Header Ads

Header ADS

Simulizi: Rama sehemu ya saba (07)

 


Siku zote mke angu alijua kuwa ananidhibiti, hakujua kuwa nina ubavu wa kumuacha. Hata baada ya kusikia kuwa nataka kumuoa Joan alikua akiamini kuwa ni hasira tu, alikua anaamini kuwa nataka kumuumiza hivyo akili zangu zikinirudia basi nitarudi kwake. Lakini kwakina Joan ni watu wa dini sana, walikataa kunipokea kwakua mimi nimuislamu, kwakua nilishachoka kuumizwa na Joan ndiyo mtu pakee niliona kama ananielewa basi nilikubali kubadilisha dini. Nilibadili dini na kuwa muikristo, ndugu zangu hawakua na shida sana kwani si watu wa duni.


Haikua na tatizo kwangu kwakua Baba mwenyewe alikua muikristo lakini akabadilisha dini kwasababu ya Mama. Mke wangu aliposikia nimebadilisha dini alichanganyikiwa, alijua fika nimemuacha kwani hata kama nilikua sijampa talaka lakini kwa sheria za kiislamu mtu mmoja anapobadilisha dini inamaanisha ndoa inakua imekufa. Alihaha sana, ndugu zake walianza kunipigia, kuniomba msamaha, vitisho na mambo kibao lakini sikujali, nilishaamua kumuoa Joan na hakuna mtu ambaye ningeruhusu kuingilia chochote.


Baada ya utambulisho nilirudi ili kujipanga, lakini siku moja Joan alikuja nyumbani, alikua kanyong’onyea sana, nilimuuliza kwanini akaniambia kuwa alikua anataka kuacha kazi. Nilimuuliza sababu akaniambia kachoka tu lakini anataka kaucha kazi ila anaogopa kwakua kuna watu wanataka kumfanyia fitina. Alinichanganya sana kwania subuhi yake wakati anaondoka alikua vizuri tu, nilijaribu kumpeleleza ndipo akaniambia kuwa alikua kapandishwa cheo na kahamishiwa kikazi Kigoma.


Kwanza nilifurahi kusikia kapandishwa cheo, lakini nilipokuja kutafakari na kusikia neno Kigoma basi nilichangayikiwa.


“Wananiambia nilazima niende, ni kazi maalum, natamanai kuacha kazi lakini unajua kuwa kazi za jeshi, unaweza hata kushitakiwa kwani cheo cheo chenyewe kimekaa kifigisu figisu.” Nilimuuliza ni lini anatakiwa kuondoka aliniambia kesho yake.


“Hii barua nilipewa tangu mwezi uliopita, ilitaka kupambana ili nisiende lakini kuna mzee jana kaniita akaniambia kuwa niende tu kwani hata huku kuhamishwa ni watu wamenipambania, nilishachomewa TAKUKURU hivyo nibora kuondoka.”


Nilimsikiliza kwa makini na baada ya kusikia ishu yake nilimuambia ni bora kuondoka kwani mimi nampenda na kama ni ishu ya kuoana basi ipo pale pale.


“Kigoma sio mbali, ni hapahapa Tanzania, naweza kuja kila mwezi, wewe nenda mambo yakikaa sawa basi tutajua chakufaya.” Nilimuambia huku nikimpa moyo, hata mimi nilikua nimechanganyikiwa, nilikua sijui nini chakufanya kuweza kuokoa mapenzi yetu. Nilishaanza kuwa na  amani, nilishaanza kuwa na mwanamke anayenipenda na kunijali na sasa alikua anaondoka, kwa wakati huo shata sikujua sababu ilikua ni nini, nilihisi ni mambo yao ya kazini wamechomeana na sikutaka kuingilia.


Siku iliyofuata kweli Joan aliondoka, niliumia sana kwani nilikua nampenda na sikujua sababu ya yeye kuondoka. Lakini kama wiki mbili baadaye nilipigiwa simu, mke wangu alikua kalazwa hospitalini na nilitakiwa kwenda. Muda ulikua umepita tangu mimi kuwasiliana naye lakini kwakua sikua na kitu cha kufanya kutokana na upweke wa kuondoka kwa Joan niliamua kwenda, nilimkuta kweli anaumwa, alikua amedondoka na kutenguka mguu. Mama yake alikuepo kumbe baada ya kumuachia nyumba Mama yake na mdogo wake wakika walikuja kuishi pale.


Niliwasalmia vizuri tu, baada ya salamu na kuona yuko sawa niliondoka zangu. Usiku alinitumia meseji.


