Simulizi: kijiji cha wachawi sehemu ya nne (04)
Hivyo aliingia ndani..akapitiliza mpaka jikoni ambako alimwacha Makongoro akila nyama,lakini cha ajabu Mzee mwakipesile hakumkuta..Ila hakukata tamaa,haraka sana alitoka ndani kisha akazipiga hatua kufuata njia ambayo ilikuwa ikifika nyumbani kwa Mzee baluguza..ambako ndiko Makongoro alikokuwa akiishi.lakini yote kwa yote hakufanikiwa kumwona..kiukweli Mzee mwakipesile alilaani kile kitendo cha Makongoro kumtoroka,kwani aliamini kua tayali anakwenda kuhitimisha kile kitu ambacho mkuu wake wa kichawi alicho mtuma.
Upande mwingine nako,katika mapori alionekana Makongoro akatimua mbio...Mbio ambazo alikimbia bila kugeuka nyuma..Kumbe wakati mzee mwakipesile alipo muaka Makongoro kwamba anakwenda chooni kujisaidia...Huku ndani alikobaki Makongoro akiendelea kula nyama ya swala,ghafla ulipita msukule kando yake..Kitendo ambacho kilimfanya Makongoro kutimua mbio kwa kupita njia za porini kuhofia kufatwa na ule Msukule.
Hivyo mala baada kufika nyumbani,alimkuta bibi yake akimenya viazi kwa niaba ya Chakula cha usiku...Bi mazoea alishtuka baada kumwona mjukuu wake kaja hima..na hivyo akawa amemuuliza kinacho msibu,lakini cha ajabu Makongoro alitabasam..tabasam la woga kisha akasema.."Mmh hamna bibi nilikuwa nafanya mazoezi tu..siunajuwa sisi watoto tulio zaliwa na kukulia mjini??...yaani tunapenda mwili mda wote uwe umechangamka..."
Alisema hivyo Makongoro,huku akitingisha mabega yake mfano wa mtu anajiweka sawa kwa niaba ya kupigana...Lakini licha ya Makongoro kumjibu namna hiyo bibi yake,ila Bi mazoea bado alionyesha waswadi usoni mwake..Na hapo ndipo alipomuuliza mjukuu wake.."Kwani tangu Asubuhi ulikuwa wapi..maana kutwa nzima hujashinda nyumbani"
Makongoro aliinamisha uso wake chini huku akijifikilia jibu la kumdanganya Bibi yake...Na baada kulipa aliinua uso wake kisha akajibu"Nilishinda kulee kuangalia mpira.."
"Mmmh mpira??..Mpira gani ambao unachezwa kuanzia asubuhi mpaka jioni hii??...Makongoro mjukuu wangu bwana kua makini na hiki kijiji..Shauli yako"
Bi mazoea alimjibu hivyo mjukuu wake,akionekana kutolidhishwa na majibu ya Makongoro..na ndio maana akawa amempa tahadhari kuhusu kile kijiji...Tahadhari ambayo ilimjengea sintofaham kijana Makongoro..na hivyo akawa anajiuliza"Kwani hiki kijiji kikoje??...eeh na yule mtu wa kutisha nilie mwona ndani ya nyumba ya Mzee mwakipesile ni nani??..je,kwanini Babu aliamua kunikataza kuzoeana na yule Mzee mwakipesile,,Mzee ambae anaonekana ni mwema kwangu??...Dah ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya filauni..Ila najuwa ipo siku ukweli utafahamika"
Alimaliza kwa kujipa imani Makongoro,huku akiingia ndani kuchochea kuni jikoni..wakati huo kwenye mafiga kuna junguu kuu lililo sheheni viazi vitam.
******************
Naam!.Hatimae usiku uliingia...hadi saa tatu inatimia Mzee baluguza alikuwa bado hajarejea nyumbani kwake...Kitendo ambacho kiliweza kumshtua Makongoro kwani alikuwa hajazoea ile hali ya babu yake kuchelewa kurudi nyumbani..Na hivyo makongoro akawa amemuuliza bibi yake mahali alipo babu yake..Lakini cha ajabu Bi mazoea alimjibu shortcut kwa kusema.."Kwani nipo nae..??.."
