Simulizi: Rama sehemu ya sita (06)
Kwakifupi ni mtu ambaye alikua na pesa zake tena kijana kabisa, niliamua kumfuata ofisini kwake na kumuambia aachene na mke wangu. Alikua ni kijana mtulivu tu ambaye alionekana kutoka kwenye familia bora. Yeye na mke wangu walikua kwenye mahusiano kwa miezi na alishangaa sana kusikia kuwa mke wangu kaolewa kwani alimuambia kuwa aliachana na mpenzi wake miaka minne kabla kutokana na kumpiga mara kwa mara hivyo alihitaji mwanaume muaminifu. Alishangaa zaidi nilipomuambia kuwa mke wangu nilikua nikiishi naye kwani katika hiyo miezi sita alishaenda mara nyingi kwa mke wangu na kulala kwake.
Aliponielekeza sehemu aliyokua kapelekwa niligundua kuwa ni nyumbani kwa Mama yake mdogo na mke wangu na siku zote ambazo mke wangu alikua akimkubalia kwenda kulala au mke wangu kwenda kwake kulala zilikua ni siku ambazo nipo safari kikazi. Niliona kabisa kachanganyikiwa na hakutaka kukubaliana na ukweli.
“Kwahiyo unataka kuniambia kuwa hata mimba aliyonayo si yangu?” Aliniuliza swali ambalo mimi lilizidi kunichanganya, sikua najua kuwa mke wangu ana mimba. Lakini sikutaka yule kijana kujua kuwa mimi sijui, nilitaka kuzidi kumchanganya.
“Mimba ni yangu, sijui kwanini anataka kuniacha lakini nimeona kuwa huwezi kumuoa mke wangu.” Nilimtolea picha zetu za harusi, picha nyngine za kawaida na picha za m,toto wetu.
“Hapana, yule mwanamke hajazaa, haiwezekani!” Alijiongelesha wakati anaangalia picha za mke wangu. alionekana kuchanganyikiwa, alichukua simu kumpigia mke wangu lakini haikupokelewa, baada ya kuona haipokelewi aliniambia.
“Nashukuru kwa kunitafuta lakini mimi nitafanya uchunguzi wangu mwenyewe, haiwezekani yeye kuwa na mwanaume mwingine. Ananioenda sana na alikua tayari kubadilisha dini uili nimuoe, wewe unafikiri nitawaambia nini wazazi wangu! kwetu wote wanamjua na wanampenda sana.”
Niliona kabisa kuwa hatuwezi kuelewana, niliondoka nikijua kabisa kuwa hawezi tena kumuoa mke wangu. Nilipotoka tu katika ile ofisi nilianza kumtumia meseji mke wangu. “Si ulikua unajifanya kuwa unaweza kunikomoa sasa nishamuona mtu wako nishakuharibia…tuone kama sasa utaolewa…nakuambia lazima utaachika na hiyo mimba nataka uitoe siwezi kulea mtoto haramu….” Kwa hasira nilijua kuwa nimemkomesha mke wangu nilianza kutuma meseji nyingi za matusi nikiwa kama namshushua mke wangu.
Hapo nadhani ndipo nilipokosea kwani mke wangu alipojua nimafanikiwa kumpata mchumba wake alimpigia simu huku akilia, alijifanya kuwa hajui kinachoendelea ndipo alianza kumlalamikia akimuambia kuwa ni bora waachane. Niliajua hayo siku iliyofuata, nikiwa ofisini sijui hili wala lile walikuja watu wawili, walivbaa kiraia lakini walijitambulisha kama askari, wakanitilea vitambulisho na kuniomba tuongozane nao, hawakuniambia kosa langu lakini walinipeleka mpaka kituni.
Nilipofika nilikutana na yule mchumba wa mke wangu, yeye ndiyo alifungua kesi kuwa nimemtishia mchumba wake. Madai yake nikuwa mke wangu alimpigia simu kuwa nimetumia meseji kuwa hawezi kuolewa, atoe mimba na nimemharibia kwa mchumba wake. Alinionyesha meseji, nilijaribu kujielezea lakini nilinyang’anywa simu na kweli walipoangalia nilionekana nimezituma mimi zile meseji.
“Ni kawaida yake, alishaachwa miaka minne iliyopita lakini kila siku anamharibia binti wa watu, yeye kashaoa ana maisha yake lakini kila binti akipata mchumba anaenda kumchafulia, nampenda sana mchumba wangu siwezi kumuacha kwakua tu umesema.”
Hapo ndipo nilijua kuwa kweli nimeharibu, kutuma meseji na simu za vitisho ingeonekana kuwa mimi nina matatizo.
