Header Ads

Header ADS

Simulizi: Rama sehemu ya nane (08)

 


“Umeona sasa, ungeniharibia? Hivi unajua kuwa huyo ni nani?” Mke wangu aliniuliza baada ya kuondoka.


“Namjua sana, lakini sijui ni kwanini unamuogopa na wewe unafanya nini hapa wakati duka lako liko kule?” Nilimuuliza na kumfuata kutaka kumpiga.


“Nilishakuambia kuwa mimi sipigwi na mwanaume, nitakufunga na kama umenichoka unanirudisha kwetu, hii ni Biashara ya watu ukileta vurugu siwezi kukutetea!” Mke wangu aliongea kwa hasira.


“Biashara ya nani?” Nilimuuliza, bado nilikua na kimuhemuhe cha hasira.


“Nitakuambia lakini utulie, wewe najua una wivu na una haki ya kuwa na wivu, ila sasa hivi nikuambie kuwa sifanyi kitu kibaya kabisa, mimi hii ni Biashara tu lakini hakuna kitu kibaya.” Aliniambia, nilimuomba aniambie pale lakini aligoma, aliniambia kuwa niondoke mpaka jioni atakuja kuniambia kila kitu, nilitamani kujua kila kitu kwa wakati huo lakini aligoma kabisa kabisa kuniambia, sikua na namna zaidi ya kuondoka na mawazo yangu.


“Yule Baba alikua ni X wangu wa zamani, nimekutana naye nikamuambia kuwa nina shida ndiyoa kanifungulia lile duka, sasa unafikiri mimi ningekataa, alinipa mtaji wa milioni 15, kaninunulia kiwanja na wala sitembei naye!” Mke wangu aliniambia, ulikua ni usiku ndiyo kwanza karudi, kwa namna alivyokua anaongea ni kama kilikua kitu cha kawaida sana kwake. Nilimuangalia huku nikitetemeka kwa hasira, nilikasirika kiasi kwamba machozi yalianza kunitoka.


“Unakasirika nini? Mwanaume mwenyewe ana sukari, tangu zamani hata kipindi niko naye alikua hawezi fanya chochote, nilimuacha mimi sasa hivi ananisaidia tu…”








RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA TISA


“Sitaki urudi katika lile duka?” Nilimuambia mke wangu, aliniangalia kwa dharau hukua kicheka.


“Una akili kweli wewe? kwakipi unachonipa hasa? Huwezi kunipangia maisha yangu kama ambavyo mimi siwezi kukupangia maisha yako! Wewe sib ado uaendelea kuwasiliana na kile ki mwanamke chako? Au unafikiri mimi sijui?” Nilinyamaza kimya kwa muda nikiwaza nini chakumuambia, nilikua nimekasirika sana lakini nilijizuia nisimpige.


“Kimwanamke gani? Mimi yule ni Mama wa mtoto wangu, siwezi kuacha kuwasiliana naye?”


“Una uhakika gani kuwa na mimi yule si Baba wa mtoto wangu? au kwakua unaona ana sukari ukadhani kuwa hana uanaume?”


Aliniuliza kwa dharau, hapo nilipata kanafasi ka kumuuliza mke wangu kuhusu yule mtoto wake wa kwanza, yule ambaye alinidanganya kuwa ni mtoto wa mdogo wake. Nilikua bado sijapata jibu la uhakika, mke wangu alikua hajamkataa wala kumkubali ingawa alishamleta pale nyumbani na alikua akimuita Mama ila kila nilipotaka kuongea naye alikwepa, siku nyingine aliniambia kuwa ni mwanae lakini nikimbana sana anasema amemlea hivyo anamuona kama mtoto wake. Hakukubali kuwa alishaolewa zaidi ya kusema “Nilikua nikiishi na Malaya mmoja akahisi kanioa ila mimi sikumchukulia kama mume.”


“Umeshaanza ujinga wako, mimi awe ni mwanangu au si mwanangu wewe inakuhusu nini? Nimepungukiwa nini kama nilizaa kabla, mbona wewe una mtoto na mwanamke mwingine lakini silalamiki, au unataka mpaka tuwekeane masharti ya kulea watoto wetu?”


