Simulizi: Rama sehemu ya nne (04)
Baada ya kuona kama hapelekwi mahakamani labda kupata dhamanai huko nilijua kuwa nimeshindwa, niliamua kutafuta wakili. Nilienda kwenye ofisi moja hivi ya uwakili, nikapaki gari langu lakini kabla ya kuingia niliona dada mmoja akitoka, nilimkumbuka, alikua ni askari ambaye mara kwa mara nilikua nikimuona kituoni, mara nyingi alikua akinisalimia vizuri na ni yeye alikua akiniingiza kinyume cha utartibu kwenda kumuona mke wangu pamoja na yeye kukataa. Yeye alikua ni askari mpelelezo, sijui alifuata nini pale lakini niliamua kumsalimia.
Niliongea naye mawili matatu, alionekana kuwa na haraka kama mtu ambaye alikua akinikwepa kuwa hataki kuongea na mimi. Ni kama kuna kitu alikua ananificha, nilimuuliza lakini hakutaka kuniambia.
“Sitakiwi hata kuongea na wewe, kuonekana na wewe hapa ni kama vile na hatarisha kazi yangu,….” Aliniambia huku akiondoka, alikuja na gari yake, aliingia kwenye gari na kutaka kuondoka, lakini kabla ya kuondoka alishusha kioo cha mbele na kuniita kwamkono.
“Acha kuhangaika, siko katika kesi ya mke wako lakini nahisi kuna mchezo wanakuchezea, mke wako si mtu wa kukosa dhamana, hujiulizi anafahamiana na mkuu wa kituo lakini analala rumande, mkeo sidhani kama analala pale, chunguza…”
Aliongea na bila kunipa majibu alikanyaga mafuta na kuondoka. Nilikaa kimya kwa muda nikajikuta sina hamu tena ya kuingia kwa wakili, wka nilivyokua namfahamu mke wangu asingekubalia kukaa mahabusu, angekua analia kila siku nihakikishe namtoa. Sidhani kama angekubali kula chakula cha mahabusu, lakini katika siku zote tano kila nikitaka kuonana naye alikua anakataa, kila nikimpelekea chakula nilikua narudishwa nacho, tena kwa ukali kabisa kuwa sitakiwi kupeleka chakula pale.
Ni kama kulikua na kitu hasa nikiuliza ni kwanini hapelekwi mahakamani na kama ni mke wangu kuwa na hasira na mimi ni kwanini alikua hata hawapigii simu ndugu zake kuja kumchukua. Niliumiza kichwa sana, niliamua kaucha mambo ya wakili na kuchunguza, nilihangaika kupata taarifa lakini sikupata, kesho yake nilimvizia yule dada wakati anaondoka nikaamua kumfuatilia nyuma mpaka kwake, nilikomaa na kumuambia kuwa siwezi kuondoka mpaka anipe majibu.
Kusema kweli yule dada alikua ananionea huruma, kuna kitu nilikiona kwake, kwa namna alivyokua ananiangalia nilihisi kama vile ananipenda hivyo niliamua kuutumia udhaifu wake huo kupata taarifa.
“Hivi kwanini unampenda yule mwanamke?” Aliniuliza, nilijisikia vibaya kidogo kumuita mke wangu mwanamke kwani niliona kama anamdhalilisha.
“Si mwanamke ni mke wangi, nina mtoto mchanga naye na nimemuoa ndiyo maana nampenda.” Nilijilazimisha kumjibu kwa ustaarabu kidogo kwani pamoja na hasira zangu lakini nilikua nahitaji sana msaada wake.
“Si kwa ubaya lakini hakustahili, anakuchezea akili tu…”
“Kivipi?” Nnilimuuliza huku nikimsogelea karibu, nilimuona kabisa kama anatetemeka, nilimshika mkono na kumvuta mpaka kwenye gari.
“Tusiongelee hapa, watu wanapita…” Nilimuambia, kweli alinifuata bila hata kuuliza, gari yake alikua kaipaki vibaya lakini hata hakujali, aliingia kwenyue gari yangu.