“Kafoji mpaka vyeti vya ndoa ili tu kumaharibia mtu.” Aliendelea kuongea, alikua na hasira na kwakua alikua na pesa niliwekwa ndani, nilikaa huko kwa siku tatu. Lakini mke wangu hakurudi Dar, hakutaka kuonekana, hakutaka kunigungulia kesi na kwakua yeye ndiyo alikua katishiwa maisha basi yule mchumba wake alinitoa lakini kwa onyo kuwa nisimsumbue tea mchumba wake, alinitishia kuwa hata kama mke wangu hataki kufungua kesi na kunifunga lakini kama nikimpigia simu au kumtishia tena maisha basi atanipoteza kwani mke wangu kabeba kiumbe chake tumboni.
Pamoja na vitisho vyote hivyo lakini sikukoma, niliendelea kumtafuta mke wangu ila hakua hewani, hata ndugu zake walikua hawapatikani ndipo nikajua tayari nimeshaachwa. Nilikaa mwenye kwa mwezi mmoja mpaka nilipokutana na Joan mjini, tulisalimiana, aliniona nilivyokua nimenyong’onyea. Aliniuliza sababu lakini sikutaka kumuambia, alishaniacha hivyo sikutaka aingilie maisha yangu tena. Lakini kumbe alikua anajua, alikua anajua kuwa nimepelekwa Polisi na mwanaume ambaye anataka kumuoa mke wangu. tuliongea kidogo, sikutaka kupoteza muda naye, niliaga na kuondoka.
Lakini jioni Joan alikuja kwangu, nilimkaribisha vizuri tu ingawa sikua katika Mood kabisa.
“Kuna kitu nilitaka kukuambia muda kidogo lakini nilisita, nilijua utarudiana na mke wako hivyo sikutaka kuumizwa.” Alianza kuongea, mimi nilimsikiliza tu, akili yangu haikua pale kabisa, nilikua na mawazo mengi kuanza kumuwaza na maneno yake.”Nina mimba yako, ina miezi mitatu, nilijua muda lakini nilikua sijapanga kama nizae au la?” Aliniambia, nilikua kama sijamsikia mpaka aliporudia tena, nilimuambia hakuna shida hata mimi nahitaji mtoto.
Kusema kweli sikua na hisia naye lakini baada ya kuniambia kuwa ana mimba yangu niliona nibora kubaki naye kuliko kuendelea kumsubiria mwanamke ambaye hanitaki. Tulirudisha tena mahusiano na wakati huu nilijitahidi sana kukata mawasiliano kabisa na mke wangu, siku mtafuta tena niliacha aendelee na mwanaume wake pamoja na uongo wake. Ilipita kama miezi mitatu hivi, muda mwingi nilikua kwa Joan, nyumba yangu ilikua na kumbukumbu nyingi za mke wangu na kwakua sikua na mfanyakazi nilikua kama nimehamia kwa Joan ingawa bado nilikua naenda enda nyumbani kwangu.
Siku moja nikiwa kazini nilipokea simu, ilikua ni namba ngeni, nilipoipokea ilikua ni sauti ya mke wangu. kitu kilinipiga Paaa! Nilitamani sana kumkatia simu lakini sikuweza, kuna kitu nilitaka kujua, kuna kitu kiliniambia kuwa msikilize huyo mtu.
“Mbona hauko nyumbani, nimekuja tangu jana lakini hujarudi nyumbani, kwanini unaiacha nyumba peke yake?” Mke wangu aliniuliza baada ya salamu ambayo hata sikuiitikia.
“Nyumbani? Unafanya nini nyumbani kwangu? wewe si ulijipa talaka mwenyewe, si ulisema kuwa hujaolewa sasa kwa taarifa yako hupati chochote, kama ni mali unataka basi tutamalizana mahakamani, sikupi kimya kimya ili huyo mwanaume wako unayemdanganya ajue ushenzi wako!” Nilimuambia kwa hasira, kwa namna nilivyokua namjua mke wangu nilijua kuwa asingeweza kuniacha kwa amani, angetaka kuchukua baadhi ya vitu hasa nyumba ambayo ilikua na jina lake.
“Nani kakuambia ana shida ya mali zako? Njoo nyumbani tuongee!” aliniambia na kunikatia simu.
RAMA; MAMA YENU AKIRUDI NAOMBA MUMUAMBIE KUWA MIMI NIMETOKA!—SABA
Nilirudi nyumbani nikiwa kama mtu aliyechanganyikiwa, akili yangu ilikua inawaza mambo mawili, jambo la kwanza nikifika nimfukuzie mbali na kuendelea na maisha yangu na jambo la pili nilitaka sana kujua sababu ya yeye kuja kwangu, nilitaka kumuacha palepale nyumbani ili aone namna nilivyonafuraha na Joan.