“Hapana lakini nataka kujua, wewe ndiyo umeianzisha hii mada, unasema yule Baba anaweza kuwa ni Baba wa mtoto wako, mtoto gani huyo?” Nilimuuliza.


“Sasa kwani kusema ndiyo lazima awe yeye, si nina watoto wawili kwanini usisieme hao au unajihakikishiaje kuwa kuna wakwako hapa?”  Aliongea tena kwa dharau, maneno yake yaliniumiza kwani alionyesha kama kusema kuwa mtoto wangu wa kwanza hakua mtoto wangu.


Nilijua hivyo kwakua mtoto wapili nilijua kabisa si wangu, pamoja na kutumia jina langu lakini nilijua kuwa ni wa yule kijana ambaye alitaka kumuoa.


“Unamaanisha nini kusema hivyo?” Nilimuuliza, alionekana kushtuka kidogo, maeno aliyoyaongea hakuyategemea ni kama aliongea kwa hasira.


“Yaishe na wewe, kama ni suala la huyo Baba mimi nuitaachana naye tataribu lakini usinilazimishe kumuacha ghalfa, kanipa vitu vingi sana akininyang’anya unafikiri mimi nitaishije. Tusiwaingize watoto kwenye mambo yetu ya kiutu uzima itakuja kuwa na athari huko baadaye.” Aliongea na kuimaliza kabisa hiyo mada, hata nilipojaribu kuileta alibaki kimya, alijifanya kununa na hakunijibu tena.


Baada ya siku ile mke wangu alibadilika sana, alianza kutoka kwa uhuru kwenda kwa yule mwanaume, aliacha kabisa kwenda kwenye duka nililokua nimemfungulia, mwanzo alilifanya stoo lakini baadaye aliliacha kabisa, alihamishia vitu vyote katika duka alilofunguliwa na yule Baba na kuwa anashinda huko. Alinipiga marufuku kwenda kumuona kule akihofia kuwa yule Baba atajua kuwa bado anaishi na mimi. Alimuambia kuwa nimemuacha na kumptelekezea watoto.


“Akijua hujaniacha atakasirika sana, nibora ajue kuwa nimetelekezwa na watoto, ananisaidia sana kuna kiwanja kaninunulia na anataka kunijengea. Huna haja ya kuwa na wasiwasi, ana Kisukari yule mashine haifanyi kazi!”


Mke wangu aliniambia, pamoja na kuambiwa yote hayo lakini kama mwanaume niliumia sana, nilikua nalia kila siku nikitamani aachane naye lakini wapi. Mke wangu hakua tayari kumuacha yule mwanaume na kila nilipokua nikimuambia kama hivyo ni bora tuachane alikataa, alishuka chini kidogo akiniambia kuwa nimpe muda wa kujipanga amuache taratibu. Alichepuka naye kwa uhuru na baada ya kama miezi sita hivi yule mwanaume alimnunulia gari, ingawa mke wangu alinidanganya kuwa ilitokana na pesa zake za Biashara lakini sikumuamini, nilijua kanunuliwa na mwanaume mwingine na mimi sikua na chakufanya zaidi ya kuvumilia.


Mtu pekee ambaye alikua akinifariji alikua ni Joan, bado tulikua tunawasiliana naye, nilikua sijamuambia kuwa nimesharudiana na mke wangu ingawa alishasikia kwa watu. Hasira zangu zote nilikua nikipeleka kwake, kila nikikorofishana na mke wangu nilikua nikimpigia ili kunifariji na kama akileta mdomo basi naishia kumtukana, tulikua tunagombana sana na kwakua mwishoni aliishia kuomba msamaha yeye basi nilikua naona fahari kidogo na kujihisi mwanaume.


“Nimeshakuambia huyu mwanaume itamuacha, lakini tuna watoto wawili, siwezi kumuacha ghafla namna hiyo, kuna mambo nakamilisha ili nikiachana naye niwachukue wanangu.” Kila siku nilikua nikimuambia hivyo Joan na yeye alikua akikubali.