“Tunaelekea wapi?” Aliniuliza, ni kama alitaka twende sehemu, sijui kwanini lakini nilijisikia vibaya, gahfla nilijihisi msaliti, niliona kama vile namsaliti mke wangu kama vile natoka nnje ya ndoa yangu, nilijaribu sana kujizuia lakini aliona.
“Unampenda sana mke wako?” Aliniuliza baada ya kuona kwamba mimi ndiyo nilikua natetemeka kwa uoga, nilikua nahisi kama kuna kitu kibaya nakifanya.
“Kwanini unauliza hivyo? Kawaida tu, si mke wangu…”
“Kwanamna unavyomhangaikia, hivi unajua kila siku nakuja tu kukuangalia, unatia huruma unayofanya huku mwanamke mwenyewe daaa…”
“Mwanamke mwenyewe nini? Mke wangu kafanya nini? Niambie! Unamanisha nini….” Aliongea kwa wasiwasi kama vile kuna kitu alitaka kuniambia lakini alisita, nilimkatisha nikiwa nimepaniki kabisa.
“Unaona wewe si wakuambiwa kitu, unaweza kuniharibia hata na kazi, nimesema hivi tu umepaniki, si unaweza enda kumuambia mke wako ukaniharibia na kazi, mke wako anakula na wakubwa, nikijulikana kama nimeongea kazi sina, kila mtu anajua….daa kuna wanawake wanapendwa lakini hata hawajui kupendwa, ningekua na mwanaume kama wewe…” Alijiongelesha, nililazimika kutulia kwnai nilishapaniki, presha imepanda nahema kama nimepanda mlima, nilitulia na kumbembeleza, aliamua kuniambia hukua kinisihi sana nisimuambie mtu yeyote.
Mke wangu alikua hataki kutoka kituoni kwakua alikua anataka niitoe ile gari, kuna pesa nyingine alikua ameahidiwa na kuhusu dhamana ni mke wangu alikua hataki kwakua alikua halali pale kituoni. Mara nyingi alikua akiletwa asubuhi na jioni mimi nikiondoka nayeye huondoka kwani alikua ni mchepuko wa muda mrefu wa mkuu wa kituo.
“Mbona kila mtu anajua, kila askari anajua na mke wako alikua anakuja mara kwa mara hapa tangu kipindi akiwa mjamzito.” Yule dada aliongea akionekana kama anamjua mke wangu kwa muda mrefu.
“Hivi mwanaume unajisikiaje kuwa na mke wa namna ile, maana hata huyo mkuu mwenyewe anaibiwa, yaani wanawake wengine….”
“Wanawake wengine nini? Wanawake wengine nini?” Nilimuuliza kwa kupaniki, ingawa nilikua najua tabia za mke wangu tangu zamani lakini kuzisikia ilikua ni kama naambiwa upya. Nilishindwa kujizuia nikajikuta hasira zinanipanda, yule dada kuona vile natye alikasirika na kushika.
“Mijitu mingine inasaidiwa lakini haijiongezi!” Aliongea huku akitoka, nilishtuka na kumuomba msamaha, hakunisikiliza sana zaidi ya kuniambia kuwa anaomba nisimuambie mtu kwani nitampotezea kazi.
“Ushauri wangu rudi nyumbani, lea mtoto wako, ukikaa siku mbili tu huajaja kujiliza liza kituoni mke wako atatoka kwa dhamana na huyo anayekudai atakubali umlipe. Sasa hivi hataki pesa zako kwakua mke wakoa najua kua huwezi kumaucha akaozea jela lazima utatoa gari.” Alinishauri na kuondoka, niliondoa gari nikiwa na hasira, mwanzo nilipanga kurudi kituoni kuongea na mke wangu, nilikua na hasira sana lakini nilipofioka nnje ya kituo niliona kama nitahaeribu, niliamua kufuata ushauri wa yule dada. Nilirudi nyumbani nikakaa na kuamua kukaa mpaka mke wangu ajitoe mwenyewe kwani niliamini kuwa ananichezea.
Nilikaa siku mbili bila kwenda kituoni, jioni ya siku ya pili nilipokea simu kutoka kwa John, alitaka kuonana na mimi, nilimuambia nipo bize lakini alilazimishia. Nilikutana naye akaniambia ameona asifuatilie kesi kwani itampotezea muda anataka nimlipe pesa zake lakin kwa riba.
