Simulizi: Rama sehemu ya pili (02)
“Ametoka tangu mchana, hivyo unakata kuniambia kuwa huyu mtoto tangu mchana hajanyonya?” Nilimuuliza binti wa kazi, hakujibu, alitingisha kichwa kukubaliana na mimi.
“Hajanyonya, nimejaribu kumpa uji lakini amekataa,a likua analia tu…” Umeniulia mwanangu wewe! uji kwa umri huu, hivu una akili za wapi wewe? Umetoka wapi wewe hujui kwamba mtoto cmhanga hatakiwi kupewa chochote?” Nilimuuliza kwa hasira huku nikimnyang’anya mtoto, alikua kachoka sana, aliionekana kulia mpaka kukaukiwa, nilichanganyikiwa sikujua hata nifanye nini.
“Hakuna maziwa ndani?” Nilimuuliza,
“hapana, niliweka kwenye uji wa mtoto lakini Akaka….” Sikutaka hata kuendelea kumsikiliza, nilitoka nnje kwa majirani kuona kama kuna mtu mwenye maziwa, ilikua usiku lakini Mama mmoja alinipa, alitaka kudadisi ili kujua kilichokua kimetokea lakini sikumpa nafasi, nilichukua maziwa na kwenda kuyachemsha kisha nikayapooza na kumpa mtoto. Lakini hakunywa, aliendelea kulia kwa sauti ya kukauka huku mwili wake ukianza kubadilika rangi na kuwa kama wa bluu.
Niliogopa na kuhisi nishamuua mtoto, akili ilifanya kazi hatakaharaka nikakumbuka kuwa nilimpa kwa kijiko, nilichukua chupa ya kumnyeshjea maziwa nikampa akawa ananyonya sema kidogo sana, alikua akijirahidi na ilionyesha kama vile anajilazimisha. Hakua na nguvu, alijitahidi sana lakini alishindwa, nilijua kama nampoteza nilichukua simu na kuanza kumpigia mke wangu ili kujua kama yuko wapil nilipiga sana lakini simu yake ilikua haipatikani.
Niliamua kuwapigia rafiki zake ili kuwauliza, kuna marafiki ambao nilijua fika ni lazima watajua alipo. Nilipiga na baadhi walipokea ila walijifanya kuwa hawajui, niliwaambia kuwa sijali kama anachepuka au la ninachoitaka kujua ni alipo kwani mtoto alikua anaumwa. Walinielekeza sehemu ya mwisho walipokua wamemuona, nilimchukua binti wa kazi, nikamuambia ampakate mtoto kisha mimi nikaanza kuzunguka Baa moja hadi nyingine kumtafuta mke wangu. kila nilipofika nikiulizia naambiwa aliondoka na mwanaume flani labda mcheki sehemu flani.
Nilizunguka baa kama tatu hivi na zote jibu lilikua ni lile lile, kila aliyenmiona alihisi kama nimechanganyikiwa lakini mimi sikujali, nilikua naangalia hali ya mwanangu hivyo wivu niliweka pembeni. Nilifika baa moja ambayo ilikua na Gest ndani yake, nilimuulizia na kweli niliambiwa alikua pale lakini alitoka, nilipouliza alipokua ameelekea hakukua na jibu la kueleweka. Nilitoka lakini wakati naondoka kuna gari ilikua imesimama sehemu ya parking, ilikua inatikisika na nilipoiangalia nilikua kama naifahamu.
Mara kadhaa nilishawahi kuiona nyumbani kwangu, kipindi hicho mke wangu akiwa mjamzito ilikua inakujaga kujaga sana. Ilikua ikija na rafiki yake mmoja wakike na mara nyingine mke wangu alikua anakuja akiiendesha yeye. Nilihisi kitu nikiamini labda mke wangu atakua ndania u huyo rafiki yake niliisogelea ile gari, niligonga kwenye kioo cha mbele lakini haikufuunguliwa, ilikua inatikisika tu, sijui kwanini lakini kuna kitu kiliniambia kuwa nifungue mlango na kweli nilifungua.