“Kwanini hukai nyumbani? Umeamua kuitelekeza nyumba?” Mke wangu aliniuliza baada tu ya kuingia ndani. Tumbo lake lilikua kubwa, ni muda nilikua sijaonana naye hivyo sikua na uhakika kama kweli ana mimba au la.
“Unafanya nini nyumbani kwangu?” Nilimuuliza huku nikikaguiakagua vitu kana kwamba naangalia kuona kama nimeibiwa au la? Hakujibu chochote, alinyanyuka na kunifuata kutaka kunikumbatia.
“Inamaana hujanimiss, hujanikumbuka, yaanui baada ya kufurahi kuwa mke wako karudi wewe unaanza kuuliza nimefuata nini? Si nimekuja kwangu jamani…” Aliniambia huku akinishika akilazimishia kunikumbatia, nilitamani kumsukuma lakini nilishindwa, bila kumgusa nilimuacha anikumbatie anavyotaka. Niliuhisi mwili wake wa moto, ghafla nilikumbuka kipindi chake cha ujauzito, namna nilivyokua napenda mimba yake, namna alivyokua amebadilika na kuwa mke mwema.
“Hapana, wewe una mume wako, nilishakupa talaka, sikutaki tena, mimi nina maisha yangu, nina mtu wangu na nampenda sana.” Nilimuambia, yeye hakujali, aliendelea kunishika, hasira zilinipanda bila kujijua nilijikuta namsukumia pembeni. Alidondoka kwenye kochi na kuanza kupiga keleel.
“Mamaaa! Uaniuaaaa! Unaniuaaaa!” Nilimsukuma kidogo lakini alipiga kelele kana kwamba nilikua nimempiga makofi na mateke. Alianza kulia na kulalamika kuwa nimemuumiza, alilia sana huku akiomba nimpeleke hospitalini. Kwanza nilidhani ananitania lakini baadaye niliona alikua siriasi, alikua kakasirika na alitaka kupelekwa hospitali.
Kwa uoga nikidhani kaumia sana nilimbeba mpaka kwenye gari na kumpeleke hospitalini. Kufika walitaka kumhudumia huku wakitaka kujua nini kilikua kimetokea.
“Mume wangu ndiyo kanipiga, ana mwanamke mwingine, mimi nimemfumania yeye ndiyo akaanza kunipiga, siowezi kutibiwa bila PF3!” Ghafla mke wangu alinigeuka na kuongea maneno ambayo yaliniumiza sana, nilibaki nikiwa nimeduwaa kama mtu aliyechanganyikiwa.
“Nikweli Baba, umemfanya nini mke wako?” Daktari aliniuliza, nikijua kama sijafanya kosa lolote nilimjibu.
“Hapana, mimi sijampiga, tulikua tunabishana nimemsukuma tu kidogo….”
“Hii si kidogo, inaonekana ana hali mbaya na hii ni ishu ya Polisi!” Daktari aliongea, nilikua nimejichanganya mwenyewe kwani nilikubali kumsukuma.
“Mke wangu acha mambo yako! Hujaumia chochote nyanyuka, kama ndiyo unataka nikusamehe namna hii basi umeharibu kabisa!” Nilimuambia mke wangu kwa hasira huku nikijaribu kumnyanyua alipokua amelala, baada ya kunisingizia kuhusu kumpiga na kumuumiza nilijua fika haumwi popote bali alikua anaigisa, sikujua sababu za yeye kufanya hivyo lakini sikutaka kufungwa kwaajili yake, nilikua najua connection aliyokua nayo Polisi hivyo niliona kama nikipelekwa basi itaniharibia sana.
“Ananipiga! Ananipiga! Nisaidieni ataniua!” mke wangu alianza tena kupiga kelele, nilitambua kosa langu na kumuachia, lakini kwakua nilikua nimemuinamia yeye ndiyo akanishika kama ananikumbatia huku akipiga kelele nimuachie. Kuona vile nilimshika kumsukuma pembeni hivyo watu kuanza kuona kama vile nilikua nampiga na kuja kunishika. Watu walijaa na kuanza kunitukana kuwa nampiga mwanamke mjamzito, maneno yalikua mengi, nikashikwa na walinzi na kufungiwa stoo mpaka Polisi walipokuja na kunichukua. Sikujua kilichoendelea mpaka jioni nilipotolewa, Joan alipata taarifa za mimi kukamatwa kwakua alikua akifahamiana na baadhi ya atu akafanya mpango nikaachiwa.