“Inamaana huwezi kusamehe, hata watoto wako hutaki kuwaona?” Aliniuliza, sikuijibu ile meseji mpaka kesho yake.


“Waao wanakukumbuka, unatakiwa kuja kutoa jina la mtoto wako mdogo, jina la dini tumempa ila wewe kama Baba yake unatakiwa kutoa jina la ukoo.” Meseji ilitumwa, nilikasirika kwani nilijua ni kama dhihaka, nilijua kabisa mtoto si wangu kwani kipindi anapata ujauzito nilikua sishirikini kabisa kimwili na mke wangu.


“Naomba usinichokonoe kabisa! Unajua kabisa kuwa mtoto si wangu hivyo usinichore!”


Nilimjibu, mke wangu alikaa kimya hakunijibu tena mpaka baad aya kama wiki moja tu. Alinipigia simu na kuniambia mtoto wangu anaumwa hivyo anahitaji niende kumuona, alikua nyumbani. Nikweli nilikua na muda sana sijamuona mtoto wangu, tangu nilipoondoka Tanga kipindi kile nilikua sijamuona. Pamoja na hasira za mume wangu lakini nilikua na hamu ya kumuona mwanangu na nilijua isingekua haki kumtelekeza mwanangu kwasababu ya mke wangu. Nilienda kumuona, ingawa alikua mdogo lakini alinitambua, alinikumbatia na kuniita Baba.


Nilifurahi sana, raha ambayo niliipata nilikua sijawahi kuipata kabla, tangu siku ile nilijikuta kila siku jioni naenda kumuona mtoto wangu, walinipokea vizuri na kila siku mke wangu alikia akiniomba msamaha ili tududiane lakini sikukubali. Akili yangu bado ilikua kwa Joan na kila siku tulikua tukiwasiliana ingawa yeye kazi zilikua zikimbana kuja kufunga ndoa. Siku moja nilikua nyumbani kwangu ambapo alikua akiishi mke wangu na ndugu zake, Mama yake alikua kaondoka kaenda Tanga.


Nilishazoea kwenda kila siku na kwa namna flani nilikua afurahia, nilikua nacheza na watoto, hata mtoto wake naye nilianza kumpenda kwani naye alinipenda, mara nyingi nikiwepo alikua akinililia na nikimlisha alikua anakula vizuri. Tofauti na siku nyingine ambapo mke wangu alikua akinisisitiza kulala siku ile ni kama alikua anataka niondoke. Kila dakika alikua akiniuliza kama naondoka saa gapi, mara akimuambia mdogo wake mchukue mtoto shemeji yako awahi nyumbani, mara akisema usiku umeingia nataka kulala.


Sikujua sababu lakini ile hali ilinishangaza na kwa kisi kikubwa ni kama alikua ananiambia subiri usiondoke. Nilikaa mpaka saa nne usiku, mke wangu alionekana kuwa na wasiwasi sana, alikua na mawazo sana mpaka nikamshitukia. Nilipomuuliza aliniambia hajisikiivizuri aataaka kulala, niliona hamna shida ngoja niondoke, nilinyanyuka kutoka lakini ile nafika getini nilikutana na yule mchumba wake wa zamani. Yule mwanaume ambaye alitaka kumuoa, kabla sijamuuliza chochote yule kijana alinivamia na kuanza kunipiga, alinidondosha chini na kuanza kunipiga hukua kinitukana.


“Kama mwanamke kakuacha kubali! Nasikia unamtishia mtoto wangu nitauja kukuua! Mshenzi mkubwa wewe! Nakuambia kuwa nitakuua! Mwanaume gani unapiga mwanamke!” Aliendelea kunipiga huku akitukana, alionekana mwenye hasira mtu aliyeumizwa, mke wangu alikua pembeni akilia tu huku akimsihi aniache lakini hakuniacha. Alinipiga sana, si kwamba alikua na mwili mkubwa hapana lakini kwakua alinivamia mimi sijajiandaa aliweza kunidhibiti, alinisukuma mpaka nnje na yeye kuingia ndani.






RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!---SEHEMU YA NANE


Nikiwa pale chini nilijifanya kuchoka, nilijifanya kuumia ili kukusanya nguvu, alizubaa kidogo nikafanikiwa kunyanyuka, nilimsukuma na kuanza kulipoa kisasi, nilimpiga sana mpaka mke wangu alipoingilia na kunishika ndipo nilimuachia.


“Anafanya nini hapa huyu mpumbavu?” Yule kijana aliuliza, bado alikua chini anaugulia maumivu huku na mimi nikiwa nimesimama lakini nikiugulia maumivu yangu.