Katika siti za mbele hakukua na mtu lakini kule nyuma kuna watu walikua wamelala uchi wanafanya mapenzi, sikua, ingawa ilikua ni usiku lakini mwanga wa taa ya ile Gest ulikua ukiwapiga hivyo niliweza kumuona mke wangu akiwa na mwanaume mwingine. Walikua wamekumbatiana wakinyonyana ndimi huku huyo mwanaume akiwa bize kumvua mke wangu, naye pia nilimfahamu kwani nilishamuona mara nyingi akiwa na huyo rafiki wa mke wangu aliyekua anakuja na lile gari na nilijua kuwa ni mchumba wake.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SEHEMU YA PILI
(ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA; Rama anatoka kazini, mkewe ambaye ana mtoto mchanga haonekani, mtoto hajanyonya na kaanza kubadilika rangi. Rama anaamua kumtrafuta mke wake, anazunguka kwenye mabaa bila mafanikio, anafanikiwa kumkuta mkewe akiwa ndani ya gari na mwanaume mwingine wamekumbatiana, je Rama atafanya nini? ENDELEA… Kama hukusoma sehemua ya Kwanza Bonyeza hapa @iddi makeng )
Hawakuniona hata nilipofungua mlango, walikua bize na mambo yao, hasira zilinipanda, nilikua nimeshika simu yangu mkononi, niliirudhsa ili kumpiga yule mwanaume lakini kwa bahati mbaya ilimpiga mke wangu kichwani, alipiga ukulele.
“Mama nakufaaaa!” Wote walishtuka walipoangalia nilikua ni mimi. Mke wangu alionekana kulewa sana, lakini yule mwanaume yeye alionekana kama hajalewa, ile kuniona alipaniki, walikua bado hawajavua nguo, mimi nilikua nimefungua mlango wa mbele.
Aliponiona alifungua mlango wa nyuma na kumvuta mke wangu kama mzigo mpaka nnje, mke wangu alipiga kelele za malalamiko kuwa anamuumiza lakini yule mwanaume hakujali, nilipoona vile nilitoka kule mbele na kumfuata kwa nyuma.
“Broo mambo gani haya tunafahamiana, inamaana hujui kama huyu ni mke wa mtu na ana mtoto mchanga?” Nilimuuliza huku nikimkunja kutaka kupigana naye, kwa kumuangalia nilikua nammudu, naye alinishika lakini kabla ya kuanza kupigana Binti wangu wa kazi alikuja, yeye ndiyo alikua kamshikilia mtoto.
Mtoto alianza kulia tena, nilikumbuka kilichokua kimenipeleka pale, nilimuachia yule Kijana na kumfuata mwanangu, pale pale alipata upenyo, akaingia kwenye gari na kuondoka zake. Nilibaki mimi, mke wangu binti wa kazi na mwanangu. Nilitamani kumpiga makofi mke wangu lakini sikua na ujasiri huo, alikua kakaa chini huku kashika kichwani anaugulia maumivu ya ile simu ambayo niliirusha kwa nguvu.
“Umeniumiza, mimi nilishasema kuwa sipigwi, kama umenichoka bora uniache, kwetu sijaua kwanini unipige. Kwanza mambo gani ya kufuatana fuatana mpaka huku sehemu za sitarehe!”
Mke wangu alilalamika, niliinama na kumshika ili kutaka kumuingiza kwenye gari lakini hakutaka. Alikataa katakata huku akilia kuwa nimempiga.
“Mimi siendi ppopote, kwanini umekuja na kunipiga, kwani siruhusiwi kutoka, tatizo lako una wivu sana, wewe umenikuta na mwanaume badala ya kuuliza kwanza kuwa ni nani na tulikua tunafanya nini unaanza mambo yako, unaanza kunipiga!” Aliongea kwa hasira huku akijilegeza na kujilaza chini kwa kugalagala, hasira zilinipanda lakini sikuweza kumpiga, nililazimika kumbembeleza ili angalau anyanyuke pale, mvua ilikua imekata lakini chini kulikua na matope, mke wangu hakujali alijilaza na kujigalagaza.
Alianza kupiga kelele, nikiona kuwa atanijazia watu nilijikaza kiume nikamshika vizuri na kuanza kumkokota mjpaka kwenye gari, nilimlazimisha kuingia na kumkalisha siti ya nyuma, niliingia kwenye gari na kumkabishi mtoto, sikujali matope, nilimvua nguop ya juu na kumlazimisha kumnyonyesha mtoto. Nilifanya hivyo mbele ya dada wa kazi, sikujali chochote, mke wangu alikua kalewa sana ni kama alikua hatambui kama ana mtoto, huwezi amini nilipomvua sidiria ilikua imeloa maziwa, sijui ni kwa namna gani alikua akinywa katika hali ile kwani maziwa yalikua yanatoka yenyewe.
Nilimsaiduia kubeba mtoto kwa kumuwekea kifuani na huwezi amini mtoto alipogusishwa tu titi la Mama yake alianza kunyonya mwenyewe, alinyonya bila kupumzika na aliposhiba alilala palepale. Nilimshukuru Mungu nikawasha gari na kumchukua mke wangu mpaka nyumbani. Kwa namna alivyokua amechafuka nisingeweza kumuingiza ndani, nilimuweka kibarazani, nikaenda kuchukua khanga, nikamvua nguo na kumfuta kidogo kisha nikaingia naye mpaka bafuni, nilimsafisha vizuri na wakati huo ndiyo kama alikua amepata fahamu kidogo.