Sikurudi nyumbani siku hiyo, nilienda moja kwa moja kwa Joan na kumuambia kitu kilichotokea. Alinipa pole na kuniambia kuwa atahakikisha ile kesi inapotea, siku iliyofuata nilipigiwa simu kuwa nahitajika Polisi, nilienda na kuambiwa kuwa mke wangu kaamua kufuta kesi ila natakiwa kurudi ustawa wa jamii kuongea na kama hatutaelewana basi kesi itaendelea, mke wangu alisema kanisamehe lakini nikaonywa kuwa kama nikipiga tena basi nitaozea jela. Tulienda ustawi wa jamii nikaeleza ya kwangu na mke wangu naye akaeleza ya kwake.
Alisema nilimrudisha kwao bila sababu yoyote, nikamfukuza na mimba yake huku mimi nikiondoka na kuishi na mwanamke mwingine ambaye ana mimba yangu. Niliulizwa na kukataa nikawaambia kilichotokea kuhusu mke wangu kutaka kuolewa na mwanaume mwingine na kujipa talaka mwenyewe. Niliulizwa ushahidi sikua nao nikaulizwa kama kweli nina mwanamke mwingine nikakubali lakini nikiwaambia yeye ndiyo aliondoka kwanza. Tulibishana sana ikaamriwa kuwa turudi nyumbani na kuishi kama mke na mume, nilikataa na kuwaambia kuwa kwa mambo aliyokua kanifanyia mke wangu basi siwezi kuishi naye na nitakachotoa ni talaka tu.
“Hata ukinipa talaka mimi siwezi kuondoka kwangu, siwezi kwenda kwangu na watoto wawili, yule mwingine nimemuachia Mama kwakua hutaki kumtunza, hujui mwanao anakula nini? Analala wapi? Akiumwa wala hujali! Hapana siwezi kuondoka, kama umenichoka basi utaondoka wewe lakini sio mimi!” Mke wangu aliondoka, ulizika ubishi sana lakini mwisho mimi ndiyo nilionekana kama nina tatizo na kuambiwa kama nina mwanamke mwingine basi niondoke mimi na mke wangu akashauriwa kunichukulia RB ili nisije kumsumbua kwani nilishampiga hapo mwanzo.
Sikutaka kubishana sana, niliondoka, nikachukua vitu vyangu na kuhamia kwa Joan. Mke wangu aliendelea kunisumbua kila siku kuniomba misamaha na kutaka turudiane lakini nilikataa katakata. Mpaka alipojifungua nilikua sina mawasiliano naye, sikurudi tena nyumbani na baadaye Joan naye alijifungua. Maisha yalikua ya amani kwa Joan, alipoenda uzazi kwao nilichukua hiyo nafasi kwenda kujitambulisha na kutoa mahari, nilishafanya maamuzi ya kumuoa Joan, nilishajiandaa kumpa mke wangu talaka na nilikua tayari kumuachia hata mali zote.
Mke wangu hakurudi kwa mapenzi, baada ya mimi kumfuata mchumba wake kazini na mke wangu kumshawishi kuwa mimi ni X wake mchumba wake alikua tayari kumuoa. Lakini kumbe yule mwanaume Mama yake naye ni mtu wa Tanga, ingawa alikua hajuani na mke wangu wala kuijua familia yake lakini wakati wanaenda ukweni kila kitu kishakamilika alikutana na Shangazi yake na mke wangu ambaye alisoma naye, yeye ndiyo alimpa ubuyu wote akimshangaa kwanini mtoto wake alikubalia kuoa mwanamke ambaye tayari ana ndoa mbili na watoto wawili.
Mama yake alimuuliza mwanae ambaye hakuonekana kujali, alionekana kujua lakini hakujali. Kile kitu kilimuumiza sana yule Mama hivyo akaanza kuhangaika kivyake mpaka wakaachana kabla ya kufunga ndoa. Mwanaume alizindika na kumkataa katakata mtoto, baada ya kuona kule kakataliwa ndiyo aliamua kuja kwangu akidai kuwa mimi bado nilikua sijamuacha kwakua nilikua sijampa talaka. Niliumia zaidi niliposikia habari hizo kwani nilijua fika kuwa mke wangu hakurudi kwangu kwa mapenzi au kwakua kanikumbuka bali alirudi kwakua ameachika huko kwingine hivyo nilijua hata kama nikirudisha moyo na kumrudia basi ipo siku anaweza kunigeuka.
****
INAENDELEA

No comments