeshea ndani ya gari basi ilikuwa ni lazima anitafute kwa kutaka kunijulia hali na hapo ndipo ambapo ningeipata namba yake ya simu.
Ni kweli kwamba nilitembea na wasichana wengi lakini kwa Nilfat hali ilionekana kuwa tofauti sana. Muda ulikuwa ukizid kwenda mbele huku moyo wangu ukiwa na hamu kubwa sana ya kutaka kupokea simu kutoka kwa Nilfat. Dakika zilikatika na hatimae usiku kuingia, hakukuwa na simu yoyote iliyoingia zaidi ya rafiki yangu Ezekiel ambaye nilimuelezea kila kitu kuhusu Nilfat.
Kwa kuwa asubuhi sikuwa nikielekea kazini kutokana na kuwa likizoni, nikaamua kukaa tu nyumbani.Kichwa changu wala hakikumfikiria Judith tena, baada ya kuona kwamba mahali pale palikuwa patupu, nikaamua kuachana nae japokuwa niliamini kwamba kuna siku moja angenitafuta.
Nakumbuka ilikuwa saa nane mchana, muda ambao nilikuwa nimetoka kula chakula katika kibanda kimoja cha mama ntilie. Nikaanza kuisikia simu yangu ikianza kuita. Kwa haraka haraka nikaichukua na kuyapeleka macho yangu katika kioo cha simu ile.
Namba ilikuwa ngeni.
Kwa kasi ya ajabu nikaipokea na kuipeleka sikioni. Mapigo yangu ya moyo yakaanza kwenda kasi mara baada ya kuisikia sauti nyembamba na nzuri iliyokuwa na lafudhi ya kiarabu ikinisalimia. Nilijihisi kuchangamka, sikutaka kuitikia kwa haraka kwani bado masikio yangu yalikuwa kama yamepigwa ganzi kwa muda.
“Hallooo....!” Sauti ile iliita mara baada ya kuona niko kimya.
“Hallooo!” Nilishtuka.
“Mambo vipi Nilfat!” Nilimsalimia.
“Nzuri. Umejuaje kama ni mimi?” Aliniuliza.
“Sauti tu”
“Ikoje?”
“Nzuri, inavutia halafu....”
“Halafu nini?”
Imependeza masikioni mwangu. Yaani kama jinsi ulivyopendeza jana” Nilimwambia maneno ambayo yalimfanya kuanza kutoa kicheko cha chini.
“Uko wapi kwa sasa?” Nilimuuliza.
“Nipo shuleni”
“Wapi?”
“Nur”
“Mhh! Iko wapi hiyo?”
“Magomeni”
“Kumbe hii ya hapa nyuma yetu?” Nilimuuliza huku nikionekana dhahiri kushtuka.
“Kwani wewe unaishi Magomeni?” Aliniuliza.
“Ndio. Si mbali sana kutoka hapo shuleni kwenu” Nilimwambia.
“Ok! Hiyo ndio namba yangu” Aliniambia.
“Nashukuru kuipata. Ungependa niisevu vipi?” Nilimuuliza.
“Jina langu. Au umelisahau?”
“Nalikumbuka lakini naona kama haitokuwa mzuka” Nilimwambia.
“Sasa wewe ulitaka kusevu vipi?”
“The future”
“Aahhahaha...unanichekesha”
“Naomba uniruhusu nilisevu jina hilo kwa ajili yako”
“Usijali. Vyovyote unavyopenda” Aliniambia na mara ghafla simu kukatika.
Hadi hapo tu nikawa na uhakika kwamba kila kitu ningekikamilisha kwa muda mchache ujao. Kitendo cha Nilfat kunigawia namba yake ya simu lilikuwa kosa kubwa sana, yaani ni kama kuurudisha mpira golini kwako huku ukijua kwamba hakukuwa na golikipa.
Nikalisevu jina lile lie huku akilini mwangu nikilisevu kwa jina jingine la tofauti sana, jina ambalo lilikuwa likinipa faraja kubwa sana. Nafikiri jina hilo litakufanya kushangaa lakini ndivyo akili yangu ilivyoamua kulisevu. Nilifurahi sana kila nilipokuwa nikilisevu jina hilo akilini mwangu, unajua jina gani? Ahahahaha....BIKIRA
Kila msichana mtaani kwetu alikuwa akinifagilia. Hawakuwa wakinifagilia kwa sababu ya kubadilisha wasichana tu, bali walikuwa wakinifagilia kutokana na sifa mbalimbali ambazo walikuwa wakinipa wasichana wote ambao nililala nao kitanda kimoja.
Kazi yangu ilikuwa kubwa kitandani, niliwaridhisha wanawake wote ambao nililala nao kiasi ambacho kila siku walikuwa wakinitafuta. Nilijivunia katika maisha yangu kutokana na kazi kubwa ambao mara kwa mara nilikuwa nikiifanya.
Kuna msichana mmoja ambaye kwa kweli nilikuwa nikimchukia, msichana huyu alikuwaakiitwa Christina. Kuna sababu nyingi ambazo zilikuwa zikinifanya kumchukia Christina. Sababu ya kwanza alikuwa mcharuko kupita kawaida, na hii ilitokana na namna ambayo alikuwa akipenda sana kuongea na wavulana.
Niliona kwamba kila mvulana mtaani kwetu alikuwa ametembea na Christina kwa namna ambayo alivyokuwa akijirahisisha. Christina alikuwa akinipenda sana japokuwa hakukuwa hata na siku moja ambayo nilikuwa nikimfikiria katika akili yangu.
Katika kipindi hicho nilikuwa bize nikitafuta Bikira, sikutaka kabisa kutembea na msichana ambaye niliamini kwamba hakuwa na bikira. Bikira ndicho kitu ambacho nilikuwa nikikitamani sana katika maisha yangu, na kama bikira zingekuwa zinanunuliwa, hakika ningetumia kiasi kikubwa cha fedha kuzinunua.
Christina. Kila siku alikuwa akinitumia zawadi mbalimbali, nilifahamu fika kwamba msichana huyu alikuwa akinihitaji. Moyo wangu haukuwa ukimuhitaji kabisa japokuwa uso wake na figa yake vilikuwa vitu vilivyokuwa vikivutia kupita kawaida.
Tatizo la Christina lilikuwa moja tu, hakuwa na bikira. Kutembea na wasichana wasiokuwa na bikira ilikuwa zamai lakini si sasa. Kwa sasa nilikuwa nikiwataka wale wenye bikira japokuwa kila nilipodhania zipo, nilikuta patupu.
INAENDELEA

No comments