“Hapa nikwake, huyu ni mume wangu, wewe si uliamua kumsikiliza Mama yako na kuniacha, sikutaki nimemrudia mume wangu na huyu mtoto ni wakwake!”


Mke wangu aliongea huku akinikumbatia, alinishika shika ili kumpa wivu na mimi bila kujali kama nilikua natumika au la nilimkumbatia mke wangu na kuanza kumla mate.


“Hakuna, kitu kama hicho! Nimekugharamia sana huwezi kuniacha kirahisi rahisi namna hiyo! Nimekuambia kama unataka kuishi kwaamani basi utaendelea kuwa mwanamke wangu! mimi nakupenda wewe na siwezi kuruhusu mtoto wangu kupewa mwanaume mwingine hata kama nikiwa maiti Mama yangu atamlea!” Yule kijana alilalamika akiwa  bado pale chini, nilimpiga vizuri na alionekana kuumia sana.


“Unaona akili zako sasa, mwanaume gani kila kitu ni Mama! Mama! Mamma! Uajiona mwanaume kweli, hivi huwezi kuwa na maamuzi yako mpaka kumshurikisha Mama yako! Unasema nimekuacha wakati Mama yako kakuozesha na mwanamke ili tu usiwe na mimi! Kwanini unahangaika na mimi, si una kimwanamke chako umepewa na Mama yako, kamfuate basi! Pesa zako lakini kutumia mpaka Mama yako. Nimekuambia uninunilie gari lakini eti mpaka Mama yako akumbie, uensema mtoto wako hujui anakula nini? Analala wapi? Wanaume wenzako wanakusaidia kulea wewe umekaa na Mama tu kupanga maujinga yenu, sikutaki! Nisharudiana na mume wangu na kwa taarifa yako hata talaka hakunipa basi!”


Mke wangu aliongea kwa kujiamini, wakati wote huo alikua kanikumbatia na ndipo niligundua kuwa kumbe bado jamaa alikua anampenda lakini tatizo lilikua ni Mama yake.


“Nimekupa vitu vingapi, nimekupa pesa kiasi gani wewe unakula na Mama yako! Mbona mimi sisemi kuhusu mambo mnayofanya na Mama yako! Yule ni Mama ana nafasi yake lakini haimaanishi kwamba kwakua kaseam tuachane ndiyo nikuache kabisa, hapana mimi bado nakupenda na una mtoto wangu, kama ni gari nimekuambia subiri mambo yapoepoe, kuna hela nakusanya nitakununulia, sitaki mwanangu ateseke lakini siwezi kukununulia kama bado utaendelea kuwa na huyu mshenzi!”


“Sio mshenzi ni mume wangu tena mheshimu sana! Mwenzako anajielewa hana umama mama kama wewe!”


“Hana Umama mama, kwahiyo mwanaume kukupiga ndiyo unaona uanaume, unataka na mimi niwe nkaupiga, nakunyima chakula, niwe malaya na kukutukana kila siku ndiyo utaniona sina umama!” Aliongea akimaanisha mimi ndiyo nilikua namfanyia mke wangu hayo mambo, nilimuangalia mke wangu mpaka akaona aibu, alionekana kunisema maneno mengi mabaya.


“Bwanaeee! Ondoka, hii ni nyumba yangu na huyu ni mke wangu, sijampa talaka na kama ni gari mimi mwenyewe nina uwezo wa kumnunulia, ondoka!”


Baada ya kuona wananizingua niliamua kumtolea uvivu, nilimfukuza yule kijana na kufunga geti, nikiwa ndani mke wangu alianza kuniomba msamaha, aliniambia ananipenda na alikua anafanya yote hayo kwakua mimi nilibadilika.


“Unakumbuka kipindi kile ulipoanza na yule mwanamke wako, mimi niliona kabisa utaniacha ndiyo maana nikaamua kutafuta mwanaume mwingine. Si unajua kuwa mimi siwezi kuwa peke yangu sasa ukawa unachelewa kurudi na mimi nikapitiwa, lakini nakupenda na siwezi kuishi bila wewe! Unaona huyu kaka kila siku ananisumbua, anasema ananitaka lakini mimi nishakuchagua wewe siwezi kukuacha.”


Mke wngu aliongea huku akilia, alilia sana hukua kinikuumbatia, aliniomba usiku ule kulala pale. Kwakua sikua na chakufanya nyumbani nilijikuta namkubalia, tulilala na kujikuta tunafanya mapenzi, nilijikuta naendelea kuja kulala nyumbani mpaka tukarudiana, nikarudisha chumba na kuhama kabisa. Nilimrudia mke wangu kimya kimya bila kumuambia mtu yeyopte, mwanzo niliona aibu kwani karibu kila mtu alikua anajua kuwa aliniacha na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine lakini baadaye sikujali, yalikua ni maisha yangu nilirudiana na mke wangu huku nikiamini kuwa atabadilika na kuwa mke bora.