“Mke wako kakaa na pesa zangu muda mrefu, kama ni kufura kasi bais unipe na riba.” Nilimuangalia kwa dharau na kunyanyuka, nilishajua mchezo waao
“Wakati mnapena pesa sikuepo, una kadi ya gari yangu utanipa au nitaenda tu kutoa ripoti kuwa imepotea basi, sitahangaika nayo na kwakua nina kila kitu kingine basi hiyo itakua kama karatasi tu.
Kuhusu mke wangu mtajuana wenyewe, mimi nishamuacha hivyo kamalizane naye.” Niliongea huku nikiondoka harakaharaka,k sijui nilipata wapi ujasiri lakini nilimkazia na kuondoka, hakuamini, wakati naondoka alinitishia tishia kuwa nitafungwa lakini sikujali, niliondoka na kuendelea na mambo yangu. Nilirudi nyumbani nikiwa na mawazo sana, bado nilikua sijui hatima ya mke wangu, nilikua sijui kama atatoka au la, pamoja na yote lakini bado nilikua nampena na nilikua tayari kumsamehe kama angeomba msamaha.
Asubuhi ya siku ya tatu nilitaka sana kwenda kituoni, nilitaka hata kumpeleka mtoto kumuona Mama yake lakini nilisita, baada ya John kunitafuta jana yake nilijua fika kuwa mke wangu kashajua nimemkatia tamaa hivyo wataacha ujinga wake. Kweli ilipofika kwenye saa nne hivi za asubuhi mke wangu alikuja nyumbani, alikua kachoka sana, nilifurahi kumuona lakini sikuonekana hata kujali. Alipoongia alianza kujiongelesha kuwa kapata dhamana, nilimuitikia bila kuuliza chochote, ingawa nilitamani kujua lakini nilitaka kuwa mgumu kidogo.
Alianza kunilaumu kwa kumuacha bila kumtembelea, kuthamini gari kuliko yeye na mambo mengi lakini sikutaka kumsikiliza, nilimuacha anaongea na kuondoka zangu. Hakuaminia lipokua akipiga simu zangu hazipokelewi, hakumini nilipokua nikiacha kujibu meseji zake, ingawa nilitamani kumjibu, kumkumbatia na kumuambia nimemsamehe lakini niliona kuwa amenichezea sana hivyo kama nikimuendekeza basi atanifanyia ujinga mwingine. Nilimchunia na kuzunguka mtaani tu nikiwa sina hili wala lile.
Kwenye saa kumi hivi za jioni bado nilikua mtaani, nilikua sitaki kurudi nyumbani kuonana na mke wangu kwani nilijua kama nikifanya hivyo nitamsamehe na kuwa mdhaifu kwake. Nikiwa sina hili wala lile simu yangu iliita, ilikua ni namba ngeni na nilipopokea ilikua ni sauti ya kike.
“Samahani, nimechukua namba yako kituoni, mimi Joan ( si jina lake halisi) yule dada dada askari…” Alianza kujitambulisha.
“Nakukumbuka, habari? Za tangu siku ile, samahani nilikua sina namba yako, nilitaka kukushukuru kwa taarifa.” Nilimuambia.
“Hakuna shida, nilisafiri ila nimekuja nimesikia mke wako katoka, wamemuachia na hakuna kesi tena.” Aliniambia, nilimuambia nikweli, mbinu aliyonipa ilisaidia.
Nilimshukuru sana na tulijikuta tunaongea sana, sikupanga lakini niliongea na Joan kwa zaidi ya masaa mawili, nilijisikia raha na wala sikujisikia vibaya kuongea naye. Tuliongea mambo mengi akaniambia hajaolewa lakini ana watoto mapacha ambao alizaa na X wake, ambaye alikua akimpiga sana akaona kuachana naye na yule X wake kumkomoa akaenda kumuoa Binamu yake mtoto wa Shangazi yake ambaye pia alikua ni rafiki yake. Stori ya mahusiano yake ilikua ya kusikitisha, niliumia sana namna alivyokua akimhangaikia huyo mwanaume lakini bado akaja kumuacha tena kwa dharau na kejeli.