Pamoja na kupenda kumpigia simu mara kwa mara lakini nilikua nikifanya hivyo kisiri, sikutaka mke wangu kusikia, si kwamba nilikua nikimuogopa sana mke wangu, hapana nilikua nakwepa kelele zake, nilijua kabisa kama akijua nawasiliana kila siku na Joan angekasirika na hata kuniacha. Siku moja Joan alinipigia simu kuwa mtoto wetu anaumwa, alikua kalazwa hospitalini, alikua na hali mbaya na hakua na pesa. Miaka miwili ilikua imepita tangu kutengana na Joan, nilikua sijawahi kwenda kumuona wala kumuona mtoto.


Kuna pesa flani nilikua nayo kama laki nane nilimtumia yote, ilikua ni pes aya ada kwaajli ya mtoto wangu wa kwanza ambaye alikua anakaribia kuanza darasa la kwanza. Niliitoa nikiamini kuwa kuna pesa nyingine nitapata, niliituma yote kwaajili ya matibabu na mambo mengine, ingawa mtoto alikua na Bima lakini kama unavyojua hospitali zetu kama huna pesa kuhudumiwa ni shida, sikutaka mwanangu ateseke. Lakini katika kuituma nilisahau kufuta meseji ya M-Pesa, mke wangu wakati anakagua simu yangu aliiona, usiku aliniuliza ni kwanini nilikua nimemtumia Joan pesa nyingi kiasi kile.


“Si aa mtoto wangu ulitaka nimtelekeze mwanangu!” Nilimjibu kwa hasira, nilikua na mawazo ya mtoto wangu kuumwa hivyo niliona kama ananichulia tu na mikelele yake.


“Nimekuvumilia sana lakini naona unataka kunipanda kichwani, kila siku nakuangalia tu, najua unawasiliana na yule Malaya wako lakini nimekaa kimya kwakua huniathiri chochote, ni ujinga wako kuwasiliana naye lakini sijali. Ila sasa umevuka mipaka, pesa zote unamtumia yeye, mimi nahangaika kutafuta ili kuwekeza kwaajili ya familia yetu wewe unapeleka pesa zote hizo kwa huyo mwanamke, uafikiri mimi siumii, au unaona kama nafurahia?”


“Siko hapa kwaajili ya kukufurahisha, mambo mangapi unafanya mimi siyafurahii lakini navumilia, hatupo hapa kufurahishana, pesa nimetuma na hunifanyi chochote?” Nilimjibu kwa hasira kwani niliona kama ananipanda kichwani.


“Nikuambie kitu naona huyo Joan kakuchanganya sasa kwa taarifa yako  naweza kumfanya chochote kile, kama niliweza kumpeleka kigoma hata jela naweza kumpeleka!” Mke wangu aliongea, mwanzo nilikua kama sijamsikia vizuri lakini alirudia tena.


“Kigoma, umanaanisha nini kusema umempeleka Kigoma?” Nilimuuliza kwa mshangao.


“Mimi nikitaka kitu kiwe kinakua, ukitembea na wakubwa hakuna kitu kinashindikana, unafikiri huyo Malaya wako Kigoma nani alimpeleka, sasa ukizidisha ujinga wako na kazi itamshinda huko uone kama huyo mtoto wako atamlea akiwa jela au akiwa hana kazi?”


Nilianza kuunganisha matukio na kujua ni kwanini mke wangu alikua anasema vile, kipindi anataka kunirudia ndicho kipindi Joan ali[pata matatizo na kuhamishwa, nilikua sijawahi kuwaza kama alikua anahusika mpaka siku ile. Kile kitendo kilinikasirisha sana, nilijikuta napata hasira na kumtandika makofi, sikujali chochote, kwa namna nilivyokasirika mke wangu alinywea, alijifanya kutania.


“Hakuna kitu nilikua nakutania, mimi nina nguvu gani ya kumhamisha mtu!” Aliniambia lakini nilikua simuamini tena, nilijikuta  napata na hasira mpaka yeye kuniogopa, sijui hata zilitoka wapi lakini niliumia sana kwani angalau nikiwa na Joan nilikua na furaha na nilikua najiona mwanaume kidogo.