Alijibu hivyo Bi mazoea,akimjibu mjukuu wake ...Ambapo Makongoro aliweza kushangazwa na lile jibu alilopewa na Bibi yake..Na ghafla alisusa kula akidai kwamba hatoweza kula bila kumwona babu yake.
Wakati huo Makongoro alipokuwa akisema hayo,tayali alikuwa amenyanyuka pole pole alianza kuzipiga hatua kutoka ndani huku akisema.."Lazima nikamtafute babu yangu haiwezekani hadi muda huu awe hajarudi nyumbani..."
Alisema hivyo Makongoro kwa sauti ya kuashilia kulia..Na punde si punde aliondoka zake..akimwacha bibi yake akimwita,lakini Makongoro hakuitika bali alizidi kuondoka.
Basi Makongoro alizipiga hatua zake,kuelekea klabuni akidhani kuwa huwenda babu yake alizidiwa na pombe..Akashindwa kurudi nyumbani...ila kabla hajafika pale klabuni,aliaskia sauti za za walevi na Nyimbo mbali mbali wakiimbi,,wakati huo sauti ya Mzee baluguza ikisika juu zaidi kuliko wengine..Na hivyo Makongoro alizidi kukazana kuelekea kule klabuni ambako ndiko kulikokuwa zikitokea zile sauti za walevi ambazo ndani yake ilisikika na sauti ya Babu yake ambae ni mzee baluguza.
Ila mala baada Makongoro kusogea kabisa jirani na kile klabu,ghafla zile sauti alizokuwa akiziskia zilipotea..Na punde si punde walitokea kundi la fisi...Fisi ambao walipiga hatua kumfuata Makongoro..Hivyo Makongoro nae baada kuona anafuatwa na kundi la Fisi,haraka sana alivua ndala kisha akatimua mbio kurudi nyumbani..wakati huo akipasa sauti ya kuomba msaada..
Basi wakati Makongoro alipokuwa akikimbia,mala ghafla alisimamishwa na mtu njiani..na hivyo makongoro akawa amesimama akijuwa kuwa huwenda yule mtu akamsaidia ..kumbe mtu aliemsimamisha hakuwa mwingine ni Mzee mwakipesile.
Na upende mwingine...Mbiyu ya kichawi ilila kijiji cha bhonde..kuashilia kuwa kuna kikao cha dhalula..na hivyo iliwalazim wachawi wote wiliokuwa na ratiba zao za kufanya mambo yao yakichawi ,kuzivunja na moja kwa moja walihudhulia kikao kile cha dhalula...Ambapo mala baada wachawi wote kukasanyika kwenye kile kikao..Walistaajabu baada kumwona Mkuu wao kuonekana kuwa na wasiwasi..hivyo walitulia kusubili kipi atakacho ongea..
Kweli mwishowe yule mkuu wa wachawi Bi kileleganya alishusha pumzi kwanza akasema .."Jamani samahani sana tena sana kwa kuharibu ratiba zenu...ila licha ya kuharibu nadhani hii itakuwa faida kwenu.."mkuu yule alikohoa kwanza,wakati huo wachawi waliokusanyika kwenye kikao wakionekana kuwa na shahuku ya kutaka kujuwa kipi kilichotokea...Hivyo mala baada mkuu kumaliza kukohoa hatimae alihitimisha kwa kusema.."leo nilipata taarifa kwamba Baluguza kafa..jamani ondoeni hiyo imani..Mzee baluguza kaonekana leo jioni Sokoni akinunua uchawi kwa yule Mzee wa kimanyema kutoka Congo..Na tayali katangaza ubaya kwa mtu alietaka kumuua..Kwahiyo habari ipo hivo,nafunga kikao maana nina safari ya kwenda Gambosh usiku huu"
Alimaliza kwa kusema hivyo yule mkuu wa wachawi,kisha akapotea.