Baada ya kumaliza kuongea nilikaa mtaani mpaka saa nne usiku, nilirudi na kukuta mke wangu hajalala, alianza kujiongelesha na kunilaumu kuwa simjali ndiyo maana sijamuuliza hata kama kesi imeisha au anadaiwa, sijauliza makubaliano ya yeye kuachiwa kama anatakiwa kumlipa John au la.
“Wakati mnakopeshana sikuepo sasa kwanini unataka kunishirikisha sasa hivi kwenye kulipana. Mtajuana wenyewe, kama mlivyokopeshana basi mlipane hivyo hivyo bila kunishirikisha mimi, na kesho nataka kadi yangu ya gari kama si hivyo huyo mtu wako namfunga na usidhani kama kituo cha polisi kipo kimoja!”
Niliongea maneno ambayo yalimshtua sana mke wangu, tangu kujuana hakuamini kama naweza kumjibu vile, alijua kuwa mimi ni mtu tu wa kumsikiliza na kufanya kile anachokitaka yeye. Nilipanda kitandani na kulala huku mke wangu akiendelea kuongea, alilalamika sana labda mimi namsaliti lakini wapi sikujali. Asubuhi nliliandaa kwajili ya kazi, nilimuacha mke wangu nyumbani, nilimpa Shilingi elfu tano.
“Yanini?” Aliniuliza.
“Kwaajili ya mboga, au hamli leo?” Nilimuuliza huku nikitaka kuirudisha mfukoni, aliniangalia kwa mshangao.
“Elfu tano? Sasa hiyo inatisha nini?” Aliniuliza nilimuangalia kwa mshangao na kumuambia.
“Kila kitu kipo ndani, kama elfu tano huwezi kununua mboga zikatutisha basi toka katafute kazi, sina pesa ya ziada.” Niliiweka juu ya meza na kuondoka zangu nikimuacha mke wangu kaduwaa.
Alilalamika sana lakini hata sikumsikiliza, nilitoka, nikiwa kwenye gari simu yangu iliita, alikua ni Joani akinisalimia tuliongea kidogo na kuagana. Kusema kweli nilijisikia vizuri, nilipokata simu nilitamani kumpigia tena simu ili kuendelea kusikia sauri yake, lakini nilijizuia mpaka mchana, nikitaka asiwe wakwanza kunipigia nilimpigia na baada ya kuongea bila kupanga nilijikuta namuuliza.
“Vipi jioni unaweza kuwa na muda, natamani sana kuonana na wewe, last time najua nilikukwaza, nahitaji kuomba msamaha uso kwa uso…” Nilimuambia, moyo ulikua unadunda nikiwaza kama atakubali ombi langu au la?
***
Ninakua na wateja wengi hivyo kumjibu kila mtu anayenitumia SMS ni ngumu, kama unahitaji ushauri ni lazima uwe umenunua vitavu vyangu, kama unahitaji ushauri wa mahusiano ya kawaida nilazima uwe umenunua Kitabu cha “Ndoa yangu Furaha Yangu” Bei yake ni Shilingi elfu kumi tu!
Kama ushauri unahusiana na mapenzi lakini unagusa upungufu wa nguvu za kiume wa mwenza wako au wewe mwenyewe mwanaume au maumbile madogo na namna ya kumrishisha mwanamke basi Kitabu ni “MWANAUME” bei yake ni Shilingi elfu ishirini.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA TANO
Ilikua ngumu sana kwangu kupata sehemu ya kukutana na Joan, mke wangu ni mtu anayefahamika hivyo nilijua kuwa kukaa na mwanamke sehemu yoyote basi angepata taarifa na kwa nilivyokua namjua basi angekuja na kunifanyia fujo. Joan alikubali kukutana na mimi, aliponiuliza wapi nilishindwa kumjibu, nilimuambia tu nitaenda kumchukua kwake, alikubali ingawa sikujua kama nampeleka wapi lakini nilitaka tu kuonana naye na kuongea naye.
Jioni hata sikurudi nyumbani, nilikaa kazini mpaka muda wa kukutana na Joan ulipofika, nilimfuata mpaka nyumbani kwake, alikua shajiandaa kavaa kapendeza, aliingia kwenye gari na kunisalimia.