Katika kipindi chote hicho mke wangu alikua ni Mama wa nyumbani, alikua si mtu wa kutaka kufanya Biashara ingawa mara nyingi nilishamtafutia Biashara na kumpa mtaji lakini aliishia kuula. Ila baada ya kurudiana ghalfa alianza kuniambia kuwa kachoka kuwa Mama wa nyumbani anataka kitu cha kufanya. Mwanzo niliona kama ni utani na kudhani kuwa kama nikimpa mtaji basi nitapoteza pesa zangu lakini kadri siku zilivyokua zinaenda ndipo nilimuona kama yupo siriasi na Biashara.


Aliniambia kuwa anataka kufanya Biashara ya Dagaa wa mwanza, alianiambia kuwa kuna rafiki yake anafanya Biashara ya namna hiyo hivyo kama nikimpa mtaji wa milioni moja basi anaweza kuifanya hiyo Biashara vizuri. Tatizo langu likawa ni kusafiri, kwa nilivyokua namfahamu mke wangu nilimuonea wivu sana kama angesafiri, tabia zake zilinitia shaaka. Nilikataa na kumuambia abadilishe Biashara kwani mtoto bado ni mdogo hivyo hawezi kusafiri na kama ni kutafuta Biashara basi atafute Biashara ambayo si ya kusafiri. Tofauti na kawaida yake ambayo anakua mbishi sana alikubali na kufungua duka la nguo.


Nilimpa mtaji wa milioni mbili pamoja na kumlipia fremu, Biashara ilianza taratibu lakini ghafla niliona inapanuka, mtaji unakua mkubwa na mke wangu anakua bize sana na kazi. Mwanzo nilifurahia lakini siku moja nilimfuata dukani, ilikua ni jioni na nilienda kumchukua ili kurudi naye. Sikumkuta dukani, duka lilikua limefungwa, nilimpigia simu ili kujua yuko wapi lakini simu ilikua haipokelewi, ilikua inaita tu. Nikiwa nimesimama pale nimeshikilia simu kuna dada mmoja wa duka la jirani, nilimsogelea na kumuuliza alipokua mke wangu.


“Mbona huyo muda wake wa kufungua bado…” Yule dada aliniambia, kwanza nilishangaa kwani ilikua kama saa kumi na moja na nusu za jioni, mara nyingi dukani mke wangu hufungua saa mbili za asubuhi na karibu kila siku saa moja jioni naenda kumchukua kasoro siku ile ndiyo nilikua nimewahi kwenda.


“Unasemaje?” Nilimuuliza kwa mshangao.


“Namuulizia mke wangu unasema sio muda wake wa kufungua, unamaanisha kufungua au kufunga.” Dada kwanza alicheka kwa dharau, alikaa kimbeambea na nilijua kuna kitu alitaka kuniambia ni kama alikua anasira, nilimkazia macho kumuonyesha kuwa nilikua siriasi.


“Huyo Dada hafungui duka mpaka saa moja kasoro na saa moja ukija kumchukua anafunga, hata hakai nusu saa dukani lakini kila siku ni mzigo mpya.” Aliongea, nikiwa hata sijajua cha kumjibu kuna gari flani VX ilisimama pembeni, ilikua na Vioo vyeusi sikuweza kuona waliokua ndani.


“Ndiyo huyo analetwa kufungua duka…” Yule dada aliongea lakini ile gari haikusimama muda mrefu, iliondoka kwa mwendo wa kasi. Nilibaki namuangalia yule dada ambaye naye hakua na chakuseama, nilimuona mmbea tu nikarudi upande wa dukani kwa mke wangu kumsubiri nikijua kabisa atakua katoka mara moja.


“Niko nyumbani mume wangu, sijisikii vizuri kabisa leo nimefunga mapema.” Ujumbe mfupi kwenye simu yangu uliingia. Nililazimika kunyanyuka taratibu nikaingia kwenye gari na kwenda nyumbani. Nilimkuta mke wangu kalala na nilipojaribu kumsemesha alijifanya kuchoka, sikuongea chochote, niliamua kunyamaza huku nikijipanga kumchunguza. Kama wiki moja hivi nilikua nikivizia nyakati za mchana nakuja kumuangalia dukani, nilikuta amefungua na kuona kuwa labda yule jirani alikua kanidanganya, lakini kumbe ni kama alishtukia kwani baada ya hapo kila nikienda dukani kwake nilikuta kumefungwa.