Basi hofu kubwa..nyuso za huzuni na wasiwasi zilitanda kwa wale wachawi waliohudhulia kikao kile cha zalula..wakati huo Mkuu wa kichawi alikuwa akijiandaa kupotea maeneo yale ili akajiunge na wachawi wenzake ambao waliahidiana kukutana sumbawanga kwa niaba ya kuelekea gambosh nchini Nigeria....Lakini kabla mkuu yule wa kichawi ambae ni Bi kileleganya hajapotea anga zile za kikao,ghafla alisikika Mama chiku akimwita mkuu wake,,ikumbukwe kuwa mama chiku ndio alietaka kumuua Mzee baluguza baada kumuwekea sumu kwenye pombe.
"Mkuuu samahani kidogo" Alisema hivyo Mama chiku huku akionekana kujawa na wasiwasi...wakati huo akizipiga hatua mbele kumfuata mkuu wake ili amwambie jambo alilokuwa nalo.
"Jamani kwani kunatatizooo?...au kunajambo lingine mtaka kulisema??.."
"Hapana mkuu hakuna tatizo,ila nina jambo dogo tu naomba unasikilize" Alijibu Mama chiku.
"Anhaa sawa sungumza nikaskia.."
Bi kileleganya Mkuu wa kichawi alimpa nafasi ya kuzunguza Mama chiku..ambapo nae baada kupewa nafasi,alianza kwa kusema.."Samahani mkuu..nadhani unafaham kuwa mimi ndio muhusika wa kutaka kumuua Mzee baluguza..kwahiyo nilikuwa naomba uweze kun.." Mama chiku aliongea hivyo huku akitetemeka..Na kabla hajamalizia sentensi yake,mala ghafla hirizi ya Bi kileleganya aliyokuwa ameivaa mkononi kama saa ilionekana kuhema kuashilia kuwa anangojewa yeye pekee katika safari ya kuelekea gambosh..kitendo ambacho kilimfanya apotee akimwacha Mama chiku akiangua kilio kwani alikuwa hajamaliza kile alichotaka kuongea.
Upande mwingine nako,alionekana Makongoro akihaha kuitafutanjia ya kurudi nyumbani kwao...huku nyuma yake wakionekana fisi wengi wakimfuata..Wakati huo Mzee mwakipesile ambae alimtokea Mwanzo alikuwa tayali kapotea..alielekea kwenye kikao ambacho kilikuwa kimeitishwa na mkuu wake.
Hvyo basi wakati kijana Makongoro alipokuwa akiendelea kuhangaika bila mafanikio ya kufika nyumbani...Ghafla aliaoneka Mzee baluguza akiwa na ungo wake,,ambapo moja kwa moja alitua nyuma ya mjukuu wake ambae alikuwa kachoka baada kukimbia mbio ndefu..Na mala baada kutua aliunyoshea kidole ungo..punde si punde ukawa umepotea..kwisha kuupoteza ungo wake,,,Mzee balu alizipiga hatua zake kumfuata mjuu wake.. Hatua ambazo alikuwa akipiga moja nyingine anapotea,anaibukia mbele...hivyo hivyo mpaka akamkalibia mjukuu wake..Ambapo aliunyoosha mkono wake wa kulia juu na punde si punde kwenye ule mkono alio unyoosha kilitokea kibuyu kidogo ambacho kilikuwa na nembo za ajabu..Alicheka Mzee balu baada kukiona kile kibuyu,,wakati huo akiushusha chini ule mkono ambao ulikuwa umeshikilia kibuyu....
Na baada kuhitimisha cheko lake,hatimae Mzee baluguza alimimina unga frani kwenye kiganja uliotoka ndani ya kile kibuyu kisha akaupuliza ule unga ambapo moja kwa moja ulimkuta Makongoro..Na hivyo ghafla akawa hajielewi,,kitendo ambacho kilimfanya Mzee baluguza kumbeba na kisha kuondoka nae huku akiusifu uchawi ule alioutumia kwa makongoro kwani hakuta kujionyesha kwa mjukuu wake yeye ni Mchawi.