“Unananipeleka wapi?” Lilikua ni swali lake la kwanza mara baada ya salamu. Nilinyamaza kidogo nikitafakari kisha nikamjibu.
“Hata sijui, mimi naona kwakua ni siku yetu ya kwanza basi tuongelee hapa kwenye gari….” Niliongea huku nikitetemeka, sijui kwanini lakini nilikua ninaogopa, ni miaka kadhaa ilikua imepita tangu kuwa na mwanamke mwingine zaidi ya mke wangu.
Si kwamba nilikua sijui kutongoza, hapana, nilikua najua sana lakini nilikua na h0fu, nilijisikia sana kumsaliti mke wangu na kwa mimi kukaa na joan namna ile niliona kama usaliti. Jibu lile lilimshangaza sana joan lakini tofauti na nilivyotegemea hakupaniki, alitulia kidogo na ni kama alikua anasoma akili yangu.
“Unamuogopa sana mke wako, najua anajulikana kila sehemu lakini huna haja ya kuwa na wasiwasi.” Aliniambia, nilinyamaza kidogo, nikiwaza kitu cha kumjibu, niliogopa na kuna wakati hata sikujiona mwanaume.
“Mwanaume gani mimi namuogopa mwanamke namna hii?” Niliwaza, Joan ambaye alikaa kiti cha abiria alipitisha mkono wake na kunitengeneza shati, alitoa kitambaa na kunifuta jasho, pamoja na kuwasha AC mpaka mwisho lakini nilikua nikitokwa jasho kama vile nimetoka kukimbia.
“Usiogope, acha kupaniki basi, washa gari nitakupeleka sehemu ambapo mke waho hajulikani kabisa. Nilimuuliza wapi lakini hakunijibu, aliniambia atanielekeza, niliwasha gari na kweli safari ilianza, tulikua tunaelekea maeneo ya Mbagala, tulienda mpaka Chamanzi.
Alinipeleka mpaka nyumba moja kubwa tu nzuri, ilionekana mpya ni kipindi kile chamanzi haijajengeka, ndiyo ilikua inaanza kujengeka taratibu. Aliniambia nipaki gari, nikijua ni nyumba ya kulala wageni alitoa funguo zake na kufungua mlango. Aliniambia niingie, huku nikiwa na wasiwasi nilimuuliza pale ni wapi aliniambia nisiogope niingie. Ilikua nyumba nzuri ya kisasa na kule ndani kulikua na karibu kila kitu, lakini kila kitu kilionekana kama ni kipya kama hakuna mtu anakaa.
Kwa hofu nilimuuliza ndipo aliniambia kuwa pale ni kwake, ni nyumba alikua anajenga muda mrefu, ishakamilika lakinia nataka mpaka aweke fenicha zoet mpya ndipo ahamie. Nilijisikia huru kidogo kwani niliona kama ni sehemu salama. Alinikaribusha tukaongea na kuongea, nilijua kuwa alikua hajaolewa lakini alikua na mtoto mmoja wakike ambaye alizaa na mwanaume mmoja ambaye aliachana naye kwakua alikua akimpiga sana, alikua akiishi naye kama mke na mume lakini ndugu zake walipoona kuwa anamnyanyasa walienda kumchukua ingawa yeye alikua hataki.
Baada ya hapo ndipo alitafutiwa nafasi jeshi la Polisi, ambapo ana miaka kama saba na kwa wakati huo alikua hana mwanaume yeyote. Mtoto wake haishinnaye anaishi kijijini na Mama yake lakini ana mpango akishahamia katika nyumba yake kwenda kumchukua. Siku hiyo tuliongea tu bila kufanya chochote, nikiwa pale mke wangu alikua akipiga simu sana lakini sikupokea, nilikaa mpaka saa nne usiku, tukarudi nikamuacha kwake na mimi kurudi kwangu.
Nilimkuta mke wangu ameshalala, niligonga mlango na binti wa kazi ndiyo alinifungulia. Chakula kilikua mezani huku mke wangu akiwa kalala, nilikua nimeshiba lakini nilitaka kula nyumbani kidogo ili kuepuka shari, kuangalia chakula ilikua ni wali kuku. Nilishtuka kidogo kwani ndani niliacha elfu tano na hakukua na mboga, nilitaka kula nikashindwa, nikarudi ndani kulala, ile kuingia tu mke wangu alishtuka, akanyanyuka na kunisalimia, kisha akaelekea chooni.