***


Kila kitu kilifanyika kimya kimya, mke wangu alikua hanisemeshi, zilikua zimapita wiki mbili tangu kumpiga makofi mke wangu baada ya kuniambia kuwa yeye ndiyo alikua sababu ya kuhamishwa kwa Joan. Alikasirika sana, akawa haongei na mimi, kila kitu alikua anaongea na binti wa kazi, hata pesa za matumizi alikua haniambii, anamuambia binti wa kazi muambie Baba nahitaji kitu flani, muambie mchele umeisha, muambie mtoto anaumwa na mambo mengine. Shughuli nyingine kama mume alikua akinidfanyia lakini kimya kimya, alikua akifua, kupika na kufanya kila kitu kasoro kuongea na mimi


Hali ile ilinichanganya sana, nyumba ilikua haina amani, kulikua hakuna furaha, kuna wakati nilitamani hata kuondoka na kumuacha na ukimya wake lakini nilishindwa, isingekua na maana. Nilitaka kumpigia simu Mama yake kumuambia aongee na mwanae lakini niliona ni kama kujidhalilisha kuwa nimeshindwa kuwa mwanaume na kuitawala nyumba yangu. Nilijitahidi sana kuwahi nyumbani, kutimiza majukumu yangu kama mume, kumnunulia zawadi, kumpa lesa lakini hakujali, alikua kakasirika ana kisirani chake. Muda mwingi aliutumia kuangalia TV na kucheza na watoto, nilijiona mpweke ndani kwangu  nilijiona kama mgeni vile.


“Hali hii itaendelea mpaka lini?” Nilimuuliza, ulikua ni usiku tumepanda kitandani nilipojaribu kumshika ili kufanya mapenzi alijiachia aliniruhusu nifanye kila kitu lakini alilala kama Gogo, hakuonyesha ushirikiano wowote.


“Wewe ni mke wangu, utaendelea kuninunia mpaka lini?” Nilimuuliza huku nikimnyanyua kwa nguvu kukalisha.


“Ungekua unatambua thamani ya mke ungenifanyia uliyonifanyia?” aliniuliza, kwa mara ya kwanza baada ya wiki kama tatu hivi alinijibu, nilijua huo ndiyo mwanzo.


“Nimekufanyia nini? Kama ni kukupiga si niemshakuomba msamaha. Kwanini bado uaendeleza vitu…”


“Msamaha wako una maana gani? Hivi ungeniua ungekuja kuomba msamaha kaburi langu?” Aliniuliza, nilinyamaza kimya na kuona kweli alikua na mantiki.


“Lakini uliniudhi,ulinikasirisha sana kumhamisha Joan….” Nilihjaribu kujitetetea lakini ndiyo kama nilipalia mkaa.


“Hicho ndiyo kilichonikera zaidi, kwamba huyo mwanamke wako ni wa muhimu kuliko mimi. Hivi kama unaweza kunipiga kwasababu tu kahamishwa akifa si unaweza kuniua!”


“Uamaanisha nini kusema akifa?” Niliuliza kwa kupaniki zaidi kwani kwa namna alivyokua anaongea ni kama alikua anapanga kumfanyia kitu kibaya, nilikua simuamini sana mke wangu hivyo niliogopa.


“Unaona sasa unavyopaniki? Kwani huyo mwanamke wako hatakufa, unafikiri ataishi milelea? Atakufa kaka sisi wengine lakini nina wasiwasi kama utakuja kumsahau kama hapo Kigoma tu unataka kuniua!” Aliona mshangao wangu na kujaribu kujielezea, bado sikumuamini, nilimuambia nampenda lakini sikufurahishwa na mambo yake, nilimuomba msamaha na kumuambia sitampiga tena.


“Mimi sijali kupigwa bali sababu ya kupigwa! Katika maisha yangu niliapa kuwa siwezi kupigwa nikigombania mwanaume na mwanamke mwenzangu…”



“Kwani nani unamgombania sasa?” Nilimuuliza kwa mshangao.


“Si ni wewe, uko na mimi lakini unahangaika na huyo mwanamke, sasa uchague kati ya mimi na yeye, kama ukiendelea kuwasiliana naye basi mimi naondoka, sitaku umpigie simu, sitaki uwasiliane naye!”


“Lakini ana mtoto wangu, siwezi kumtelekeza mtoto wangu…” Nilijaribu kujitetea, sikuona sawa kabisa kuacha kuwasiliana na Joan.


INAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.