Nilienda kwa zaidi ya mwezi kila siku mchana kumefungwa lakini jioni nakuta kumefunguliwa, roho iliniuma nikiwaza mke wangu alikua akienda wapi? Sikua na jibu, siku moja asubuhi nilimuaga kuwa naenda kazini, niliondoka lakini baadaye nilirudi nyumbani kwa mguu, nilivizia mpaka ule muda mke wangu anaondoka kwenda dukani na kuanza kumfuata nyuma. Kutoka nyumbani mpaka dukani ulikua ni mwendo wa kama dakika kumi kwa Gari, alichukua Bajaji na mimi nikachukua, nikamfuatilia, hakwenda dukani kweake bali alishika njia nyingine.


Aliondoka mpaka mtaa kama wa tatu hivi, alifika na kushuka, nikidhani labda anaenda nyumbani kwa mwanaume niliona anafungua duka jingine. Lilikua duka la nguo pia lakini kubwa kuliko duka nililokua nimemfungulia yeye. Lilikua kubwa zaidi ya kama mara tatu hivi, aliingia na kuanza kuuza, nilijikuta nakaa pale mpaka mchana nikimuangalia, nilikua nimejibanza katika baa flani jirani nakunywa soda, mchana lile gari ambalo lilipita siku ile na kusimama kisha kuondoka lilifika pale, lilisimama na akashuka baba mmoja mtu mzima, aliingia dukani kwa mke wangu.


Alisimama kwa muda upande wa wateja kisha akaingia kwa ndani sikumuona tena. Nilishikwa na hasira, wivu ulinijaa, kichwani nilikua na maswali mengi, nilitamani sana kwenda kufanya vurugu lakini nilijua kuwa haiwezi kusaidia. Nilijikuta naondoka bila kufanya chochote, jioni kama kawaida mke wangu alikuja dukani, akafungua na mimi nilipoenda nilimchukua. Nilimuuliza kuhusu siku yake alishukuru kuwa Biashara nzuri tukaenda nyumbani, kwake kila kitu kilikua kama kawaida, kama vile hakuna kitu kimetokea, wakati mimi nikichanganyikiwa kwa mawazo yeye alijaribu kuchangamka kama vile hakuna kitu kimetokea.


Siku iliyofauata nilienda kazini, lakini mchana nilishindwa kuvumilia, nilimfuata mke wangu mpaka kwenye duka lake jipya. Alishangaa sana kuniona sehemu ile, alikua peke yake.


“Unafanya nini hapa? Inamaana unanifuatilia?” Aliniuliza kwa wasiwasi, alikua akiangalia saa mara kwa mara, mwanzo nilihisi kuwa ule wasiwasi ulikua ni kutokana na mimi kugundua anayoyafanya lakini mwisho nilikuja kujua kuwa kumbe hata alikua hajali kama mimi niko pale au la, alikua akiwaza mtu wake.


“Ondoka, nitakuelezea kila kitu nikifika nyumbani, naomba usipaniki kwani utaniharibia! Sio kama unavyofikiria, sikusaliti, naapa nitakuambia ukweli!”


Aliongea kwa wasiwasi, nilimuangalia kwa hasira bila kusema chochote, niliomuona anatetemaka kabisa kwa uoga.


“Rama ondoka Pleassseee! Utaniharibia kwakweli, kuna ishu ya maana nafuatilia, naomba ondoka….” Aliongea huku bado akiangalia saa, nilijua ule ulikua ni muda wa jamaa yake kuja, sikutaka kuondoka, nilitaka aje anikute pale nimuone tuonane nione mke wangu atafanya nini. Nliingia ndani na kuanza kuchagua chagua nguo, kweli haukupita muda yule Baba alikuja, nilimuona kwa karibu alikua ni mtu ambaye namfahamu, mtu mkubwa tu na cheo chake, nilimfahamu kutokanja na umaarufu wake.


Alinisalimia vizuri lakini kwakua ni mtu na familia yake alijifanya kuchagua nguo na kuondoka, mwanzo nilihisi labda kaniheshimu anajua kuwa mimi ni mume wa mchepuko wake lakini baadaye ndipo nilipojua kuwa kilichomuondoa nikwakua alikua ni mume wa mtu na ana cheo kikubwa serikalini hivyo hakutaka kuonekana kama anacheuka na hakua akinijua.


BONYEZA HAPA UPATE MESEJI NZURI ZA MAPENZI


INAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.