Basi baada Mzee baluguza kutoweka na mjukuu wake...upande mwingine wale fisi waliokuwa wakimfukuzia Makongoro ghafla waligeuka kuwa watoto ambapo waliangua kicheko kikubwa huku wakigongeana mikono na kisha kucheza michezo mbali mbali ya kitoto...kumbe hakuwa fisi bali ni watoto ambao wazazi wao wanajihusishs na masuala ya kichawi.
Kwingine nako,,mzee baluguza alitua salama huku akiwa sambamba na Mjukuu wake ambae tayali alikuwa hajui kinachoendelea...na kabla hajamwingiza ndani,alirudia kuunyoosha mkono wake tena juu..ghafla uliotea mkoba chakavu ambao ndani yake kulikuwa na hirizi pamoja na zana mbalimbali za kichawi...Alirudia kutabasam Mzee baluguza huku akijisemea "Walinibpu sasa mimi nawapigia...sina utani..Ngoja nikamlaze mjukuu wangu kisha nianze msako.."
Alisema maneno hayo kijasili kabisa Mzee buguza huku akimkumbatia mjukuu wake,,na punde si punde alitokea chumbani kwa Makongoro...hivyo akawa amemlaza kitandani kwake kisha akamluka mala tatu ili kumzindua..
Baada kufanya hivyo Mzee baluguza aliingia chumbani kwake..moja kwa moja akazama uvunguni mwa kitanda alichokua akilalia,,Akatoka na jungu lake kukuu ambalo lilikuwa mahususi kwa kutunza mazagazaga ya kichawi...Wakati huo huo ulivuma upepo mkali kisha kwenye kona ya chumba alitokea Bi mazoea mke wa Mzee baluguza,,,ambapo mala baada kumwona mume wake yupo bize alishtuka kwani alijua tayali anaenda kulipa kisasi kwa mtu aliemuwekea Sum kwenye pombe kwa nia ya kutaka kumuua.
"Za saa hizi Babu Makongoro..." Bi mzoea aliamsalimia mume wake,lakini Mzee balu alinyamanza kimya bila kuijibu salam aliyopewa na Mke wake..kitendo ambacho kilifanya kimya kidogo kutawala ndani ya robo saa...Na mala baada Mzee balu kukamilisha kile alichokuwa akikifanya,aliinua uso wake kumtazam mke wake ambae nae alikua kitandani kalala..kisha Mzee balu akasema.." naondoka na ntakacho rudi nacho naomba ukawatangazie wachawi wenzako...pumbaffu mwanamke gani mwenye roho mbaya kama simba yani upo tayar mumeo nife ili mfrahishe nafsi zenu.. nakuchukia sana Bi mazoea laiti kama ungelikuwa binti mdogo basi ungerudi kwenu.."
Mzee baluguza alisema maneno hayo kwa hisia kali huku akijichora chora usoni kwake kwa niaba kwenda kulipa kisasi...Wakati huo Bi mzoea nae akiwa kimya kitandani akijifanya kasinzia huku moyoni akijisemea "Mahali yenyewe hadi leo hujanitolea kazi kuropoka...kufaa tu"
Aliongea ndani ya nafsi yake Bi mazoea..maneno ambayo laiti kama Mzee baluguza angeyaskia basi kinuka.
Basi Mzee baluguza alipotea mle ndani mwake...akajikuta yuko nje.Ambapo moja kwa moja alifanya ishara ya kuita ungo ambao ndio chombo kikuu cha kusafiria wachawi..punde si punde ungo ulitokea hivyo haraka sana Mzee balu aliweka katika ule ungo kila dhana ya kichawi...Akiwa katika vazi la kitambaa cheusi ambacho nacho alikivaa kiunoni,,hatimae mzee balu alipaa angani akiwa na ungo wake kuelekea kwa Mama chiku..mama muuza pombe ambae alitaka kumuua Baluguza kwa kumuwekea sumu kwenye pombe.