Cha ajabu hakuniuliza kwanini nilikua nimechelewa, hakuniuliza kama nilikua na nani! Nilisubiri labda akiwa katika chooni kama mimi angelalamika lakini wapi, alipanda kitandani na kujifunika. Simu yangu iliita, alikua ni Joan, kwa makusudi nikijua kuwa mke wangu atasikia niliipokea na kuongea kidogo, mke wangu alisikia lakini hakuniuliza chochote. Nilijikuta nalala kwa shida nikiwaza ni kwanini mke wangu haniulizi chochote, labda hanipendi, labda ana mwanaume mwigine, labda anataka kuniacha na mawazo mengine mengi mengi lakini sikua na jibu.
Kwakua sikupata kabisa usingizi asubuhi nilikua wakwanza kabisa kuamka, nilijiandaa kwaajili ya kwenda kazini, mke wangu alikua bado kalala, hata nilipokua namuaga kuwa naondoka hakugeuka, nilipokua nampa pesa hakugeuka aliniambia.
“Mimi nimechoka, weka hapo kwenye meza!”
“Hutaki hata kujua nimekuachia Shilingi ngapi?” nilimuuliza huku nikiwa nimeshikilia shillingi elfu tano yangu mkononi, niliona kama vile namkomoa kumuachia pesa kidogo.
“Unafikiri hata najali, mimi hata usipoacha pesa ya kula nitakula tu. Umenikuta mtu mzima nakula, kama hukunilisha utotoni huwezi kunitisha na pesa ukubwani, hata mimi najua kutafuta.”
Alinipa jibu ambalo mpaka leo linanichoma, alinivunja nguvu kabisa, nilisi kama kuna mtu kanikatakata vipande vipande na kuvichemsha. Sikuweza kuendelea kuongea, niliacha ile eelfu tano mezani na kuondoka zangu. Nikiwa njiani Joan alinipigia simu, aliniuliza kama nimeshafika kazini nikamuambia bado. Alianza kunishukuru kwa siku ya jana alianza kuniambia namna alivyofurahia lakini sikujali.
“Niko barabarani naendesha, naomba nikutafute baadaye.” Nilimuambia nakukata simu bila hata kusubiri jibu lake, kichwani nilikua nimechanganyikiwa, nilikua na mawazo mengi sana kuhusu mke wangu hasa kwanini hajali mimi kuchelewa au kumuachia pesa kidogo.
****
Kila siku jioni nilikua nikimtafuta Joan, sikufanya siri tena, ni kama nilitaka mke wangu kujua, sikua nikifanya kama kujifurahisha bali ni kamja nilitaka kumtia wivu, nilikua na maumivu makali moyoni kiasi kwamba niliamini kwa mimi kuachepuka au kutaka kumuonyesha mke wangu kuwa nachepuka basi ingesaidia kumuumiza kama nilivyokua naumia. Nilikutana na Joan sehemu za wazi kabisa tena sehemu ambazo nilijua kabisa kuwa ni lazima mke wangu angesikia na hata kuja kutufumania.
Lakini haikutokea hivyo, pamoja na kuchelewa kurudi, wakati mwingine kurudi asubuhi lakini mke wangu hakuwahi kuniuliza kama nimetoka wapi, hakuwahi kuniyonyesha kisirani kama kile ninachomuonyesha kitu ambacho kilizidi kuniumiza.
“Mbona hauko sawa, una uhakika unataka kufanya hiki kitu?” Joan aliniuliza, ilikua ni siku ya jumamosi, nilimpeleka joan Bagamoyo, baada ya kuwa naye kwenye mahusiano kwa meizi sita na baadhi ya ndugu zake kunifahamu nilikua tayari kufanya naye mapenzi, katika kipindi chote hicho tulikua kama marafiki tu.
Ingawa alitaka sana lakini nilijikuta nakataa, nilijizuia na nilijiona kama siko tayari.
BONYEZA HAPA UPATE VICHEKESHO KUPITIA SIMU YAKO
INAENDELEA

No comments