Alishangaa kujikuta yuko nyumbani, alianza kulalamika kuwa kichwa kinamuuma, ni kama mtu ambaye fahamu zilikua zikimjia na kuondoka kwani aliniuliza kuwa alifikaje pale lakini wakati mwingine alinilaumu kwa kumpiga simu. Sikutaka kugombana naye usiku huo, baada ya kumsafisha nilimrudisha kitandani ili apumzike. Alipanda kitandani na dakika mbili tu tayari alishalala. Nilibaki namuangalia kwa hasira, nilitamani hata kumuua, kichwa kilikua kinaniuma, mishipa ya kichwa imenisimama huku kila dakika nikimuomba Mungu anijaalie nisije kumuua mke wangu kwani nilikua naumia sana.
Nilipitiwa na usingizi lakini nilikuja kushtuka kwenye saa tisa na nusu hihvi, mke wangu alikua kaamka na alikua akitapika, alitapikia kitanda kizima huku akijifuta kwa mashuka. Nilitaka kumnyanyua mpaka bafuni lakini hakutaka, alitapika sana vitu vinanuka pombe sijui alikua kanywa nini kwani haikua kawaida yake, ni mnywaji mzuri na hata siku moja nilikua sijawahi kumuona akitapika vile. Alitapika sana na abada ya kumaliza alijifuta na shuka kisha akatoka na kwenda kulala chumba kinginge akiniacha mimi pale ndani na matapishi yake, sikuweza kulala nilitoka na kulala sebuleni.
Asubuhi niliamka mapema sana, ilikua ni siku ya kazi, nilitoa mashuka na kufanya usafi ndani, yeye bado alikua kalala, niliyaloweka mashuka nikamuangalia mtoto alikua anaendelea vizuri. Kabla ya kuondoka nilimuamsha, alikua kachoka sana hangover bado inamsumbua.
“Mambo gani ya kusumbuana asubuhi?” Aliniuliza huku akijigeuzia upande mwingine.
“Hivi wewe hukumbuki ulichokifanya?” Nilimuuliza, bila kunyanyuka alinisonya na kujifunika shuka. Sikutaka kuharibu siku yangu, nilitoka nikaingia kwenye gari na kuondoka kwenda kazini, mchana kutwa nilikua napiga simu kwa dada wa kazi ili kujua kama yuko nyumbani na alikua amemnyonyesha mtoto.
Aliamka kama hakuna kitu kilichokua kimetokea na kuanza kumtukana binti wa kazi kwa kuacha mashuka yenye matapishi, binti wa watu alilazimika kufua huku yeye akitoka kunywa supu. Mchana nilirudi kumuangalia mtoto, alikua vizuri kachangamka, sikutaka kuliongelea lile swala na yeye alikaa kimya tu bila kuongea, alinichangamkia kama vile hakuna kitu kilichokua kimetokea, alikua kachangamka na nikiwa hapo rafiki yake mwingine alikuja. Wakati naondoka nilimuita ndani na kumuambia siku hiyo sitaki atoke kabisa na kama akitoka basi atanitambua.
“Utanifanya nini? Nikutambue wewe kama nani?” Alinijibu kwa dharau, nilijikuta napandwa na hasira na kumtandika makofi mawili. Yalikua ni makofi madogo lakini alianza kupiga mayowe huku akijigaragaza chini, rafiki yake bila kujali kuwa ni kwangu aliingia mpaka chumbani eti anataka kunishika kwakua nampiga rafiki yake, alinikuta nimesiomama pembeni kabisa namuangalia anavyogalagaza, alitaka kuongea lakini kwa namna nilivyomuangalia alinyamaza kimya. Sikutaka kuendelea kubaki pale nilitoka na kurudi zangu kazini kuendelea na mambo yangu.
Kama nusu saa hivi baada ya kufika kazini nilipigiwa simu, ilikua ni namba ngeni, nilipokea nikidhani ni mtu anahitaji huduma lakini nilishangaa na kutana na matusi, kelele na vitu vingine vingi vya kukera.
“Kama mwanangu huwezi kumlea, kama unaona tabia zake zimekushinda basi nirudishie. Ulimchukua kwangu mzima, hana kovu sasa unataka kuniulia mwanangu kisa nini? Si ulimkuta anakunywa pombe ndiyo nini unataka aache, mtu kanywa bia mbili unataka kumuua!” Ingawa namba haikua yake lakini ilikua ni sauti ya Mama mkwe wangu, sikutaka kumjibu kwani niliona kama nitamkosea heshima.
INAENDELEA
BONYEZA HAPA UPATE MAKALA MBALIMBALI ZA

No comments