Lakini wakati Mzee baluguza alipokuwa angani akielekea kwa Mama chiku,,mala ghafla alidondoshewa bundi kwenye ungo wake,bundi ambae nae alirusharusha mbawa zake mda mfupi tu akawa amefariki...Mzee balu alishtuka baada kumwona yule bundi..alipomtazama vizuri aligundua kuwa ni yule bundi wake ambae alikuwa akimtuma kunasa taarifa mbalimbali..Hivyo roho ilimuuma sana Mzee balu kwa kumpoteza mtoa taarifa wake,wakati huo nyuma yake alionekana Mchaw mmoja akiwa na tochi mbili akimfuata kwa kasi baluguza.
Safari ya Mzee baluguza angani ilianza kuwa ya mashaka,baada kufiwa na bundi wake ambae alikuwa akimsaidia kunasa taarifa mbalimbali..wakati huo nyuma yake ikionekana touch mbili zikimfuata nyuma.
Hivyo baada Mzee baluguza kugundua kuwa anafuatwa nyuma,,haraka sana alifungua mkoba wake mdogo aliokuwa nao..kisha ndani ya ule mkoba alichukua hirizi yake kubwa kisasi,,ambayo nayo alijifunga mkononi huku akiongea maneno ya kirugha kitendo ambacho kilimfanya Mzee baluguza kugeuka popo...ambapo aliweza kuzikimbia zile touch mbili zilizokuwa zikimfuata nyuma.
Hatimae Mzee baluguza alifika nyumbani kwa mama chiku..mama ambae alithubutu kutaka kumuua...na hivyo ujio wake Mzee baluguza ni kutaka kulipa kisasi na sio kitu kingine.
"Lazima nifyeke kichwa chake mwanamke huyu mshenzi" Alisema Mzee baluguza huku akijiandaa jinsi ya kuingia ndani ya nyumba ya mama chiku.
Na mala baada kuwa tayali Mzee baluguza alipiga hatua kuelekea kwenye nyumba ya mama chiku..ambapo baada kuifikia aliegemea ukata,haraka akajikuta yupo chumbani kwa mama chiku...akaweza kumwona mbaya wake akiwa amelala usingizi mzigo...na hiyo ndio ikawa nafasi ya Mzee baluguza kumfanyia unyama wa kutisha mama chiku kwa kumkata shingo yake huku dam akiikinga kwenye kibuyu chake ambacho nacho kilijaa...hivyo dam ya mama chiku ikawa bado inaendelea kusambaa akitandani... wakati huo mwili wake ukiendelea kurusha baadhi ya viungo vya mwili.
Baada kufanya kitendo hicho Mzee baluguza alicheka kidogo..kisha akanywa kidogo ile dam aliyokinga kutoka kwenye mwili wa mama chiku...ambapo baada kuimeza alitikisa kichwa kuashilia kuikubali kuwa dam ile ya mama chiku nitamu sana.
"mhm unadam tam sana wewe mwanamke..lakini tatizo lako moja tu,ulitaka kushindana na mwamba usiwezekanika...na ili nionekane kuwa mimi ni Shujaa!!ngoja niondoke na kichwa chako" Yalikuwa ni maneno ya kijasili ambayo Mzee baluguza alikuwa akiyaongea,,wakati huo akitumia kisu chake kuikata shingo ya mama chiku ilikutenganisha kichwa na kiwiliwili...hivyo ndani ya muda wa dakika mbili tayali Mzee baluguza alikuwa amefanikisha zoezi hilo...ambapo moja kwa moja alipotea mle chumbani kwa mama chiku..ghafla akaonekana nje huku mkononi mwake akiwa na kichwa cha mama chiku...ambapo alizipiga hatua mbili na kisha kupotea maeneo Yale ya nyumbani kwa mama chiku.
SOMA HAPA MAKALA ZA MAFANIKIO
ITAENDELEA
.jpeg)
No comments